JamiiForums
56.2K subscribers
32.8K photos
1.86K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na hoja za upande wa utetezi na sasa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu halitaendeshwa kwa njia ya Mtandao badala yake Lissu atafikishwa Mahakamani hapo

Uamuzi huo umetolewa wakati wa mchakato wa kuendesha kesi hiyo kwa njia ya Mtandao, leo Mei 6, 2025 ambapo Mahakama ilikuwa inatoa maamuzi ya mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Lissu wakiongozwa na Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini kwenye shauri la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni likiwa ni shauri la 2 linalomkabili Lissu

Soma https://jamii.app/LissuKufikishwaMahakamani

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025
Mdau wa JamiiForums.com anasema anaipenda Kazi yake lakini hajui atumie mbinu gani kumwambia Mwajiri wake ukweli kuhusu tabia inayomkera ya kumgombeza mbele za Wateja

Hebu mpe Mdau ushauri wa kutatua changamoto hiyo

Mjadala zaidi https://jamii.app/BosiUkweliTabia

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories
DAR: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Mei 5, 2025 kilizindua ripoti ya hali ya Haki za Binadamu Nchini kwa Mwaka 2024 ambapo kuanzia Januari 2015 hadi Februari 2025, LHRC imerekodi jumla ya matukio 100 ya utekaji na kupotea kwa watu kwa njia isiyofahamika

Ripoti hiyo inaeleza Takriban theluthi mbili ya matukio hayo (64) yaliripotiwa Mwaka 2022 (31) na 2024 matukio 33. Hakukuwa na tukio lolote lililoripotiwa Mwaka 2019 na 2020. Zaidi ya theluthi moja ya matukio hayo (35%) yaliripotiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha (26%)

Mratibu wa Utafiti, Wakili Fundikila Wazambi amesema ripoti hiyo inaonesha wimbi la Watu kukamatwa na kutiwa kizuizini bila kufuata Sheria, ambapo matukio zaidi ya 600 ya Watu kukamatwa na kutiwa kizuizini yaliripotwa kwa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/LHRCReport2024

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #CivilRights #HakiZaBinadamu
ZANZIBAR: Chama cha #ACTWazalendo kimesema kinawasilisha malalamiko rasmi dhidi ya kauli na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja, Idrisa Kitwana Mustafa aliyoitoa Aprili 24, 2025 ya kuwataka Watumishi wa Umma wanaoishi Mkoani hapo kumkabidhi nakala za Vitambulisho vyao vya Kupigia Kura

Msemaji wa Ofisi - Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf amesema “Kauli hiyo inaelekeza matumizi mabaya ya madaraka kwa nia ya kuwatisha na kuwavunjia heshima Watumishi wa Umma, hivyo kuondosha dhana ya msingi wa Utawala Bora na dalili za kuingilia Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

ACT imetoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kukemea hadharani kauli hiyo, Kufanya uchunguzi huru na wa haraka na kutoa mapendekezo ya hatua stahiki, Kumtangaza RC Idrisa kuwa amekiuka misingi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu, hivyo hastahili kuendelea kushika nafasi ya Uongozi wa Umma.

Soma https://jamii.app/ACTDhidiYaRC

#JamiiForums #Accountability #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu205
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Peter Kibatala ambaye ni mmoja wa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ametoa wito kwa Wananchi watakaohudhuria kesi inayomkabili mteja wao katika Mahakama ya Kisutu, kuwa na utulivu ili wasije kufanya tukio ambalo linaweza kutumika kuwa kisingizio cha kuharibu mwenendo wa kesi

Awali kesi hiyo iliendeshwa kwa njia ya Mtandao lakini leo Mei 6, 2025 Mahakama imeruhusu Umma kuhudhiria kesi hiyo itakayotajwa tena Mei 19, 2025 katika Mahakama ya Wazi

Zaidi https://jamii.app/KibatalaMei6

#JFMatukio #JamiiForums #Democracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Kampuni 95 zilizopewa Leseni za Uchimbaji Madini na hazijafanyiwa kazi inavyotakiwa atazifutia Leseni hizo

Amesema hayo, leo Mei 6, 2025 bila kutaja majina ya wawekezaji hao na kwamba Wizara yake imetoa siku 30 kwa wahusika kujieleza na kama hakutakuwa na mrejesho sahihi Leseni zitafutwa hata kama zina majina ya 'Watu wakubwa'

Soma https://jamii.app/MavundeLeseni

#Uwajibikaji #Accountability #JamiiForums
UTEUZI: Rais Samia amemteua Lazaro Jacob Twange kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akichukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kufariki kwa ajali Mkoani Mara usiku wa kuamkia Aprili 13, 2025

Kabla ya uteuzi huo Twange alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, ambapo nafasi hiyo itashikwa na Albert Gasper Msando akitokea Wilaya ya Handeni

Soma https://jamii.app/TwangeEDmpyaTanesco

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
Leo Mei 6, 2025, IMS, JamiiAfrica na UTPC kwa pamoja wamezindua Mradi wenye lengo la “Kuwawezesha Wanahabari kwaajili ya Jamii yenye taarifa sahihi Tanzania.”

Kupitia ushirikiano huu, Wanahabari watajengewa uwezo wa kuelewa mahitaji ya jamii na kutayarisha maudhui yanayoendana nayo, tafiti zitafanyika kutambua na kujaribu mbinu anuai za kupambana na upotoshaji na Vyombo vya Habari vitawezeshwa kuweza kutekeleza mbinu hizo kwa manufaa ya Umma

Soma https://jamii.app/JamiiAfricaIMSUTPC

#JamiiForums #JamiiAfrica #CitizenEmpowerment #PressFreedom
Watoto hujifunza kwa kuangalia, si kwa kusikiliza tu. Ikiwa tunataka wawe Wapole, Waadilifu na wenye Heshima, basi nasi tuwe mfano wa hayo. Maneno yana nguvu, lakini matendo yetu ndiyo yanayowalea.

#MaleziBora #JamiiAfrica #JamiiForums #GoodMorning #AmkaNaJF #ParentingInAction
MBEYA: Mimi ni Mkazi wa Isyesye, tunashukuru kwa maboresho ya barabara yanayofanyika lakini anayehusika kutengeneza njia ya michepuko (diversion) hajatengeneza na zilizopo hazipitiki, tunapata shida sana

Mkandarasi anafunga barabara pasipo kuweka alama za kuonesha tunatakiwa kupita wapi matokeo yake tunapita vichochoroni kwenye njia zisizo rasmi, hiyo ni mbaya kwa Vyombo vya Usafiri vinavyotumika

Soma https://jamii.app/MbeyaMkandarasi

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability