JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UCHAGUZI2020: FACEBOOK KUDHIBITI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

> Facebook imezindua programu za kukabiliana na taarifa potofu ili kulinda Demokrasia kipindi hiki cha Uchaguzi

> Itahakikisha matangazo ya Kampeni yanathibitishwa kwa ajili ya uwazi

Soma https://jamii.app/FacebookUchaguzi
#JFLeo
BAKWATA MKOANI MTWARA YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Mtwara Mjini limetoa tamko la kumuombea na kumuunga mkono Dkt. Magufuli ili achaguliwe kuwa Rais wa #Tanzania kwa awamu nyingine

Soma https://jamii.app/BakwataKuraMagufuli
#TZ2020
UCHAGUZI MKUU 2020 NA UDHALILISHWAJI WA WAGOMBEA WANAWAKE

> Inaelezwa Mgombea Ubunge Tarime Mjini, Esther Matiko (CHADEMA) amekuwa akidhalilishwa na baadhi ya watu huku wengine wakiwa ni viongozi kama Polisi anayedaiwa kumtukana juzi

Soma - https://jamii.app/MilaWagombeaKe
#Uchaguzi2020
DR CONGO: WANASAYANSI WATAHADHARISHA KUHUSU MLIPUKO WA VOLKANO

> Kuna hatari ya Mlima Nyiragongo uliopo Goma, Mashariki mwa nchi hiyo kulipuka ndani ya miaka minne

> Januari mwaka 2002, Mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya watu 250

Soma - https://jamii.app/VolcanoDRC
#JFLeo
TUNDU LISSU: MAGUFULI AMEBAKIZA SIKU 14 KUKAA IKULU

> Akiwa Ukerewe amesema akichaguliwa kuwa Rais manyanyaso dhidi ya Wavuvi yatakuwa mwisho

> Ataboresha Sheria za uvuvi, kupanua Bandari ya Nansio na kujenga daraja la Kisorya-Ukerewe

Soma https://jamii.app/LissuUkerewe
#Uchaguzi2020
TUNDU LISSU KUJIBU MASWALI YA WANANCHI KUPITIA JAMIIFORUMS

> Mwanachama wa JamiiForums na Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu atajibu maswali ya Wananchi kupitia JamiiForums

> Ni kesho Oktoba 15, 2020 kuanzia saa 2 hadi 4 asubuhi

Uliza swali lako hapa https://jamii.app/LissuOnJF
DKT. MAGUFULI: NATAMANI KUFIKA KILA ENEO KUFANYA KAMPENI LAKINI SIWEZI

> Amesema hawezi kwasababu na yeye ni binadamu

> Amesema mbali na kuwa Mgombea, yeye pia ni Rais ambaye anapaswa kufanya majukumu ya Serikali ambayo bado yanamkabili

Soma - https://jamii.app/DktJPMKawe
#TZ2020
ZANZIBAR: ADA-TADEA YAAHIDI KUINUA SEKTA YA MICHEZO ILI ISITEGEMEE WAFADHILI

> Mgombea Urais wa Chama hicho, Juma Khatib amesema ataweka bajeti maalum kuendesha Ligi Kuu

> Wafadhili watapewa nafasi, lakini bajeti ya Serikali haitaondolewa

Soma https://jamii.app/ADATADEA
#TZ2020
NIGERIA: WANANCHI WAENDELEA NA MAANDAMANO KUPINGA UKATILI WA POLISI

> Licha ya Serikali kufuta kikosi cha #SARS kilichopewa kazi ya kupambana na wahalifu, wananchi wanasema hawajaridhika na hatua hiyo na wanachokitaka ni Mageuzi kwenye Jeshi

Soma https://jamii.app/NigeriaProtests
UPDATE: Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kumuuliza maswali Lissu; imebidi apate muda kuyapitia maswali yote (takriban 1,000)

> Tunatarajia kufikia kesho atakuwa ameyapitia maswali hayo na yote yatajibiwa

> Shukrani kwa wote walioshiriki
MAALIM SEIF ATAKIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI YA MAADILI LEO

> Mgombea wa Urais wa #Zanzibar (ACT-Wazalendo) anadaiwa kukiuka maadili ya Uchaguzi kutokana na kuwaambia watu wakapige kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28 iliyopangwa na ZEC

Soma - https://jamii.app/SeifKamatiMaadili
#Uchaguzi2020
SIKU YA KIMATAIFA YA KUNAWA MIKONO: OSHA MIKONO OKOA MAISHA

> Oktoba 15 ni Siku ya Kimataifa ya Unawaji Mikono. Ni siku maalum ya kuhamasisha watu kunawa mikono ili kuepuka maradhi

> Kaulimbiu ya Kitaifa ni β€˜Osha Mikono Okoa Maishaβ€˜

Soma - https://jamii.app/KunawaMikono
UCHAGUZI 2020: JINSI MPIGA KURA ANAVYOWEZA KUTAMBUA KITUO CHAKE CHA KUPIGIA KURA

> Orodha ya wapiga kura kwa kila kituo itabandikwa siku nane (8) kabla ya Siku ya Uchaguzi

> Kujua jinsi ya kuhakiki kituo chako cha kupigia kura, fungua > https://jamii.app/HakikiKituoKura

#Uchaguzi2020
SERIKALI KUTUMIA HELIKOPTA KUZIMA MOTO MLIMA #KILIMANJARO

> Waziri wa Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema wanatazamia kutuma Helikopta kuuzima moto unaowaka kwa siku ya 5 sasa

> Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka

Soma - https://jamii.app/NdegeMotoKLM
MICHEZO: Wachezaji wa Klabu ya #Juventus wameamua kujiweka Karantini baada ya Kiungo wa Timu hiyo, Weston McKennie kuthibitika kuwa na maambukizi ya #CoronaVirus

> Taarifa za Weston zinakuja ikiwa ni siku 2 tangu Cristiano Ronaldo athibitike kuwa na Virusi hivyo

#JFSports
#UGANDA: POLISI WADAIWA KUIBA NYARAKA ZA BOBI WINE KUGOMBEA URAIS

> Amesema nyaraka za uteuzi wake wa kugombea Urais zimepotea baada ya uvamizi kutoka Vikosi vya Usalama jana mchana

> Timu yake tayari ilikuwa imeshakusanya sahihi Milioni 6

Soma - https://jamii.app/BobiOfficeRaid
UNICEF: WATU BILIONI 3 DUNIANI HAWANA VIFAA VYA KUNAWIA MIKONO

> Takriban robo tatu ya watu katika nchi masikini wanakosa vifaa hivyo

> Aidha 43% ya Shule hazina vifaa vya kunawia mikono, na hivyo kuwaathiri watoto wapatao Milioni 818

Soma - https://jamii.app/UNICEFTakwimu
GEITA: POLISI KUWASAKA WALIOVAMIA NYUMBA 3 ZA WAGOMBEA WA CHADEMA

> Watu zaidi ya 10 wanatuhumiwa kuchoma moto Bajaji 2, kuvunja vioo vya madirisha kwa mawe pamoja na kubomoa madirisha 2 ya nyumba usiku wa kuamkia Oktoba 13

Soma - https://jamii.app/BajajiMotoCDM
#Uchaguzi2020