JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZIMBABWE: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (ZEC) imemtangaza Emmerson Mnangagwa kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais kwa 53% ya Kura zilizopigwa. Kiongozi aliingia Madarakana mwaka 2017 kwa kumpindua Robert Mugabe

ZEC imesema Mpinzani Mkuu wa Mnangagwa, Nelson Chamisa anayeongoza Chama cha Citizens's Coalition for Change (CCC), alipata 44% ya Kura, hata hivyo Chamisa amekataa Matokeo hayo

Agosti 26, 2023 Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU OEM) walidai Uchaguzi huo haukuwa Huru na Haki

Soma https://jamii.app/ResultsZMB

#JamiiForums #Governance #Democracy #SociajlJustice #ZimbabweDecides
πŸ‘12❀1
PROF. MKENDA: HATUPASWI KUWA NA SHULE ZISIZOKUWA NA VYOO AU ZENYE VYOO VIBOVU

Akizungumza katika Mkutano na Wathibiti Ubora wa Shule Jijini #Arusha, Prof. Adolf Mkenda amesema "Maeneo ambayo ningependa muyawekee macho ya ukaribu ni changamoto ya Vyoo vya Wanafunzi na Walimu. Ninajua kuwa Halmashauri hazishindwi kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vyoo, hivyo hatupaswi kuwa na Shule zisizokuwa na Vyoo ama zenye Vyoo vibovu. Nasisitiza katika hili embu geukeni kuwa Wanaharakati”

Kauli hii ya Waziri wa Elimu inakuja ikiwa ni takriban wiki mbili tangu JamiiForums itoe taarifa kuhusu ubovu wa majengo ikiwemo vyoo vya Shule ya Msingi Shungubweni iliyopo Mkoa wa Pwani

Soma https://jamii.app/ShuleMaudhui

#ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #JamiiForums
πŸ‘10
Kukatika kwa umeme kwa saa kadhaa sehemu mbalimbali ikiwemo uwanjani hapo ambapo hakukuwa na Jenereta la akiba, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria

Alex Gitari amefutwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkomen ambaye pia amesema Uwanja wa Jomo Kenyatta ulikabidhiwa majenereta mawili miaka kadhaa iliyopita na imebainika hayajaunganishwa

Soma https://jamii.app/KEAirport

#ServiceDelivery #Accountability #Governance #JamiiForums
πŸ‘10❀1😱1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#UWAJIBIKAJI: Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumuondoa kazini Hanafi Hassan Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kwa maelezo amekuwa akipokea hongo na kuhamisha Miradi ya Maendeleo na kuipelekea sehemu isiyohitajika, kitendo kilichofanya Wananchi kukerwa na kurudisha Kadi za Chama cha Mapinduzi (CCM)

Rais amesema hawezi kustahimili kuona Kadi za Chama zinarudishwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wapo na walipoulizwa, Wakuu hao walijibu kuwa eneo walilohamisha miradi lina Wapinzani wengi

Soma https://jamii.app/DCMtwara

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji23 #SerikaliBilaRushwa #SocialJustice #KemeaRushwa
πŸ‘5
El NiΓ±o ni Mfumo wa Hali ya Hewa unaosababishwa ongezeko kubwa la Joto la Bahari katika eneo la kati la Kitropiki kwenye Bahari ya Pasifiki. Hali hii huambatana na Vipindi vya Mvua kubwa vinavyoweza kusababisha mafuriko

El NiΓ±o inaweza kusababisha mabadiliko ya Hali Mbaya ya Hewa, ikiwemo Ukame, Mafuriko, Vimbunga, na Vipindi visivyotabirika vya Joto ambavyo vyote ni Hatari kwa Afya ya Binadamu

Kwa mujibu tafiti mbalimbali za Kijiografia, El NiΓ±o inatarajiwa kuathiri maeneo mengi duniani ikiwemo Tanzania hasa kuelekea mwisho wa mwaka 2023

