JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amependekeza kupunguza ada ya usajili wa pikipiki za biashara kutoka Tsh. 340,000 hadi Tsh. 170,000 kwa miaka mitatu, huku akisema ada hiyo husika italipwa wakati wa usajili wa awali pekee

Vile vile amependekeza kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, bajaji na guta kutoka Tsh. 70,000 hadi Tsh. 30,000

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Kukosea siyo tu jambo la kawaida, bali pia ni muhimu sana kwa ukuaji na kujifunza.

Tunajifunza kutokana na makosa yetu, tunaboresha ujuzi wetu na tunakuwa watu wenye Hekima zaidi.

Makosa yanatuonesha pale tulipofanya vibaya na kutupa fursa ya kurekebisha na kusonga mbele.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DIPLOMASIA: #Israel imefanya mashambulizi Nchini #Iran katika Mji wa #Tehran ikiwa ni sehemu ya Oparesheni kwa kile ambacho Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema walilenga kudhoofisha Miundombinu ya Nyuklia ya Iran na Viwanda vya Makombora ya masafa marefu

Pamoja na hivyo, Israel imetangaza hali ya hatari, ikisema inatarajia mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa Iran, wakati ambapo Iran imesema mashambulizi hayo yameathiri Makazi ya raia na kuua Watu kadhaa wakiwemo Watoto

Wakati huohuo, Rais wa Marekani, #DonaldTrump amekiambia Kituo cha #FoxNews kuwa alikuwa na taarifa kuhusu mashambulizi hayo kabla lakini Nchi yake haikuhusika kwa namna yoyote

Soma https://jamii.app/IsraelAgainstIran

#Diplomacy #Governance #HumanRights #JamiiForums #JamiiAfrica
UTEUZI: Rais Samia amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika Juni 15, 2025 Ikulu, Chamwino - Dodoma, Saa 4.00 Asubuhi

Soma https://jamii.app/UteuziGeorgeMcheche

#Uteuzi #JamiiForums #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mifumo ya Hali ya Hewa haioneshi uwepo wa mvua hivi karibuni hapa nchini badala yake kutakuwa na ukavu na ubaridi ambapo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za kujilinda na baridi

Meneja wa Utabiri wa TMA, Dkt. Mafuru Kantamla amesema mvua zilizonyesha hivi karibuni Ukanda wa Pwani zimetokana na ongezeko la Joto katika Bahari ya Hindi hususan katika Mwambao wa Pwani lakini hazitakuwa na mwendelezo kwa kuwa joto la Bahari limeanza kupungua kwa kasi

Soma https://jamii.app/HaliYaHewaJuni

Video Credits: Torch Media

#ClimateChange #JamiiForums #JamiiAfrica
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mdau wa JamiiForums.com anaeleza kuwa Daraja lililopo Kata ya Mkonze, Mtaa wa Muungano linalounganisha Mtaa wa Muungano na Goba limeharibika na halijafanyiwa maboresho kwa muda mrefu

Anadai vyombo vyote vya usafiri na wanaotembea kwa miguu wanalazimika kupita pembeni kwa kuwa eneo la katikati halipitiki

Anaongeza kuwa ikinyesha mvua ukiwa upande mmoja kati ya maeneo hayo lazima usubiri mpaka maji yapungue ndio uvuke, anatoa wito kuwa Daraja liboreshwe kwa kuwa hali ilivyo ni mateso kwa wapitaji wa hapo

Soma https://jamii.app/DarajaLaMuunganoGoba

#JamiiForums #Accountability #Miundombinu
KENYA: Maafisa Polisi wamemkamata Askari anayefahamika James Mukhwana kwa kuhusika na mauaji ya cha mwalimu na mwanablogu, Albert Omondi Ojwang' aliyefariki akiwa kizuizini baada ya kushikiliwa kwa kuchapisha taarifa za uongo

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi imesema kuwa Askari James wa Kituo cha Polisi cha Kati Nairobi alikamatwa Juni 12, 2025 na kuwekwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Capitol Hill na anatarajiwa kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya Ojwang'

Ikumbukwe Albert Ojwang' (Mwanaharakati na Mwanamtandao) alifariki Dunia Juni 8, 2025, Siku moja baada ya kukamatwa Nyumbani kwake Kakot, Homa Bay, akiwa chini ya uchunguzi kuhusu chapisho alilodaiwa kumdhalilisha Naibu Mkuu wa Polisi kwenye Mtandao wa Kijamii wa X

Soma https://jamii.app/AskariJamesKifoOjwang

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
DAR: Klabu ya #Simba imesema Serikali imeruhusu watumie Uwanja wa Mkapa kufanya mazoezi Juni 14, 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya #Yanga unaoratajiwa kuchezwa Juni 15, 2025

Barua hiyo imeeleza kuwa uwanja upo tayari kwa mchezo na wameruhusiwa kwa mujibu wa Kanuni kwa kuwa Simba itakuwa ugenini katika mchezo huo ambao Yanga imekuwa ikisisitiza haitaingiza timu uwanjani

Barua imeandikwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Boniface Tamba kwenda kwa Simba na nakala kwa Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu

Soma https://jamii.app/SimbaMazoezi

#JFSports #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Mdau anadai changamoto ya foleni ya magari ya mizigo mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma ni kero kubwa, inakwamisha Uchumi wa Watu wengi na kuwafaidisha wachache

Anadai kuna Kiongozi wa Usalama hapo anamiliki eneo la kuegesha (parking) anatoza Sh 10,000 kwa siku badala ya Tsh. 5,000 inayotozwa kwingine na kwamba Mwanausalama huyo anatoa kipaumbele kwa Wateja wake kuvusha magari huku wengine wakibaki kucheleweshewa mchakato

Pia, Mdau anadai hali ya Watumishi kukosa uadilifu inachangia foleni kwa kuwa michakato inafanyika kwa kasi ndogo kwa baadhi ya Maafisa kujali maslahi binafsi

Ikumbukwe, Aprili 2025, Mkuu wa Mkoa, Daniel Chongolo aliunda Kamati Maalumu kuchunguza msongamano huo ambapo baadhi ya Wadau walimwambia inatengenezwa na Watu wachache kwa sababu wanazozijua wao

Soma https://jamii.app/TundumaFoleniJuni

Video Credits: CHAWAMATA TV

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability
SIMIYU: Mdau anakumbushia kuwa Machi 2021, Waziri wa Nishati (wakati huo), Dkt. Medard Kalemani alishiriki kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo, ambapo shamrashamra zilikuwa kubwa na kuwapa matumaini makubwa Wananchi

Mdau anasema Kalemani alieleza Kituo kitajengwa ndani ya Mwaka mmoja kwa gharama ya Tsh. Bilioni 75, anamnukuu "Umeme utakaozalishwa hapa ni mkubwa utauwezesha mkoa huu na mikoa jirani kuendesha shughuli za viwanda na uwekezaji unaohitaji umeme mwingi."

Hivyo, Mdau anadai kilichotokea mradi haujakamilika na hakuna majibu ya kueleweka kutoka kwa Mamlaka na kwamba changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara bado ipo kwa kuwa kituo hicho kilitegemewa kutatua changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/UmemeSimiyu

#JamiiForums #Accountability #Governance