JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI 2020: JE, UNAFAHAMU MAJUKUMU YA TUME YA UCHAGUZI?

> Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura ktk Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa JMT

> Kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia wanaotoa elimu hiyo

Soma - https://jamii.app/MajukumuNEC
#Uchaguzi2020
QUEEN SENDIGA: UZURI WA VIPAUMBELE VYA ADC UTANIPA USHINDI

> Amesema, Ilani ya Chama imetoa kipaumbele kwa Elimu, Afya na Kilimo kutokana na umuhimu wake kwa kila mtu

> Mgombea huyo wa Urais anaamini Uchaguzi Mkuu utakuwa Huru na wa Haki

Soma - https://jamii.app/QueenUshindiADC

#TZ2020
SERIKALI YAFUTA MTAALA WA UALIMU WA NGAZI YA CHETI

> Wizara ya Elimu imetangaza kufuta Mtaala wa Ualimu wa ngazi ya Cheti kwa Elimu ya Awali na Msingi ili kuboresha Sekta hiyo

> Imesema, hakuna Mwalimu atakayefukuzwa kazi kutokana na hilo

Soma - https://jamii.app/MtaalaUalimuCheti
LADY JAYDEE ADAIWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA BANGI KWENYE WIMBO WAKE

> Msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura anadaiwa kufanya hivyo kwenye wimbo wake mpya wa β€˜One Time’

> BASATA wanaendelea kufanya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na Wimbo huo

Soma https://jamii.app/JayDeeBangi
SIKU YA MAKAZI DUNIANI: WENYE KIPATO CHA CHINI KUWEZESHWA KUPATA NYUMBA BORA

> Ktk kuadhimisha siku hii, Waziri wa Nyumba na Makazi amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa Sera ambayo itawezesha upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu

Soma https://jamii.app/SeraMakazi
CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI CHAMTAKA MBOWE AOMBE RADHI KWA KAULI ALIYOITOA

> Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha Uchaguzi huu washindani ni CHADEMA na CCM, vyama vingine vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"

Soma https://jamii.app/UpinzaniKutumika
#TZ2020
RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI 3

> Amepokea Hati za utambulisho wa Balozi wa Uingereza nchini, David William Concar, Balozi wa Pakistan nchini, Muhammad Saleem na Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot

Soma - https://jamii.app/HatiMabalozi3
RAIS MAGUFULI ATENGUA KUFUTWA KWA MAFUNZO YA UALIMU KWA NGAZI YA CHETI

> Amewataka Walimu kupuuza taarifa inayoeleza kuwa Serikali imefuta mafunzo ya Ualimu wa Shule za Msingi na Awali kwa ngazi ya cheti na kuwa mafunzo yataanzia diploma

Soma - https://jamii.app/TenguziUalimuCheti
LIBERIA: RAIS WEAH AWASHUKIA WANAOMTUKANA WAKATI WAKIOMBA MSAADA

> Rais George Weah amesema hatatoa msaada wowote kwa watu ambao wameonesha kumvunjia heshima

> Pia, amekemea tabia ya vijana kutaka kujitegemea badala ya kukaa kwa wazazi

Soma - https://jamii.app/RaisMsaadaLBR
DKT. BASHIRU: TUNAZO FEDHA ZA KUENDESHA UCHAGUZI, HATUHITAJI MSAADA

> Katibu Mkuu wa CCM, amesema wamejipanga kwasababu walijua kuna Uchaguzi

> Amesema wanaotembeza mabakuli ya pesa hawajajiandaa kwasababu Uchaguzi ulijulikana tangu 2015

Soma - https://jamii.app/DktBashiruZNZ

#TZ2020
MTAALAM: MATUMIZI YA LIMAO KUSAFISHIA UKE NI HATARI KIAFYA

> Dkt. Fatima Abdulahi ktk hospitali ya Marie Stopes, Abuja amesema Limao inasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha Tindikali cha 14/1/14 wakati uke una kiwango cha 3.8/14 na 4.5/14

Soma - https://jamii.app/LemonVagina
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: SIFA ZA MTU ANAYESTAHILI KUPIGA KURA

- (i) Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura:

- (ii) Awe ana Kadi ya Mpiga Kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi

- (iii) Awe katika kituo alichojiandikisha kupiga kura

Zaidi, soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums
NEC: SHERIA ZA NCHI ZISIVUNJWE KWA KIGEZO CHA UCHAGUZI

> Tume imesema wakati huu nchi inapoelekea katika Uchaguzi, Sheria nyingine hazijasimama

> Wagombea wametakiwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi na kuepuka lugha za kashfa na uchochezi

Soma https://jamii.app/NECVyamaSheria
#TZ2020
JE, UTARATIBU GANI UTATUMIKA SIKU YA KUPIGA KURA? (28.10.2020)

> Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake

> Anatakiwa kupanga mstari na kusubiri hadi zamu yake

Soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #Siasa
JE, UTARATIBU GANI UTATUMIKA SIKU YA KUPIGA KURA? (28.10.2020)

> Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni

> Baada ya kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani

Soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: NITAKUWA RAIS WA WANYONGE, WAVUVI WATAPATA STAHIKI ZAO

> Akiwa Mkoani Mwanza, Mgombea huyo amesema atawasimamia wavuvi ili wapate stahiki zao

> Pia, atahakikisha kila mvuvi aliyenyang'anywa na kuchomewa nyavu analipwa fidia

Soma https://jamii.app/ProfLipumbaMWZ
#TZ2020
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA DKT. SEMAKAFU

> Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

> Nafasi yake itajazwa baadaye

Soma > http://jamii.app/AvemariaOut
DKT. MWINYI: KILA NITAKAYEMTEUA ATAWAJIBIKA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE

> Mgombea Urais Zanzibar (CCM) amesema atajenga mawasiliano na wafanyakazi ili kusikiliza changamoto zao na kuzitatua

> Hatakuwa na huruma kwa wabadhirifu na wala rushwa

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiMwinyi
#TZ2020
ZEC: KURA YA MAPEMA HAITAHUSISHA ASKARI WOTE

> Tume ya Uchaguzi imesema watakaopiga kura Oktoba 27 ni watu maalum ikiwemo Watumishi wa Tume, Wasimamizi wa Uchaguzi na Askari ambao watahusika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28

Soma https://jamii.app/KuraMapemaZNZ

#Uchaguzi2020