JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS TRUMP AFIKISHWA HOSPITALI KWA HELIKOPTA

> Ni baada ya kupata #COVID19. Rais huyo amepewa kingamwili ya majaribio na alikuwa na uchovu

> Imesisitizwa kuwa, amefikishwa Hospitali kama tahadhari na ataendelea kufanya kazi kutoka hapo

Soma - https://jamii.app/TrumpHospCorona
KENYA: CHAMA TAWALA CHAPENDEKEZA NAIBU RAIS KUFUTWA UONGOZI

> Jubilee kimependekeza William Ruto kuondolewa ktk nafasi yake kama Naibu Kiongozi wa Chama

> Katibu Mkuu wa Jubilee, amedai Ruto ni mjeuri, ana dharau na hamuheshimu Rais Kenyatta

Soma https://jamii.app/JubileeRutoKE
KAMATI YA MAADILI: TAFSIRI YA KWAMBA LISSU AMEADHIBIWA NA NEC SIO SAHIHI

> Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa amesema Lissu ameadhibiwa na Kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Rais

Soma - https://jamii.app/KamatiMaadiliLissu
#Uchaguzi2020
POLEPOLE: WAPINZANI HAWAONGEZEKI HADI CCM WAWE NA MGOGORO NDANI YA CHAMA

> Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema awamu hii CCM haikuwa na migogoro ya ndani hivyo imekuwa ngumu kwa Upinzani kuongezeka

Soma https://jamii.app/UpinzaniCCM
#Uchaguzi2020
DKT. MWINYI: MUUNGANO UNALETA UMOJA WA KITAIFA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Mwinyi amesema, Muungano unaleta amani, utulivu na unatoa fursa kwa Wazanzibari kufanya biashara na kumiliki ardhi Tanzania Bara

Soma https://jamii.app/DktMwinyiMuungano
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: MIPAKA YA TANZANIA SIO YA KURITHI KWA WAKOLONI

> Amesema nchi nyingi za Afrika zina mipaka iliyowekwa na kipindi cha Ukoloni lakini Muungano wa #Tanganyika na #Zanzibar unaifanya #Tanzania kuwa nchi isiyo na mipaka ya kurithi

Soma https://jamii.app/TzMipakaUkoloni
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: NIKICHAGULIWA, NITAPATA SHIDA KUMPATA WAZIRI WA ULINZI

> Amesema Waziri wa Ulinzi ana uwezo hata wa kupindua nchi kutokana na vifaa vyote kuwa chini yake

> Amesema ni vigumu kumpata mtu mwadilifu kama alivyokuwa Dkt. Mwinyi

Soma https://jamii.app/WaziriUlinziRais
#TZ2020
ZITTO KABWE: LENGO LETU NI KUMSHINDA MAGUFULI

> Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo akiwa kwenye Kampeni Tandahimba amewaambia wananchi wamchague Mgombea wanayeona ana Nguvu za Kumshinda Dkt. Magufuli (CCM) na wala wasizigawe kura zao

Angalia https://youtu.be/nJYE7F1RC_8
#Uchaguzi2020
QUEEN SENDIGA: TUTAHAKIKISHA KILA MVUVI ANAKUWA MVUVI BORA

> Mgombea Urais kupitia ADC amesema watahakikisha Mvuvi wa Kitanzania anakuwa Mvuvi bora kwa kupatiwa elimu ya Uvuvi, vitendea kazi bora na kuondolewa tozo zisizoendana na uwezo wake

Soma https://jamii.app/SendigaBagamoyo
#TZ2020
CHINA YATOA CHANJO YA MAJARIBIO YA #COVID19

> Maelfu wametumia chanjo licha ya kwamba hatua ya 3 ya majaribio kuthibitisha ubora wake ilikuwa haijakamilika

> Maafisa wa Afya wanasema hatua hiyo imeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)

Soma https://jamii.app/CoronaVaccineCH
MICHEZO: YANGA SC YASITISHA MKATABA WAKE NA KOCHA ZLATKO KRMPOTIC

