JamiiForums
56.2K subscribers
32.9K photos
1.87K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
#KENYA: Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (KCCB) limeikosoa Serikali ya Rais #WilliamRuto kwa kushindwa kutimiza ahadi zake kwa Wakenya na kudumisha Utamaduni wa uongo na kutumia Mitambo ya Serikali kunyamazisha Wapinzani

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Askofu Maurice Muhatia amewashutumu Viongozi wa Serikali kwa kushindwa kutimiza ahadi walizoahidi wakati wa Uchaguzi, kutojali kilio cha Wananchi na kurudisha nyuma Mafanikio ya Kidemokrasia ya Kenya

Askofu Muhatia amesema "Utamaduni wa Uongo unabadilisha kwa haraka Uadilifu na Heshima wanayostahili Wakenya. Kwa kifupi, inaonekana kuwa ukweli haupo, na kama upo, ni ule tu ambao Serikali inasema"

Soma https://jamii.app/RutoUtamaduniUongoUkome

#JamiiForums #KenyanPolitics #Accountability #Governance #HumanRights
#INDIA: Wabunge wa Upinzani wamewasilisha Hoja ya kulitaka Bunge liishinikize Serikali kuchunguza Kashfa za #Rushwa zinazoibuliwa dhidi ya Mfanyabiashara Gautam Adani, mmiliki wa Adani Group

Hoja hiyo imeripotiwa kusababisha mvutano kiasi cha shughuli za Bunge kusitishwa kwa muda, ingawa Chama Tawala kimeendelea kutounga mkono hoja hiyo. Upinzani unashinikiza kampuni za Adani zinazofanya Uwekezaji katika Kilimo, Nishati, Makaa ya Mawe na Miundombinu zichunguzwe

Hivi karibuni, Serikali ya #Kenya ilisitisha mkataba wa Uendelezaji na Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta kati yake na moja ya kampuni za Adani kutokana na shinikizo la Wananchi na Wafanyakazi wa Uwanja huo

Novemba 27, 2024, Mtandao wa Reuters uliripoti kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Plasduce Mbossa, imesema itaendelea na Mkataba wake na Adani kwakuwa wao hawana tatizo na kampuni hiyo.

Soma https://jamii.app/AdaniScandals

#JamiiForums #Governance #Accountability #Transparency #Economy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Rais #WilliamRuto amesema Nchi yake imeachwa nyuma katika masuala ya Mwingiliano wa Biashara za Ukanda baada kupitwa na #Tanzania kwenye Huduma za Biashara za Uagizaji, Uingizaji bidhaa kwa Nchi za Afrika Mashariki

Akizungumza katika Maadhimisho ya 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jijini Arusha, Ruto amesema "Naipongeza Tanzania kwa kuipita #Kenya katika Huduma za Biashara ya Bidhaa ambazo tunanunua na kuuza Afrika Mashariki. Kenya ilikuwa nchi inayoongoza eneo hili, sasa Tanzania imeipita Kenya."

Taarifa ya Benki Kuu ya Uganda imeeleza hadi Novemba 2024, Tanzania iliipita Kenya na kuwa chanzo kikuu cha bidhaa zinazoagizwa na Uganda Barani Afrika, Mwaka ulioishia Juni 2024, Tanzania ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya Tsh. Trilioni 10.98 kwenda #Uganda, ikichangia 42.56% ya bidhaa zote zilizoagizwa kutoka Afrika huku Kenya ikichangia 19.55%

Soma https://jamii.app/KenyaLaggs

#JamiiForums #Governance #Accountability #AfricanEconomy
UCHUMI: Ripoti ya Makadirio ya Ukuaji wa Uchumi ya Benki ya Dunia (WB) imeonesha Uchumi wa #Kenya utashuka kutoka 5.0% ya makadirio ya awali hadi 4.7% huku Mafuriko, Maandamano dhidi ya Serikali na Juhudi hasi za Uimarishaji wa Uchumi vikitajwa kuathiri ukuaji huo

Pia, ripoti imeonesha Kenya bado inakabiliwa na hatari kubwa ya kuelemewa na mzigo wa Madeni huku Deni la Serikali likizidi kuwa dhaifu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama za kulipa deni hilo pamoja na kukosa malengo ya mapato

Aidha, WB imeitaka Serikali kukabiliana na hali ya kukosekana kwa usawa wa Kimuundo ambayo imetajwa kuwa chanzo cha kufifisha malengo ya ukuaji endelevu na shirikishi wa Uchumi.

Soma https://jamii.app/WBKenya

#JamiiForums #Governance #AfricanEconomy #Accountability
#KENYA: Wadau mbalimbali wa masuala ya Haki za Binadamu wakiwemo Wanasiasa wametoa wito kwa Rais #WilliamRuto kukemea na kukomesha Vitendo vya Utekaji wa Wananchi wengi wakiwa ni wakosoaji wa Serikali yake

Miongoni mwa waliotoa wito huo ni pamoja na Mahakama, Wanasiasa Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Chama cha Wanasheria (LSK), Naibu Rais aliyeondolewa Madarakani, Righathi Gachagua, Vyama vya ODM, Wiper, DAP-K na baadhi ya Maseneta

KNCHR imehusisha matukio ya Utekaji na Maandamano yaliyofanyika Miezi michache iliyopita ya Vijana Wadogo (Gen Z) dhidi ya Serikali ya Rais Ruto ambapo wengi kati ya walioripotiwa Kutekwa walikuwa wakipinga utawala wa Ruto kupitia Mitandao ya Kijamii

Wakati hali ikiwa hivyo Nchini Kenya, Agosti 9, 2024 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu kuongezeka kwa Vitendo vya Utekaji na Watu kupotea Nchini Tanzania ambapo ripoti hiyo ilionesha Watu 83 Walitekwa.

