JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: 5 WAHUKUMIWA KUNYONGWA KWA MAUAJI YA DKT. SENGONDO MVUNGI, 1 AACHIWA HURU

> Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Novemba 3, 2013

> Aliwahi kugombea Urais wa JMT 2005 kupitia NCCR-Mageuzi na alikuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba ya Jaji Warioba

Soma https://jamii.app/HukumuWauajiDrMvungi
SINGIDA: MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MTOTO WAKE

> Hamisi Mtanda (37) amekutwa na hatia ya kumbaka mwanaye wa kike wa kumzaa wa miaka 11

> Katika kujitetea, mshtakiwa alisema mtoto huyo alifanya ngono na mwalimu bila kutaja ni mwalimu yupi

Soma https://jamii.app/BabaAmbakaMwanaye
#JFLeo
DIAMOND PLATNUMZ ASHIRIKISHWA KWENYE ALBUM YA ALICIA KEYS

> Alicia Keys ametoa Album mpya inayoitwa 'Alicia' ambapo Msanii kutoka Tanzania, Naseeb Abdul amepata nafasi ya kushirikishwa kwenye wimbo wenye jina Wasted Energy

Soma https://jamii.app/DiamondAliciaKeys
#JFBurudani #Entertainment
1
DKT. MAGUFULI ATOA WITO KWA WASIOAMINI MUNGU WAJE KUJIONEA TANZANIA

> Dkt. John Magufuli ametoa wito kwa wasioamini Mungu waje wajionee Mungu alivyoifukuza #CoronaVirus Tanzania

> Pia amesema, hata wale waliobeza awali na kusema watu milioni 4 wangekufa kwa #COVID19, hawana la kusema sasa

Soma https://jamii.app/WitoKuaminiMungu
#TZ2020
IGP SIRRO AONGEZEWA MWAKA 1 ZAIDI KUIONGOZA EAPCCO

> Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika wamemtaka IGP Simon Sirro kuendelea kuwa Mwenyekiti wao

> IGP Sirro amesema watahakikisha wanabadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja

Soma https://jamii.app/IGPSirroEAPCCO
#JFLeo
JE, ILANI YA NCCR-MAGEUZI IMEZUNGUMZA NINI KUHUSU AFYA NA USTAWI WA JAMII?

> Itaimarisha afya ya Mama na Mtoto kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na makazi ya watu

- Itaongeza mishahara na marupurupu kwa watumishi wa Sekta ya Afya

Soma https://jamii.app/IlaniNCCR
#Uchaguzi2020
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DKT. MAGUFULI ATAJA MPANGO WA KUPANUA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

> Mgombea Urais (CCM) amesema wanataka Airbus ziwe zinatua ktk Uwanja wa Ndege wa Kigoma ili kukuza utalii

> Asema, Sekta ya Utalii imeajiri watu milioni 4 kwa miaka 5 iliyopita

Soma https://jamii.app/WitoKuaminiMungu
#TZ2020
KAGERA: SERIKALI YATOA 250,000 KWA FAMILIA ZILIZOFIWA KATIKA AJALI YA MOTO

> Ni rambirambi kwa kila familia iliyofiwa na mtoto ktk ajali ya moto, Shule ya Msingi Islamic Byamungu

> Pia, Serikali inawagharamia wanafunzi 6 wanaopatiwa matibabu

Soma https://jamii.app/AjaliKageraSerikali
#JFLeo
JE, WAJUA UMUHIMU WA JESHI LA POLISI TANZANIA?

> Jeshi la Polisi lipo kuhakikisha usalama wa raia na mali zao

> Pia, kubaini na kupambana na uhalifu na kuhakikisha kila mtu anafuata Sheria

Soma https://jamii.app/UmuhimuWaPolisi
#JFMaarifa
MPANDA: JELA MIAKA 60 KWA KUMTOROSHA NA KUMBAKA MWANAFUNZI

> Said Selemani(20), amekutwa na hatia ya kumbaka Mwanafunzi wa Kidato cha Pili

> Katika utetezi mshtakiwa alidai alikuwa naye ili amsaidie kumrejesha kwao kwani alikuwa amefukuzwa

