JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, anawasilisha Bungeni hotuba ya Mapendekezo ya Serikali kuhusu Bajeti Kuu kwa mwaka wa Fedha 2025/2026

Serikali imependekeza ukomo wa Bajeti wa Tsh. trilioni 57.04 kwa Mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya Tsh. trilioni 50.29 ya Mwaka wa Fedha unaomalizika Juni 30, 2025.

Fuatilia https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji
Akisoma Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Katika Bajeti ya 2024/25, Serikali ilipanga kukusanya Tsh. Trilioni 50.29, hadi Mei 25, 2025 Tsh. Trilioni 45.07 zimekusanywa sawa na Asilimia 86.6 ya lengo la Mwaka

Ameongeza kwa kusema "Serikali ya Awamu ya Sita imefanya mageuzi makubwa ambayo yameongeza mapato ya ndani, hivyo kila Mtanzania anatakiwa kuelewa kuwa Kodi yetu ndio Maendeleo yetu na Maendeleo hayawezi kupatikana kwa kutegemea Misaada, ni lazima tulipe kodi"

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema uwiano wa mapato ya ndani kwa Pato la Taifa umeongezeka kufikia 15.0% Mwaka 2023/24 kutoka 13.7% Mwaka 2020/21, ambapo amesema Mwenendo huu chanya unadhihirisha mageuzi makubwa kwenye ukusanyaji wa mapato

Aidha, amesema kuwa hadi Mei 2025, Serikali imefanikiwa kusaini mikataba 169 na wawekezaji mbalimbali. Amesema, hii itatusaidia kuondoa uwezekano wa kulea utovu wa tija (inefficiency) kwa wale wanaopata vivutio na kuhakikisha kuwa wanakuwa na kuhitimu kutoka katika mahitaji ya kulindwa.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imesema baadhi ya maeneo yaliyopelekewa Fedha katika kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025 ni ugharamiaji wa Deni la Serikali Tsh. Trilioni 11.16, ugharamiaji wa Mishahara ya Watumishi wa Umma Tsh. Trilioni 10.27; na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Tsh. Bilioni 741.5.

Akisoma Bajeti Kuu Bungeni, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeendelea kulipa madeni yaliyohakikiwa ya Wakandarasi, Wazabuni na Watoa Huduma katika kujenga Taifa, ambapo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.01 kimelipwa

Amesema ulipaji wa Madeni umesaidia kulinda Mitaji na kuchochea shughuli za kiuchumi Nchini

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji
Serikali imesema Tsh. Trilioni 1.58 zilitolewa katika ujenzi wa Barabara, Madaraja na Viwanja vya Ndege; Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Reli ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) Tsh. Trilioni 1.68

Aidha, Mradi wa Kufua Umeme katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) MW 2,115 na Mradi wa kusambaza Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) zilitolewa Tsh. Bilioni 574.8; na Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya Mpira kwa ajili ya Maandalizi ya AFCON 2027 Tsh. Bilioni 179.8

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imesema Tsh. Bilioni 636.0 zimetolewa katika Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na Vyuo vya Kati; Programu ya Elimu ya Msingi na Sekondari bila Ada Tsh. Bilioni 444.7

Waziri Mwigulu Nchemba amefafanua kuwa Miradi ya Maji Mijini na Vijijini Tsh. Bilioni 378.7; Ununuzi wa Dawa, Vifaa, Vifaa tiba na Vitendanishi kwa ajili ya Hospitali za Mikoa, Kanda na Rufaa Tsh. Bilioni 414.7; Ujenzi na Ukarabati wa Hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Rufaa Tsh. Bilioni 47.2; na Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati Tsh. Bilioni 7.3.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akisoma Bajeti Kuu Bungeni, amesema Hadi Aprili 2025, Deni la Serikali lilikuwa Tsh. Trilioni 107.70, ambapo kati ya kiasi hicho, Deni la nje ni Tsh. Trilioni 72.94 na Deni la ndani ni Tsh. Trilioni 34.76

Amesema, tathmini ya Uhimilivu wa Deni iliyofanyika Oktoba 2024 imeonesha kuwa deni ni Himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji
Serikali imesema Mwaka 1961 tulikuwa na Shule za Msingi 3,270, Walimu 9,885 na Wanafunzi 486,470. Shule za Sekondari 41, Walimu 764 na Wanafunzi 11,832. Vyuo vya Ualimu 8, Walimu 164, na Wanafunzi 1,723, Chuo kikuu kimoja, Wahadhiri 6 na Wanafunzi 14.

