JamiiForums
56.2K subscribers
32.9K photos
1.87K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
UGANDA: Maandamano ya Kupinga Vitendo vya Rushwa na Ufisadi Serikalini yanayoratibiwa na Vijana wa Mitandaoni yameanza leo Julai 23, 2024, yakidaiwa kuiga mfano wa #Maandamano ya Vijana wa #Kenya yaliyoanza kwa kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha

Msemaji wa Polisi, Kituuma Rusoke amesema Mamlaka nchini humo hazitaruhusu Maandamano yatakayohatarisha Amani na Usalama wa Nchi

Inaelezwa, Polisi waliovalia mavazi ya Askari wa Kutuliza Ghasia na wengine sare za Kivita wamesambaa katika Mitaa ya Jiji la Kampala pamoja na kuweka Vizuizi Barabarani

Soma https://jamii.app/UgandaGenZDemos

#JamiiForums #UgandaGenZ #Accountability #Democracy #Uwajibikaji
Serikali ya #Kenya imeruhusu Maduka ya Dawa za Binadamu kutoa huduma ya kwanza ya Dawa ya Kuzuia Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (PrEP) baada ya tafiti kuonesha zitasaidia Watu kuzipata kwa haraka na kuzitumia

Imeelezwa Majaribio yaliyofanywa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Magonjwa ya Kuambukiza (NASCOP) na PharmPrEP katika maeneo yenye maambukizi makubwa yamekuwa na matokeo chanya na Watumiaji wa PrEP wameongezeka kutoka 10,000 Mwaka 2016 hadi 438,003 Mwaka 2023

Kwa mujibu wa takwimu za Afya, matumizi ya Dawa za PrEP ndani ya muda unaotakiwa, yanapunguza hatari ya mtu aliyefanya ngono katika mazingira hatarishi kuambukizwa Virusi Vya UKIMWI kwa takriban 99%.

Soma https://jamii.app/PharmPrEP

#JamiiForums #PublicHealth #JFAfya #Governance #ServiceDelivery
AFYA: Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha Mkutano wa Dharura kujadili hali ya usambaaji wa Homa ya Nyani (#Mpox), ambapo Takwimu kutoka kwa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (CDC) zinaonesha ongezeko la 160% la Homa hiyo ikilinganishwa na Mwaka 2023

Takwimu zimeonesha tangu Januari hadi Julai 28, 2024, Visa 14,250 vimeripotiwa katika nchi kadhaa zikiwemo Burundi, Cameroon, Ghana, Liberia, Nigeria, #Rwanda, #DRCongo, na Afrika Kusini. Pia, katika kipindi cha Miezi 12 iliyopita, nchi 17 zimeripoti homa ya Mpox

Aidha, #AfricaCDC imeripoti ongezeko la vifo 461, huku 450 vikitokea DR Congo ambako Ugonjwa huo umesambaa zaidi. Takwimu hizo ni nje ya maambukizi mapya yaliyoripotiwa katika nchi za #Kenya na #Uganda.

Soma https://jamii.app/MpoxCases

#JamiiForums #PublicHealth #Governance #MpoxAwareness #JFAfyaJamii #JFDATA
Kumeibuka andiko la mtandao wa X lenye jina la #GodblessLema, Mbunge wa zamani Arusha Mjini, likitoa hoja kuwa kinachoendelea #Ngorongoro kwa sasa kimepandikizwa na baadhi Jamii ya wafanyabiashara wa utalii kutoka #Kenya wenye ndugu #Tanzania

Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck.com umebaini taarifa hii iliyoanza kusambaa Mtandaoni Agosti 18, 2024 imetengenezwa na haikuchapishwa na akaunti halisi ya Lema kama inavyodaiwa

Pia, Agosti 19, 2024 kupitia Mtandao wa X, Godbless Lema alikanusha taarifa hii kwa kusema "Puuzeni Propaganda za Chawa na Kunguni. Ujumbe hapo chini sio wangu bali ni Photoshop. Sijapokea simu kwa mtu yoyote kutoka Kenya katika sakata hili"

Soma https://jamii.app/LemaNgorongoro

#Misinformation #Disinformation #FactsMatter #VisitJamiiCheck #MisDis04
#KENYA: Mahakama ya Juu imemhukumu Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi, Gilbert Masengeli kifungo cha Miezi 6 jela kwa Kosa la Kudharau Mahakama

