JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ILANI YA CHADEMA ISEMAVYO KUHUSU SERIKALI YA MUUNGANO

> Itabadili Muundo wa Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3; kutakuwa na Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali kamili ya Zanzibar

Soma https://jamii.app/IlaniCDM
#Uchaguzi2020
BELARUS: RAIS LUKASHENKO AAPISHWA BILA HAFLA KUTANGAZWA

> Uchaguzi Mkuu ulifanyika Agosti na Kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 26 amedai ameshinda kwa kishindo

> Upinzani unamshutumu kuiba kura, umeandaa maandamano kushinikiza ajiuzulu

Soma - https://jamii.app/RaisKiapoBelarus
HOJA/MALEZI: NI KWELI MZAZI HUMPENDA MTOTO MMOJA ZAIDI KULIKO MWINGINE?

> Mdau wa JamiiForums.com anasema mara nyingi inatokea kwenye familia Mzazi/Mlezi anaonekana akizidisha upendo kwa maneno ama kwa vitendo kwa Mtoto mmoja au baadhi

> Baadhi ya wadau wanasema hakuna Mzazi anayempenda Mtoto 1 kuliko mwingine ila Mzazi humpenda kila Mtoto kutokana na tabia zake

Je, una mtazamo gani kuhusu hili?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/FavouriteChild
#JamiiForums #Malezi #Familia
TLS: KAMATI YA MAADILI HAIJAHUSIKA KUMUONDOA FATMA KARUME KWENYE ORODHA YA MAWAKILI

> Baraza la Uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Tanzania Bara limesema uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Mawakili kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili

Soma https://jamii.app/TLSFatmaKarume
SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI NAMBA 6 (2010)

> Mgombea hatokuwa na hatia na vitendo vilivyokatazwa kwenye Sheria hii viliyofanywa na chama chake cha siasa bila matakwa yake au kuridhia kwake yeye mgombea iwe moja kwa moja au la

Zaidi, soma > https://jamii.app/UchaguziGharama

#KemeaRushwa #Uchaguzi2020
PROF. JANABI: UKUAJI UCHUMI UTAONGEZA MAGONJWA YA MOYO

> Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema watu wanakuwa hatarini kupata magonjwa hayo kwasababu wanakuwa na fedha za kununua vyakula vingi, na wanatumia usafiri binafsi

Soma - https://jamii.app/UchumiMagonjwaMoyo
PROF. KABUDI: SERIKALI HAIKUWA NA LENGO LA KUVIZUIA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA

> Amesema, lengo ni kutambua vyombo hivyo vinashirikiana na vyombo gani nchini

> Amesema, vyombo vyote vya kimataifa vimetekeleza agizo hilo na kupata leseni

Soma - https://jamii.app/SerikaliLeseni
TMA YATOA TAHADHARI YA UPEPO MKALI LINDI NA MTWARA

> Inatarajiwa leo kutakuwa na upepo unaofikia Kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika Mita 2

> TMA imesema vipindi vya hali mbaya ya hewa sio vya muda mrefu, vinaweza kukoma kesho

Soma https://jamii.app/TMAUpepoUtabiri
IGP SIRRO: VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA BILA SABABU

> Amesema, zaidi ya watu 40 wanashikiliwa na Polisi Pemba kwa tuhuma za kuwashambulia wafuasi wa CCM kwa mapanga

> Amewataka vijana wasikubali watu wachache kuwaingiza kwenye fujo

Angalia - https://youtu.be/tomQpgGIIt0
#Uchaguzi2020
WANAOWATOZA FEDHA WAJAWAZITO NA WAZEE KWENYE VITUO VYA AFYA KUSHUGHULIKIWA

> Kassim Majaliwa amewataka Watendaji wa Zahanati na Hospitali kuacha kuwatoza fedha wajawazito, watoto chini ya miaka 5 na wazee na wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua

Soma https://jamii.app/HudumaBureAfya
#KENYA KUJA NA KANUNI ZA KUWADHIBITI WANASIASA WANAODAIWA KUFANYA UCHOCHEZI