Hadi kufikia Mwaka 2024, Tanzania ilifikisha Shule za Msingi 20,533, Walimu 229,840 na Wanafunzi 11,391,185. Shule za Sekondari 6,269, Walimu 128,686 na Wanafunzi 3,314,198. Vyuo vya Ualimu 65, Walimu 1,633 na Wanafunzi 16,002, Vyuo Vikuu 79, Wahadhiri 8,625 na Wanafunzi 334,854

Serikali pia imeendelea kuongeza Vyumba vya Madarasa ya Elimu ya Msingi kutoka 128,425 Mwaka 2020 hadi Madarasa 155,330 Mwaka 2024 na Vyumba vya Madarasa ya Elimu ya Sekondari kutoka 46,928 Mwaka 2020 hadi 81,052 Mwaka 2024.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema "Kipindi cha Serikali ya Awamu ya 4 ulitokea uhalifu wenye sura ya Ugaidi uliohusisha urushwaji wa Mabomu kwenye Nyumba za Ibada, Mikusanyiko ya Watu na Mashambulizi ya Mtu mmoja mmoja wakiwemo Watu wenye Ulemavu wa Ngozi. Tumesahau hili? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vilisimama imara na kukomesha Uhalifu huo”

Ameongeza "Kipindi cha Serikali ya Awamu ya 5, ulitokea uhalifu wa Watoto kutekwa na kuuwawa, Mtu mmoja mmoja kupigwa risasi kwenye makazi yake au katika Utekelezaji wa majukumu yake. Waliuawa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wanaotokana na CCM na tulishuhudia pia miili iliyokuwa kwenye Magunia na Mifuko ikiwa imetupwa Baharini. Na haya tumesahau? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vilisimama imara na kukomesha Uhalifu huo.”

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imesema Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kupandisha Vyeo Watumishi wa Umma 476,470 ambapo Jumla ya Tsh. Bilioni 689.9 zimetumika

Pia, kipindi cha kuanzia Mwaka 2021/22 hadi Mei 2025, Serikali imelipa madai ya malimbikizo ya Mishahara jumla ya Tsh. Bilioni 318.37 kwa Watumishi na Wastaafu 187,152.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imependekeza kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha Tsh. 50 kwa kilo ya 'crisps' zinazozalishwa Nchini, na Tsh. 100 kwa kilo ya 'crisps' zinazoingizwa kutoka nje ya Nchi

Akisoma Bajeti Kuu, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema Lengo la hatua hii ni kupunguza athari za Kiafya ikiwemo ongezeko la uzito (Obesity) zinazotokana na matumizi ya bidhaa hizo na kuongeza Mapato ya Serikali. Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 6,475;

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imependekeza kupunguza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye Vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy drinks) vinavyozalishwa ndani ya Nchi kutoka Tsh. 561 kwa kila Lita hadi Tsh. 134.2 kwa kila lita

Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amesema Lengo la hatua hii ni kuweka unafuu kwa Wazalishaji wa ndani, kuongeza Ushindani na kuchochea Uwekezaji Nchini. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 170.2

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango 5% kwa Soseji na bidhaa zingine zinazofanana na hizo zinazozalishwa Nchini, na 10% kwa zile zinazoingizwa kutoka nje ya Nchi

Waziri Mwigulu Nchemba, amesema lengo ni kuongeza mapato ya Serikali, kuvutia Uwekezaji Nchini na kulinda Wazalishaji wa ndani. Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 2,413.9

Pia imependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha 10% kwenye sabuni zinazoingizwa kutoka nje ya Nchi, Lengo likiwa kulinda Wazalishaji wa ndani na kuongeza Ajira, hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa Tsh. Milioni 143,395.8

