JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Kesi Namba 993/2025 inayomkabili Mwanasiasa mkongwe, Dkt. Willbroad Slaa (76), inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, imeahirishwa mpaka Februari 18, 2025 ambapo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi umekamilika

Dkt. Slaa anakabiliwa na tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye Mtandao wa X ambapo inadaiwa ametenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya Mwaka 2015.

Ikumbukwe, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) amekata rufaa katika Mahakama ya Rufani, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ulioelekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya Dkt. Slaa na kuangalia uhalali wa kesi ya jinai inayomkabili kwa haraka

Soma https://jamii.app/SlaaFeb6

#JFMatukio #JamiiForums
Idadi ya Utumiaji wa Intaneti imeongezeka kwa 16% kutoka Milioni 41.4 kwa robo mwaka iliyoishia Septemba 2024 hadi Milioni 48 kwa robo ya mwaka iliyoishia Desemba 2024.

Idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma hiyo angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu

Aidha, kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Utumiaji wa Intaneti umeongezeka kutoka 26,078,506 kwa mwaka 2020 hadi 48,028,227 kwa mwaka 2024

Soma https://jamii.app/IntanetiData

#JamiiForums #JFData #JamiiAfrica #Internet
👍1
MANYARA: Timu ya Fountain Gate imeilazimisha Simba sare ya Goli 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Matokeo ambayo yanaifanya Simba ibaki nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kwa kuwa na alama 44 nyuma ya Yanga yenye pointi 45

Timu ya #Simba ilianza kufunga kupitia kwa Leonel Ateba dakika ya 57 lakini Fountain Gate ambayo imefikisha alama 21 ilipata goli kupitia kwa Ladack Chasambi aliyejifunga dakika ya 75

Soma https://jamii.app/GatesSimba

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
2
ARUSHA: Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeiamuru Tanzania kufuta adhabu ya kifo katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu, (Sura ya 16) ndani ya mwaka mmoja kutokea Februari 5, 2025 ilipotoa hukumu hiyo

Mahakama imesema Jamhuri ilikiuka Haki ya Kuishi na Haki ya Utu chini ya Kifungu cha 4 na 5 cha Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu katika utekelezaji wa adhabu ya kifo, yaani kunyongwa

Aidha, Mahakama imeiamuru Jamhuri kuchapisha nakala ya Hukumu hiyo kwenye tovuti za Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria, ndani ya miezi mitatu tangu kutolewa kwake na kuhakikisha nakala hiyo inapatikana kwenye tovuti hizo walau ndani ya mwaka mmoja tangu itakapochapishwa.

Soma https://jamii.app/HukumuYaKifo

#CivilRights #HumanRights #JamiiForums
KENYA: Kiongozi wa Chama cha Thirdway Alliance, Ekuru Aukot, amesema Kenya ina Rasilimali za kutosha, lakini Mifuko ya umma inakauka kutokana na Ubadhirifu wa Viongozi walafi, ambao wangedhibitiwa basi wasingehitaji misaada kama ya Shirika la Marekani la USAID

Februari 5, 2025, USAID ilitangaza kuwa Wafanyakazi wake wote watawekwa kwenye likizo ya Kiutawala Duniani kote, isipokuwa wale walioteuliwa kushughulikia majukumu muhimu ya Shirika hilo, Uongozi wa Msingi, na Miradi maalum

Kufuatia tangazo hilo, mamia ya Miradi ya USAID yenye thamani ya Mabilioni ya Dola katika utoaji wa misaada ya kuokoa Maisha Duniani imesimama ghafla, hivyo kuzua wasiwasi mkubwa kuhusu Ajira na athari zake kwenye Sekta ya Afya

Soma https://jamii.app/USAIDKenya

#JamiiForums #TrumpExcutiveOrders #Accountability #ServiceDelivery #Governance
#MICHEZO: Dirisha dogo la Usajili wa Januari 2025 limefungwa siku chache zilizopita, Klabu za Premier League zimetumia takriban Pauni Bilioni 2 (Tsh. Trilioni 6.3) katika madisha mawili ya 2024-25 season

Brighton ambayo imekuwa na matokeo ya kuridhisha msimu huu ndio ambayo imetumia fedha nyingi kuliko timu nyingine zote, imetumia Pauni Milioni 231.4 (Tsh. Bilioni 732.5) kwa muda huo

Soma https://jamii.app/KlabuUsajiliMsimu

#JamiiForums #JFMichezo
1
Nchini Tanzania, Serikali kwa kushirikiana na Wadau ili kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake ikiwemo Ukeketaji imeanzisha Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto 18,618 kwenye Mikoa, Halmashauri, Kata hadi ngazi za Vijiji/Mtaa

Pia, zimeanzishwa Nyumba salama 9 (Safe homes) kwaajili ya kuwatunza wanaokimbia na Waathirika wa Ukeketaji kwenye Mikoa yenye kiwango cha juu cha Ukeketaji, Vituo vya mkono kwa mkono 32 (one stop centres) Tanzania Bara na Dawati la Jinsia na Watoto katika vituo 420 vya Jeshi la Polisi Nchini

Soma https://jamii.app/FGMDay2025

#JamiiForums #FGM #EndFGM #InternationalDayofZeroToleranceforFemaleGenitalMutilation #HerVoiceMatters
FARAGHA: Unapojisajli kwenye Mtandao wowote, huwa kuna Sera ya Faragha (Privacy Policy) pamoja na Vigezo na Masharti (Terms & Conditions) zinazoelezea taarifa zinazokusanywa kwenye programu au Mtandao huo na jinsi gani taarifa hizo zinatumika, ambapo kama hukubalini na vigezo hivyo upo huru kutojiunga nao

Ni muhimu kusoma vigezo hivyo ili ujue wanachukua Taarifa gani na jinsi gani zinavyotumika ili kulinda Taarifa zako zisije kutumiwa vibaya.

Mjadala zaidi https://jamii.app/SeraFaraghaTaarifaBinafsi

#JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #TaarifaZakoMaishaYako
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, jiulize, je, unachagua viongozi kwa maono yao na uwezo wa kuleta maendeleo, au kwa sababu ya pesa wanazokupatia wakati wa kampeni?

Rushwa katika uchaguzi si tu inavuruga demokrasia, bali pia inaingiza kwenye mzunguko wa uongozi mbovu unaoweka maslahi binafsi mbele ya mahitaji ya Wananchi. Usiuze haki yako kwa 'noti' za kampeni

#ChaguaKiongoziSioPesa #KemeaRushwa25 #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
BUNGENI: Akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole ambaye alitaka kufahamu kuhusu mipango ya Serikali kulingana na mabadiliko ya Sera za nje ya nchi ambazo zinatajwa kuathiri Sera za Elimu, Afya na Uchumi Nchini, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa Watanzania kushirikiana kutumia Rasilimali na Maliasili zilizopo ili kuimarisha uchumi wa ndani

Soma https://jamii.app/MajaliwaFeb6

#JamiiForums #Governance #Diplomacy #Accountability
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko amependekeza Serikali ipange kiasi sahihi ambacho Mwanafunzi atatakiwa kukilipa kwaajili ya chakula kwa Mwezi

Anasema Vipato vya Wazazi/Walezi wengi havipo sawa hivyo utaratibu wa kumtaka Mtoto aende na hela kila Siku Shuleni unakuwa mgumu kwa baadhi ya Watu

Soma https://jamii.app/MdauChakulaShule

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #Accountability #Uwajibikaji #ElimuKwaUsawa