Soma https://jamii.app/UtekajiKE

#JamiiForums #Governance #HumanRights #SayNoToAbductions
#KENYA: Maandamano ya Kupinga vitendo vya Utekaji yaliyoitishwa na Wanaharakati wa Haki za Binadamu na Ndugu na Jamaa wa Watu walioripotiwa kutoweka katika Mazingira yenye utata, yameanza leo licha ya Jeshi la Polisi kuyaita ni haramu

Hatua hiyo inafuatia kupita Saa 48 za wito wa kuachiwa huru kwa Watu waliotekwa, muda uliotolewa na Wanaharakati kwenda kwa Mamlaka zinazotuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo, wakiwemo Maafisa wa Idara za Ulinzi na Usalama wa Serikali

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa Mitandao Desemba 29, 2024, Waitishaji wa Maandamano hayo wamesema wataendelea kuandamana bila kukoma hadi pale ndugu zao watakapoachiwa na hawajali itachukua siku ngapi.

Soma https://jamii.app/KenyaUtekaji

#JamiiForums #Governance #HumanRights #Accountability #EndAbductionsKE
#KENYA: Jeshi la Polisi limeagizwa kuwaachia huru au kuwafikisha Mahakamani leo Desemba 31, 2024 Watu 6 wanaodaiwa kutekwa na kushikiliwa na Polisi pamoja na Vyombo vingine vya Usalama kinyume na Sheria

Jaji Bahati Mwamuyé ametoa amri hiyo (Habeas Corpus) inayotaka Walalamikaji hao kufikishwa Mahakamani kwa lazima leo isipokuwa tu kama Mamlaka zinazowashikilia zitatoa sababu halali ya kuzuiliwa kwao

Matukio ya Utekaji na Watu Kupotea yameibua Maandamano ya Watetezi wa Haki za Binadamu na Wanaharakati wanaoitaka Serikali kueleza ni wapi walipo ndugu na jamaa takriban 29 ambao hawajulikani walipo hadi sasa.

Soma https://jamii.app/HighCourtKE

#JamiiForums #Governance #HumanRights #EndAbductionsKE #Accountability
#KENYA: Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni, Kimani Ichung'wah, amemtuhumu aliyekuwa Naibu Rais, #RigathiGachagua kufadhili vitendo vya Utekaji na Mauaji Nchini humo kwa lengo la kuichafua Serikali ya Rais Ruto

Ichung'wah amesema "Yule aliyekuwa Kiongozi wa Siasa za ukabila, Naibu Rais aliyepita, alikuwa akifadhili utekaji ili lawama zimwendee #WilliamRuto. Tunawajua na tunawaona mchana na tutawatangaza mchana hadharani.”

Awali, Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, akizungumza katika mazishi ya Mama Mzazi wa Spika wa Bunge, Moses Wetangula, alitoa wito kwa Serikali kukomesha matukio ya Utekaji, hoja inayodaiwa kuibua hisia kali kutoka kwa Wabunge wanaomteta Rais Ruto.

Soma https://jamii.app/GachaguaUtekaji

#JamiiForums #HumanRights #Governance #Accountability
Barua ya Babu Owino kwa Rais Samia imedai alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Maafisa wa Uhamiaji walimzuia na kumjulisha hataruhusiwa kuingia nchini

Anasema hatua hiyo inakiuka haki yake ya kusafiri kama raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mwakilishi wa Bunge la #Kenya, ambalo pia linawakilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

Zaidi https://jamii.app/BabuOwinoTanzania

#JamiiForums #Diplomacy #Accountability #Governance
Viongozi wa Nchi ambao wamekuwa wakirushiana maneno hivi karibuni, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame wanatarajiwa kukutana Dar es Salaam, mnamo Februari 8, 2025 kujadili kuhusu mgogoro unaoendelea Nchini DRC

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa #Kenya, #WilliamRuto ametoa taarifa kuwa mkutano huo utahusisha Viongozi wa Nchi za EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Ruto amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo na kuwa Viongozi hao wa DRC na Rwanda ni miongoni mwa waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo utakaotanguliwa na mkutano wa Mawaziri Ijumaa, Februari 7, 2025

Soma https://jamii.app/MeetingInDar

#JFDiplomacy #JamiiForums
KENYA: Ripoti ya Wizara ya Afya kwa ushirikiano wa African Population and Health Research Centre (APHRC) na Taasisi ya Guttmacher imeeleza kuwa kati ya Aprili 2023 na Mei 2024, zaidi ya visa 792,000 vya utoaji mimba vimeripotiwa Nchini #Kenya

Ripoti imeeleza namba hiyo ni sawa na wastani wa visa 57.3 kati ya Wanawake 1,000 wenye umri wa miaka 15 – 49, na Asilimia 80 ya wanaofanya hivyo wapo kwenye ndoa

Mtafiti Mkuu wa Guttmacher, Margaret Giorgio amesema “Wanaotoa wanafanya hivyo kwa kuwa hawajajiandaa kuwa wazazi, pia wengine ambao tayari wameshakuwa na Watoto wanachukua hatua hiyo kutokana na kuhofia gharama za maisha kuwa kubwa.”

Soma https://jamii.app/AbortionsKenya

#PublicHealth #JamiiForums #PublicHealth