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha 10% kwenye malipo ya Kamisheni inayotokana na matangazo ya Michezo ya kubahatisha

Amesema Kodi hii itakuwa ni kodi ya mwisho (final), lengo la hatua hii ni kuendana na Kanuni za usawa za utozaji kodi na kupanua wigo wa kodi, na hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 6,787.2

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha 30% kwenye vifaa vya Sigara za Kielektroniki na vimiminika vya Sigara za Kielektroniki, ili kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya bidhaa hizo na kuongeza wigo wa Kodi

Amesema hatua hiyo inatarajia kuongeza Mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Milioni 3,322.2

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kupunguza ada ya usajili wa pikipiki za biashara kutoka Tsh. 340,000 hadi Tsh. 170,000 kwa miaka mitatu, huku akisema ada hiyo husika italipwa wakati wa usajili wa awali pekee

Vile vile amependekeza kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, bajaji na guta kutoka Tsh. 70,000 hadi Tsh. 30,000

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Kukosea siyo tu jambo la kawaida, bali pia ni muhimu sana kwa ukuaji na kujifunza.

Tunajifunza kutokana na makosa yetu, tunaboresha ujuzi wetu na tunakuwa watu wenye Hekima zaidi.

Makosa yanatuonesha pale tulipofanya vibaya na kutupa fursa ya kurekebisha na kusonga mbele.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DIPLOMASIA: #Israel imefanya mashambulizi Nchini #Iran katika Mji wa #Tehran ikiwa ni sehemu ya Oparesheni kwa kile ambacho Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema walilenga kudhoofisha Miundombinu ya Nyuklia ya Iran na Viwanda vya Makombora ya masafa marefu

Pamoja na hivyo, Israel imetangaza hali ya hatari, ikisema inatarajia mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa Iran, wakati ambapo Iran imesema mashambulizi hayo yameathiri Makazi ya raia na kuua Watu kadhaa wakiwemo Watoto

Wakati huohuo, Rais wa Marekani, #DonaldTrump amekiambia Kituo cha #FoxNews kuwa alikuwa na taarifa kuhusu mashambulizi hayo kabla lakini Nchi yake haikuhusika kwa namna yoyote

Soma https://jamii.app/IsraelAgainstIran

#Diplomacy #Governance #HumanRights #JamiiForums #JamiiAfrica
UTEUZI: Rais Samia amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika Juni 15, 2025 Ikulu, Chamwino - Dodoma, Saa 4.00 Asubuhi

Soma https://jamii.app/UteuziGeorgeMcheche

#Uteuzi #JamiiForums #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mifumo ya Hali ya Hewa haioneshi uwepo wa mvua hivi karibuni hapa nchini badala yake kutakuwa na ukavu na ubaridi ambapo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za kujilinda na baridi

Meneja wa Utabiri wa TMA, Dkt. Mafuru Kantamla amesema mvua zilizonyesha hivi karibuni Ukanda wa Pwani zimetokana na ongezeko la Joto katika Bahari ya Hindi hususan katika Mwambao wa Pwani lakini hazitakuwa na mwendelezo kwa kuwa joto la Bahari limeanza kupungua kwa kasi

Soma https://jamii.app/HaliYaHewaJuni

Video Credits: Torch Media

#ClimateChange #JamiiForums #JamiiAfrica
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mdau wa JamiiForums.com anaeleza kuwa Daraja lililopo Kata ya Mkonze, Mtaa wa Muungano linalounganisha Mtaa wa Muungano na Goba limeharibika na halijafanyiwa maboresho kwa muda mrefu

Anadai vyombo vyote vya usafiri na wanaotembea kwa miguu wanalazimika kupita pembeni kwa kuwa eneo la katikati halipitiki

Anaongeza kuwa ikinyesha mvua ukiwa upande mmoja kati ya maeneo hayo lazima usubiri mpaka maji yapungue ndio uvuke, anatoa wito kuwa Daraja liboreshwe kwa kuwa hali ilivyo ni mateso kwa wapitaji wa hapo

Soma https://jamii.app/DarajaLaMuunganoGoba

#JamiiForums #Accountability #Miundombinu