JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CHINA: ANTENA YA REDIO KUBWA ZAIDI DUNIANI YAANZA KUFANYA KAZI

>Antena hiyo ya mawimbi ya redio iliyopewa jina la 'FAST' ina ukubwa sawa na Viwanja vya Mpira 30 na ujenzi wake ulichukua miaka 5 na ulikamilika 2016

> Gharama za ujenzi ni dola za Marekani milioni 180 (zaidi ya bilioni 400 za Kitanzania), ina uwezo wa kukusanya taarifa zenye ukubwa wa Gigabyte 38 ndani ya sekunde 1

Soma - https://jamii.app/FASTRadioTelescope
#JFTeknolojia
KENYA vs TANZANIA: SIFA ZA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS

- Moja ya sifa katika Katiba ya Tanzania ni kuwa Mgombea awe Mwanachama wa Chama cha Siasa na ateuliwe na chama

- Katiba ya Kenya inaeleza kuwa Mgombea awe ameteuliwa na Chama cha Siasa au awe Mgombea Binafsi

- Katiba ya Tanzania inamtaka Mgombea awe amefikisha miaka 40 huku Kenya akitakiwa kuwa na miaka 35

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-KenyaVsTanzania

#Katiba
TANZANIA vs KENYA: KUHOJI UHALALI WA UCHAGUZI WA RAIS BAADA YA MGOMBEA KUTANGAZWA

- Katiba ya Tanzania: Hakuna Mahakama yenye Mamlaka ya kuhoji Uchaguzi wake

- Katiba ya Kenya: Mtu anaweza kutoa ombi katika Mahakama Kuu la kupinga Uchaguzi huo ndani ya siku 7

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-KenyaVsTanzania

#Katiba
JE, LUGHA YA KUFUNDISHIA NI KIKWAZO AU KUNA SABABU NYINGINE?

> Ukiangalia matokeo ya Darasa la Saba 2019, shule za 'English Medium' zimeongoza kwa ufaulu kwenye somo la Kiswahili kuliko shule zinazotumia lugha ya Kiswahili kwenye masomo yote

> Pia, ukiangalia mfano wa Raia wa China Congcong Wang aliyepata Alama “B” ya Kiswaili katika Matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2016 na kushika Nafasi ya Pili Kitaifa

Kwa mjadala zaidi Soma https://jamii.app/EnglishMediumKufauluKiswahili
Februari 11, 2019 Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema nchi za Bara la Afrika zimeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika mapambano dhidi ya Rushwa

- Aliyasema hayo wakati akitoa muhtasari wa yaliyojiri kwenye Mkutano wa 32 wa Wakuu wa nchi za Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia

#KemeaRushwa
MADHARA YA MICHORO MWILINI (TATTOOS)

> Unaweza kukosa fursa mbalimbali kama kuajiriwa Jeshini

> Madhara mengine ni Saratani ya Ngozi, kuwa na aleji/mzio, matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI na kushindwa kuchangia damu

Soma https://jamii.app/MadharaTattoo
DEWJI AJIUZULU UENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SIMBA

- Mohamed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya Simba kupoteza Fainali ya Kombe la Mapinduzi

- Amesema atabaki kama Mwekezaji, akiendeleza miundombinu na Soka la Vijana

Soma https://jamii.app/DewjiAjiuzuluSimba
BARCELONA YAMTUPIA VIRAGO KOCHA WAKE

- Klabu ya Barcelona imemfukuza Kocha Ernesto Valverde (55) na kumtangaza Kocha wa Zamani wa Real Betis, Quique Setien (61) kuchukua nafasi yake

- Inaelezwa kuwa, Barcelona chini ya Valverde, mara kadhaa imecheza Soka lisiloshawishi

#JFLeo
TAKUKURU ARUSHA: WATUHUMIWA 22 WALIPANDISHWA KIZIMBANI OKTOBA HADI DESEMBA, 2019

> Miongoni mwa watuhumiwa ambao walishtakiwa kipindi hicho ni Askari Polisi, Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma na mashauri yao bado yanaendelea Mahakamani

Soma https://jamii.app/Mbaroni22-TakukuruAR
MAREKANI YAIONDOA CHINA KWENYE ORODHA YA WADHIBITI WA KIWANGO CHA KUBADILISHA FEDHA

> Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani inasema, kwa sasa hakuna Nchi Mshirika wa Kibiashara wa Marekani anayefikia vigezo vya kisheria vya kudhibiti thamani ya sarafu yake

Soma - https://jamii.app/USCurrencyExchangeChina
DKT. BASHIRU: UCHAGUZI SIO NAMBA, UCHAGUZI NI UAMUZI WA UMMA

