JamiiForums
53K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZANIA YAONGOZA KWA KUWA NA SIMBA WENGI BARANI AFRIKA

> African Wildlife Foundation imesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na Simba wengi Afrika na iko nafasi ya 3 kwa upande wa Tembo

> Kwa Tembo, Botswana inaongoza ikifuatiwa na Zimbabwe

Soma - https://jamii.app/TzOngozaSimbaAfrika
#JFLeo
INDIA: UCHAGUZI KUFANYIKA MWEZI UJAO, UTAHUSISHA WAPIGA KURA MILIONI 900

> Waziri Mkuu, Narendra Modi anatarajiwa kuibuka mshindi katika uchaguzi huo ambao kwa mujibu wa Msemaji wa Tume Uchaguzi, Sunil Arora, utafanyika Aprili 11

Soma > https://jamii.app/UchaguziMkuuIndia

#JFInternational
MULEBA, KAGERA: WAKAMATWA KWA KUFOJI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI

> Watu 3 akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Rutoro Kata ya Ngenge Wamekamatwa kwa tuhuma za kufoji vitambulisho vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya Wajasiriamali

Soma > https://jamii.app/VitambulishoMuleba
#JFLeo
KUMRADHI: JamiiForums tunawaomba radhi watumiaji na watembeleaji wa huduma yetu (tovuti) kutokana na kutopatikana kwa tovuti yetu

> Chanzo cha tatizo lililojitokeza kimebainika na kurekebishwa na huduma itarejea muda si mrefu
SHEHENA YA SAMAKI WENYE SUMU WALIOINGIA NCHINI YATEKETEZWA

> Waliingia nchini wakitokea China na waliteketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi Jijini Dar

> Walibainika kuwa na kemikali ya Zebaki inayosababisha saratani na kuharibu kizazi

Soma => https://jamii.app/SamakiSumuMoto

#JFLeo
ALGERIA: RAIS BOUTEFLIKA ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA KWA MUHULA WA 5

> Abdelaziz Bouteflika(82) ameiongoza Algeria kwa zaidi ya miongo 2. Wananchi waliandamana alipotangaza nia ya kugombea tena

> Amesema afya na umri havimruhusu

Soma > https://jamii.app/BouteflikaKutogombea

#JFInternational
SEHEMU YA SOKO LA TOI NCHINI KENYA YATEKETEA KWA MOTO

> Sehemu ya Soko la Toi lililopo Kibera, Nairobi imeteketea kufuatia moto uliozuka usiku wa kuamkia leo Jumanne, Machi 12

> Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na umeteketeza mali zenye thamani ya mamilioni ya pesa na kuwaacha wafanyabiashara na hasara kubwa

#JFInternational
MAFURIKO MALAWI: WATU 28 WAPOTEZA MAISHA

> Idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Kusini mwa Malawi imefikia watu 28 huku idadi ya walioathirika inakadiriwa kuongezeka zaidi

> Baadhi ya maeneo hayana huduma za umeme na maji

Soma - https://jamii.app/DeathFloodsMalawi
#JFInternational
ILBORU SAFARI LODGE YAUNGUA MOTO NA KUJERUHI BAADHI YA WATU

> Hoteli ya Kitalii ya Ilboru Safari Lodge iliyopo Ilboru, Wilaya ya Arumeru, Arusha imeteketea kwa moto kiasi cha kutookoa kitu chochote na kujeruhi baadhi ya watalii waliokuwa wamelala katika nyumba hizo

> Chanzo cha moto bado hakijajulikana ila inahofiwa kuwa ni hitilafu ya Umeme

Soma - https://jamii.app/HoteliIlboruMoto
#JFLeo
PINGAMIZI LA CUF UPANDE WA MAALIM SEIF LAZUIA MKUTANO WA CUF UPANDE WA PROF. LIPUMBA

> Wajumbe kutoka CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad walipeleka pingamizi Polisi

