JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TABORA: WAHAMIAJI HARAMU 32 WAKUTWA NA KADI ZA KUPIGIA KURA

> Raia hao wa Burundi wamekamatwa Mkoani Tabora wakitokea Kigoma kuelekea Dar na Mbeya

> 25 walikamatwa Wilayani Urambo ndani ya Treni na 7 walikamatwa Kituo Kikuu cha Mabasi Tabora

Soma https://jamii.app/WahamiajiKadiKura
ARUSHA: WATU WATANO MBARONI KWA MAKOSA YA KIMTANDAO

> Walikamatwa ktk ofisi za aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema

> Wanadaiwa kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kibenki na kuendesha mafunzo ya kutenda uhalifu wa kijinai

Soma https://jamii.app/Kada5CDMUhalifu
RAIS CHAKWERA AMFAGILIA RAIS MAGUFULI, ATAMANI KUSHIKILIA KOTI LAKE

> Rais Chakwera amesema, "Nilimwambia Rais Magufuli kama inawezekana ningependa kushikilia koti lake tu ili anapokimbia aweze kunivuta nami niende haraka kwa kasi yake"

> Naye Rais Magufuli amesema Tanzania na Malawi wamekuwa marafiki tangu ukoloni na watawafundisha mbinu za kukusanya kodi kama Tanzania ilivyofanikiwa

Soma - https://jamii.app/JPMChakweraIkulu
TUNDU LISSU ATEMBELEA SOKO LA KARIAKOO HUKU AKITUMIA USAFIRI WA UMMA

> Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, leo ameamua kutembelea viunga vya Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam huku akitumia usafiri wa Mwendokasi kutokea Kinondoni Morocco

Angalia https://youtu.be/89_XiJwLC5Q
#JFSiasa
KENYA: WATUHUMIWA WAWILI WA SHAMBULIO LA WESTGATE WAKUTWA NA HATIA

> Mohammed Ahmed Abdi na Hussein Hassan Mustafa wamekutwa na hatia ya kupanga njama ya ugaidi na kusaidia kundi la magaidi

> Pia, Mahakama imemuachia huru Liban Abdullah Omar

Soma https://jamii.app/Hatia2Westgate
JE, WAJUA UZAZI WA MFULULIZO UNAWEZA KUSABABISHA MAMA AJIFUNGUE MTOTO NJITI?

> Mama kuzaa mfululizo ni kichocheo cha Mama kujifungua #MtotoNjiti

> Mama anayejifungua mfululizo mlango wake wa kizazi huwa katika hatari ya kufunguka wakati wowote

Soma > https://jamii.app/UzaziMtotoNjiti
UFAHAMU MFUMO WA UCHAGUZI WA TANZANIA

> Tanzania inatumia mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post)

> > Mfumo mwingine unaotumika ni ule wa uwiano wa kura (Proportional Representation) ambao hutumika kupata Wabunge, Madiwani na Wabunge wa Viti Maalum

Zaidi, soma > https://jamii.app/MfumoUchaguziTz

#Uchaguzi2020
UFAHAMU MZUNGUKO WA UCHAGUZI UNAOTUMIKA TANZANIA

> Ibara za 42 (2) na 65 ya Katiba ya JMT na kifungu cha 12 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa zinaelekeza Uchaguzi Mkuu ufanyike kila baada ya miaka mitano (5)

Mzunguko wa Uchaguzi wa #Tanzania umegawanyika katika awamu tatu (3) kama ifuatavyo;

> 1: Kabla ya Uchaguzi: Kutenga bajeti, Elimu kwa Wapiga Kura, mafunzo kwa watendaji na uandikishaji wa Wapiga Kura

> 2: Wakati wa Uchaguzi: Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi, Upigaji Kura na kutangaza matokeo hufanyika kwa usimamizi wa Tume ya Uchaguzi (NEC)

> 3: Baada ya Uchaguzi: Hufanyika, tathmini ya Uchaguzi, mabadiliko ya sheria na uboreshaji wa daftari la wapiga kura

Soma > https://jamii.app/MfumoUchaguziTz

#Uchaguzi2020
AFRIKA KUSINI: WAFANYAKAZI WAANDAMANA KUPINGA UPOTEVU WA AJIRA NA UFISADI

> Chama kikubwa zaidi cha Wafanyakazi (COSATU) kimewataka wanachama wake zaidi ya Milioni 1 kutofanya kazi kufuatia madai mbalimbali ikiwemo kutoongezewa mishahara

Soma - https://jamii.app/SAWorkersProtest
WANAOISHI NA WAVUTA SIGARA HATARINI KUPATA MATATIZO

