JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PWANI: MAHABUSU ALIYEKUWA NA KESI YA MAUAJI AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

> Mahabusu Musa Haji Mchana amefariki na wafungwa wanne wamejeruhiwa kwa radi ktk gereza la Mng'aro

> Polisi wamesema hakuna mfungwa aliyetoroka na ulinzi umeimarishwa

Soma https://jamii.app/MahabusuRadi
#JFLeo
RWANDA YARUHUSU KILIMO CHA BANGI KWA SABABU ZA KIBIASHARA

> Serikali imehalalisha kulimwa na kuuzwa kwa bangi nje ya nchi ili kunufaika kiuchumi

> Soko la zao hilo duniani lina thamani ya Dola Bilioni 345 (takriban Tsh. Trilioni 800)

Soma https://jamii.app/RwandaBangi
#JFLeo
HALIMA MDEE: NATUHUMIWA KUMCHONGANISHA GWAJIMA NA MADHEHEBU MENGINE

> Mgombea Ubunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee amesema atakata rufaa NEC dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Maadili ambayo yamemsimamisha kufanya kampeni kwa siku 7

Soma https://jamii.app/AdhabuMdee
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: SIJAWAHI KUOMBWA KUWASAIDIA WANANCHI WA KAWE

> Akiwa eneo la Basihaya lililopo Boko jijini Dar, Dkt. John Magufuli amesema jana alipigiwa simu na Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Josephat Gwajima kuhusu adha ya maji

> Amesema wakimchagua Gwajima atawatengea Tsh. Bilioni 5 ili kukarabati mitaro ya Jimbo hilo

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#Uchaguzi2020
DKT: MAGUFULI: VYAMA VYENYE BENDERA ZILIZO NA RANGI NYEKUNDU VINAASHIRIA MABAYA

> Ameeleza kuwa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata Uhuru wa nchi hii bila kumwaga damu, ndio sababu bendera ya taifa haina rangi nyekundu

> Amesema kuna baadhi ya vyama vya siasa vina bendera zenye rangi nyekundu ambayo haiashirii dalili nzuri

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#Uchaguzi2020
UCHAGUZI 2020: IJUE HAKI YA VYAMA VYA SIASA NA WAGOMBEA KUTEUA MAWAKALA

> Chama kinaruhusiwa baada ya kupata ridhaa ya Mgombea/Wagombea kuteua na kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina ya mawakala siku 7 kabla ya siku ya #Uchaguzi

Soma > https://jamii.app/UteuziMawakala

#TZ2020
KIKWETE ASHAURI GHARAMA ZA MAZOEZI KWA WATOTO WENYE USONJI ZIPUNGUZWE

> Amesema kila zoezi moja ambalo watoto hufanyiwa ni Tsh. 20,000 Hospitali ya Muhimbili na Tsh. 50,000 Hospitali binafsi

> Mtoto anatakiwa kufanyiwa mazoezi 6 kila siku

Soma https://jamii.app/GharamaUsonji
#JFLeo
DKT. BASHIRU: SIFA YA MAENDELEO YA WATU NI KUJITAWALA WENYEWE

> Katibu Mkuu wa CCM Taifa, amesema maendeleo ya watu ni uwezo wa kujitawala, kuchapa kazi na kuwa na mahusiano mazuri

> Pia, amemsifu Dkt. Magufuli kwa kuleta maendeleo ya watu

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#TZ2020
TUNDU LISSU ALAZIMIKA KUTUMIA MTUMBWI KUFIKA UKEREWE

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na msafara wake wamelazimika kutumia Mitumbwi kufika Ukerewe kwa ajili ya Kampeni baada ya kuambiwa Kivuko cha Kisorya-Ngoma ni kibovu

Tazama https://youtu.be/hjbVHnKcOJ8
#Uchaguzi2020
ALI KIBA AOMBA MWALIMU NYERERE ATENGENEZEWE β€˜DOCUMENTARY’

> Msanii huyo amemuomba Dkt. Magufuli atenge fedha kwa ajili ya documentary ya Baba wa Taifa

> Amesema itasaidia kukuza tasnia ya filamu nchini na kufanya Nyerere afahamike kwa vijana

Soma https://jamii.app/NyerereDocumentary
#JFLeo
#UCHAGUZI2020: FACEBOOK KUDHIBITI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

> Facebook imezindua programu za kukabiliana na taarifa potofu ili kulinda Demokrasia kipindi hiki cha Uchaguzi

> Itahakikisha matangazo ya Kampeni yanathibitishwa kwa ajili ya uwazi

Soma https://jamii.app/FacebookUchaguzi
#JFLeo
BAKWATA MKOANI MTWARA YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Mtwara Mjini limetoa tamko la kumuombea na kumuunga mkono Dkt. Magufuli ili achaguliwe kuwa Rais wa #Tanzania kwa awamu nyingine

Soma https://jamii.app/BakwataKuraMagufuli
#TZ2020
UCHAGUZI MKUU 2020 NA UDHALILISHWAJI WA WAGOMBEA WANAWAKE

> Inaelezwa Mgombea Ubunge Tarime Mjini, Esther Matiko (CHADEMA) amekuwa akidhalilishwa na baadhi ya watu huku wengine wakiwa ni viongozi kama Polisi anayedaiwa kumtukana juzi

Soma - https://jamii.app/MilaWagombeaKe
#Uchaguzi2020
DR CONGO: WANASAYANSI WATAHADHARISHA KUHUSU MLIPUKO WA VOLKANO

> Kuna hatari ya Mlima Nyiragongo uliopo Goma, Mashariki mwa nchi hiyo kulipuka ndani ya miaka minne

> Januari mwaka 2002, Mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya watu 250

Soma - https://jamii.app/VolcanoDRC
#JFLeo
TUNDU LISSU: MAGUFULI AMEBAKIZA SIKU 14 KUKAA IKULU

> Akiwa Ukerewe amesema akichaguliwa kuwa Rais manyanyaso dhidi ya Wavuvi yatakuwa mwisho

> Ataboresha Sheria za uvuvi, kupanua Bandari ya Nansio na kujenga daraja la Kisorya-Ukerewe

Soma https://jamii.app/LissuUkerewe
#Uchaguzi2020
TUNDU LISSU KUJIBU MASWALI YA WANANCHI KUPITIA JAMIIFORUMS

> Mwanachama wa JamiiForums na Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu atajibu maswali ya Wananchi kupitia JamiiForums

> Ni kesho Oktoba 15, 2020 kuanzia saa 2 hadi 4 asubuhi

Uliza swali lako hapa https://jamii.app/LissuOnJF