Soma https://jamii.app/ElNino

#JamiiForums #Governance #ClimateChange #ElNino
πŸ‘9πŸ₯°2πŸ€”2
Marufuku hiyo ya Uongozi wa #Taliban imehusu Hifadhi ya Band-e-Amir katika Jimbo la Bamiyan, ambapo Kaimu Waziri wa Maadili wa #Afghanistan, Mohammad Khaled Hanafi amesema Wanawake wamekuwa hawazingatii mavazi ya hijabu wanapokuwa ndani ya hifadhi hiyo

Amewataka Viongozi wa Dini na Vyombo vya Usalama kuwakataza Wanawake kuingia hadi suluhu ipatikane juu ya utaratibu wa mavazi hayo

Miezi ya hivi karibuni, Taliban ilipiga marufuku Wanawake kwenda Saluni za Kike na pia iliwazuia kufanya Mitihani ya Kitaifa ya kuingia Chuo Kikuu

Soma https://jamii.app/Taliban2023

#Governance #JamiiForums
😁10πŸ‘6πŸ‘Ž4πŸ‘1
ZANZIBAR: Mchezo wa ngumi Zanzibar ulizuiwa kwa miaka mingi baada ya Rais Abeid Karume kuuzuia mchezo huo mwishoni mwa miaka ya 1960. Leo, Agosti 27, 2023 Rais Hussein Mwinyi amezindua mchezo huo baada ya zuio kuondolewa

> Rais Mwinyi amesema mchezo wa ngumi unatoa fursa kwa vijana na vijana watakaofaidika na ngumi sio Wapiganaji tu, bali Wadau wote wa Mchezo huo

Soma https://jamii.app/NgumiZnz

#JFMichezo #JamiiForums
πŸ‘14πŸ‘Ž2
ZANZIBAR: Bondia Karim Mandonga amepigwa kwa pointi na Othmani Kiluwa katika pambano la Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar

Pambano hilo la Raundi Sita limeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye amezindua mashindano hayo yaliyopigwa marufuku Kisiwani hapo zaidi ya mika 50 iliyopita ambapo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59

Hii ni mara ya tatu mfululizo Mandonga kupigwa. Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola

Soma https://jamii.app/NgumiZnz

#JFMichezo #JamiiForums
😁15❀3πŸ‘3πŸ€”1
ZANZIBAR: Bondia kutoka Dar, Abdallah Pazi, maarufu kama Dullah Mbabe amemshinda kwa β€˜Knock Out’ mpinzani wake kutoka Zanzibar, Mussa Nassor 'Banja' kwenye mzunguko wa kwanza

Banja alianguka na kulala chini akiwa amejikunja baada ya kushindwa kuvimilia ngumi za Dullah hali iliyomfanya refa kumaliza pambano. Mchezo huu ni katika Tamasha la Uzinduzi wa Ngumi Zanzibar

Soma https://jamii.app/NgumiZnz

#JFMichezo #JamiiForums
😁9❀6πŸ‘1πŸ‘1
ZANZIBAR: Bondia kutoka Zanzibar, Khamis Muay Thai ameshindwa kwa kusalimu amri kwa bondia kutoka Dar es Salaam, Ibrahim Class katika raundi ya 7 kwenye pambano la raundi 8

Khamis alinyoosha mikono juu kuashiria kuwa hataki kuendelea na pambano baada ya kuelemewa kuanzia raundi ya 6. Pambano hili limefanyika Viwanja vya Mao Tse Tung, Zanzibar katika Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar

Soma https://jamii.app/NgumiZnz

#JFMichezo #JamiiForums
😁17πŸ‘3❀1
UFARANSA: Wizara ya Elimu imetangaza Kanuni hiyo inatarajiwa kuanza Mwaka mpya wa masomo wa Septemba 4, 2023 katika shule zote za Serikali

Waziri wa Elimu, Gabriel Attal amesema "Unapoingia darasani hautakiwi kumtambua Mwanafunzi kwa imani yake ya dini kwa kumuangalia."