> Dkt. Fransis Furia(MUHAS) amesema, watoto wanaokaa na watu wanaotumia bidhaa za Tumbaku wako hatarini kupata Saratani

> Kwa mjamzito, husababisha mtoto kuzaliwa njiti au mimba kuharibika

Soma https://jamii.app/SigaraWatoto
TANZIA: KATIBU MWENEZI WA CHADEMA, KATA YA MHINTIRI AUAWA KWA MAPANGA

> Katibu Mwenezi wa CHADEMA Kata ya Mhintiri, Jimbo la Singida Magharibi, Nicholas Andrea Gui anadaiwa kukutwa ameuawa kwa kukatwa mapanga majira ya saa moja jioni jana

Soma - https://jamii.app/KatibuCDMAuawa
MGAYWA (SAU): SERA ZETU ZINATEKELEZEKA KUTOKANA NA UTAJIRI WA TANZANIA

> Mgombea huyo wa Urais ameomba kura ili afanikishe Sera zinazolenga kumpa raha Mtanzania

> Miongoni mwa Sera za SAU ni pamoja na kumwezesha kila mwananchi Milioni 1

Soma - https://jamii.app/KuraSeraSAU
#TZ2020
RAIS MAGUFULI NA RAIS CHAKWERA KUWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA MABASI MBEZI

> Marais hao leo wataweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Kisasa cha Mbezi Luis - Dar

> Inaelewa kuwa, Mradi huo tayari umeshakamilika kwa 80%

Angalia - https://youtu.be/CjIoCuKLvJ8
JAJI MKUU: MAHAKAMA IMEJIPANGA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UCHAGUZI

> Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema mafunzo ya kuendesha mashauri hayo yametolewa

> Pia, Majaji na Mahakimu wamefundishwa namna bora ya kuandika Hukumu

Soma - https://jamii.app/KesiUchaguzi
#Uchaguzi2020
UWEKAJI JIWE LA MSINGI, MBEZI: RAIS MAGUFULI AAGIZA MRADI KUKAMILIKA KABLA YA NOVEMBA

> Amesema, "Mradi huu ulitakiwa umalizike mwezi wa 7, haujamalizika. Na hili lazima niliseme kwa dhati, kisingizio ni #CoronaVirus. Mimi nataka wafanye kazi mpaka wawe wanafia hapa na Corona lakini jengo limalizike haraka"

> Amesema, fedha za mradi huo ni za Watanzania masikini ambao wamewekeza ili kupata faida

Soma - https://jamii.app/JPM-MradiMbezi
SUGU: CHADEMA WAKICHAGULIWA SADAKA ZITAONGEZEKA

> Amewaomba Viongozi wa Dini wawaombe waumini wachague Wagombea wa Chama hicho kwasababu Serikali ya CHADEMA ina Sera za Uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini

Soma - https://jamii.app/SuguCDMSadaka
#Uchaguzi2020
RAIS TRUMP ASITISHA MJADALA WA JITIHADA ZA KUNUSURU UCHUMI KUTOKANA NA #COVID19

> Amesema Spika wa Bunge, Nancy Pelosi hakuwa na nia njema ktk majadiliano hayo

> M/kiti wa Hazina ya nchi ameonya kuhusu hali ya uchumi inavyozidi kuwa mbaya

Soma https://jamii.app/USEconomyCorona
VYAMA NANE VYAMTAKA MBOWE AJIELEZE KWA MSAJILI

> Makatibu Wakuu wa ADC, NRA, DP, UMD, SAU, UPDP, Demokrasia Makini na AFP wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kumuita Freeman Mbowe, ili ajielezee kwa madai ya kuviita Vyama hivyo bandia

Soma - https://jamii.app/VyamaMboweMsajili
#TZ2020
WAGOMBEA WATAKIWA KUKEMEA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

> Wametakiwa kuwa na ajenda ya kupambana na vitendo hivyo ili Wanawake na Watoto wawe salama

> Jamii kukataa kutoa ushahidi Mahakamani ni kati ya sababu ya kesi za udhalilishaji kufutwa

Soma - https://jamii.app/WagombeaUdhalilishaji
#TZ2020
MAJALIWA: WATANZANIA TAMBUENI UMUHIMU WA KURA ZENU

> Amesema inatakiwa kumchagua Rais anayeweza kuleta maendeleo na sio maneno pekee

> Amewataka wananchi kuwasikiliza na kuwapima Wagombea mbalimbali huku wakiwa wanafahamu umuhimu wa kura zao

Soma https://jamii.app/UmuhimuKura
#TZ2020