JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa ameeleza katika kipindi hiki cha mchakato wa vyama kuwapata Wagombea, kumekuwa na usambazaji wa vifaa vyenye nembo ya chama. Anadai matukio hayo yanaweza kuibua mjadala kuhusu ushawishi, kwani bado haijathibitishwa kama vinaweza kuathiri maoni ya Wapiga Kura kwa makusudi.

Amehoji, Je, wahusika wanahakikisha hakuna uvunjifu wa Sheria za Uchaguzi wakati wa usambazaji wa vifaa hivyo?

Zaidi Soma https://jamii.app/KablaYaKampeni

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
2
Mtaalamu wa Saikolojia, Ndoa, Mahusiano na Malezi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Chris Mauki, amesema “Mara nyingi, mtu anayeandika maneno ya chuki huonesha changamoto zake binafsi za kisaikolojia huenda zimetokana na malezi magumu, ukosefu wa upendo au mazingira yenye chuki aliyokulia. Kwa bahati mbaya, maumivu haya huishia kuwagusa wengine, na walioumizwa nao huanza kuwaumiza watu wengine.”

Aidha amesema “Wanaoshuhudia au kukutana na kauli za chuki mtandaoni nao huweza kuziendeleza kwa kuzisambaza kwa watu wengine na mzunguko wa maumivu unaendelea.”

Tembelea JamiiForums.com

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
1
GEITA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema linaendelea kuchunguza tukio la kutoweka kwa Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Wilaya ya Bukombe, ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 21, 2025, Polisi wameeleza walipokea malalamiko kwamba mnamo Agosti 19, 2025 saa 10:00 jioni, Elisha alichukuliwa na watu watatu wasiojulikana akiwa studio ya MAS J, Kilimahewa kata ya Bulangwa, waliokuwa na gari jeupe lisilojulikana usajili wake.

Aidha, Jeshi limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa ya kuweza kusaidia kupatikana kwa Elisha asisite kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Zaidi soma https://jamii.app/JumaElishaWasiojulikana

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #JFMatukio #UtawalaBora #HakiZaBinadamu
1
MOROGORO: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa wito kwa Mamlaka za Serikali kuanzia ngazi za Vitongoji, Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Askari, Wilaya, Mkoa na Mamlaka husika kufuatilia na kutatua mgogoro wa Wakulima na Wafugaji hasa maeneo ya Dumila na Kimamba.

Pia, Mdau amezitaka Mamlaka za juu kudhibiti vitendo vya #rushwa vinavyoendeleza kukandamiza suluhisho la Mgogoro huo akisema "Rushwa imetawala sana Kilosa, Viongozi Wanapokea kutoka kwa Wafugaji ili kuwakandamiza Wakulima, inauma sana na inatuumiza wengi wetu ambao hatuna kipato kikubwa."

Soma zaidi https://jamii.app/WafugajiWakulima

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #JFHuduma #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza leo Agosti 21, 2025 katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Waziri wa Habari Prof. Palamagamba Kabudi amewataka Waandishi wa Habari kuacha rushwa na bahasha za kahawia, akisema Wananchi wanahitaji habari zenye uzito wa hoja, siyo uzito wa posho.

Ameongeza “Rushwa hupoteza uaminifu wa Vyombo vya Habari, kudhoofisha #demokrasia, inakuza ufisadi na kuhatarisha maisha ya waandishi waadilifu."

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiRushwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Governance
1
Afya ndiyo msingi wa Maisha. Bila Afya njema, utajiri na upendo hauwezi kuwa kamilifu.

Itunze na kuijenga Afya yako Mdau 🙂‍↕️

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com ambaye ni Mkazi wa Njombe Mjini ametoa wito kwa Halmashauri hiyo kuweka wazi ikiwa imetoa maelekezo kwa Shule za Msingi kutoza Wanafunzi hadi Tsh. 10,000 kwa ajili ya mitihani ya kila wiki, na kuongeza kuwa gharama hizo zimekuwa mzigo kwa Wazazi na Walezi.

Zaidi soma https://jamii.app/ShuleNjombeHalmashauri

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Askofu Dkt. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe akiongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Ihembe, Wilaya ya Karagwe, Agosti 11, 2025, amewaasa Watanzania kutumia busara katika kuchagua Viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ili kupata Viongozi wanaostahili.

Zaidi soma https://jamii.app/BagonzaUchaguziBusara

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo - Bara, Isihaka Mchinjita, akihojiwa na kituo cha Redio cha #EastAfrica, Agosti 20, 2025 ameeleza kuwa Luhaga Mpina si mgeni ndani ya chama hicho kwani alijiunga nacho muda mrefu na tayari ni sehemu ya harakati zao.

Aliongeza kwa kusema kuwa mjadala mkubwa ulijikita kwenye namna bora ya kumtumia Mpina ili kuleta faida ya kisiasa kwa chama, ama kubaki kama Mbunge wa Kisesa au kuingia moja kwa moja kwenye siasa za kitaifa, na baada ya tathmini, chama kiliona atakuwa na mchango mkubwa zaidi kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu.

Zaidi soma https://jamii.app/MpinaActUfafanuzi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
👍1
BURUDANI: Mdau, ni nukuu/mstari/kauli ipi (Punchline) kutoka kwenye filamu uliyoipenda zaidi? Ulisikia kwenye filamu gani na kwanini unaikubali?

Kushiriki mjadala soma https://jamii.app/NukuuMuvi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFBurudani #JFMoviesQuotes