> Hatua hii imefikiwa kwa maafikiano baina ya pande zote mbili

> Mwalimu Zlatko Krmpotic alitangazwa rasmi kujiunga na Yanga SC mnamo 28 Agosti 2020

Soma > https://jamii.app/YangaVsZlatko
PROF. LIPUMBA: SERIKALI YA CUF ITAHAKIKISHA 50% YA SHULE ZA UMMA ZINATUMIA TEHAMA IFIKAPO 2025

> Akiwa Shinyanga, Mgombea huyo amesema hatua hiyo itawezesha wanafunzi kusoma Shule zitakapofungwa kwa dharura kama ilivyokuwa wakati wa #COVID19

Soma https://jamii.app/CUF-Elimu
#TZ2020
DC ARUSHA: SITARAJII WANANCHI KUINGIA KATIKA MAANDAMANO YA UVUNJIFU WA AMANI

> Kenani Kihongosi ameonya wanaopanga kufanya maandamano kuacha mara moja ili kuepuka kupata matatizo

> Pia amesema, Serikali haitavumilia wenye mipango ovu

Soma https://jamii.app/AmaniArushaDC
#Uchaguzi2020
JAJI MUTUNGI: TUSIMAMIE HAKI ILI KUSIWE NA TAFRANI

> Msajili wa Vyama vya Siasa amevitaka Vyama vya Siasa na Wadau kuheshimu Sheria za Uchaguzi ili kuepuka migogoro

> Amewaomba kuimarisha Demokrasia kwa kufanya siasa kistaarabu

Soma https://jamii.app/JajiMutungi
#Uchaguzi2020
ACT-WAZALENDO YAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

> Katiba ya Zanzibar imesaidia kutoa mwongozo wa Ilani hiyo yenye Sura 19

> Baadhi ya masuala yaliyomo katika Ilani ni Mamlaka ya Zanzibar, Muungano, Uongozi, Ulinzi na Usalama

Soma - https://jamii.app/IlaniACT-ZNZ
#Uchaguzi2020
SIMANJIRO, MANYARA: BWENI LA SHULE YA SEKONDARI OLJORO LATEKETEA KWA MOTO

> Chanzo cha moto huo ulioteketeza bweni la wasichana na kusababisha uharibifu wa miundombinu pamoja na vifaa vya wanafunzi bado hakijafahamika

Soma - https://jamii.app/MotoShuleOljoro
CHADEMA: LISSU HATOENDELEA NA MIKUTANO YA KAMPENI

> Mbowe amesema Lissu hatokosa cha kufanya ktk siku 7 kwasababu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho

> CHADEMA itampangia programu mahususi na atafanya majukumu ya kijamii na kisiasa

Soma - https://jamii.app/TamkoCHADEMA
#Uchaguzi2020
MUOSHA HUOSHWA: BAADA YA KUIPIGA MAN. CITY 5-2, LEICESTER YAPIGWA 3-0 NA WEST HAM

- Leicester City ikiwa nyumbani (King Power Stadium) imekutana na kipigo cha 3-0 kutoka kwa West Ham katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Soka England

- Katika mchezo mwingine, klabu ya Southampton imepata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya West Brom

#Michezo #JFSports
MBOWE: CHADEMA INAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

> Mwenyekiti wa Chama hicho amesema Mgombea wao, Said Issa Mohamed ameridhia kumuachia Maalim Seif awe Mgombea ambaye CHADEMA watamuunga mkono ktk Uchaguzi Mkuu wa Okt. 28

Soma - https://jamii.app/TamkoCHADEMA
#TZ2020
FAHAMU MAWAKALA WA UCHAGUZI KWA MUJIBU WA SHERIA

> Wakala wa Chama cha Siasa ktk Uchaguzi huteuliwa na Chama baada ya kupata ridhaa ya Mgombea

> Ili kuwa Wakala wa Uchaguzi, mtu anatakiwa awe na akili timamu, na umri wa miaka 18 na kuendelea

Soma https://jamii.app/MawakalaUchaguzi
#TZ2020