Pia, Ufaransa imepiga marufuku alama kubwa za Kidini katika Shule na Majengo ya Serikali kwa maelezo zinakiuka Sheria ya Nchi

Soma https://jamii.app/AbayasFrance

#Governance #JamiiForums
πŸ‘14πŸ‘Ž10❀4
MBEYA: Watu 40 wakiwemo Madiwani, Wataalamu wa TEHAMA (IT), Watendaji wa Kata, Wakusanya Ushuru na Watumishi kutoka maeneo ya Mbeya, Njombe, Rukwa, Songwe na Ruvuma wanashikiliwa na wengine wanachunguzwa na TAKUKURU kwa tuhuma za Kuingilia Mifumo ya Kifedha na Kuiba Tsh. Milioni 450

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Denis Mwila, amesema baadhi yao wamefikishwa Mahakamani tangu Julai 12, 2023 ambapo uchunguzi umebaini walikuwa wakishirikiana kuiba Fedha hizo tangu 2018

Soma https://jamii.app/WiziMbeya

#JamiiForums #Governance #SerikaliBilaRushwa #JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa
πŸ‘6πŸ€”2❀1
DAWASA KIBAHA: TUMEREJESHA HUDUMA YA KUUNGANISHA MAJI KWA WATEJA WAPYA

Baada ya Agosti 19, 2023, Mdau wa JamiiForums.com kusema Wakazi wa #Kibaha walioomba kuunganishiwa maji hawapati huduma hiyo kwa miezi kadhaa kwa madai hakuna vifaa, Mamlaka ya #DAWASAKibaha imesema huduma zimerejeshwa na Wateja wapya wanapata maji

Akitoa ufafanuzi alipozungumza na JamiiForums, Meneja wa DAWASA Kibaha, Alfa Ambokile amesema β€œKila Taasisi inaweza kupitia kipindi fulani cha jambo fulani kukwama lakini huduma ya kuunganisha maji imerejeshwa na hata leo hii (Agosti 28, 2023) tumehudumia Wateja wapya wa kuunganishiwa maji”

Soma https://jamii.app/MajiDAWASAKibaha

#JFUwajibikaji23 #Governance #JFHuduma #JamiiForums
πŸ‘4
Hii ilikuwa Mechi ya kwanza kati ya Manchester United na Arsenal katika msimu wa Mwaka 2011/12 wa Ligi Kuu ya England ambayo ilichezwa Agosti 28, 2011 huko Old Trafford

Manchester United ilishinda kwa Magoli 8-2 na kukifanya kuwa kipigo kizito zaidi kwa Arsenal katika Ligi tangu Mwaka 1927, Miaka 84 nyuma walipofungwa Magoli 7-0 na West Ham United katika Ligi ya Daraja la Kwanza ya Ligi ya Soka ya wakati huo

#JamiiForums #JFKumbukizi #Sports
πŸ‘4
Je, unafahamu?

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 (Kifungu 60 (3)(b) na 60 (6)(a)), kutoa taarifa binafsi za Mtu mwingine kama namba ya Simu bila idhini ya mwenye namba ni kosa linaloweza kukugharimu Faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kwa kipindi kisichozidi Miaka kumi au vyote kwa pamoja.

#JamiiForums #JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy
πŸ‘3
DAR: Upande wa Mashtaka katika kesi inayowakabili Watumishi 16 wakiwemo Wahasibu wa Jiji la Dar es Salaam wanaodaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 8.9, umesema umekamilisha upelelezi kuhusu watuhumiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 143 na unaandaa taarifa ya Kuiwasilisha Mahakama Kuu

Katika Kesi ya msingi imeelezwa kati ya Julai 1, 2019 na Juni 30, 2021 jijini Dar es Salaam washtakiwa waliongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa Fedha na kujipatia Fedha ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kinyume na Sheria.

Soma https://jamii.app/WiziJijiDar

#JamiiForums #Governance #SerikaliBilaRushwa #JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa
πŸ‘7❀1πŸ‘Ž1
UTEUZI: BALOZI ALI IDI SIWA MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Balozi Siwa anachukua nafasi ya Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi

Soma https://jamii.app/UteuziBaloziSiwa

#JamiiForums #Governance #Uteuzi
πŸ‘3