JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UWEKAJI JIWE LA MSINGI, MBEZI: RAIS MAGUFULI AAGIZA MRADI KUKAMILIKA KABLA YA NOVEMBA

> Amesema, "Mradi huu ulitakiwa umalizike mwezi wa 7, haujamalizika. Na hili lazima niliseme kwa dhati, kisingizio ni #CoronaVirus. Mimi nataka wafanye kazi mpaka wawe wanafia hapa na Corona lakini jengo limalizike haraka"

> Amesema, fedha za mradi huo ni za Watanzania masikini ambao wamewekeza ili kupata faida

Soma - https://jamii.app/JPM-MradiMbezi
SUGU: CHADEMA WAKICHAGULIWA SADAKA ZITAONGEZEKA

> Amewaomba Viongozi wa Dini wawaombe waumini wachague Wagombea wa Chama hicho kwasababu Serikali ya CHADEMA ina Sera za Uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini

Soma - https://jamii.app/SuguCDMSadaka
#Uchaguzi2020
RAIS TRUMP ASITISHA MJADALA WA JITIHADA ZA KUNUSURU UCHUMI KUTOKANA NA #COVID19

> Amesema Spika wa Bunge, Nancy Pelosi hakuwa na nia njema ktk majadiliano hayo

> M/kiti wa Hazina ya nchi ameonya kuhusu hali ya uchumi inavyozidi kuwa mbaya

Soma https://jamii.app/USEconomyCorona
VYAMA NANE VYAMTAKA MBOWE AJIELEZE KWA MSAJILI

> Makatibu Wakuu wa ADC, NRA, DP, UMD, SAU, UPDP, Demokrasia Makini na AFP wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kumuita Freeman Mbowe, ili ajielezee kwa madai ya kuviita Vyama hivyo bandia

Soma - https://jamii.app/VyamaMboweMsajili
#TZ2020
WAGOMBEA WATAKIWA KUKEMEA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

> Wametakiwa kuwa na ajenda ya kupambana na vitendo hivyo ili Wanawake na Watoto wawe salama

> Jamii kukataa kutoa ushahidi Mahakamani ni kati ya sababu ya kesi za udhalilishaji kufutwa

Soma - https://jamii.app/WagombeaUdhalilishaji
#TZ2020
MAJALIWA: WATANZANIA TAMBUENI UMUHIMU WA KURA ZENU

> Amesema inatakiwa kumchagua Rais anayeweza kuleta maendeleo na sio maneno pekee

> Amewataka wananchi kuwasikiliza na kuwapima Wagombea mbalimbali huku wakiwa wanafahamu umuhimu wa kura zao

Soma https://jamii.app/UmuhimuKura
#TZ2020
KENYA: MUSWADA WA KURUHUSU POLISI KUSIKILIZA MAWASILIANO YA SIMU WAPENDEKEZWA

> Muswada huo unaopendekezwa na Mbunge wa Kiambaa unaomba idhini kwa Polisi kusikiliza mawasiliano ya simu iwapo watakushuku unahusika na biashara ya #DawaZaKulevya

Soma https://jamii.app/PolicePhoneConv
MAREKANI: MATATIZO YA NDANI YAPELEKEA CITIBANK KUTOZWA FAINI YA DOLA MILIONI 400

> Mamlaka zimesema Benki imeshindwa kutatua changamoto ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa, kitendo kinachoashiria imeshindwa kuwa na mkakati wa kudhibiti majanga

Soma https://jamii.app/CitibankFineUS
MBEYA: ACHOMWA KISU BAADA YA UGOMVI WA KUTOA SIRI ZA MICHEPUKO KWA WATU

> Tabia Abdalah (38) amechomwa kisu shingoni na Salome Buya (23) baada ya kuzuka ugomvi uliomtuhumu Salome kuwatangaza wenzake kwa watu pindi wakichepuka nje ya ndoa zao

Soma https://jamii.app/KisuMichepuko
PROF. LIPUMBA: UKUAJI WA UCHUMI HAUJAPUNGUZA WATU MASIKINI