> Katibu Mkuu wa CCM amesema Uchaguzi sio Namba, Uchaguzi ni Uamuzi wa Umma, namba ni kitu cha baadae kwasababu Wananchi hufanya maamuzi kabla ya Siku ya Kupiga Kura, siku ya kupiga kura ndio siku ya kudhihirisha uamuzi wao

Soma - https://jamii.app/BashiruMaanaUchaguzi
KAMPUNI YA DHAHABU YA CANADA KUISHITAKI SERIKALI YA TANZANIA KWA KUKIUKA MIKATABA

> Kampuni ya Winshear Gold Corp imeitaarifu Serikali ya Tanzania nia ya kuishitaki kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya Kimataifa baada ya kukiuka Mikataba ya Uwekezaji kati ya Tanzania na Canada

> Ikiwa matokeo hayatapatikana ndani ya miezi 6 ijayo, Kampuni itawasilisha madai yake mbele ya Baraza la Usuluhishi la Kimataifa na kutafuta fidia kwa uharibifu

Soma - https://jamii.app/WinshearIntentSubmitArbitration
TIKETI ZOTE ZA MABASI KUKATWA KIELEKTRONIKI KUANZIA MWEZI UJAO

> Katibu wa TABOA, Enea Mruto amesema, Mfumo wa Kielektroniki utawarahisishia wateja kupata tiketi na kuondoa msongamano

> TABOA wanashirikiana na TRA kufanikisha mpango huu

Soma - https://jamii.app/ElectronicBusTickets
FAHAMU UNYANYASAJI WA WATOTO KWA WATOTO WAWAPO MASHULENI (BULLYING)

> Unyanyasaji wa watoto kwa watoto wawapo mashuleni unaweza kujidhihirisha katika namna nyingi ikiwemo kusukumwa hovyo, kupigwa, kuitwa majina yasiyofaa, matusi au vitisho

> Hali hii huweza kumuathiri mtoto kisaikolojia na kihisia na kumtengenezea mazingira ya kutokujiamini, kukosa furaha, kujiona ni mtu wa kushindwa kila siku na kujitenga na wenzake

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/ChildBullyingSchools
MICHEZO: Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba @moodewji ametangaza kurudi kwenye wadhifa huo baada ya kutangaza kujiuzulu kutokana na mwenendo wa Timu hiyo kutokuwa mzuri

> Kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema “Mimi ni Simba damu damu, Tuko pamoja”

#JFMichezo
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI 4 KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI MBALIMBALI
-
Walioapishwa ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kuwa Balozi Afrika Kusini, Dkt. Modestus Fransics Kipilimba kuwa Balozi Namibia
-
Wengine ni Profesa Emmanuel Mwaluko Mbennah kuwa Balozi Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Nigeria

Soma - https://jamii.app/UapishoMabalozi
#JFLeo
NIGER: MKUU WA MAJESHI AFUKUZWA KUTOKANA NA WANAJESHI 89 KUUAWA

> Mkuu wa Jeshi la Niger amefukuzwa kazi kutokana Wanamgambo wa Kijihadi kuwaua wanajeshi 89 walipovamia Kambi ya Jeshi

> Viongozi wengine waandamizi 3 wa Jeshi hilo wamevulia nyadhifa zao baada ya Kikao cha Baraza la Mawaziri

Soma - https://jamii.app/ArmyChiefGenSackedNiger
PEMBA: MAALIM SEIF NA SALIM BIMANI WATUHUMIWA KUFANYA MKUTANO BILA KIBALI

> Viongozi hao kwa sasa wameachiwa kwa dhamana na Chama chao kupitia Mtandao wa Twitter kimedai walifanya Mkutano wa ndani usiohitaji kibali

Soma - https://jamii.app/ViongoziACTPolisi
RAIS WA ZAMBIA AYATAKA MATAIFA YA ULAYA KUACHA KUINGILIA UONGOZI WA AFRIKA

> Rais Edgar Lungu amesema, haikubaliki kwa watu wa nje kuamuru jinsi Nchi za Afrika zinavyopaswa kuongozwa kwasababu Afrika inapaswa kuruhusiwa kuamua jinsi inavyojitawala badala ya kuamrishwa na watu wa nje

Soma - https://jamii.app/OutsidersAfricanGovernment
TRAFIKI ANAYEDAIWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI HAJULIKANI ALIPO

> Polisi walisema wamemtia nguvuni, lakini taarifa zimedokeza kuwa hajawahi kamatwa

> Jumbe za simu, zinathibitisha mahusiano yao. Mtoto alisema hata simu alipewa na huyo polisi

Soma https://jamii.app/TrafikiMimbaMwanafunzi