> Wizara ya Usalama wa Ndani iko mbioni kutengeneza kanuni itakayodhibiti ghasia wakati wa Uchaguzi

> Wanaoeneza chuki wadaiwa kuwa kiini cha migawanyiko ya kisiasa

Soma https://jamii.app/KanuniUchocheziKE
DKT. ABBAS: HAKUNA SIRI KATIKA FEDHA ZA MIRADI, ZINAPITISHWA NA BUNGE

> Ameeleza kuwa, fedha zote za miradi zipo kwenye bajeti na zinapitishwa Bungeni kila mwaka

> Amesema fedha za miradi yote inayotekelezwa zimetengwa kwa mujibu wa Sheria

Soma - https://jamii.app/FedhaMiradiSerikali
BOTSWANA KUANZA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI SHULENI

> Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema Serikali ya #Botswana inakusudia kuanzisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shule za Msingi ndani ya siku zijazo

Soma - https://jamii.app/UseSwahiliBotswn
#JFLeo #Swahili
CUF: ADUI WA CUF NI ADUI WA CHADEMA NA ADUI WA CHADEMA NI ADUI WA CUF

> Meneja Kampeni wa CUF akiwa Kagera amesema, wapinzani wanapaswa kujitafakari kwani yawezekana kuna eneo wanapishana lakini lengo lao ni 1, kuiondoa CCM Madarakani

Soma https://jamii.app/CDMCUFKagera
#Uchaguzi2020
LOWASSA: SINA SHAKA NA MAGUFULI KUSHINDA

> Amesema, β€œSina mashaka juu ya Rais Magufuli kushinda, mashaka yangu ni atashinda kwa kura ngapi? Huko wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo kwenye TV, tumemwambia usitishike hata kidogo"

Soma - https://jamii.app/LowassaUshindiCCM
#TZ2020
UMOJA WA ULAYA WASEMA LUKASHENKO SIO RAIS HALALI WA BELARUS

> Umoja huo umesema, uapisho wake umekosa uhalali wa kidemokrasia na unapingana na idadi kubwa ya wananchi ambao wamekuwa wakiandamana tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti

Soma - https://jamii.app/EUBelarus
FAHAMU KUHUSU WATOTO NJITI (PREMATURE BABIES) - 1

> Watoto njiti ni wale ambao huzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito

> Inakadiriwa watoto Milioni 15 huzaliwa kabla ya muda kila mwaka duniani, ikimaanisha kati ya watoto 10 mtoto 1 ni njiti

> Mtoto anapozaliwa kabla ya muda, baadhi ya viungo vyake vinakuwa havijakomaa ipasavyo

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti
SERIKALI YA TANZANIA IMEKANUSHA TUHUMA ZA KUWALAZIMISHA WAKIMBIZI KUONDOKA

> Serikali imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri wa Masuala ya Wakimbizi Nchini #Uganda kuhusu kuwalazimisha Wakimbizi waliopo Nchini kurejea #Burundi bila ridhaa yao

Soma - https://jamii.app/WakimbiziTZ
MGOMBEA AFUKUZWA NA WANANCHI WAKATI AKIOMBA KURA

> Jasson Rweikiza ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Bukoba Vijiji (CCM), amefukuzwa na Wanachi wakati akiomba Kura

> Rweikiza alikuwa Mbunge (2015-2020) na sasa anatetea nafasi hiyo

Angalia - https://www.youtube.com/watch?v=zpw4HpT1Y_M
#Uchaguzi2020
ACT-WAZALENDO YAMJIBU MSAJILI: HATUJAUNGANA NA CHADEMA

> Kimesema kauli na imani ya Maalim Seif kuwa Lissu atakuwa Rais wa JMT haimaanishi wameungana bali wana imani ya pamoja kuwa Mgombea wa CCM hatokuwa Rais baada ya Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MsajiliMaelezoACT

#Uchaguzi2020