JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CHADEMA: LISSU HATOENDELEA NA MIKUTANO YA KAMPENI

> Mbowe amesema Lissu hatokosa cha kufanya ktk siku 7 kwasababu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho

> CHADEMA itampangia programu mahususi na atafanya majukumu ya kijamii na kisiasa

Soma - https://jamii.app/TamkoCHADEMA
#Uchaguzi2020
MUOSHA HUOSHWA: BAADA YA KUIPIGA MAN. CITY 5-2, LEICESTER YAPIGWA 3-0 NA WEST HAM

- Leicester City ikiwa nyumbani (King Power Stadium) imekutana na kipigo cha 3-0 kutoka kwa West Ham katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Soka England

- Katika mchezo mwingine, klabu ya Southampton imepata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya West Brom

#Michezo #JFSports
MBOWE: CHADEMA INAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

> Mwenyekiti wa Chama hicho amesema Mgombea wao, Said Issa Mohamed ameridhia kumuachia Maalim Seif awe Mgombea ambaye CHADEMA watamuunga mkono ktk Uchaguzi Mkuu wa Okt. 28

Soma - https://jamii.app/TamkoCHADEMA
#TZ2020
FAHAMU MAWAKALA WA UCHAGUZI KWA MUJIBU WA SHERIA

> Wakala wa Chama cha Siasa ktk Uchaguzi huteuliwa na Chama baada ya kupata ridhaa ya Mgombea

> Ili kuwa Wakala wa Uchaguzi, mtu anatakiwa awe na akili timamu, na umri wa miaka 18 na kuendelea

Soma https://jamii.app/MawakalaUchaguzi
#TZ2020
DHAHAMA: MAN. UTD YAKUNG’UTWA GOLI 6-1 OLD TRAFFORD

- Manchester United imejikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa goli 6-1 na Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Ligi Kuu Soka England, mzunguko wa 4

- Man. Utd imefungwa magoli manne katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Premier League kwa mara ya kwanza. Huu ni mchezo wao wa 1,079 katika michuano hii

#JamiiForums #JFSports #JFMichezo #Michezo #Sports
LIVERPOOL YAKUMBANA NA KIPIGO CHA β€˜MBWA KOKO’ KUTOKA KWA ASTON VILLA

- Bingwa Mtetezi wa Ligi Kuu Soka England, Liverpool imekumbana na kipigo kizito cha goli 7-2 kutoka kwa Aston Villa katika mchezo wa Ligi hiyo

- Liverpool ni Bingwa Mtetezi wa kwanza wa Ligi Kuu Soka England kufungwa goli 7 katika mchezo mmoja wa Ligi hiyo tangu Arsenal ifungwe hivyo na Sunderland mnamo Septemba 1953

#JamiiForums #JFSports #JFMichezo #Sports #Michezo
ATHARI ZA #COVID19: BENKI YA DUNIA YAHIMIZA NCHI MASIKINI KUSAMEHEWA MADENI

> Rais wa Benki hiyo amesema #COVID19 inaweza kusababisha changamoto ya kulipa madeni

> Wawekezaji watakiwa kuwa tayari kutoa misaada inayoweza kujumuisha madeni kufutwa

Soma https://jamii.app/CoronaDebtsWB
INDIA: MAOFISA 5 WA POLISI WAFUKUZWA KWA KUHARIBU USHAHIDI

> Wanatuhumiwa kuharibu ushahidi wa tukio la binti (19) kubakwa na kuuliwa na wanaume 4

> Waliuchoma mwili wa marehemu bila ridhaa ya familia na kuzuia Wanahabari kuongea na familia

Soma https://jamii.app/GangRapeIndia
MALEZI YA WATOTO NJITI: UTUNZAJI WA KANGARUU

> Utunzaji huu ulipewa jina la Kangaruu kwa kurejelea jinsi Mnyama Kangaruu wanavyowatunza ndama wake

> Njia hii ni bora ktk kuwatunza Watoto waliozaliwa chini ya wiki 37 za ujauzito na uzani wa chini

Soma > https://jamii.app/MaleziKangaruu

#WatotoNjiti
SIKU YA MWALIMU: #COVID19 YATAJWA KUWAATHIRI WALIMU KISAIKOLOJIA

> Leo ni maadhimisho ya #WorldTeachersDay. Iliasisiwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF na ILO

> Changamoto kubwa bado ni idadi kubwa ya wanafunzi kuliko Walimu

Soma https://jamii.app/TeachersDay
KENYA: VURUGU KATI YA WAFUASI WA KENYATTA NA RUTO ZAPELEKEA VIFO 2

> Polisi wametumia mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwa wakishambuliana

> Wafuasi wa Rais Kenyatta wamekuwa wakidai Ruto ameanza kampeni miaka 2 kabla ya Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/VuruguVifoKE
MAALIM SEIF: TUTAONGEZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo amesema watapandisha mshahara kutoka Tsh. 300,000 hadi Tsh. 500,000

> Atawafutia Wazanzibar deni wanalodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu

Soma https://jamii.app/KimaMshahara
#Uchaguzi2020
UCHAGUZI 2020: JE, UNAFAHAMU MAJUKUMU YA TUME YA UCHAGUZI?

> Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura ktk Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa JMT

> Kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia wanaotoa elimu hiyo

Soma - https://jamii.app/MajukumuNEC
#Uchaguzi2020
QUEEN SENDIGA: UZURI WA VIPAUMBELE VYA ADC UTANIPA USHINDI

> Amesema, Ilani ya Chama imetoa kipaumbele kwa Elimu, Afya na Kilimo kutokana na umuhimu wake kwa kila mtu

> Mgombea huyo wa Urais anaamini Uchaguzi Mkuu utakuwa Huru na wa Haki

Soma - https://jamii.app/QueenUshindiADC

#TZ2020
SERIKALI YAFUTA MTAALA WA UALIMU WA NGAZI YA CHETI

> Wizara ya Elimu imetangaza kufuta Mtaala wa Ualimu wa ngazi ya Cheti kwa Elimu ya Awali na Msingi ili kuboresha Sekta hiyo

> Imesema, hakuna Mwalimu atakayefukuzwa kazi kutokana na hilo

Soma - https://jamii.app/MtaalaUalimuCheti
LADY JAYDEE ADAIWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA BANGI KWENYE WIMBO WAKE

> Msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura anadaiwa kufanya hivyo kwenye wimbo wake mpya wa β€˜One Time’

> BASATA wanaendelea kufanya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na Wimbo huo

Soma https://jamii.app/JayDeeBangi
SIKU YA MAKAZI DUNIANI: WENYE KIPATO CHA CHINI KUWEZESHWA KUPATA NYUMBA BORA

> Ktk kuadhimisha siku hii, Waziri wa Nyumba na Makazi amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa Sera ambayo itawezesha upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu

Soma https://jamii.app/SeraMakazi
CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI CHAMTAKA MBOWE AOMBE RADHI KWA KAULI ALIYOITOA

> Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha Uchaguzi huu washindani ni CHADEMA na CCM, vyama vingine vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"

Soma https://jamii.app/UpinzaniKutumika
#TZ2020
RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI 3

> Amepokea Hati za utambulisho wa Balozi wa Uingereza nchini, David William Concar, Balozi wa Pakistan nchini, Muhammad Saleem na Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot

Soma - https://jamii.app/HatiMabalozi3