JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UGANDA: RAIA WAANDAMANA KUPINGA GHARAMA ZA MAISHA

Maandamano ya kupinga ongezeko kubwa la bei ya vyakula, mafuta na bidhaa nyingine yamesababisha ghasia. Polisi wamefyatua mabomu ya machozi na kukamata waandamanaji 8

Mara kadhaa, Rais Yoweri Museveni amepuuza wito wa kupunguza Kodi, na badala yake amewataka Raia kuwa na matumizi makini zaidi

Soma - https://jamii.app/ProtestsUG
👍13
MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA AFRIKA

Julai 11 ilipitishwa na Umoja wa Afrika (AU) kuwa Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika. Kwa mwaka 2022, Maadhimisho yana Kaulimbiu "Mikakati na Mifumo ya Wazi ya Usimamizi ya Fedha za UVIKO-19"

Tangu kuanza kwa janga la #COVID19 kumekuwa na taarifa nyingi za Rushwa, wizi na matumizi mabaya ya fedha

Vitendo hivyo vimehusishwa na kukosekana kwa Uwazi na #Uwajibikaji

Soma - https://jamii.app/RushwaBaraniAfrika

#AfricaAgainstCorruption #KemeaRushwa
👍8
RUSHWA AFRIKA: Kumekuwepo upotoshaji mkubwa wa Taarifa na ukosefu wa Uwazi katika jinsi Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) zimetumia Rasilimali Fedha za COVID-19

Fedha zilizotengwa kukabiliana na athari za #CoronaVirus katika Mataifa mbalimbali Barani Afrika zinawanufaisha Raia?

Soma - https://jamii.app/RushwaBaraniAfrika

#AfricaAgainstCorruption #KemeaRushwa
👍3
RAIS SAMIA: Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi ametoka ziara Mikoa ya Kusini, ameniambia ameona maradhi mapya yameingia. Watu wanatokwa damu puani na kudondoka

Hatujui ni kitu gani ila Wanasayansi wamehamia huko kwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni Watu wengi wanaougua kwa mfululuzo

Yote ni kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule walikowekwa na Mungu, tunawasogeza kwetu wanatuletea maradhi

Soma https://jamii.app/UgonjwaMpya

#PublicHealth #JFAfya
👍4🤔2😁1
PACHA WALIOTENGANISHWA, MMOJA AFARIKI DUNIA

Pacha Neema amefariki wakati akiendelea na matibabu baada ya hali yake kubadilika ghafla

> Pacha mwenzie, Rehema bado yupo Muhimbili katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU)

Soma https://jamii.app/PachaMmojaAfariki

#JFAfya #PublicHealth
😢16👍1
MAXENCE MELO: Asasi za Kiraia nchini jukumu letu ni kushirikiana katika kupambana na rushwa kwa vitendo

Mfano, JamiiForums kuna uwanja unaokuruhusu kutoa taarifa kwa faragha na zile zinazohusu rushwa tunahakikisha zinafanyiwa kazi

Soma - https://jamii.app/KemeaRushwa

#KemeaRushwa
👍13
#KEMEARUSHWA: Rushwa inaendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa Mataifa ya Afrika kutimiza Ajenda 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu

Jitihada kubwa zinahitajika kupambana na Rushwa katika utoaji wa Huduma za Msingi ambazo huathiri zaidi Wananchi walio katika mazingira magumu, na hutegemea zaidi Huduma za Umma

Soma - https://jamii.app/RushwaBaraniAfrika

#AfricaAgainstCorruption
👍7
KASSIM MAJALIWA: Rushwa ni adui wa Haki na Maendeleo, pia hudumaza maadili katika Taifa

> Taasisi zetu za kupambana na Rushwa (Bara na Zanzibar) zimejitahidi kuboresha utendaji. Hatua zinachukuliwa haraka tofauti na awali

Soma https://jamii.app/KemeaRushwa

#KemeaRushwa
👍4😁1
RAIS HUSSEIN MWINYI: Tunaanza Ziara rasmi ndani ya mwezi huu katika maeneo yote ambayo fedha za #UVIKO19 zimefika

Ningependa niwaambie wanaohusika wote wahakikishe wana maelezo mazuri. Na kazi hizo ziwe zina ubora unaoendana na fedha zilizotolewa

#KemeaRushwa #AfricaAgainstCorruption
👍4
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amesema ipo haja ya kuongeza kasi na umahiri katika kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi

Amesisitiza, jitihada za Taasisi za Kupambana na Rushwa pekee (TAKUKURU na ZAECA) haziwezi kuleta ushindi katika mapambano hayo, na Wadau wote wanapaswa kuhusika

#KemeaRushwa #AfricaAgainstCorruption
🔥1
DAR: MSTAAFU WA JESHI ATUHUMIWA KUUA KWA RISASI

