JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZANIA YAFUNGUA ANGA KWA NDEGE ZA KENYA KUTUA

> Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeruhusu mashirika ya Ndege kutoka #Kenya kutua nchini baada ya Kenya kuondoa sharti la raia wa #Tanzania kukaa karantini kwa siku 14 wanapoingia nchini humo

Soma https://jamii.app/TCAAVsKE
#JFLeo
ILANI YA UCHAGUZI YA NCCR INASEMA NINI KUHUSU SERA YA ELIMU?

- Kubadili sera ya elimu ya Taifa kwa kuipa maudhui na upeo kulingana na mahitaji ya kimaadili ya maendeleo

- Itaweka 30% kuwa kiwango cha chini cha bajeti ya Taifa ya elimu

Soma https://jamii.app/IlaniNCCR
#Uchaguzi2020
ILANI YA CHADEMA INASEMA NINI KUHUSU MASLAHI YA WALIMU?

- Bila mwalimu mwenye motisha na aliyepewa mafunzo vizuri hakuna chochote tutakachofanikiwa

- Walimu hawathaminiwi; mishahara, marupurupu, maslahi hayalingani na kazi yao ngumu

Soma https://jamii.app/IlaniCDM
#Uchaguzi2020
ZANZIBAR: KESI YA ULAWITI YAFUTWA BAADA YA MASHAHIDI KUTOFIKA MAHAKAMANI

> Mahakama ya Mkoani Wete imeiondoa kesi iliyokuwa inamkabili Khamis Abdalla Khamis(35) aliyetuhumiwa kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wa kiume mwenye miaka 10

Soma https://jamii.app/PembaKesi
#JFLeo
SULTAN WA ZANZIBAR JAMSHID BIN ABDULLAH ARUHUSIWA KUINGIA OMAN

> Sultan wa mwisho wa Zanzibar ameruhusiwa kuingia Oman toka apinduliwe Januari 12, 1964

> Alipewa hifadhi nchini Uingereza ambako ameishi kwa miaka 50 katika mji wa Portsmouth

Soma https://jamii.app/SultanZnzOman
#JFLeo
ILANI YA UCHAGUZI YA SAU INASEMA NINI KUHUSU ELIMU?

> Inasema, itatoa ajira mpya kwa Walimu ili kupata Walimu wa kutosha na kufikia uwiano wa Wanafunzi 20-29 kwa Mwalimu 1

> Watahakikisha Elimu ya Awali (Chekechea) inaboreshwa na kuzingatiwa

Soma https://jamii.app/IlaniSAU
#Uchaguzi2020
NEC YAWEKA WAZI MASHARTI YA KUZINGATIWA SIKU YA KUPIGA KURA (28 OKTOBA 2020)
-
Haitaruhusiwa mtu yeyote kutumia simu ya kiganjani ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura

> Wasimamizi wa Kituo ndio watakao ruhusiwa

Soma > https://jamii.app/NECMashartiUchaguzi

#Uchaguzi2020
JAPAN: YOSHIHIDE SUGA ATHIBITISHWA KUWA WAZIRI MKUU

> Bunge limemthibitisha Yoshihide Suga(71) kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Shinzo Abe ambaye alijiuzulu kutokana na changamoto za kiafya

> Bunge limempitisha kwa theluthi mbili ya kura

Soma https://jamii.app/SugaPMJapan
#JFLeo
GEITA: MBARONI KWA KUWAUNGUZA WATOTO KUTOKANA NA KULA SAMAKI WA WAGENI

> Ester John anatuhumiwa kuwaunguza na majimoto watoto wake 2 wa kambo na kuwafungia ndani bila kuwapatia matibabu yoyote

> Watoto hao ni wa miaka nane na mwingine minne

Soma https://jamii.app/GeitaMajiMoto
#JFLeo
ZANZIBAR: ACT-WAZALENDO YAWATAKA POLISI KUMUACHIA AU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MWENYEKITI WA JIMBO LA OLE