Imeelezwa, Masengeli alipuuza agizo la Mahakama takriban mara 7 la kumtaka kufika mbele ya Jaji Lawrence Mugambi kueleza walipo Watu Watatu wanaodaiwa kutekwa na Maafisa wa Polisi katika Mji wa Kitengela, wakati wa Maandamano Julai, 2024

Aidha, Jaji Lawrence amemtaka Masengeli kujisalimisha kwa Kamishna Mkuu wa Magereza mara moja na iwapo atakosa kufanya hivyo, basi Waziri wa Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki atoe agizo la kukamatwa kwake na kupelekwa Gerezani

Soma https://jamii.app/InspektaKifungoMiezi6

#JamiiForums #Accountability
SIASA: Bunge la #Kenya linatarajiwa kuanza kujadili hatma ya Naibu Rais, Rigathi Gachagua kuanzia leo, Oktoba 3, 2024 kuhusu tuhuma mbalimbali zinamzokabili pamoja na nia ya kumng'oa madarakani

Hoja hiyo imewasilishwa Bungeni na Mbunge wa Kibwezi Magharibi, Eckomas Mwengi ambapo ameorodheza mashtaka 10 dhidi ya Gachagua ambaye amedumu madarakani kwa Miaka miwili

Soma https://jamii.app/10Gachagua

#KenyanPolitics #Governance #Accountability #JamiiForums
UCHUMI: Serikali ya Tanzania inafanya mazungumzo na Adani Group ya India na Gridworks Development Partners ya Uingereza, kwaajili ya kuingia ubia wa uwekezaji katika Mradi wa Umeme kwa Dola Milioni 900 (Tsh. Trilioni 2.4) na Dola Milioni 300 (Tsh. Bilioni 817) mtawalia

Mtandao wa India Times umeandika kuwa Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema mazungumzo yanaendelea

Aidha, Kampuni ya Adani imesaini Mkataba wa Miaka 30 katika Bandari ya Dar es Salaam na inataka kuwekeza katika umeme Nchini #Kenya katika Mradi wa Dola Milioni 736 (Tsh. Trilioni 2)

Soma https://jamii.app/AdaniToTanzania

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance
#KENYA: Aliyekuwa Naibu Rais, #RigathiGachagua, kupitia Wanasheria wake amewasilisha ombi la kuzuia Rais #WilliamRuto kuteua Mtu atakayejaza nafasi ya Naibu Rais baada ya kuvuliwa Madaraka na Bunge la Seneti

Gachagua ameiomba Mahakama kuagiza Bunge la Taifa na Seneti kufuta au kurekebisha taarifa zozote za uongo zilizomo kwenye hoja za kumvua Madaraka akidai hazina ushahidi wa kutosha

Aidha, Wabunge wa Kenya wamepiga kura ya kuridhia Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais kwa kura 236 huku kukiwa hakuna iliyoharibika

Soma https://jamii.app/GachuaguaKupingaUteuziNaibuRais

#JamiiForums #Democracy #KenyanPolitics #Governance #Accountability
KENYA: Rais #WilliamRuto ametoa kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni inamlenga aliyekuwa Naibu Rais, #RigathiGachagua, baada ya kumwambia Naibu Rais aliyeapishwa, Profesa Kithure Kindiki kuwa Serikali yake inahudumia Wananchi wote wa #Kenya na sio Familia au Jamii fulani ya Watu

Amesema “Nahitaji sauti yako, nahitaji uwezo wako kunisaidia mimi na Baraza la Mawaziri, nimekuwa mpweke kwa muda katika utendaji.”

Ameongeza “Naamini wewe ni mwelewa, nina uhakika utafanya kile ambacho nimekosa kwa Miaka miwili iliyopita. Najua utaweza.”

Soma https://jamii.app/KindikiKE

#KenyaPolitics #Governance #Democracy #JamiiForums
CHAN: SUDAN YASONGA MBELE, TANZANIA KUSHIRIKI KAMA MWENYEJI

Timu ya Sudan imeweza kusonga mbele kwenye michuano ya #CHAN baada ya kuifunga Tanzania kwa mikwaju ya penati 6-5 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano hiyo mwaka 2025. Sudan sasa inaenda kukutana na Ethiopia

Timu hizo zimepiga penati baada ya Tanzania kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa leo na hivyo kufanya timu hizo kulingana kwa idadi ya magoli kwani katika mchezo wa kwanza Sudan ilipata ushindi wa goli 1-0

Licha ya Sudan kusonga mbele, #Tanzania itashiriki michuano hiyo inayofanyika Februari 01 - 28, 2025 kwa tiketi ya Mwenyeji kwani #Kenya, #Uganda na Tanzania ndio zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo

Zaidi https://jamii.app/CHAN_TZ_SUD

#JFSports
Kwa mujibu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment Programme), 80% ya watu wanaokimbia Makazi yao duniani kote kutokana na mabadiliko ya TabiaNchi ni Wanawake au Wasichana ambao hukabiliwa na hatari kubwa ya Umasikini, Ukatili au mimba zisizotarajiwa katika mchakato wa kuhamia katika maeneo salama zaidi

Ripoti hiyo imeeleza Ukame mkubwa uliotokea Nchini #Kenya mwaka 2022 ni moja ya mifano mingi ambapo Wanawake waliathirika zaidi kwa utapiamlo na upungufu wa maji mwilini. Wakati huo huo, visa vya Ukeketaji, ndoa za utotoni, na ukatili wa kijinsia viliripotiwa kuongezeka

Soma https://jamii.app/EffectsOfClimateChangeOnWomen

#JamiiForums #JFWomen #WanawakeNaTabianchi #Accountability #ClimateChange #ClimateIsssues
KENYA: Kongamano la Maaskofu wa Katoliki Kenya (KCCB) limepinga vikali pendekezo la kuongeza muda wa Urais kutoka Miaka Mitano hadi Saba wakidai ni pendekezo lenye ubinafsi kutokana na tamaa ya viongozi wa kisiasa nchini humo

Pia, Maaskofu hao wamekosoa Sera za Kodi za Serikali wakidai zinatozwa kupita kiasi na kuathiri uchumi wa Wananchi kufuatia maandamano ya kupinga Bajeti ya Muswada wa Fedha, Juni 2024

Aidha, wameungana na vikundi vya Binadamu kulaani vitendo vya utekaji wakidai ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu na uminyaji wa uhuru wa kujielezea na hivyo wanahimiza Serikali kuchukua hatua haraka kulinda usalama na uhuru wa raia wote wa #Kenya

Soma https://jamii.app/MaaskofuWapingaUraisMiaka7

#JamiiForums #KenyanPolitics #Accountability #Governance #HumanRights
#KENYA: Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (KCCB) limeikosoa Serikali ya Rais #WilliamRuto kwa kushindwa kutimiza ahadi zake kwa Wakenya na kudumisha Utamaduni wa uongo na kutumia Mitambo ya Serikali kunyamazisha Wapinzani

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Askofu Maurice Muhatia amewashutumu Viongozi wa Serikali kwa kushindwa kutimiza ahadi walizoahidi wakati wa Uchaguzi, kutojali kilio cha Wananchi na kurudisha nyuma Mafanikio ya Kidemokrasia ya Kenya

Askofu Muhatia amesema "Utamaduni wa Uongo unabadilisha kwa haraka Uadilifu na Heshima wanayostahili Wakenya. Kwa kifupi, inaonekana kuwa ukweli haupo, na kama upo, ni ule tu ambao Serikali inasema"

Soma https://jamii.app/RutoUtamaduniUongoUkome

#JamiiForums #KenyanPolitics #Accountability #Governance #HumanRights
#INDIA: Wabunge wa Upinzani wamewasilisha Hoja ya kulitaka Bunge liishinikize Serikali kuchunguza Kashfa za #Rushwa zinazoibuliwa dhidi ya Mfanyabiashara Gautam Adani, mmiliki wa Adani Group

Hoja hiyo imeripotiwa kusababisha mvutano kiasi cha shughuli za Bunge kusitishwa kwa muda, ingawa Chama Tawala kimeendelea kutounga mkono hoja hiyo. Upinzani unashinikiza kampuni za Adani zinazofanya Uwekezaji katika Kilimo, Nishati, Makaa ya Mawe na Miundombinu zichunguzwe

Hivi karibuni, Serikali ya #Kenya ilisitisha mkataba wa Uendelezaji na Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta kati yake na moja ya kampuni za Adani kutokana na shinikizo la Wananchi na Wafanyakazi wa Uwanja huo

Novemba 27, 2024, Mtandao wa Reuters uliripoti kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Plasduce Mbossa, imesema itaendelea na Mkataba wake na Adani kwakuwa wao hawana tatizo na kampuni hiyo.

