JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ungana nasi katika Mjadala huu kupitia Clubhouse ya Jamiiforums

#Afya #JamiiForums #Cancer #Saratani
Yanayojiri katika Mjadala kuhusu Saratani kwa Watoto unaoendelea kupitia Clubhouse ya JamiiForums

Fuatilia > https://www.clubhouse.com/event/xlyWAOzz

#Saratani #Cancer
SARATANI NI NINI?

Miili yetu ina chembechembe hai nyingi ambazo huzaliana, hukua, na kufa kwa mpangalio maalum

Chembechembe za Saratani zinazaliana haraka zaidi bila mpangilio na kukua haraka

Zisipotibiwa mapema zinaweza kusambaa na kuota sehemu nyingine mwilini

Soma - https://jamii.app/SarataniOR

#JFAfya #Cancer #Saratani
NINI HUSABABISHA SARATANI?

Hakuna sababu moja, Saratani tofauti zina vyanzo vyake. Miongoni mwa Visababishi visivyozuilika ni Umri

Umri unapokuwa mkubwa, uwezekano wa kutokea dosari katika mabadiliko ya DNA yanayosababisha Kansa huongezeka

Baadhi ya Visababishi vinavyozuilika ni pamoja na uvutaji wa sigara, ulaji mbovu, kutumia pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi

Soma - https://jamii.app/SarataniOR

#JFAfya #Cancer #Saratani
SARATANI: Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya (WHO) Mwaka 2020 zinaeleza ongezeko la Visa vipya vya Saratani linakadiriwa kufikia Milioni 19.3, huku Vifo vikiwa Milioni 10

Ulimwenguni kote, inakadiriwa Visa vipya Milioni 28.4 vya Saratani vinaweza kutokea hadi kufikia Mwaka 2040, huku ongezeko kubwa likiwa katika Ukanda wa Nchi zinazoendelea

#JamiiForums #Cancer #JFData
SIKU YA KIMATAIFA YA UFAHAMU WA VIRUSI VYA PAPILLOMA - HPV

'Human Papilloma Virus' au #HPV ni kirusi ambacho husambaa kwa njia ya kujamiiana. Asilimia kubwa ya Watu wenye maambukizi ya HPV hupata vipele au #GenitalWarts, maumivu au Damu wakati wa Tendo, kuwashwa n.k

HPV huweza kusababisha aina mbalimbali za Saratani kwenye Mwili wa Binadamu ikiwemo Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani Njia ya Haja kubwa n.k. Takriban Saratani zote za Shingo ya Kizazi hutokana na HPV za aina mbili, HPV16 na HPV18.

Soma - https://jamii.app/HPVDay2022
#Afya #Cancer
Saratani inapogunduliwa mapema, uwezekano wa Matibabu kufanya kazi ni mkubwa zaidi

Ni muhimu kwa Watoto wanaomaliza Matibabu kuendelea kusimamiwa kwa karibu ili kugundua ikiwa Ugonjwa utarudi
-
#JamiiForums #JFAfya #ChildhoodCancer #Cancer #PublicHealth
👍5
KENYA: Katibu Mtendaji wa Umoja wa Kitaifa wa Walimu (KNUT) katika Tawi la Nandi, Boniface Tenai ametoa wito kwa Serikali kutenga Rasilimali za kutosha kukabiliana na Ugonjwa wa Saratani ambao umeshambulia idadi kubwa ya Watu nchini humo

Umoja huo umesema Ugonjwa wa Saratani umekuwa mzigo kwa Wananchi kutokana na gharama kubwa za Matibabu na kwamba familia nyingi zimekuwa Maskini baada ya kutumia mali zao zote kuhudumia Wagonjwa wao

Kila mwaka nchi hiyo inakadiriwa kuwa na visa vipya 39,000 vya Saratani na zaidi ya vifo 27,000 vitokanavyo na Ugonjwa huo, huku
Saratani zinazoongoza zikiwa ni za Matiti, Shingo ya Kizazi, Tezi Dume na Koo

Soma https://jamii.app/SarataniKenya

#JamiiForums #Cancer #CancerAwareness #CancerInKenya #Afya #PublicHealth
👍43