JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LOWASSA: SINA SHAKA NA MAGUFULI KUSHINDA

> Amesema, β€œSina mashaka juu ya Rais Magufuli kushinda, mashaka yangu ni atashinda kwa kura ngapi? Huko wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo kwenye TV, tumemwambia usitishike hata kidogo"

Soma - https://jamii.app/LowassaUshindiCCM
#TZ2020
UMOJA WA ULAYA WASEMA LUKASHENKO SIO RAIS HALALI WA BELARUS

> Umoja huo umesema, uapisho wake umekosa uhalali wa kidemokrasia na unapingana na idadi kubwa ya wananchi ambao wamekuwa wakiandamana tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti

Soma - https://jamii.app/EUBelarus
FAHAMU KUHUSU WATOTO NJITI (PREMATURE BABIES) - 1

> Watoto njiti ni wale ambao huzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito

> Inakadiriwa watoto Milioni 15 huzaliwa kabla ya muda kila mwaka duniani, ikimaanisha kati ya watoto 10 mtoto 1 ni njiti

> Mtoto anapozaliwa kabla ya muda, baadhi ya viungo vyake vinakuwa havijakomaa ipasavyo

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti
SERIKALI YA TANZANIA IMEKANUSHA TUHUMA ZA KUWALAZIMISHA WAKIMBIZI KUONDOKA

> Serikali imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri wa Masuala ya Wakimbizi Nchini #Uganda kuhusu kuwalazimisha Wakimbizi waliopo Nchini kurejea #Burundi bila ridhaa yao

Soma - https://jamii.app/WakimbiziTZ
MGOMBEA AFUKUZWA NA WANANCHI WAKATI AKIOMBA KURA

> Jasson Rweikiza ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Bukoba Vijiji (CCM), amefukuzwa na Wanachi wakati akiomba Kura

> Rweikiza alikuwa Mbunge (2015-2020) na sasa anatetea nafasi hiyo

Angalia - https://www.youtube.com/watch?v=zpw4HpT1Y_M
#Uchaguzi2020
ACT-WAZALENDO YAMJIBU MSAJILI: HATUJAUNGANA NA CHADEMA

> Kimesema kauli na imani ya Maalim Seif kuwa Lissu atakuwa Rais wa JMT haimaanishi wameungana bali wana imani ya pamoja kuwa Mgombea wa CCM hatokuwa Rais baada ya Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MsajiliMaelezoACT

#Uchaguzi2020
BoT YAWAFIKISHA 10 MAHAKAMANI KWA KUTENGENEZA NA KUSAMBAZA NOTI BANDIA

> Imeeleza wasiwasi wake kuhusu wahalifu kulenga minada ya mifugo na mazao

> Hii ni mara ya pili kwa BoT kuonya kuhusu mzunguko wa noti bandia katika kipindi cha mwaka 1

Soma https://jamii.app/FakeNotesBoT
MABAHARIA WANAWAKE WAHIMIZA WASICHANA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

> Ni siku ya leo katika kusherekea Siku ya Mabaharia Duniani

> Kampeni ya kuhamasisha itafanyika katika Kanda za Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa

Soma - https://jamii.app/MabahariaKike
MICHEZO: SAMATTA AWASILI UTURUKI, MAZUNGUMZO NA FENERBAHCE YANAENDELEA

> Mbwana Samatta amesema mazungumzo na Klabu hiyo yanaendelea na hawajasaini hadi sasa

> Januari mwaka huu, Mtanzania huyo alijiunga na Aston Villa akitokea Genk

Soma - https://jamii.app/SamattaUsajiliUturuki

#JFMichezo
#COVID19 KENYA: MAAFISA WA SERIKALI WAHUSISHWA KWENYE KASHFA YA UFISADI

> Serikali ilipokea msaada wa takriban Dola Bil. 2 ili kupambana na mlipuko huo

> Wachunguzi wanatarajia kupendekeza Maafisa na Wafanyabiashara takriban 15 kushtakiwa

