JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Kuna wakati unaweza kujikuta umetembea umbali mrefu kwa miguu, ama kwa hiyari yako au kutokana na mazingira uliyokuwa nayo wakati husika kukulazimisha ufanye hivyo, je, imewahi kukutokea na ilikuwaje?

Soma https://jamii.app/KutembeaDar

#JamiiForums #JFChitChats
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA – Taifa, Tundu Lissu amefikishwa Mahakama ya Mkazi Kisutu, leo Mei 19, 2025 kwa ajili ya kesi kusikiliza kesi mbili zinazomkabili ambapo viongozi kadhaa wa chama hicho nao wamefika kufuatilia

Ikumbukwe Mei 6, 2025 mchakato wa kesi hiyo uliendeshwa kwa njia ya Mtandao ambapo Mahakama ilitoa uamuzi wa kesi hiyo kusikilizwa leo na kuruhusu Wananchi kuhudhuria

Aidha, Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, Willy Mutunga na baadhi ya Waandishi wa Habari na Wanasiasa kutoka Kenya waliosafiri kufuatilia kesi hii inadaiwa wameshikiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu Saa 9 Usiku

Zaidi https://jamii.app/KesiYaLissuLeo

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
2
DAR: Wananchi wamejitokeza kwa wingi leo Mei 19, 2025 katika Mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu

Ulinzi umeimarishwa Mahakamani hapo ambapo kuna idadi kubwa ya Askari Polisi na Askari wa Jeshi la Magereza

Awali, kesi hiyo iliendeshwa kwa njia ya Mtandao, Mei 6, 2025 Mahakama iliruhusu Umma kuhudhuria kesi hiyo ambapo Lissu anakabiliwa na tuhuma za Uhaini na Kutoa Taarifa za Uongo

Soma https://jamii.app/KesiYaLissuLeo

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #CitizenParticipation #Transparency
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu alivyowasili ndani ya Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kuanzia kusikiliza kesi zinazomkabili, leo Mei 19, 2025

Soma https://jamii.app/KinachojiriKesiLissu

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
🔥2👎1
DAR: Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauri la kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Wakili Tundu Lissu haujakamilika hivyo kuomba kesi hiyo ihairishwe hadi Juni 02, 2025

Aidha, Jopo la Mawakili wa utetezi likiongozwa na Mawakili Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala na Peter waliwasilisha maombi Mahakamani ikiwemo kuomba Mahakama 'kulazimisha' upande wa Jamhuri ueleze nini hasa kinachokwamisha upelelezi kwa sababu mwanzo ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa ushahidi wote kuhusiana na shauri hilo upo mtandaoni

Mawakili wa Serikali upande wa Jamhuri wamejibu kuwa hakuna sehemu yoyote ya Kisheria na Kikatiba inayowalazimisha kueleza hatua ya upelelezi waliyofikiwa na kwamba mambo ya upelelezi sio ya kuwekwa hadharani

Soma https://jamii.app/KesiLissuKusogezwa

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
2👏1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Jopo la Mawakili wa utetezi likiongozwa na Mawakili Waandamizi Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala na Peter Kibatala wamewasilisha ombi Mahakamani kutoa amri ya kuwaondoa Askari wote 'wanaomlinda' mteja wao, Tundu Lissu ndani ya chumba cha Mahakama

Mawakili hao wamedai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Mahakama haimtambui mtuhumiwa kama 'mkosaji' na kwamba kitendo cha mteja wao kuzungukwa na Askari wengi hakikubaliki

Aidha, upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa licha ya kwamba Katiba imeeleza hivyo lakini haijatoa maelekezo ya aina gani ya ulinzi unahitajika kwa mtuhumiwa na kwamba ikiwezekana wanaomba ulinzi huo uongezwe kwani suala la ulinzi lina faida kwa mtuhumiwa mwenyewe, Mahakama na Maafisa wa Mahakama kwa ujumla

Soma https://jamii.app/KesiLissuKusogezwa

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
1
Kitambulisho chako (ID) kinachukuliwa kuwa Taarifa Binafsi kwasababu kina taarifa zako kama Jina, Nambari ya Utambulisho, Picha, Tarehe ya Kuzaliwa, n.k.

Unamshauri Mdau afanye nini hapo?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MkopoSimuKitambulisho

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #PersonalDataProtection #DataPrivacy
DAR: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Devotha Minja, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila, Salum Mwalimu na Makada wengine waliotangaza kujiondoa CHADEMA wameonekana wakishiriki kwenye shughuli za Chama cha Ukombozi wa Umma (#CHAUMMA)

Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip, panakofanyika Mkutano Mkuu wa CHAUMMA, leo Mei 19, 2025

Zaidi https://jamii.app/G55WatuaCHAUMMA

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #Governance
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanachama wa JamiiForums.com anasema Magari makubwa ya Mizigo kuruhusiwa kupita katika Barabara za Juu (Flyovers) inaweza kuleta Changamoto pale itakapotokea hitilafu kwenye Gari hilo na Madhara yanaweza kuwa makubwa

Anahoji je, tunasubiri Madhara yatokee ili tuunde Kamati?

Soma https://jamii.app/BarabaraZaJuu

#Accountability #JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #JFMdau2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Rais Samia amesema "Nimeona mtiririko wa Wanaharakati katika Ukanda wetu huu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu. Sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku"

Ameyasema hayo leo Mei 19, 2025 katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam.

Soma https://jamii.app/WanaharakatiKudhibitiwa

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Diplomasia