JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZANZIBAR: WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Mohammed Aboud Mohammed amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Amekuwa mwanachama wa 20 wa chama hicho kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho

Soma https://jamii.app/MohammedUraisZNZ
#JFSiasa
RAIS MAGUFULI ATAJA SABABU YA KUTENGUA UONGOZI WA ARUSHA

> Rais Magufuli amesema ametengua uteuzi wa RC Mrisho Gambo, DC Gabriel Daqarro na Mkurugenzi wa Arusha, Dkt. Maulid Madeni kwa kuwa zaidi ya miaka miwili viongozi hao wamekuwa wakigombana huku kila mmoja akitaka kuwa bosi wa mwingine

Angalia; https://youtu.be/-7XtOPFg25c
#JFLeo
ASKARI POLISI AFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA BANGI

> Koplo Anthony Francis wa Kituo cha Polisi Kisarawe amekamatwa akiwa na Kg 76 za Bangi kwenye gari yake, Mkoani Morogoro

> Pia, Polisi inawashikilia watu 22 kwa kuhusika na biashara hiyo

Soma https://jamii.app/BangiPolisi
ZIMBABWE: MATAJIRI WATAKAOSHINDWA KUELEZEA UTAJIRI WAO, MALI ZAO KUTAIFISHWA

> Mwenyekiti wa Tume ya kupambana na Ufisadi, Jaji Loyce Matanda-Moyo ndiye ameanzisha operasheni hiyo

> Zimbabwe sio nchi ya kwanza kuchukua hatua hiyo duniani

Soma https://jamii.app/ZimbabweUtajiri
#JFLeo
ZANZIBAR: BAKARI RASHID BAKARI ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Kada wa CCM, Bakari Rashid Bakari amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Anakuwa Mgombea wa 21 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/BakariRashidZNZ
#JFSiasa
ZANZIBAR: HUSSEIN IBRAHIM MAKUNGU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Kada wa CCM, Hussein Ibrahim Makungu amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Anakuwa Mgombea wa 22 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/HusseinIbrahimZNZ
#JFSiasa
ZANZIBAR: MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Ayoub Mohamed Mahmud amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Amekuwa mgombea wa 23 kujitokeza kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/AyoubMahmudZNZ
#JFSiasa
MATAIFA 188 YATHIBITISHA KUWA NA #COVID19

> Hadi sasa mlipuko wa #COVID19 ulioanza Desemba, 2019, umesababisha Vifo 474,823, maambukizi 9,772,296 na waliopona 4,605,114 wameripotiwa

> Marekani inaongoza kwa maambukizi ikifuatiwa na Brazil

Soma https://jamii.app/Corona188Nchi
#JFCOVID19_Updates
DR CONGO: WATU 19 WAUAWA. 9 KATI YAO WALITEKWA IJUMAA

> Watu tisa kati ya hao walitekwa Ijumaa na wapiganaji wa ADF na miili yao ikakutwa Kaskazini mwa Kivu wakiwa wamefariki

> ADF pia waliwaua kwa mapanga na risasi raia 10 wa kijiji cha Bukaka

Soma https://jamii.app/19CongoADF
#JFLeo
MANYARA: MBARONI KWA KUWEKA MADIRISHA YALIYO CHINI YA KIWANGO KATIKA IKULU NDOGO

> Mzabuni Patrick J. Kauky aliweka madirisha tofauti na yaliyotakiwa kuwekwa

> Pia, TAKUKURU imebaini Kauky alipata Kandarasi hiyo kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma

Soma https://jamii.app/MzabuniTAKUKURU
#JFLeo
KENYA: MAAMBUKIZI YA #COVID19 YAFIKIA 4,797, VIFO VYAFIKA 125

> Watu 59 zaidi wamethibitika kuwa na #CoronaVirus, huku watu 2 wakiripotiwa kufariki na kufanya vifo kufikia 125