Soma https://jamii.app/CovidCorruptionKE
AIDAN EYAKUZE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MWENZA WA ASASI ZA KIRAIA KATIKA OGP

> Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mweza wa Asasi za Kiraia katika Open Government Partnership (OGP)

> Muhula wake kwa kushirikiana na Serikali ya Italia utaanza mwaka 2021. Hii ni mara ya pili kwa Tanzania na Twaweza kutoa Mwenyekiti Mwenza

Soma - https://jamii.app/AidanCo-ChairOGP
#CORONAVIRUS-UK: VISA ZAIDI YA 6,600 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

> Visa vipya 6,634 vimerekodiwa, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa tangu kuanza kwa mlipuko

> Mapema wiki hii Waziri Mkuu alitangaza masharti mapya ili kudhibiti maambukizi

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
KISUTU, DAR: KESI ZA TUNDU LISSU KUSIKILIZWA BAADA YA UCHAGUZI

> Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Augustina Mmbando amekubali ombi lililowasilishwa na Wakili wa utetezi na kuahirisha kesi hizo hadi Novemba 6 ambapo zitasikilizwa mfululizo

Soma https://jamii.app/LissuKesiNov6
MALI: RAIS WA MPITO KUAPISHWA LEO

> Bah Ndaw (70) ataongoza Serikali ya Mpito kwa miezi 18. Kanali Assimi Goita atakuwa Makamu wa Rais

> Ndaw alikuwa Waziri wa Ulinzi katika utawala wa Rais aliyepinduliwa na Jeshi, Ibrahim Boubacar Keita

Soma - https://jamii.app/RaisMaliKiapo
PROF. LIPUMBA: UCHAGUZI USIWE CHANZO CHA UVUNJIFU WA AMANI

> Mgombea Urais kupitia CUF amesema, Tanzania imekuwa Kisiwa cha Amani kwa kipindi kirefu hivyo watanzania wanao wajibu wa kuhakikisha amani hiyo inadumu hasa kipindi hiki

Soma - https://jamii.app/LipumbaAmaniTZ
#Uchaguzi2020
MUHAS YATAJWA KAMA CHUO NO.1 TANZANIA

> Ni kwa mujibu wa University Ranking by Academic Performance (URAP)

> Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kinashika nafasi ya 1,551 duniani, huku UDSM ikiwa ya 2,047 na SUA 2,206

Soma https://jamii.app/URAPRankings
MAJALIWA: KITI CHA URAIS SIO MCHEZO, KINAHITAJI MTU MAKINI

> Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, β€œUongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, linataka kiongozi makini, anayetetea rasilimali na anayetetea wanyonge dhidi ya rushwa na ufisadi"

Soma https://jamii.app/KitiUraisMajaliwa
#Uchaguzi2020
RASMI: SAMATTA AJIUNGA NA FENERBAHCE YA UTURUKI

> Mbwana Samatta amejiunga na Fenerbahce kwa mkopo wa mwaka mmoja huku Fenerbahce wakieleza kuwa baada ya muda huo wamekubaliana kumpatia Samatta mkataba wa miaka minne

Soma - https://jamii.app/SamattaUsajili
#JFMichezo
POLEPOLE: TUME YA UCHAGUZI IMEWAPENDELEA UPINZANI

> Msemaji wa CCM, Humphrey Polepole amesema, Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ingefuata Sheria bila kutumia Hekima wagombea wasingerudishwa kwenye Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/PolepoleNEC
#Uchaguzi2020
MANYARA: TAKUKURU YAAGIZA KUONDOLEWA KWA MILANGO 83 YA KITUO CHA AFYA KWA KUKOSA UBORA

> Milango hiyo inayodaiwa kuwa ni mipya ktk kituo cha Hirbada imeonekana kupasuka huku mingine ikiwa imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika

Soma - https://jamii.app/MilangoUbora