JamiiForums
55.9K subscribers
33K photos
1.92K videos
30.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Susan Kiwanga aliyekuwa Mbunge Jimbo la Mlimba 2015- 2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa Miaka 20, akitangaza kujiondoa katika Chama hicho Mei 13, 2025, ametaja miongoni mwa sababu zilizomfanya aingie kwenye Kundi la G-55 ni Kaulimbiu ya 'No reforms, No election' kufanywa azimio la Chama

Soma https://jamii.app/KaulimbiuChama

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #Governance
KENYA: Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema Chama chake kiitwacho 'Democracy for the Citizens Party (DCP)' kinalenga ujumuishaji na kina Wanachama wa makundi yote wakiwemo #GenZ

Gachagua pia alitaja Viongozi wa Chama hicho wakiwemo David Mingati (Mwenyekiti), Cleophas Malala (Naibu Kiongozi wa Muda wa Chama) na Cate Waruguru (Kiongozi wa Wanawake)

Aidha, Gachagua ametangaza kuwa Chama hicho kitazinduliwa rasmi Juni 4, na baadaye ataanza ziara ya Miaka Miwili kote nchini kueneza Sera za chama na kuomba uungwaji mkono. Pia, amewataka wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa 2026 kupitia Chama hicho kuanza kujisajili

Soma https://jamii.app/ChamaKipyaGachagua

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Demokrasia
Ukimuuliza Mtanzania kuhusu Nchi za #Nordic, yaani Sweden, Norway, Denmark, Finland au Iceland, wengi watasema: “Aaah zile nchi za maisha bora! Kule hakuna rushwa! Elimu ni bure na watu wao wana furaha kweli kweli”

Lakini, ni hayo tu unayoyajua?

Je, unajua uhusiano wao na Afrika ukoje? Wanavyotumia teknolojia kusaidia jamii? Tamaduni zao za kipekee? Au ushirikiano wao wa kimataifa unaoleta maendeleo ya kijamii?

Ni muda wa kuonesha maarifa yako. Bofya link na uone ni kwa kiasi gani unaelewa kuhusu Nchi za Nordic: https://jamii.app/NordicDodoso

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
Taasisi ya CIPESA (Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa) kwa kushirikiana na wadau wengine, wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, Safaricom na Airtel Kenya, kupinga vitendo vya kiholela na visivyo halali vya kuzuia huduma ya intaneti nchini humo

Kesi hiyo inajikita kwenye ushahidi wa kiteknolojia kutoka Mashirika ya Kimataifa kama Cloudflare, Open Observatory of Network Interference (OONI) na Internet Outage Detection and Analysis (IODA), ambayo yamedhihirisha kuwepo kwa vitendo vya makusudi vya kupunguza kasi ya intaneti na kufunga baadhi ya majukwaa kama vile Telegram

Zaidi https://jamii.app/KeepItOnKE

#DigitalRights #JamiiForums #JamiiAfrica #FreedomOfExpression #Governance #Accountability
Mdau wa JamiiForums.com anasema Stendi ya Makumbusho imechakaa na imekuwa kero kwa watumiaji na madereva wa daladala. Anadai hata maeneo ya abiria kuketi wakiwa wanangojea magari nayo yamechakaa, mvua ikinyesha ndio majanga, abiria wanakimbilia kujisitiri kwenye maduka ya watu au kwenye magari

Anadai kuna wakati magari yanalazimika kushusha abiria maeneo ya nje ili kuepuka kuingia stendi, lakini hata ikifanyika hivyo wahusika wanayanyapia na kutoza faini. Anatoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuwajibika kurekebisha stendi hiyo

Soma https://jamii.app/StendiMakumbusho

#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #Governance #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Uwajibikaji
Ikiwa unashiriki Mazungumzo na Watu wanaopiga Majungu dhidi ya wengine, ni ishara kwamba hata wewe hutahifadhiwa pindi utakapoondoka.

#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifelessons #Maisha #AmkaNaJF #GoodMorning
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Mwananchi wa Mtaa wa Somelo, Kata ya Zingiziwa, Ilala amembana Diwani wake kwa maswali, akitaka kufahamu yapi ameyafanya Diwani huyo tangu alipoingia Madarakani, akidai toka wamchague hajawahi kufika hata kuwashukuru Wananchi wake kwa kumchagua

Zaidi https://jamii.app/DiwaniWaSomelo

#JamiiForums #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii #ServiceDelivery #Accountability #Governance
Mei 14, 2025, Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia Ukurasa wake rasmi katika Mtandao wa X alisema utani wa Kisiasa ni mzuri lakini ni muhimu sana kufanyika kwa namna ambayo unalinda Heshima na Utu wa Wanawake

Soma https://jamii.app/UtuWanawakeSiasa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Demokrasia #JFWomen #WomenInPolitics
Katika dunia yenye maneno mengi na vitendo vichache, uaminifu umekuwa rasilimali adimu. Si kila anayesema ukweli anaishi kwa ukweli na si kila anayeahidi ana nia ya kutimiza.

Uaminifu wa kweli huonekana pale mtu anapochagua kuwa mwaminifu hata kama hakuna anayemuangalia, anapotimiza wajibu wake bila kulazimishwa na anaposhikilia ahadi zake hata kama ni vigumu

Tunapokaribisha mapumziko ya Mwisho wa wiki tujiulize; Je, tunaishi yale tunayoyasema?

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #Lifelessons
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akihojiwa na Kituo cha #Clouds, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Shabani Hamis Taletale (Babu Tale) amesema hana la kusema kuhusiana na Matukio ya Utekwaji wa Raia kwasababu hakuna mtu aliyetekwa jimboni kwake

Aidha, ameongeza kuwa hajawahi kushiriki kwenye mambo mengine sababu alipoingia #Bungeni 'focus' yake ilikuwa ni kwenye jambo moja tu (Jimbo lake) kuhakikisha wanapata Barabara na mwaka huu Rais ameridhia ombi lake hivyo amefanya kazi yake kikamilifu

Zaidi https://jamii.app/UtekajiMoro

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #SocialJustice #Uwajibikaji #Accountability #Governance #Kuelekea2025