> Mgombea Urais kupitia CUF, amesema ukuaji wa Uchumi wa #Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini, bali idadi ya watu masikini imeongezeka

Soma - https://jamii.app/LipumbaTarakea
#Uchaguzi2020
WHO: WATOTO MILIONI 2 HUFIA TUMBONI KILA MWAKA

> Ripoti ya WHO, UNICEF na washirika wake imesema vifo vinatokea zaidi kwenye nchi zinazoendelea

> Mkurugenzi wa UNICEF amesema kila sekunde 16, mjamzito hupata matatizo ya mtoto kufia tumboni

Soma - https://jamii.app/2milStillbirth
MAREKANI: TRUMP KUTOSHIRIKI MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS KUPITIA MTANDAO

> Amesema hatoshiriki kwakuwa uamuzi huo unalenga kumlinda Joe Biden

> Tume imesema imebadili mfumo kulinda afya za washiriki baada ya Rais Trump kupata #COVID19

Soma - https://jamii.app/TrumpDebateUS
MANYARA: MWALIMU MKUU MBARONI KWA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA DARASA LA 7

> Oscar Waluye anatuhumiwa kuwalazimisha Wanafunzi wawili wa Darasa la 6 kufanya mitihani hiyo badala ya Watahiniwa, ambao uwezo wao darasani ni wa kiwango cha chini

Soma https://jamii.app/MwlMitihani7
BRAZIL: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 5

> Wizara ya Afya imetangaza visa vipya 31,553 na idadi ya wenye Virusi hivyo imefikia 5,000,694

> Wataalamu wana hofu ya kutokea kwa awamu ya pili ya maambukizi kabla ya kwanza haijadhibitiwa

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
DKT. MAGUFULI KUFANYA KAMPENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

> Mgombea Urais wa #Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya Mkutano wa Kampeni leo Oktoba 09, kuanzia saa 2 asubuhi katika Uwanja wa Mkapa, Temeke

Soma - https://jamii.app/MagufuliDar
#Uchaguzi2020
DKT. MWINYI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI

> Amesema Serikali inawathamini wawekezaji kwasababu wanasaidia ukuaji wa Pato la Taifa

> Aahidi kuwawekea mazingira bora akiingia madarakani ili wafanye kazi bila ya kikwazo

Soma - https://jamii.app/DktMwinyiZNZ
#Uchaguzi2020
#CORONAVIRUS: KENYA KUANZA MAOMBI YA KITAIFA YA SIKU 3 LEO

> Wakenya wametakiwa kuliombea Taifa huku wakizingatia taratibu za kujikinga na maambukizi

> Hii ni mara ya pili kwa Kenya kufanya maombi tangu kuanza kwa mlipuko huo

Soma - https://jamii.app/NationalPrayerKE
NEC: ALIYEHAMA MAHALI ALIPOJIANDIKISHA HATAWEZA KUPIGA KURA SEHEMU NYINGINE

> Mjumbe wa NEC, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kama watu husafiri kuja Dar ili kuangalia mpira wa Simba na Yanga, basi suala la kupiga kura ni la muhimu zaidi

Soma https://jamii.app/VituoKupigaKura
#Uchaguzi2020
ZANZIBAR: MAALIM SEIF KUKOMESHA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

> Amesema Kikosi cha Kupambana na #DawaZaKulevya kimekuwa kinafanya kazi ya kuwakamata wauzaji wadogo, huku wahusika wakubwa wakiendelea na biashara hiyo bila wasiwasi

Soma - https://jamii.app/MaalimMadawa
#Uchaguzi2020
MATUMIZI HOLELA YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO YAONGEZA SARATANI YA MATITI KWA MABINTI

> Taasisi ya Saratani(ORCI) imesema kuna ongezeko la Saratani kwa mabinti kuanzia miaka 25, na inachochewa na matumizi ya vidonge hivyo kinyume na taratibu

Soma https://jamii.app/SarataniMabinti