JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika mdahalo kuhusu amani na #Demokrasia uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC, Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma amesema "Kama kuna mtu alisema atakinukisha naona kama sasa hivi ananuka yeye".

Soma zaidi https://jamii.app/Watakaokinukisha

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza na East Afrika Redio, leo Agosti 20, 2025, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo, Monalisa Ndala amesema hakubaliani na utaratibu wa chama chake kuchukua wagombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (#CCM), akidai wengi wao wanaenda Upinzani kutafuta jukwaa la kutoa nyongo na kujibizana kisha baada ya Uchaguzi hurudi CCM.

Baadhi ya Wanasiasa wakubwa kutoka CCM waliowahi kuhamia vyama vya upinzani wakati wa Uchaguzi na kisha kurejea ni marehemu Bernard Membe (ACT), Edward Lowassa (#CHADEMA) na Frederick Sumaye (CHADEMA)

Soma https://jamii.app/MpinaNdala

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa ameibua hoja kuhusu wimbi la baadhi ya Watu maarufu na Wanasiasa kujipendekeza kwa Watawala maarufu kama ‘uchawa’ hali ambayo imeonekana kuzidi kushamiri kadri joto la Uchaguzi linavyopanda.

Amedai kuwa tabia hiyo haimfurahishi kwani inaleta madhara kwa Taifa, ikiwemo kupotosha Wapiga Kura na kuharibu mwelekeo wa Demokrasia.

Je, Wanasiasa wanaojipendekeza wanatafuta nafasi za Uongozi kwa maslahi ya Taifa na Wananchi, au ni kwa ajili ya maslahi yao binafsi?

Zaidi Soma https://jamii.app/KujipendekezaWagombea

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025
1👍1
Salum Mwalimu alianza safari yake ya #Siasa kikamilifu Mwaka 2014 ambapo aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa #CHADEMA upande wa Zanzibar, alishika nafasi mbalimbali katika chama hicho na sasa amechaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha #CHAUMMA.

Uamuzi wa kuhamia CHAUMMA alitangaza rasmi Mei 19, 2025 baada ya maamuzi ya Salum na Wanachama wengine wa CHADEMA kujitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na maamuzi ya Uongozi mpya ikiwemo kutoshiriki Uchaguzi Mkuu 2025 pamoja na madai ya chama kupoteza dira.

Zaidi https://jamii.app/SalumMwalimuWasifu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Transparency #UchaguziMkuu2025 #PresidentialCandidates #Siasa
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Mahusiano ameeleza changamoto anayopitia katika ndoa yake ya Miaka mitatu, akiwa na mke na Mtoto mmoja wa Kike.

Anasema ana tabia ya kuacha pesa kwenye 'wallet' na alianza kuhisi kama hela zinapungua lakini hakuwa na uhakika hivyo akaamua kuwa makini ili ajue kama kweli pesa yake inatolewa.

Amesema siku moja aliweka Tsh. 70,000 kwenye wallet lakini baada ya siku kadhaa alipokagua alikuta kuna Tsh. 55,000 alimuuliza mke wake kuhusu hela hiyo mwanzo alikataa lakini baadaye akakubali baada ya kumbana na akairudisha, pia alikiri alishawahi kuchukua pesa nyingine bila ruhusa.

Unamshauri nini Mdau kuepuka changamoto hiyo?

Mjadala zaidi soma https://jamii.app/MkeMdokozi

#JamiiForums #Maisha #JFStories #Mikasa #JFLifestyle
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (#Sugu) akizungumza leo Agosti 20, 2025 amesema “Ifike mahali tukae kama Taifa tuzungumze ili kusaidia nchi yetu, kusaidia isiingie kwenye machafuko ni uzalendo wa kweli kwa Taifa, sio mpaka tuumizane, tuuane wenyewe kwa wenyewe kama ilivyotokea Kenya Mwaka 2007 ndio tukae mezani, haifai.”

Zaidi soma https://jamii.app/SuguMachafuko

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Askofu Gervas Nyaisonga amewaasa vijana kutojishughulisha na dhambi ya mauaji pamoja na matukio ya utekaji akisisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki juu ya uhai wa mtu mwingine.

Ameyasema hayo leo Agosti 20 wakati wa mahubiri kwenye Misa Takatifu ya Ufunguzi wa Kongamano la 6 la Viwawa Taifa ambalo linafanyika Jimbo kuu la Mbeya katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya.

Zaidi soma https://jamii.app/MshirikiDhambiMauaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akihojiwa Julai 23, 2023 katika kipindi cha Power Breakfast cha #CloudsTV, alieleza kuwa hakuna kitu kinachoitwa Udikteta nusu. Alifafanua kuwa Udikteta ni kuwanyima Watu fursa ya kutoa maoni.

Zaidi soma https://jamii.app/KikweteUdikteta

#JamiiAfrica #JamiiForums #UtawalaBora #Governance #JFKumbukizi
Mdau, imekuchukua muda gani kuiona herufi 'O'?

Ndivyo ilivyo hata kwenye maisha, vitu vizuri havipatikani kwa haraka, unahitaji subira!

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia ameizawadia Timu ya Taifa ya Tanzania #TaifaStars kiasi cha Tsh. Milioni 200 ikiwa ni sehemu ya motisha kuelekea mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Morocco katika Michuano ya CHAN, unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa Agosti 22, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akikabidhi Fedha hizo jana Agosti 20, 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema “Tumekuja kuwapongeza kwa hatua kubwa mliyofikia pamoja na kuwatakia heri kwa mchezo ujao dhidi ya Morocco.”

Soma zaidi https://jamii.app/SamiaStars

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
1