Jonas Ziganyige (71) anatuhumiwa kusababisha kifo cha Patient Romwadi kwa kumpiga na risasi kutokana na mgogoro wa mipaka

> Baada ya tukio Mtuhumiwa alikimbia, amekamatwa akiwa Kibaha-Pwani

Soma https://jamii.app/TuhumaZaMauaji

#JFMatukio
👍4👏1
KIMARA, DAR: Polisi inamshikilia Selemani Haruna 'Kwata' (24) kwa mauaji ya Editha Charles (22) aliyekuwa akifanya Kazi za Ndani

> Mtuhumiwa alifika ktk nyumba anayofanya kazi Editha na kumshambulia na kitu chenye ncha kali, kisha kuiba Tsh. 1,800,000

Soma https://jamii.app/DarMauaji

#JFMatukio
😢14👍5👎1🔥1🤯1
ACP AHMED MAKARANI: Siku za karibuni kumekuwa na changamoto ya Waendesha Mashtaka kufanya kazi ya kupeleleza Washtakiwa wa Rushwa na Uhujumu Uchumi

> Asema hiyo ni kazi ya Wapelelezi yaani Polisi na Watu wa #DawaZaKulevya na si ya TAKUKURU

Soma https://jamii.app/KemeaRushwa

#KemeaRushwa
🤔6👍4
KAGERA: AJALI YAUA NANE, WATANO NI FAMILIA MOJA

Ni baada ya Lori kugongana na Toyota Succeed katika ya Barabara Lusahunga - Nyakahura, Wilayani Biharamulo leo Julai 12, 2022

> Ndugu wa Familia moja waliofariki ni Mama na Watoto wake wanne

Soma https://jamii.app/AjaliYauaNane

#JFMatukio
😢18👍2🤔2👎1
#SRILANKA: KAKA WA RAIS AZUIWA KUTOKA NJE YA NCHI

Basil Rajapaksa ambaye Mwezi Aprili ajiuzulu Uwaziri wa Fedha amezuiwa na Maafisa wa Uhamiaji kuondoka nje ya Sri Lanka

Familia ya Rajapaksa imeshikilia Siasa za Taifa hilo kwa muda mrefu, na wananchi wengi wanailaumu kwa matatizo yanayoikumba Nchi hiyo kwa sasa

Soma - https://jamii.app/BasilZuioSL

#Accountability
👍5
SERIKALI: WATOTO 3,333 WAREJESHWA SHULE

Watoto hao walishindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo Ujauzito

> 900 kati yao wamerejea Mfumo wa Elimu wa Kawaida huku wengine wakijiunga na Mfumo wa Elimu Mbadala wanaosoma kwa miaka miwili

Soma https://jamii.app/WarejeaShuleni

#HakiMtoto #JFElimu
👍19👎5
SRI LANKA: RAIS GOTABAYA RAJAPAKSA AKIMBIA NCHI

Ikiwa ni saa chache kabla ya kutakiwa kujiuzulu rasmi, Rais Rajapaksa ameondoka kwa ndege ya kijeshi ikidaiwa ameshawasili Mji Mkuu wa Maldives, Male

Inaelezwa, Rais Rajapaksa alitaka kutoka #SriLanka kabla ya kujiuzulu ili asikamatwe

Soma - https://jamii.app/RaisAtokaSL

#Democracy
👍13
SIMIYU: Watu wanne wamepoteza maisha baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso eneo la Nyaumata-Bariadi Julai 12, 2022

> Kamanda wa Polisi-Simiyu amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na Madereva wanashikiliwa na Polisi

Soma https://jamii.app/AjaliBariadi

#JFMatukio
😢9👍3👎1
KAIMOSI, KENYA: ATUHUMIWA KUMUUA BINAMU KATIKA UGOMVI WA KUCHAJI SIMU

Inadaiwa alimuua kwa kumchoma mshale kifuani wakati kila mmoja alipokuwa akitaka kuwa wa kwanza kuanza kuchaji simu

Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio na anatafutwa na Polisi

Soma > https://jamii.app/AmuuaBinamuKE

#JFMatukio
😢14👍11👎1
Fuatilia Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Shindano la Stories Of Change Mwaka 2022 litakaloanza Julai 15

Bonyeza > https://fb.watch/eecsLXntHU/

#StoriesOfChange #SOC2022
👍5
AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA "STORIES OF CHANGE" YAZINDULIWA

Shindano linakusudia kuongeza maudhui bora Mtandaoni na kuhamasisha ushiriki wa raia

Andiko linatakiwa kuchochea mabadiliko kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia

Kwa taarifa zaidi - https://jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange #SOC2022
👍11