> Mkutano huo uliokuwa ufanyike katika Hoteli ya Lekam, Buguruni

Soma > https://jamii.app/CUFLipumbaVsMaalim

#JFLeo
ZITTO ATAKIWA KUELEZA SABABU ZA KUTOFIKA MAHAKAMANI

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini na wadhamini wake, kueleza sababu za kutofika kwenye kesi jana

> Upande wa utetezi ulitoa taarifa kwamba Zitto anaumwa

Soma- https://jamii.app/ZittoKutofikaMahakamani
#JFLeo
KUKOSEKANA KWA UMEME VENEZUELA: WATU 17 WAPOTEZA MAISHA

> Kwa mujibu wa Kiongozi wa Upinzani, Juan Guaido mpaka sasa baadhi ya maeneo muhimu hayana umeme ikiwemo Hospitali na watu takribani 17 wamepoteza maisha kwa kushindwa kufanyiwa upasuaji

> Shughuli mbalimbali ikiwemo shule na ofisi za Serikali zimesitishwa kwa saa 48 kuanzia jana, Machi 11
 
Soma - https://jamii.app/PowerCrisisVenezuela
#JFInternational
MKUU WA MKOA MBEYA: UKIIBIWA MUME/MKE NITUMIE UJUMBE

> Akiwa eneo la Matundasi Mkoani humo, RC Albert Chalamila amewaambia wakazi wa eneo hilo kuwa atakaye ibiwa Mume/Mke basi mtumie ujumbe kwenye simu na yeye atashughulika na mwizi huyo

Soma => https://jamii.app/RCMbyVsWeziMkeMume

#JFLeo
AJERUHIWA KWA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KORODANI

> Mwanaume, mkazi wa Moshi mwenye umri wa miaka 53, amejeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika korodani moja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lyakrimu; wa kiume (18) na wa kike (14)

Soma - https://jamii.app/AjeruhiwaKorodani
#JFLeo
ILALA, DAR: ALIYESHTAKIWA KWA SHERIA ZA NJE AACHIWA HURU

Mahakama imemuachia huru, Isidory Karume (57) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kukutwa akimiliki risasi mbili za bastola

> Alishtakiwa kwa sheria isiyokuwepo Tanzania

Soma > https://jamii.app/AachiwaHuruRisasi

#JFLeo
SHERIA YA HALI YA HATARI NCHINI SUDAN YAPUNGUZWA MUDA

> Muda wa kutekelezwa sheria ya hali ya hatari nchini Sudan umepunguzwa kutoka mwaka mmoja na kuwa miezi sita

> Tangazo la kupunguza muda wa sheria hiyo limetolewa na Bunge

Soma - https://jamii.app/MudaSheriaHatari
#JFInternational
UINGEREZA: BUNGE LAUKATAA MPANGO WA BREXIT

> Bunge la Uingereza laukata mpango wa nchi hiyo kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya uliowasilishwa na Waziri Mkuu, Theresa May

> Kura 391 zaukataa mpango huo huku Wabunge 242 wauukiunga mkono

Soma => https://jamii.app/MayBrexit

#JFLeo
MAREKANI KUWAONDOA WANADIPLOMASIA WAKE VENEZUELA

> Itawaondoa wafanyakazi wake wote wa ubalozi waliobakia nchini Venezuela kwasababu hali imezidi kuwa mbaya nchini humo

> Uwepo wao unazuia Marekani kuchukua hatua juu ya Venezuela

Soma - https://jamii.app/UsVenezuelaCrisis
#JFInternational
SINGIDA: MWENYEKITI WA HALMASHAURI ASHAURI 'UCHANGUDOA' UHALALISHWE

- Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba, Simon Tyosela amesema biashara hiyo itasaidia kuinua mapato

- Ni baada ya Mkuu wa Mkoa kusema madada poa na machangudoa watakamatwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwnyktIrambaUchangudoa