JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZITTO KABWE APATA AJALI YA GARI KIGOMA

> Kiongozi huyo wa Chama cha ACT-Wazalendo amepata ajali wakati akitokea Kalya kuelekea Lukoma kwaajili ya kampeni

> Alikuwa na watu watano kwenye gari na wote wapo salama licha ya kupata majeraha

Soma - https://jamii.app/ZittoAjali
TFF YATAMBULISHA JEZI MPYA ZITAKAZOTUMIWA NA TAIFA STARS

> Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetambulisha jezi mpya ikiwemo jezi ya nyumbani, ya ugenini na jezi namba 3

> Oktoba 11, 2020 Tanzania itacheza mchezo wa kirafiki na Burundi

Soma https://jamii.app/JeziTaifaStars
AFISA HABARI WA ACT-WAZALENDO ATUHUMIWA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO TWITTER

> Dotto Rangimoto amefikishwa Mahakama ya Kisutu akidaiwa kutenda kosa hilo kwa jina la James Michael

> Amepata dhamana (Mdhamini 1 ambaye ni Mkazi wa Dar) na Bondi ya Tsh. Milioni 5

Soma https://jamii.app/DottoKizimbani
MAJALIWA: TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI ANAYEWEZA KUPAMBANA NA MAFISADI

> Amesema Kiongozi anatakiwa kusimamia Serikali na kuhakikisha aliowateua wanatekeleza majukumu

> Amewataka wananchi wasichague viongozi kwa ushabiki ili wasije kujilaumu

Soma https://jamii.app/MajaliwaKiongoziTZ
#TZ2020
KENYA: WANAFUNZI WA DARASA LA 4, 8 NA KIDATO CHA 4 KUREJEA SHULE JUMATATU IJAYO

> Shule zimetakiwa kuendelea kufuata kanuni za kudhibiti maambukizi ya #COVID19 kama kuvaa barakoa, kupima joto la Wanafunzi na Walimu pamoja na kunawa mikono

Soma https://jamii.app/SchoolResumeKE
RAIS WA #MALAWI KUFANYA ZIARA NCHINI #TANZANIA

> Rais Dkt. Lazarus Chakwera anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa kuanzia Oktoba 7 - 9, 2020

> Yeye na Rais Magufuli wataweka jiwe la msingi ktk Kituo cha Mabasi ya Mkoani cha Mbezi Mwisho, Dar

Soma https://jamii.app/ZiaraRaisMalawi
RAIA WA KIGENI KUDHIBITIWA KUSHIRIKI KTK UCHAGUZI

> Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imezielekeza Kamati za Ulinzi na Usalama zilizopo mipakani kuwadhibiti raia wa kigeni kushiriki ktk Uchaguzi Mkuu, kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na Sheria

Soma https://jamii.app/NECWageniUchaguzi
#TZ2020
IMF YAIDHINISHA MSAADA WA DHARURA KWA NCHI 28 IKIWEMO TANZANIA

> Msaada wa Shirika la Fedha unalenga kuzisaidia nchi kupunguza madeni na kukabiliana na athari za #COVID19

> Hii ni awamu ya pili ya msaada huo, awamu ya kwanza ilihusisha nchi 25

Soma https://jamii.app/IMFAidTZ
JamiiForums: TUTATOWEKA HEWANI KWA DAKIKA KADHAA NA KUREJEA

> Mtandao wetu wa JamiiForums.com utatoweka hewani kwa dakika kadhaa ili kurekebisha masuala kadhaa na kuboresha upatikanaji wa huduma

> Zoezi hili linatarajiwa kutumia takribani dakika 30. Tunashukuru kwa uelewa na uvumilivu wako
JamiiForums: TUMEREJEA HEWANI BAADA YA MABORESHO YA DAKIKA 15

> Mtandao wetu wa JamiiForums umerejea hewani baada ya kutokuwa hewani kwa dakika 15 za maboresho ya upatikanaji wa huduma

> Zoezi hili limekamilika salama. Tunashukuru kwa uvumilivu wako muda wote ambao hatukuwa hewani
QUEEN SENDIGA: MABORESHO KATIKA SEKTA YA KILIMO NI MUHIMU

> Mgombea Urais wa JMT kupitia ADC, akiwa Wilaya ya Liwale amesisitiza maboresho ktk Sekta ya Kilimo ni ya muhimu na ndio tiba pekee ya kuwapelekea wananchi maendeleo ya kweli

Soma - https://jamii.app/ADCLiwale
#uchaguzi2020
UPDATE: ZITTO NA WENZAKE WANAENDELEA VIZURI

> Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema anaendelea vizuri kufuatia ajali aliyopata jana mkoani Kigoma

> Amesema yeye na wenzake ni wazima na kuwashukuru Wahudumu na Madaktari

Soma - https://jamii.app/ZittoAjaliKgm
TLS KUMSAIDIA FATMA KARUME KUKATA RUFAA YA ADHABU ALIYOPEWA

> Baraza la Uongozi wa TLS limegundua Mwanasheria Mkuu aliwasilisha upya malalamiko yake kwa Kamati ya Mawakili kinyume na amri na maelekezo ya Jaji Kiongozi

> Muundo wa Kamati ya Mawakili una uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa upendeleo au muonekano wa upendeleo

Soma - https://jamii.app/TKSRufaniFatma
TLP, UDP ZAJITOA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Ni baada ya Ofisi ya Msajili kuvitaarifu kuwa havikufuata Kanuni na Sheria za Uchaguzi

> UDP wameendelea na kazi za kampeni, wakiwa na Mgombea wao. TLP ambao waliweka mabango wameyatoa

Soma https://jamii.app/TLP-UDPMagufuli
#TZ2020
MICHEZO: Bodi ya Ligi Kuu imesema Mechi ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Oktoba 18, 2020 imesogezwa mbele hadi Novemba 7

> Sababu ni uwezekano wa kuwepo kwa vikwazo vya usafiri kwa wachezaji wa Kimataifa kutokana na kalenda za FIFA

Soma - https://jamii.app/HairishoSimbaYanga
DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUNA UBAGUZI WA KIDINI, KIJINSIA NA KIKANDA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM ameahidi kupambana na vitendo hivyo na kusema, mtu anayetafuta uongozi wa nchi hawajibiki kwa wanaompigia kura tu, bali hata kwa Mungu

Soma - https://jamii.app/UbaguziZbar
#TZ2020
MAASKOFU WAHIMIZA NEC KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA HAKI

> Chama cha Maaskofu na Wachungaji (TPA) kimesema Watanzania wanatarajia kuona Tume ya Uchaguzi inasimamia haki na kufuata Sheria za Uchaguzi kuepuka malalamiko yanayoanza kujitokeza

Soma - https://jamii.app/TPA-NECUchaguzi

#Uchaguzi2020
ECOWAS YAIONDOLEA VIKWAZO MALI BAADA YA KUUNDA SERIKALI YA MPITO

> Imefikia uamuzi huo kwa kuzingatia hatua ambazo Mali imepiga kurudi katika Mfumo wa Kikatiba

> Mali iliwekewa vikwazo kufuatia mapinduzi yaliyomtoa Ibrahim Keita madarakani

Soma - https://jamii.app/VikwazoMali
RAIS WA MALAWI, DKT. LAZARUS CHAKWERA AWASILI NCHINI

> Rais Chakwera amepokelewa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Pia, akiwa JNIA amekagua gwaride la heshima aliloandaliwa

>Marais hao wawili wanatarajia kufanya mazungumzo baadaye

Soma - https://jamii.app/RaisChakweraTZ
SINGAPORE: SERIKALI KUWALIPA WANANCHI ILI WAZAE KIPINDI HIKI CHA #COVID19

> Wananchi wengi waliokusudia kupata watoto wanadaiwa kusitisha hilo kutokana na kukosa fedha/ajira

> #Singapore ni nchi yenye kiwango kidogo cha watu kuzaliana

Soma - https://jamii.app/BirthPaySingap