JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kifungu hicho cha 52 (3) kinaeleza kuwa Mtu yeyote anayemnyanyasa mtu anayetoa taarifa za rushwa atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo cha muda usiozidi mwaka mmoja au vyote kwa pamoja

- Kifungu hicho kimeeleza kuwa kumnyanyasa ni kumfanyia vitendo ama vya Kumletea Majeraha, Kumtisha au Kumdhalilisha

#KemeaRushwa
ASKARI WA UPELELEZI ARUSHA AKAMATWA KWA RUSHWA YA TSH. 650,000
-
Sajenti Michael Njau amekamatwa na Maofisa wa TAKUKURU
-
Alitaka rushwa kutoka kwa mkazi aliyekuwa na shida ya kusaidiwa nduguye aliyekamatwa na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi

Soma https://jamii.app/AskariMbaroniRushwa
RUKWA: MVUA YABOMOA MADARAJA MANNE, WATATU WAFARIKI

> Mawasiliano baina ya mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi yamekatika

> Mkuu wa Mkoa ashauri wananchi wasipite kwenye maeneo yenye mafuriko

Zaidi, soma - https://jamii.app/MadharaMvuaRukwa
MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA VISIWANI ZANZIBAR

- Leo, Zanzibar inatimiza miaka 56 tangu yafanyike Mapinduzi yaliyouondoa madarakani Utawala wa Sultan Jamshid bin Abdullah uliokuwa umedumu Zanzibar kwa miaka mingi

- Baada ya Mapinduzi, Abeid Amani Karume aliiongoza Zanzibar lakini hadi leo nafasi ya John Okello, anayeaminika kuwa aliongoza Mapinduzi bado haijawekwa rasmi katika historia
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema “Wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza si kwamba rushwa haikuwepo, ilikuwepo lakini tulikuwa wakali sana.”

- Alisema, “Ikithibitika Mahakamani kuwa mtu ametoa au kupokea rushwa hatukumuachia Hakimu nafasi ya kutoa hukumu peke yake. Tukasema atakwenda ndani kwa miaka miwili na viboko 24, kumi na viwili siku anaingia kumi na viwili siku anatoka akamuonyeshe na mkewe."

#KemeaRushwa
IRAN: RAIA WAANDAMANA KUIPINGA SERIKALI BAADA YA KUKIRI KUITUNGUA NDEGE

> Kundi la waandamanaji limetaka Kiongozi wa Juu, Ayatollah Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi kujiuzulu nyadhifa zao baada ya kukiri kuitungua Ndege ya Boeing 737-800, mali ya Shirika la Ndege la Ukraine (UIA) na kusababisha vifo vya watu 176

Soma - https://jamii.app/IranProtestGovernment
UKRAINE: FAMILIA ZA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE IRAN KULIPWA FIDIA

> Ukraine itatoa Dola 8,000 kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo

> Rais Zelensky amesema Iran italazimishwa kulipa fidia

Soma - https://jamii.app/FidiaFamiliaAjaliNdegeUkrn
WIKI 1 YA KIFO CHA KAMANDA SOLEIMANI: KIONGOZI WA HEZBOLLAH AAPA KULIPIZA KISASI

> Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah amesema kutakuwa na operesheni mbalimbali dhidi ya Vikosi vya Marekani katika Kanda ya Mashariki ya Kati ili kulipiza kisasi Marekani kwa kuwaua Makamanda wa Iran na Iraq

> Amesema, Marekani haina chaguo lingine ila kuwaondoa wanajeshi wake kwa hiari au kurudisha miili yao ikiwa katika majeneza

Soma - https://jamii.app/HezbollahAvengeSoleiman
WAZIRI LUKUVI ATOA ONYO KWA WANAOJENGA BILA KUFUATA UTARATIBU

> Amesisitiza kuwa serikali haina mpango wa kubomoa nyumba zilizojengwa kiholela

> Ametoa wito kwa wananchi kufuata utaratibu na kupata vibali vya ujenzi

Soma - https://jamii.app/OnyoWanaojengaKiholela
KENYA, GARISSA: WALIMU 3 WAUAWA NA WANAMGAMBO WA KUNDI LA AL-SHABAAB

> Watu 3, wote Walimu wameuawa mapema leo kwa kupigwa risasi na watu wanaoaminiwa kuwa Wanamgambo wa Kundi la Al-Shabaab

> Mnara wa Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom umeharibiwa na gari la polisi kuteketezwa kwa moto

Soma - https://jamii.app/TeachersDeadAlShabaab
ARUSHA: POLISI WAMKAMATA MFANYABIASHARA KWA UTAPELI WA VIWANJA 51

> Joseph Rwekeza anashikiliwa na Polisi kwa kushindwa kutoa hati za viwanja zaidi ya 51 alivyouza

> Alipata Milioni 590 na kutokomea kusikojulikana

Soma - https://jamii.app/MbaroniUtapeliViwanja51
MFAHAMU MTU MWENYE TATTOO NYINGI DUNIANI