> ACT-Wazalendo wamedai Rashid Ali Hamadi anashikiliwa kwa tuhuma za uchochezi

> Wamedai ana wiki yuko rumande na amenyimwa dhamana

Soma https://jamii.app/PolisiVsACT
#JFSiasa
LISSU: TUME IKITAKA AMANI, IHAKIKISHE UCHAGUZI UNAKUWA WA HAKI
-
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amewataka NEC wawarudishe wagombea wote wa CHADEMA walioenguliwa

> Asema wakikosewa watadai haki kwa namna wanavyojua

Soma https://jamii.app/HakiItaletaAmani
#Uchaguzi2020
MEMBE: ATAKA MSAIDIZI WAKE ARUDI BILA MCHUBUKO

> Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema waliomteka Jerome Luanda wamuachie

> Aidha, amesema sio vyema kutumia Polisi kama kichaka cha kujificha

Soma https://jamii.app/MembeLuanda10
#JFSiasa
ALIYEKUWA KAIMU MKURUGENZI WA BONDE LA RUFIJI AFUNGWA MIAKA 14

> Aloyce Masanja, amesomewa hukumu hiyo kwa hatia ya kosa la wizi wa Shilingi Milioni 86.

> Mahakama yaamuru alipe fidia ya Milioni 86

Soma > https://jamii.app/AloyceMasanjaJela

#JFLeo #JamiiForums #JamiiTalks #KemeaRushwa
KATAVI: MBARONI KWA KUCHOMA NYUMBA 100 ZA WAVUVI

> Wanaoshikiliwa na Polisi kwa mahojiano ni Sungusungu wawili huku wengine wakiendelea kusakwa

> Tukio hilo lilitokea Septemba 16, 2020 saa 8 mchana katika Kata ya Itenka, Wilayani Mpanda

Soma https://jamii.app/KataviSungusungu
#JFLeo
FAHAMU ILANI YA ACT-WAZALENDO INASEMA NINI KUHUSU ELIMU YA JUU

> ACT itarudisha uhuru wa wanataaluma na watafiti ktk kuzalisha na kukuza fikra za kimapinduzi.

> Kutoa ruzuku ya 40% ili Vyuo Vikuu vifanye tafiti

Soma > https://jamii.app/IlaniACT

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DKT. MAGUFULI: WASANII NI WATU MUHIMU KATIKA MAENDELEO

> Mgombea urais kupitia CCM amesema Tasnia ya Sanaa na Michezo imekuwa ya tatu katika kukuza uchumi wa nchi

> Amesema, Wasanii ni watu muhimu katika kuelimisha jamii na kuburudisha

Angalia - https://youtu.be/xEm7tLulNVE
KITAMBI KINAWEZA KUATHIRI MFUMO WA UPUMUAJI NA KUPUNGUZA UWEZO WA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

- Dkt. Makala anasema, Mafuta yana faida mwilini lakini yanapozidi husababisha msuli wa upumuaji (diaphragm) kukosa nafasi nzuri ya kushuka na kupanda

Soma https://jamii.app/AthariKitambi
#JFAfya
DAR: AFIKISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI ZAIDI YA TSH. MILIONI 48

> Geoffrey Kilimba ameshtakiwa kwa uhujumu uchumi na kuisababishia TRA hasara

> Pia, amedaiwa kujihusisha na genge la uhalifu Agosti 29, 2013 hadi Agosti 8, 2020

Soma https://jamii.app/Milioni48Uhujumu
#JFLeo
MAALIM SEIF: MKINICHAGUA WAKULIMA WA KARAFUU NA VIUNGO WATAKUWA HURU KUUZA MAZAO YAO POPOTE DUNIANI

> Kazi ya Serikali yake itakuwa ni kukusanya kodi ndogo ili kuwafanya wakulima wapate faida kubwa ili waweze kuendeleza kazi yao

Soma > https://jamii.app/SeifWakulimaZNZ

#Uchaguzi2020
MAMBOSASA: WANAODAI MSAIDIZI WA MEMBE AMETEKWA NI WAONGO

> Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa, amesema Jerome Luanda ambaye ni Msaidizi wa Mgombea Urais wa JMT, Bernard Membe yuko mikononi mwa Polisi na ni mzima wa afya

Soma https://jamii.app/JeromeHakutekwa
#JFLeo