> Watu 73 wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 1,682

Soma https://jamii.app/59CoronaKE
#JFCOVID19_Updates
MALAWI KUFANYA UCHAGUZI JUNI 23, BAADA YA MAHAKAMA KUBATILISHA MATOKEO YALIYOPITA

> Rais Peter Mutharika alitangazwa kuwa mshindi Mei 2019 lakini upinzani walipinga matokeo

> Lazarus Chakwera atakabiliana na Mutharika katika Uchaguzi huo

Soma https://jamii.app/MalawiUchaguzi
#JFSiasa
WAZIRI JAFO AWATAKA VIONGOZI KUTOFANYA MAMBO YATAKAYOMTWEZA RAIS MAGUFULI

- Amewasihi Viongozi wanaopewa dhamana katika maeneo mbalimbali kumsaidia Rais

- Ameongeza kuwa Rais ni Mtu na Urais ni Taasisi na kuwa Rais ana mambo mengi ya kufanya

Angalia Video; https://youtu.be/9QnWDxhL3-I
TATIZO LA HARUFU MBAYA KINYWANI NA NAMNA YA KULIEPUKA

> β€˜Halitosis’ inaweza kusababishwa na magonjwa ya meno, magonjwa ya fizi au maambukizi kwenye koo la hewa au kwenye mapafu

> Kutotumia Sigara na kupiga mswaki vizuri kunaweza kusaidia kupunguza tatizo hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/KunukaKinywa
#JFAfya
CHADEMA: TUTAISHINDA CCM JINSI ILIVYO. NG'OMBE HUYU MARA HII HAGEUZIWI KIBLA, ANACHINJWA ALIVYO

- Wamesema Serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura na katika Uchaguzi huu hawajitoi

- Wamesema wanajua hakuna Tume Huru ila wanaenda kushinda Kituoni

Angalia Video; https://youtu.be/Npxg1I3z2Vk
#Siasa #JFSiasa
UNAIDS: #COVID19 YAATHIRI UPATIKANAJI NA GHARAMA ZA ARVs

> Utafiti umebaini kubaki ndani na ufungwaji wa mipaka kuepuka #COVID19 kumeleta changamoto katika uzalishaji na usambazaji wa ARVs

> Huenda ikasababisha vifo 500,000 Kusini mwa Jangwa la Sahara

Soma https://jamii.app/ARVsCOVID19
#JFLeo
VANESSA MDEE: WASANII WENZANGU WAMENISHUKURU KWA KUFUNGUKA KUHUSU TASNIA YA MUZIKI

- Vanessa alitangaza kujitoa katika tasnia ya muziki wiki iliyopita kupitia β€˜podcast’ yake akidai ilimpelekea kupata msongo wa mawazo

- Ameeleza kuwa maisha ya wasanii hayana uhalisia kwani wanalazimika kuendana na ukubwa wa brand zao hata wanapokosa uwezo huo

Soma https://jamii.app/VanessaMdeeMuziki
#COVID19 YASABABISHA SAUDI ARABIA KUZUIA RAIA WA KIGENI KWENDA KUFANYA HIJJA

> Raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia wataruhusiwa kufanya Hijja

> Hatua hiyo itawawezesha kutokaribiana wakati wa ibada hiyo

Soma https://jamii.app/Hijja2020SaudiArabia
#JFLeo
CHINA YAINGIA KATIKA USHINDANI WA β€˜NAVIGATION SATELLITE SYSTEM’ KWA KURUSHA SATELAITI YA MWISHO

> Leo Juni 23, China imezindua satelaiti ya kukamilisha mfumo wa β€˜Geolocation’

> Mfumo huo utaleta ushindani kwa GPS wa Marekani, GLONASS wa Urusi na Galileo wa Umoja wa Ulaya

> Hatua hii inaifanya China kuacha kuitegemea Marekani na Ulaya

Soma https://jamii.app/ChinaBeiDou
#JFLeo