> Lucky Diamond Rich, pia ametoboa masikio na kuyavuta (kama Wamasai) na amejitoboa sehemu kadhaa za mwili wake

> Alianza kujiweka michoro mwilini akiwa na miaka 16 na alimaliza akiwa na miaka 28

Soma https://jamii.app/RekodiTattoo2019
APEWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KWA KUSINGIZIA AMEKUFA ILI ALIPWE MAFAO KWA MKUPUO

> George Mbuga alitakiwa kulipwa kwa mafao yake kwa Awamu Tano baada ya kustaafu. Aliamua kutumia njia ya mkato (Kujifanya amekufa) kupata fedha hizo

Soma - https://jamii.app/AdaiKufaMalipoMkupuo
AFYA: Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na virusi aina ya ''Human Papilloma'' ambapo mtu anaweza kupatwa na virusi hivi wakati wa kujamiana

> Visababishi vingine ni kufanya mapenzi katika umri mdogo ambapo Wanawake wanaofanya mapenzi chini ya miaka 16, wanadaiwa kuwa katika hatari kubwa ya kuugua

> Dalili zake ni kutokwa na damu ukeni, kutokwa na uchafu au usaha, maumivu makali wakati wa kujamiiana na kusababisha kutokwa na damu, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na maumivu ya kiuno

Kwa uelewe zaidi, soma - https://jamii.app/SarataniShingoKizazi
#JFAfya
UPDATE: Baraza la Usalama la Niger limesema Askari wake 89 na Wanajihadi 77 wameuawa katika mapigano yaliyotokea kwenye Kambi ya Chinagoder

> Aidha, Serikali imetangaza siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kuanzia leo ambapo Bendera zitapeperushwa Nusu Mlingoti nchi nzima

#JFLeo
JESSICA COX, RUBANI MWANAMKE ASIYE NA MIKONO

- Alipata leseni yake mnamo Oktoba 10, 2008 baada ya kupata mafunzo kwa Miaka Mitatu

- Pia, ana Mkanda Mweusi katika 'Taekwondo', anapiga piano, anapiga mbizi na ni 'Motivational Speaker'

Soma https://jamii.app/RubaniHanaMikono
#JFLeo
UGANDA: MWANAMKE AKAMATWA AMEBEBA VIPODOZI HARAMU AKIDAI NI MTOTO

> Vipodozi hivyo vilivalishwa nguo na kujenga picha kuwa ni mtoto

> Mamlaka ya Mapato yasema mbinu hiyo inafahamika hivyo sio rahisi kupitisha Vipodozi Haramu

Soma - https://jamii.app/MbaroniVipodoziFeki
DAR: Mahakama ya Kisutu imeifuta kesi ya Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita baada ya Wakili wake kuomba iondolewe kwa kuwa haina maana na hajapewa Haki ya Msingi ya Kusikilizwa

> Meya huyo leo alishindwa kuingia ofisini baada ya kukuta 'Password' za mlango zimebadilishwa

#JFLeo
PAPA BENEDICT AMEMTAKA PAPA FRANCIS KUTOLEGEZA KAMBA KUHUSU SHERIA YA USEJA

> Amesema hayo katika Kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah

> Ni katika kujibu pendekezo la kuruhusu waliooa kutawazwa kama Makasisi huko Amazon

Soma https://jamii.app/PapaSheriaUseja
TABORA: WAJAWAZITO WAJIFUNGULIA MAPOKEZI, WAUGUZI KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

> Ni Wauguzi wa Zahanati ya Kirumbi, Kisanga na Lembeli na watumishi walevi nyakati za kazi

> Inaelezwa, mmoja wa wajawazito alilazimika kujifungulia mapokezi baada ya Muuguzi wa Zamu kudai hawezi kumsaidia kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri

Soma - https://jamii.app/WajawazitoKujifunguaMapokezi
USHAURI KILIMO: MATUMIZI SAHIHI YA DAWA HUZUIA MAGUGU KUOTA SHAMBANI

> Uchaguzi wa dawa utategemea aina ya Magugu na hatua yaliyofikia. Mkulima unashauriwa mvua zikinyesha usikimbilie kupanda bali subiri kama wiki 2 au 3 ili majani yaote

> Kwa zao la Mpunga; Kama majani hayajaota shambani, tumia Pendamethatlin au Oxidiazon 250g/lt. Puliza dawa yoyote kati ya hizo baada ya kupanda Mpunga na hakikisha umekausha maji shambani saa 24 kabla ya kunyunyizia dawa

> Iwapo Magugu yameanza kuota tumia Bretilaclo, Pyribenzole, Tiller Gold, Penoxulum (Rainbow), Propanil, Garil, 2,4D Amine, Bentazole 480g/It

Fahamu zaidi - https://jamii.app/KilimoPaliziMazao
#JFKilimo