JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com kupitia jukwaa la Siasa ameibua hoja kuhusu magari yenye plate number za aina ya SSH 25-30 au SSH 2530, akisema kuna magari mengi yenye namba zinazofanana na wengi mtaani wanajiuliza iwapo wamiliki wake ni viongozi au la!

Amehoji iwapo tukio kama ajali au uhalifu likitokea litahusianishwa na gari lipi? Je, hii si aina ya kampeni ya mapema?

Kushiriki mjadala huu https://jamii.app/PlateNumberZaSamia

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji #Misinformation #Disinformation #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Akizungumza na Waandishi wa Habari, Agosti 16, 2025, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Saipulan Ramsey amesema “Chama Cha Mapinduzi hakijatoa kwa Mwanachama yeyote wala Mwananchi yeyote wala kutoa ruksa ya utengenezaji wa Namba za 'SSH 2530'. Ziko mamlaka husika zinazohusika na utoaji wa vibao vya namba za magari.”

Ameongeza “Chama hakina mamlaka ya kutengeneza vibao vya namba za magari, zipo mamlaka husika zinazoshughulika na jukumu hilo. Naomba mamlaka zinazohusika na utoaji wa namba za magari pamoja na usafirishaji zifuatilie yeyote aliyeweka namba hizo awaeleze amezipata wapi.”

Video Credit: Arusha Zone

Soma zaidi https://jamii.app/NambaZaSSH2530

#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #UchaguziMkuu2025
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda, leo Jumatatu Agosti 18, 2025 amefafanua suala la Mtoto Mkazi wa Nyakato, Wilayani Ilemela aliyesemekana kulawitiwa na Steven Ibasa (Baba Claudia), kwa kueleza kuwa suala hilo limefikishwa Mahakamani na kwamba mtuhumiwa amekosa mtu wa kumdhamini, amepelekwa Gerezani Butimba.

Akiwa ofisini kwake, RC Mtanda amewataka Wananchi kuwa na imani na Muhimili wa Mahakama kwakuwa utatenda haki katika suala hilo.

Ikumbukwe, suala hilo liliibuliwa na Mdau wa JamiiForums.com akidai kuna mazingira ya kumlinda Mtuhumiwa huyo ambaye alishikiliwa katika Kituo cha Polisi Nyakato kisha Kituo cha Polisi Kirumba, hivyo akaomba Mamlaka za Juu kuingilia kati ili Haki ipatikane.

Soma zaidi https://jamii.app/SaidMtandaUpdates

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema "Tukiona moshi unafuka hatutasubiri moto uwake, tutachukua hatua. Tukiona matamshi ambayo hayastahili, tunajua huku anakoelekea huyu siyo sahihi, lazima tuzuie kabla ya kutokea madhara."

Soma https://jamii.app/MishimeMoshi

#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Uwajibikaji #Accountability #UchaguziMkuu2025
1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Kulwa Steven Ibasa (37) anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto wa Kiume (4), amefikishwa Mahakama ya Ilemela, jana Agosti 18, 2025 na baada ya shauri lake kutajwa alikosa Mtu wa kumdhamini akapelekwa Gerezani Butimba.

Hati ya Mashtaka imesomwa na Wakili wa Serikali, Mwanahawa Changali mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Juma Opudo imeeleza Kesi hiyo Namba 20028/2025, Ibasa ameshtakiwa kwa shtaka la kulawiti, kinyume na Kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya Mwaka 2023.

Mshtakiwa alikana mashtaka ambapo kesi imepangwa kutajwa tena Septemba 1, 2025 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa upande wa mashahidi.

Ikumbukwe, Agosti 15, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alihoji ukimya wa Mamlaka kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa, Saidi Mtanda, akatoa maelekezo suala hilo lifanyiwe kazi ndipo Agosti 18 mtuhumiwa akafikishwa Mahakamani.

Zaidi soma https://jamii.app/NyakatoMatukio

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza Agosti 18, 2025 kwenye Baraza la Wafanyakazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ametoa onyo kwa Watumishi wanaovujisha siri za Serikali, akibainisha kuwa ofisi yake itawafuatilia kwa ukaribu na kuchukua hatua za kinidhamu kwani ni kinyume na miongozo, Kanuni na Sheria za nchi, pia kufanya hivyo ni sawa na kujipiga risasi mwenyewe.

Pia, alieleza kusikitishwa na uwepo wa Mawakili wa Serikali wenye tabia za uongo, akisema jambo hilo linaweza kuipunguzia heshima taaluma ya Sheria na kuichafua taswira ya Serikali mbele ya umma.

Soma zaidi https://jamii.app/MwanasheriaSerikali

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa ushauri kwa Mamlaka za Jiji kuangalia changamoto ya baadhi ya Maafisa wa Usalama katika Barabara kati ya Soko Kuu na Sokoine, akidai hawatendi haki kwa baadhi ya madereva wanaopita njia hiyo kiasi kwamba wengine wanatengeneza mazingira ya usumbufu ili 'wamalizana pembeni'.

Soma zaidi https://jamii.app/FainiArusha

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #JFMdau2025 #Accountability
👍1
KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Wilaya ya Mpanda anatoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (#TANESCO) kushughulikia changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara, akihoji mbona wanapodai madai yao hutumia magari ya matangazo kuzunguka Mtaani kufikisha ujumbe, lakini suala la kukata umeme hutumia makundi ya WhatsApp ambayo Wananchi wengi hawana au hawatumii?

Zaidi soma https://jamii.app/UmemeMpanda

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji
ETHIOPIA: Wizara ya Elimu imetoa mwongozo unaopiga marufuku utoaji wa Shahada za Heshima (Honorary Doctorate) kwa Viongozi wa Serikali na Wanasiasa walioko madarakani, agizo hilo limetiwa saini na Waziri wa Elimu, Profesa Berhanu Nega, na limeelekezwa kwa Vyuo Vikuu na taasisi zote za elimu.

Mwongozo huo umeweka masharti mapya, ukiwataka wanaotunukiwa wawe ni waliotoa mchango mkubwa katika taaluma au kazi zao. Viongozi walioko kazini na Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu na Wajumbe wa Seneti, hawataruhusiwa kupokea shahada hizo wakiwa bado kazini.

Aidha, vyuo vitakavyotoa shahada ya heshima vinapaswa kutoa kozi za PhD, viwe na angalau awamu nane za wahitimu, na viwe vinatambulika Kitaifa na Kimataifa.

Upande wa Tanzania, miongoni mwa waliotunukiwa Shahada za Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere (1966, 1986), Balozi Juma Mwapachu (2005), na Rais Mstaafu Hayati Benjamin Mkapa (2006). Licha ya mchango wao mkubwa, hawakuwahi kutumia cheo cha “Daktari wa Heshima”.

Zaidi soma https://jamii.app/EthiopiaMarufukuPhD

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa ameibua hoja kuhusu wimbi la baadhi ya Watu maarufu na Wanasiasa kujipendekeza kwa Watawala maarufu kama ‘uchawa’ hali ambayo imeonekana kuzidi kushamiri kadri joto la Uchaguzi linavyopanda.

Amedai kuwa tabia hiyo haimfurahishi kwani inaleta madhara kwa Taifa, ikiwemo kupotosha Wapiga Kura na kuharibu mwelekeo wa Demokrasia.

Je, Wanasiasa wanaojipendekeza wanatafuta nafasi za Uongozi kwa maslahi ya Taifa na Wananchi, au ni kwa ajili ya maslahi yao binafsi?

Zaidi Soma https://jamii.app/KujipendekezaWagombea

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025
1👍1