Soma https://jamii.app/Jela60Kubaka
#JFLeo
ZANZIBAR: TAMWA YALAANI WATOTO KUCHOMWA SINDANO BILA SABABU

> Septemba 15, 2020 iliripotiwa tukio la watoto 3 kuchomwa sindano na mtu asiyejulikana

> Tukio kama hilo si la kwanza, TAMWA wanaona huo ni udhalilishaji unaopaswa kukemewa

Soma https://jamii.app/WatotoZnz
#JFLeo
YAJUE MAMLAKA YA POLISI

> Polisi ana mamlaka kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi na kufanya mahojiano na mtuhumiwa

> Kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama katika jamii

Soma https://jamii.app/UmuhimuWaPolisi
#JFMaarifa
ILANI YA UCHAGUZI YA CHADEMA INAAHIDI NINI KUHUSU SEKTA YA AFYA?

> CHADEMA itatoa motisha kwa watendaji wa Sekta ya Afya kulingana na nafasi zao

> Itaboresha mifumo ya huduma za dharura ktk maeneo yote ya utoaji huduma za afya

Soma https://jamii.app/IlaniCDM

#Uchaguzi2020
DAR: AFISA MAUDHUI WA CHADEMA KIZIMBANI

> Dominic Mgaya amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchapisha maudhui bila kuwa na leseni ya TCRA

> Alifanya hivyo kupitia channel ya CHADEMA MEDIA TV kati ya Oktoba 14, 2017 na Septemba 1, 2020

Soma https://jamii.app/MakosaYaMtandaoCHADEMA
#JFLeo
KATIBU MKUU WA CCM AKEMEA VIKALI WANAOJIPANGA KUKISALITI CHAMA

- Dkt. Bashiru ameeleza kuwa kuna WanaCCM wamepanga kukisaliti chama hicho kwa maslahi yao

- Aahidi kuwa watawachukulia hatua kali watakaobainika ikiwemo kuwafukuza Uanachama

Soma > https://jamii.app/WasalitiCCM

#JFLeo
Dkt. Bashiru: Wanaohama kutoka CCM wakidhani wana nguvu, wakitoka wanakuwa kama vichaa!

Hakuna mwana-CCM maarufu kuliko CCM, ukiona wewe maarufu ujue umeazimwa umaarufu na chama chako

Siku chama kikikutupa/ukikitupa na umaarufu unakoma hapohapo

Tazama👇🏾

https://youtu.be/RdpuGk2NSPw
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: JENGO LA UTAWALA LA CHUO KIKUU CHA MAKERERE LATEKETEA KWA MOTO

> Moto huo mkubwa umezuka usiku wa kuamkia leo

> Hadi sasa chanzo na kiwango cha hasara iloyosababishwa na moto huo havijajulikana

Soma > https://jamii.app/MakerereFire

#MakerereFire #Makerere #MakerereUniversity
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UCHAGUZI 2020: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima akiulizwa maswali na mpiga kura wa Jimbo hilo wakati wa kampeni zake

> Je, wananchi wanatambua majukumu na wajibu wa Mbunge wanayemchagua? Je, Wabunge wanatambua wajibu wao kwa wananchi?

#Uchaguzi2020 #TZ2020
LIGI KUU ENGLAND: TOTTENHAM YASHINDA. LIVERPOOL NA CHELSEA KUVAANA BAADAYE

- Tottenham imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Southampton huku Heung-Min Son akiibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga magoli manne

- Mchezo unaoendelea sasa ni kati ya Newcastle na Brighton. Majira ya saa 12:30 jioni (Saa za Afrika Mashariki), Chelsea itakutana na Liverpool

#JFSports #Michezo
CUF YAAHIDI KUWAJALI WALEMAVU

> Mgombea Mwenza (CUF), Hamida Huweishi amesema, CUF ikishinda Uchaguzi nafasi ya Urais, itatenga Fungu Maalum la kuwawezesha watu wenye ulemavu wapate elimu pamoja na kutoa mafunzo stahiki ili waweze kuwaajiri

Soma https://jamii.app/CUFVsWalemavu