Soma https://jamii.app/AdaniScandals

#JamiiForums #Governance #Accountability #Transparency #Economy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Rais #WilliamRuto amesema Nchi yake imeachwa nyuma katika masuala ya Mwingiliano wa Biashara za Ukanda baada kupitwa na #Tanzania kwenye Huduma za Biashara za Uagizaji, Uingizaji bidhaa kwa Nchi za Afrika Mashariki

Akizungumza katika Maadhimisho ya 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jijini Arusha, Ruto amesema "Naipongeza Tanzania kwa kuipita #Kenya katika Huduma za Biashara ya Bidhaa ambazo tunanunua na kuuza Afrika Mashariki. Kenya ilikuwa nchi inayoongoza eneo hili, sasa Tanzania imeipita Kenya."

Taarifa ya Benki Kuu ya Uganda imeeleza hadi Novemba 2024, Tanzania iliipita Kenya na kuwa chanzo kikuu cha bidhaa zinazoagizwa na Uganda Barani Afrika, Mwaka ulioishia Juni 2024, Tanzania ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya Tsh. Trilioni 10.98 kwenda #Uganda, ikichangia 42.56% ya bidhaa zote zilizoagizwa kutoka Afrika huku Kenya ikichangia 19.55%

Soma https://jamii.app/KenyaLaggs

#JamiiForums #Governance #Accountability #AfricanEconomy
UCHUMI: Ripoti ya Makadirio ya Ukuaji wa Uchumi ya Benki ya Dunia (WB) imeonesha Uchumi wa #Kenya utashuka kutoka 5.0% ya makadirio ya awali hadi 4.7% huku Mafuriko, Maandamano dhidi ya Serikali na Juhudi hasi za Uimarishaji wa Uchumi vikitajwa kuathiri ukuaji huo

Pia, ripoti imeonesha Kenya bado inakabiliwa na hatari kubwa ya kuelemewa na mzigo wa Madeni huku Deni la Serikali likizidi kuwa dhaifu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama za kulipa deni hilo pamoja na kukosa malengo ya mapato

Aidha, WB imeitaka Serikali kukabiliana na hali ya kukosekana kwa usawa wa Kimuundo ambayo imetajwa kuwa chanzo cha kufifisha malengo ya ukuaji endelevu na shirikishi wa Uchumi.

Soma https://jamii.app/WBKenya

#JamiiForums #Governance #AfricanEconomy #Accountability
#KENYA: Wadau mbalimbali wa masuala ya Haki za Binadamu wakiwemo Wanasiasa wametoa wito kwa Rais #WilliamRuto kukemea na kukomesha Vitendo vya Utekaji wa Wananchi wengi wakiwa ni wakosoaji wa Serikali yake

Miongoni mwa waliotoa wito huo ni pamoja na Mahakama, Wanasiasa Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Chama cha Wanasheria (LSK), Naibu Rais aliyeondolewa Madarakani, Righathi Gachagua, Vyama vya ODM, Wiper, DAP-K na baadhi ya Maseneta

KNCHR imehusisha matukio ya Utekaji na Maandamano yaliyofanyika Miezi michache iliyopita ya Vijana Wadogo (Gen Z) dhidi ya Serikali ya Rais Ruto ambapo wengi kati ya walioripotiwa Kutekwa walikuwa wakipinga utawala wa Ruto kupitia Mitandao ya Kijamii

Wakati hali ikiwa hivyo Nchini Kenya, Agosti 9, 2024 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu kuongezeka kwa Vitendo vya Utekaji na Watu kupotea Nchini Tanzania ambapo ripoti hiyo ilionesha Watu 83 Walitekwa.

Soma https://jamii.app/UtekajiKE

#JamiiForums #Governance #HumanRights #SayNoToAbductions
#KENYA: Maandamano ya Kupinga vitendo vya Utekaji yaliyoitishwa na Wanaharakati wa Haki za Binadamu na Ndugu na Jamaa wa Watu walioripotiwa kutoweka katika Mazingira yenye utata, yameanza leo licha ya Jeshi la Polisi kuyaita ni haramu

Hatua hiyo inafuatia kupita Saa 48 za wito wa kuachiwa huru kwa Watu waliotekwa, muda uliotolewa na Wanaharakati kwenda kwa Mamlaka zinazotuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo, wakiwemo Maafisa wa Idara za Ulinzi na Usalama wa Serikali

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa Mitandao Desemba 29, 2024, Waitishaji wa Maandamano hayo wamesema wataendelea kuandamana bila kukoma hadi pale ndugu zao watakapoachiwa na hawajali itachukua siku ngapi.

Soma https://jamii.app/KenyaUtekaji

#JamiiForums #Governance #HumanRights #Accountability #EndAbductionsKE