JamiiForums
53K subscribers
34.3K photos
2.41K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TCRA YAFICHUA ‘MADUDU’ VITUO VYA REDIO KANDA YA ZIWA

> Yawapa miezi 4 kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyobainika walipofanya ukaguzi kwenye vituo takribani 36

> Wafanyakazi hawana mikataba, wana elimu zisizokidhi na baadhi ya vituo havina vyoo

Zaidi, soma https://jamii.app/TCRA-RedioKandaZiwa
COLOMBIA: WATU 14 WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE

- Imepata ajali jana huko San Carlos de Guaroa ikiwa inatokea San Jose del Guaviare kuelekea Villavicencio

- Ni muda mchache baada ya rubani kutuma ishara ya dharura kwa kituo cha udhibiti

Zaidi, soma https://jamii.app/14WafaAjaliNdege-CLMB
NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA YAPATA AJALI, WENGI WAHOFIWA KUFARIKI

- Boeing 737 imepata ajali ikiwa safarini kutoka Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya

- Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege hiyo ilikuwa na abiria 149 pamoja na Wafanyakazi 8

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
WATU WOTE KWENYE NDEGE ILIYOPATA AJALI LEO ETHIOPIA WAFARIKI

> Ni 157, idadi ikijumuisha abiria 149 na wafanyakazi 8 wa ndege

> Imetajwa kuwa na raia kutoka nchi 33 tofauti

> Sababu za ajali bado hazijafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
ALGERIA: WANAFUNZI WA VYUO WAPEWA LIKIZO YA MAPEMA

- Ni ili kudhoofisha maandamano ya Wanafunzi hao ambao wanapinga Rais Abdelaziz Bouteflika kugombea kwa muhula wa 5

- Likizo hiyo huwa ya wiki 2 kuanzia Machi 21 hadi Aprili 5 kila mwaka

Zaidi, soma https://jamii.app/VyuoVyafungwaMapemaALG
MANUFAA YA KULA WADUDU KIAFYA NA KIMAZINGIRA

> Wana virutubisho karibu vyote yaani protini, madini mengi na asidi za amino

> Pia wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazoongeza joto duniani, hawahitaji maji mengi wala eneo kubwa la kuwafuga

Zaidi, soma https://jamii.app/FaidaKulaWadudu
SERIKALI: WAPINZANI WANAOMTUKANA RAIS KWENYE VIKAO VYA NDANI WAKAMATWE

- Waziri Lugola ametoa agizo hilo kwa Polisi akiwataka washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya

- Asema baadhi ya wapinzani wanatukana, wanabeza na kuchonganisha Wananchi na Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/WapinzaniWanaotukanaWakamatwe
SHINYANGA: AUAWA KATIKA UGOMVI WA RABA

> Daniel Gudugudu(30) ameuawa kwa kuchomwa kisu kwenye mkono wa kushoto na Rashid Mustapha(48) huko Nyihogo wilayani Kahama

> Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na kudaiana viatu aina ya raba zenye rangi nyeusi

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiKisuSHY
NHC KUWAFUKUZA WADAIWA SUGU KATIKA MAJENGO YAKE

- Ni kwa wale walioshindwa kulipa kodi ya pango ya jumla ya Tsh. Milioni 44.3

- Ni mpango wa kutaka kumaliza kukusanya kodi ambapo hadi sasa shirika limekusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.9(73%)

Zaidi, soma https://jamii.app/WadaiwaNHCKuondolewa
TUNISIA: WAZIRI AJIUZULU KUTOKANA NA VIFO VYA WATOTO

> Waziri wa Afya, Abdurrauf esh-Sherif amejiuzulu baada ya kutokea vifo 11 vya watoto ktk Hospitali ya Serikali mjini Tunis

> Uchunguzi unafanyika kubaini sababu ya vifo hivyo

Soma - https://jamii.app/WaziriAjiuzuluVifoWatoto
#JFInternational
SERIKALI YATAKA TAARIFA ZA WAAJIRI WALIOFUKUZA KAZI WANAWAKE BAADA YA KUPATA UJAUZITO

> Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka apewe taarifa hasa za sekta binafsi za waliowafukuza Wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito

