NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com ambaye ni Mkazi wa Njombe Mjini ametoa wito kwa Halmashauri hiyo kuweka wazi ikiwa imetoa maelekezo kwa Shule za Msingi kutoza Wanafunzi hadi Tsh. 10,000 kwa ajili ya mitihani ya kila wiki, na kuongeza kuwa gharama hizo zimekuwa mzigo kwa Wazazi na Walezi.
Zaidi soma https://jamii.app/ShuleNjombeHalmashauri
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji

❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Askofu Dkt. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe akiongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Ihembe, Wilaya ya Karagwe, Agosti 11, 2025, amewaasa Watanzania kutumia busara katika kuchagua Viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ili kupata Viongozi wanaostahili.
Zaidi soma https://jamii.app/BagonzaUchaguziBusara
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
Zaidi soma https://jamii.app/BagonzaUchaguziBusara
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo - Bara, Isihaka Mchinjita, akihojiwa na kituo cha Redio cha #EastAfrica, Agosti 20, 2025 ameeleza kuwa Luhaga Mpina si mgeni ndani ya chama hicho kwani alijiunga nacho muda mrefu na tayari ni sehemu ya harakati zao.
Aliongeza kwa kusema kuwa mjadala mkubwa ulijikita kwenye namna bora ya kumtumia Mpina ili kuleta faida ya kisiasa kwa chama, ama kubaki kama Mbunge wa Kisesa au kuingia moja kwa moja kwenye siasa za kitaifa, na baada ya tathmini, chama kiliona atakuwa na mchango mkubwa zaidi kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu.
Zaidi soma https://jamii.app/MpinaActUfafanuzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
Aliongeza kwa kusema kuwa mjadala mkubwa ulijikita kwenye namna bora ya kumtumia Mpina ili kuleta faida ya kisiasa kwa chama, ama kubaki kama Mbunge wa Kisesa au kuingia moja kwa moja kwenye siasa za kitaifa, na baada ya tathmini, chama kiliona atakuwa na mchango mkubwa zaidi kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu.
Zaidi soma https://jamii.app/MpinaActUfafanuzi
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
👍1👎1
BURUDANI: Mdau, ni nukuu/mstari/kauli ipi (Punchline) kutoka kwenye filamu uliyoipenda zaidi? Ulisikia kwenye filamu gani na kwanini unaikubali?
Kushiriki mjadala soma https://jamii.app/NukuuMuvi
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFBurudani #JFMoviesQuotes

This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza Agosti 21, 2025, Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila amesema Chama kimefanikiwa kuteua wagombea wa Udiwani 3,182 kati ya Kata 3,962 Tanzania Bara, na wagombea hao wanaruhusiwa kuchukua fomu katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) huku akibainisha kuwa mchakato kwa Kata zilizobaki unaendelea.
Zaidi soma https://jamii.app/WagombeaChaummaUdiwani
#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Governance #UtawalaBora

👎1
SOMALIA: Marais watatu wastaafu Sharif Sheikh Ahmed, Abdiqasim Salad Hassan na Mohamed Abdullahi Farmaajo wameungana kutoa tamko dhidi ya Serikali ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, wakiilaani kwa uporaji na uuzaji holela wa ardhi ya umma bila kuzingatia taratibu za Kisheria na usimamizi unaostahili.
Viongozi hao wamesema Serikali imekuwa ikihamisha umiliki wa ardhi bila kuhusisha Mamlaka ya Mikataba ya Taifa, na kutoingiza mapato kwenye Hazina ya Taifa. Hali inayosababisha Wananchi maskini wa Mogadishu kufukuzwa na kuondolewa katika makazi yao.
Wametaka Wananchi na Wafanyabiashara kuepuka kununua au kushiriki katika mali zilizopatikana kwa njia zisizo halali, wakisema ni mikataba hatarishi na isiyo na uhalali, hatua ambayo imepongezwa na makundi ya uharakati.
Soma zaidi https://jamii.app/Somalia
#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance

DAR: Mwenyekiti wa Asasi ya Wanafunzi Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Antony Severine amesema mustakabali wa Vijana katika #Siasa unaathiriwa na ilani za vyama, kwani wengi hufuata fursa ili watoboe. Ameeleza nafasi nyingi zinazotolewa nchini haziangalii uwezo wa Vijana bali zinawapendelea wale waliopo ndani ya vyama.
Alisema hayo Agosti 21, 2025 katika mahojiano ya Kipindi cha Malumbano na Hoja cha ITV.
Soma zaidi https://jamii.app/VijanaSiasa
#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Democracy

👍3❤2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza kwa njia ya Mtandao, Susan Lyimo ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#BAZECHA), amesema Uchaguzi Mkuu wa 2025, ukifanyika kwa Sheria na Kanuni zilizopo, utakosa mvuto wa Kitaifa na Kimataifa kutokana na madhila kwa Vyama vya Upinzani, hususan CHADEMA.
Amesema hayo leo Agosti 22, 2025, ambapo ameongeza kuwa, "BAZECHA tunawataka watawala kusikiliza matakwa ya Watanzania na kufanya mabadiliko ya Kikanuni na Kisheria ili Taifa liingie kwenye Uchaguzi Huru na wa haki."
Soma zaidi https://jamii.app/SuzanUhalali
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
Amesema hayo leo Agosti 22, 2025, ambapo ameongeza kuwa, "BAZECHA tunawataka watawala kusikiliza matakwa ya Watanzania na kufanya mabadiliko ya Kikanuni na Kisheria ili Taifa liingie kwenye Uchaguzi Huru na wa haki."
Soma zaidi https://jamii.app/SuzanUhalali
#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025
❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila ametoa kiasi cha Tsh. 20 Milioni na Viwanja viwili Kigamboni kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (#TaifaStars) ikiwa ni sehemu ya motisha kuelekea mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Morocco katika Michuano ya CHAN, unaotarajiwa kuchezwa leo Agosti 22, 2025, kuanzia Saa 2:00 Usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
RC Chalamila amesema fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji bila kujali matokeo ya mchezo huo.
Zaidi soma https://jamii.app/ChalamilaAmwagaPesa
#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports

Mwanamitindo na Mtangazaji, Ney Paul ameshauri Vijana kufikiria kabla ya 'kuposti' kauli za Chuki Mtandaoni kwa kujiuliza kama wanajenga au wanabomoa wangejisikiaje iwapo Mtu mwingine angetumia kauli hiyo kwao.
Amesema “Epuka jazba, Usijibu kwa hasira Chukua muda kupumua na kufikiri kabla ya kujibu maoni au jumbe zinazokukasirisha”.
Aidha, amesema Mitandao imebeba fursa nyingi na fedha nyingi, hivyo ni vizuri kama Vijana wataamua kuitumia vizuri.
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa