JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Serikali ya Uganda imethibitisha kuwa imeingia makubaliano na Marekani yatakayohusisha Wahamiaji kutoka Marekani kupokelewa nchini humo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa #DonaldTrump unaolenga kuwarudisha maelfu ya Wahamiaji walioko katika hifadhi za Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema wapo tayari kupokea Wahamiaji hao na kudokeza kuwa itawapa kipaumbele zaidi wale ambao wana asili ya Kiafrika na ambao hawana rekodi yoyote ya Uhalifu.

Kando na Uganda nchi nyingine kutoka Afrika ambazo zimekubali kupokea wahamiaji kutokea Marekani ni Eswatini, Rwanda pamoja na Sudan ya Kusini.

Zaidi Soma: https://jamii.app/WahamiajiUganda

#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Utawala
3
KIGOMA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa imewahukumu kifungo cha Miaka 22 jela aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Athuman Msabila pamoja na Watumishi wenzake watatu baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi nyaraka na utakatishaji fedha.

Msabila na Salum Juma wamehukumiwa Miaka 20 kwa utakatishaji fedha na Miaka miwili kwa kughushi nyaraka, huku Ferdinand Filimbi na Frank Nguvumali wakihukumiwa miaka miwili kwa kosa la kughushi nyaraka.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa, Misana Majula katika kesi ya Jinai Namba 5546 ya Mwaka 2024 iliyowakabili Watumishi 11 wa Serikali.

Zaidi Soma https://jamii.app/KigomaJela

#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Sheria #Uwajibikaji
ZIMBABWE: Mfungwa anayefahamika kwa jina la Emmanuel Mugede, ambaye tayari alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa ubakaji wa mtoto, amehukumiwa miaka 20 zaidi gerezani kwa kumlawiti mfungwa mwenzake mwenye umri wa miaka 24 Julai 23, 2025 katika gereza kuu la Harare.

Tukio hilo lilishuhudiwa na wafungwa wengine, Tinashe Muyambo na Antony Chambarambanda, ambao walidai kumwona Mugede akiingia bafuni na kushuhudia kumfanyia mfungwa mwenzao kitendo hicho, Hatimaye, taarifa iliripotiwa kwa afisa wa gereza na polisi.

Aidha, Hakimu Letwin Rwodzia amemuongezea hukumu Emmanuel, huku akisisitiza kuwa mashambulizi ya kijinsia yenye ukatili hayakubaliki hata ikiwa ni gerezani.

Zaidi https://jamii.app/KubakaGerezani

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #CivilRights
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la JF Chit-Chats and Jokes anauliza umewahi kusahau kitu nyumbani kikakulazimisha kurudi haraka, kwa sababu bila hicho huwezi kuendelea na kazi zako ofisini au katika shughuli zako nyingine?

Ni kitu gani hicho bila kuwa nacho huwezi kufanya kazi zako kwa amani?

Zaidi https://jamii.app/NyumbaniKitu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats #JFUtani
Serikali ya Nigeria imewafukuza raia wa kigeni wakiwemo Wachina 50 baada ya msako mkali uliofanyika Jijini Lagos, ambapo jumla ya raia wa kigeni 192 walikamatwa huku 148 wakiwa ni raia wa China wakihusishwa na makosa ya udanganyifu na uwizi Mtandaoni.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Ufisadi nchini humo (EFCC) imeeleza tangu operesheni hiyo ilipoanza Agosti 15, 2025 jumla ya Wageni 102 wameshafukuzwa ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali ya Nigeria wa kukomesha uhalifu wa kimtandao.

Kulingana na takwimu za Mwaka 2024 za Chuo cha Oxford, Nigeria iko kwenye orodha ya nchi 5 zinazoongoza kwa uhalifu Mtandaoni, ikizidiwa na Urusi, Ukraine, Marekani na China.

Zaidi https://jamii.app/WachinaNigeria

#JamiiForums #JamiiAfrica #CyberCrimes #DigitalFrauds
3
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa imetangaza mabadiliko katika safu yake ya Uongozi, ambapo imemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Amos Makalla ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Aidha, Dkt. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM akichukua nafasi ya Dkt. Emmanuel John Nchimbi ambaye chama kimempitisha kuwa Mgombea Mwenza wa Dkt. Samia Suluhu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Soma Zaidi: https://jamii.app/MigiroKatibuCCM

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uteuzi #Siasa
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Taifa, imemteua Tauhida Gallos kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Tauhida aliingia bungeni akiwa Ubunge wa Viti Maalum Mwaka 2020 akiwakilisha Mkoa wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar.

Zaidi Soma https://jamii.app/MigiroKatibuCCM

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uteuzi #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Nape Nnauye alipokuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati akizungumza na Wananchi Julai, 2024 katika Soko la Kashai Mjini Bukoba alisema aliyekuwa Mbunge Stephen Byabato atashinda uchaguzi ujao, akibainisha matokeo ya kura si lazima yatokane na yaliyomo kwenye maboksi ya kura bali yanategemea anayehesabu na kutangaza.

Nape kwa sasa ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama ambapo atawania nafasi hiyo kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

Soma https://jamii.app/NapeUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #JFDemocracy #Demokrasia
Mdau, umepata funzo gani kupitia picha hii?

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning
1
GUINEA: Serikali ya kijeshi nchini imesitisha kwa miezi mitatu shughuli za vyama vitatu vikubwa vya Siasa, ikiwemo chama cha Rais wa zamani Alpha Condé (RPG), Union of Democratic Forces kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Cellou Dalein Diallo na chama cha Renewal and Progress. Hatua hii imechukuliwa wakati Taifa hilo linajiandaa kwa Kura ya Maoni ya Katiba Septemba 21, 2025.

Wapinzani na Asasi za Kiraia pamoja wametangaza maandamano makubwa kuanzia Septemba 5, 2025 kupinga kile wanachokiita jaribio la kunyakua madaraka. Tangu Doumbouya achukue madaraka Mwaka 2021 kupitia mapinduzi, maandamano yamepigwa marufuku na viongozi wa upinzani wengi wamewekwa kizuizini au kulazimishwa uhamishoni.

Mashirika ya kimataifa ya kutetea Haki za Binadamu yameilaani Guinea kwa hatua hizi, yakionya #Demokrasia changa ya Taifa hilo ipo hatarini.

Zaidi soma https://jamii.app/Guinea

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #JFAfricanPolitics