Soma > https://jamii.app/UjauzitoKazi

#JFLeo
CHINA, ETHIOPIA ZASITISHA KUTUMIA BOEING 737 MAX 8

> China imeyaamuru mashirika ya ndege ya ndani ya nchi kusimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 kufuatia ajali iliyotokea Ethiopia na nyingine nchini Indonesia

> Shirika la ndege la Ethiopia nalo limetangaza kusitisha safari za ndege zake zote aina ya Boeing 737 Max 8 kuanzia Machi 10 mwaka huu kama tahadhari ya ziada licha ya kuwa bado chanzo cha ajali iliyotokea jana na kuua watu 157 bado hakijafahamika mpaka sasa

Soma - https://jamii.app/ChinaBansBoeing737
#JFInternational
UINGEREZA: MBUNGE AITUHUMU QATAR KWA KUTOA RUSHWA FIFA

> Taifa la Qatar linatuhumiwa kutoa kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 937 kwa FIFA ili ipewe uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022

Zaidi, soma => https://jamii.app/FIFAQatarScandal

#JFLeo
AJINYONGA BAADA YA UGOMVI NA SHANGAZI KUHUSU CHAPATI

> Binti Sharon (20), mkazi wa Kisumu, Kenya, amejinyonga hadi kufa baada ya ugomvi na shangazi yake kuhusu chapati

> Alitumia fedha ya chakula cha familia kujinunulia chapati na maharage

Soma - https://jamii.app/BintiAjinyongaChapati
#JFLeo
MPANDA, KATAVI: WANAFUNZI WALALA BWALONI BAADA YA BWENI KUTEKETEA KWA MOTO

> Ni Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Msaginya wamelazimika kulala katika bwalo la chakula tangu mabweni yao yateketee kwa moto wiki iliyopita

Zaidi, soma => https://jamii.app/WanafunziWalalaBwaloni

#JFLeo
MAKAMU WA RAIS KUMUWAKILISHA RAIS KWENYE MKUTANO WA ANS UGANDA

> Samia Suluhu anaondoka nchini leo kuelekea Kampala kwenye Mkutano wa "Africa Now Summit"

> Atazungumzia mada ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika

Soma - https://jamii.app/SamiaMkutanoANS
#JFLeo
MWENDELEZO: KISANDUKU CHA TAARIFA KUTOKA NDEGE YA ETHIOPIA CHAPATIKANA

> Kisanduku(Black Box) cha kurekodia taarifa za ndege wakati wa safari kilichokuwa cha ndege ya Boeing 737 MAX 8 iliyoanguka na kuua watu 157 chapatikana

Soma => https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes

#JFInternational
UUZAJI WA SILAHA DUNIANI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 8

> Taasisi ya masuala ya amani duniani (SIPRI) imesema uuzaji wa silaha za kivita duniani umeongezeka kati ya 2014 hadi 2018

> Marekani yaongoza kwa kuuza zaidi ya 36% ya silaha zote

Zaidi, soma - https://jamii.app/OngezekoUuzajiSilaha
#JFLeo
FAHAMU MAMBO YA MSINGI KATIKA KILIMO CHA MIHOGO

> Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari na maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm 1200 kwa mwaka

> Mbegu ya Naliendele huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe na mbegu ya Kiroba huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/KilimoMihogo
#JFKilimo
SOKO LA SABASABA DODOMA LAKOSA UONGOZI KWA ZAIDI YA MIEZI 5

> Soko kuu la Sabasaba Dodoma halina uongozi kwa muda mrefu kutokana na uongozi wa awali kuvunjwa na Mkurugenzi wa Jiji, Septemba 2018 kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za soko hilo

Soma - https://jamii.app/UongoziSabasabaDodoma
#JFLeo
WANAWAKE WALIOANDAMANA SUDAN WAHUKUMIWA KWENDA JELA

> Mahakama ya Khartoum imemhukumu kifungo cha wiki 1 Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani pamoja na wenzake na kuwatoza faini ya dola 42 kwa kushiriki maandamano ‘haramu’

Soma - https://jamii.app/WaandamanajiJelaSudan
#JFInternational