JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#MAISHA: Unampa Ushauri gani Mdau huyu wa JamiiForums.com ili aweze kuyashinda Mawazo ya kuona anaelekea kufeli Maisha

Mjadala zaidi https://jamii.app/KutoboaMshaharaSerikali

#JamiiForums #LifeLessons #JFStories #JFChitChats #JamiiAfrica
👍1
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com anasema Watoto wengi ambao walijuana na Wazazi wao ukubwani/kulelewa na Mzazi mmoja huwa na maswali mengi ambayo wengi hawayaulizi, huku Wazazi nao wakiwa na maelezo mengi sana ya nini kilitokea, lakini hawajui waanzie wapi kuwaeleza Watoto

Soma zaidi Mjadala huu https://jamii.app/WazaziMsamahaWatoto

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFStories #JFChitChats #LifeLessons
Ikiwa unashiriki Mazungumzo na Watu wanaopiga Majungu dhidi ya wengine, ni ishara kwamba hata wewe hutahifadhiwa pindi utakapoondoka.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifelessons #Maisha #AmkaNaJF #GoodMorning
Katika dunia yenye maneno mengi na vitendo vichache, uaminifu umekuwa rasilimali adimu. Si kila anayesema ukweli anaishi kwa ukweli na si kila anayeahidi ana nia ya kutimiza.

Uaminifu wa kweli huonekana pale mtu anapochagua kuwa mwaminifu hata kama hakuna anayemuangalia, anapotimiza wajibu wake bila kulazimishwa na anaposhikilia ahadi zake hata kama ni vigumu

Tunapokaribisha mapumziko ya Mwisho wa wiki tujiulize; Je, tunaishi yale tunayoyasema?

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #Lifelessons
👍1
Kujisamehe na kusamehe wengine ni hatua muhimu ya kujikomboa kutoka katika maumivu ya zamani

Kujisamehe ni kujipa nafasi ya kukua na kujifunza, bila kujihukumu milele, huku kusamehe wengine kukituondolea mzigo wa chuki na machungu

Msamaha hauhalalishi makosa, bali huleta uhuru wa ndani na kutupa amani ya kweli. Kuanzia leo tujifunze kusema "Nimesamehe na najisamehe pia"

Jumapili Njema!

#GoodMorning #AmkaNaJF #Maisha #LifeLessons #Lifelessons
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com anasema alipomaliza Darasa la saba alipewa kazi ya kupanda miti kwenye shamba la Ekari moja alilonunua Baba yake mpaka muda wa kwenda Kidato cha 1 ulipofika

Pia, alipomaliza Kidato cha 4 alikabidhiwa Shamba la Vitunguu kuanzia kuandaa Shamba hadi kuvuna kipindi cha likizo ya kusubiri Kidato cha 5

Mafunzo yote hayo aliyopitishwa na Wazazi wake anasema yamemjengea Kujiamini na kuw na Ujuzi wa kufanya vizuri kwenye Ajira aliyojiajiri na kuweza kuwasimamia aliowaajiri.

Soma zaidi https://jamii.app/MtotoKufanikiwaMalezi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeLessons #Parenting
1
Unapochagua eneo moja na kuwekeza Muda, Nguvu na Akili zako zote, unajitengenezea nafasi kubwa ya kuwa Mbobezi wa kile unachokifanya (mastery)

Hii inakuwezesha kufanya kwa ubora zaidi, kukua kwa kasi na hatimaye kufikia mafanikio makubwa, ambayo usingeweza kuyafikia kwasababu kugusagusa kila kitu kwa uchache.

JamiiAfrica inakutakia Mapumziko mema ya mwisho wa Wiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend #GoodMorning #AmkaNaJF #Lifelessons
Katika Maisha, mara nyingi wale wanaofanya mabaya huendelea kwa Amani kana kwamba hawaguswi, ilhali wale wanaojitahidi kuwa Waaminifu na Waadilifu hupitia maumivu na changamoto nyingi kama misumari inayogongwa kila mara. Ukweli huu unauma, lakini mara nyingi ndivyo ilivyo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend #GoodMorning #AmkaNaJF #Lifelessons
1👍1
Mdau wa JamiiForums.com ameshauri tuache kulalamika pale ambapo marafiki wakitutenga au wakibadilika kwani kuna sababu zinazofanya marafiki kuja na kuondoka katika maisha

Unakubaliana na hoja ya Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UsiogopeKupotezaMarafiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle #Lifelessons
2🔥1
Kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, Mwanachama anasema baadhi ya Wafanyakazi wenzake ambao ni 'wakongwe' hapo Ofisini wamemchukia na hata hawamsalimii baada ya kugundua analipwa Mshahara mkubwa zaidi yao wakati yeye ni Mfanyakazi mpya

Je, nawe umeshawahi kupitia changamoto hii, ulifanyaje?

Tembelea mjadala huu zaidi https://jamii.app/MshaharaKuchukiwaKazini

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons