JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila ametoa kiasi cha Tsh. 20 Milioni na Viwanja viwili Kigamboni kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (#TaifaStars) ikiwa ni sehemu ya motisha kuelekea mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Morocco katika Michuano ya CHAN, unaotarajiwa kuchezwa leo Agosti 22, 2025, kuanzia Saa 2:00 Usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

RC Chalamila amesema fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji bila kujali matokeo ya mchezo huo.

Zaidi soma https://jamii.app/ChalamilaAmwagaPesa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
1
Mwanamitindo na Mtangazaji, Ney Paul ameshauri Vijana kufikiria kabla ya 'kuposti' kauli za Chuki Mtandaoni kwa kujiuliza kama wanajenga au wanabomoa wangejisikiaje iwapo Mtu mwingine angetumia kauli hiyo kwao.

Amesema “Epuka jazba, Usijibu kwa hasira Chukua muda kupumua na kufikiri kabla ya kujibu maoni au jumbe zinazokukasirisha”.

Aidha, amesema Mitandao imebeba fursa nyingi na fedha nyingi, hivyo ni vizuri kama Vijana wataamua kuitumia vizuri.

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
KENYA: Safari ya Timu ya Taifa ya #Kenya imekwama kuingia Nusu Fainali ya Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (#CHAN) baada ya kufungwa na Madagascar kwa penati 4-3, muda mfupi baada ya matokeo ya sare ya Goli 1-1 katika dakika 120.

Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Moi International Sports Centre Jijini Nairobi leo Agosti 22, 2025.

Michezo ya Robo Fainali ya Agosti 23, 2025 itakuwa ni Uganda dhidi ya Senegal (Uwanja wa Mandela National, Kampala), Sudan wakikipiga na Algeria (Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

https://jamii.app/CHANRobo

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #CHAN2024
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (#JAB), Wakili Patrick Kipangula ametoa angalizo kwa Waandishi wa Habari wasiokuwa na ithibati, kuwa hawataruhusiwa kuripoti Uchaguzi Mkuu 2025.

Amefafanua kuwa Mwandishi kufanya kazi bila kitambulisho cha Bodi ya Ithibati ni kosa linaloweza kusababisha faini ya hadi Tsh. Milioni 5 au kifungo cha miaka mitatu hadi mitano. Ameeleza hayo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki, Agosti 21, 2025.

Zaidi soma https://jamii.app/JABWaandishiUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #JFSiasa
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika maombi ya Novena Takatifu yanayoratibiwa na Kanisa Katoliki kufikia kilele cha maombi hayo Agosti 23, 2025, kwa ajili ya kuliombea taifa amani, haki na mshikamano wa kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho , John Heche amesisitiza umuhimu wa maombi hayo akisema: “Ninawasihi tuliombee taifa letu liwekwe mikononi mwa Mungu, tukimwomba atujalie hekima, ujasiri wa kudai haki, na mabadiliko ya msingi kwa mustakabali wa taifa letu. Pia tuliombee amani ya kweli itakayojengwa juu ya haki na umoja wa wananchi bila kujali dini au itikadi.”

Ikumbukwe, Juni 19, 2025, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (#TEC) lilitangaza maombi ya kitaifa na mfungo kuombea haki na amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Zaidi soma https://jamii.app/KatolikiChademaMaombi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #UchaguziMkuu2025
1
DAR: Timu ya Taifa ya Tanzania (#TaifaStars) imeondolewa katika Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (#CHAN2024) kwa kufungwa Goli 1-0 dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Mkapa, mfungaji akiwa ni Oussama Lamlioui.

Hivyo, Morocco inatarajiwa kucheza na timu itakayoshinda kati ya Uganda dhidi ya Senegal. Wakati huohuo Madagascar ambayo imeiondoa Kenya, yenyewe itacheza na mshindi wa mchezo wa Sudan dhidi ya Algeria.

Michezo mingine ya Robo Fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 23, 2025, itakuwa ni Uganda Vs Senegal (Uwanja wa Mandela National, Kampala), Sudan Vs Algeria (Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

Zaidi soma https://jamii.app/CHANRobo

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #CHAN2024
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JF KUMBUKIZI: Akizungumza siku ya Mei Mosi, 1995, katika hotuba yake Mwl. Julius Kambarage #Nyerere alisema kuwa mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, ukayakubali, anakudharau.

"Na wewe una akili, anajua unajua kwamba ni ya kipumbavu, ukayakubali, anakudharau."

Zaidi Soma https://jamii.app/MawazoKipumbavu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Siasa #JFKumbukizi #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning
5
Serikali ya Uganda imethibitisha kuwa imeingia makubaliano na Marekani yatakayohusisha Wahamiaji kutoka Marekani kupokelewa nchini humo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa #DonaldTrump unaolenga kuwarudisha maelfu ya Wahamiaji walioko katika hifadhi za Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema wapo tayari kupokea Wahamiaji hao na kudokeza kuwa itawapa kipaumbele zaidi wale ambao wana asili ya Kiafrika na ambao hawana rekodi yoyote ya Uhalifu.

Kando na Uganda nchi nyingine kutoka Afrika ambazo zimekubali kupokea wahamiaji kutokea Marekani ni Eswatini, Rwanda pamoja na Sudan ya Kusini.

Zaidi Soma: https://jamii.app/WahamiajiUganda

#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Utawala
2
KIGOMA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa imewahukumu kifungo cha Miaka 22 jela aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Athuman Msabila pamoja na Watumishi wenzake watatu baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi nyaraka na utakatishaji fedha.

Msabila na Salum Juma wamehukumiwa Miaka 20 kwa utakatishaji fedha na Miaka miwili kwa kughushi nyaraka, huku Ferdinand Filimbi na Frank Nguvumali wakihukumiwa miaka miwili kwa kosa la kughushi nyaraka.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa, Misana Majula katika kesi ya Jinai Namba 5546 ya Mwaka 2024 iliyowakabili Watumishi 11 wa Serikali.

Zaidi Soma https://jamii.app/KigomaJela

#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Sheria #Uwajibikaji
ZIMBABWE: Mfungwa anayefahamika kwa jina la Emmanuel Mugede, ambaye tayari alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 14 kwa ubakaji wa mtoto, amehukumiwa miaka 20 zaidi gerezani kwa kumlawiti mfungwa mwenzake mwenye umri wa miaka 24 Julai 23, 2025 katika gereza kuu la Harare.

Tukio hilo lilishuhudiwa na wafungwa wengine, Tinashe Muyambo na Antony Chambarambanda, ambao walidai kumwona Mugede akiingia bafuni na kushuhudia kumfanyia mfungwa mwenzao kitendo hicho, Hatimaye, taarifa iliripotiwa kwa afisa wa gereza na polisi.

Aidha, Hakimu Letwin Rwodzia amemuongezea hukumu Emmanuel, huku akisisitiza kuwa mashambulizi ya kijinsia yenye ukatili hayakubaliki hata ikiwa ni gerezani.

Zaidi https://jamii.app/KubakaGerezani

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #CivilRights