JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI YAHIMIZA RAIA WAKE KUONDOKA UKRAINE

Ni kutokana na vitisho vya Urusi kuchukua hatua za Kijeshi kuongezeka. Rais Biden asema hatotuma Vikosi kuokoa Wamarekani ikiwa Ukraine itavamiwa

Urusi imekuwa ikikataa kuwa na Mipango ya kuvamia Ukraine

Soma https://jamii.app/USUkraine

#Governance
JE, WAJUA: Utafunaji wa Chingamu (Maarufu Big G/Jojo) ulipigwa Marufuku Nchini #Singapore tangu Mwaka 1992 kwa lengo la kuhifadhi Mazingira na kuyaweka Safi

Mnamo Mwaka 2004, Marufuku hiyo ilifanyiwa marekebisho na kuruhusiwa kwa Chingamu zinazotumika kwa Matibabu ya Kinywa ambazo hununuliwa Hospitalini au Famasi

#JamiiForums #JFMaarifa
MDAU: MZAZI NI KIUMBE WA KIPEKEE SANA

Anasema Siku zote ni ngumu Mzazi kutoa laana kwa Mtoto, lakini hii haimaanishi laana hazitoki. Laana na Baraka hutokana na mapokeo ya Moyo kwa kile anachotendewa na Mtoto wake

Ukiona Mzazi anaomba msaada kwa Mwanaye tambua ana shida kweli kwasababu Wazazi wengi hawapendi kuonekana wasumbufu

Soma, zaidi - https://jamii.app/MzaziMtoto

#JFMdau
VIJANA TUWE WABUNIFU, WAAMINIFU NA TUSAIDIE JAMII ZETU

Mdau anasema wimbi kubwa la Vijana wamekuwa Wavivu wa kubuni, wanatumia muda mwingi katika starehe zisizo za ulazima na hata kukosa muda wa kupumzika. Wanasahau kufikiria kuisaidia Jamii

Kuishi ndani ya matendo na kauli nzuri kutafanya wajenge thamani katika Jamii

Msome - https://jamii.app/UshauriVijanaSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
Jamii Forums kwa kushirikiana na Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS), Muhimbili National Hospital (MNH), Tumaini la Maisha (TLM) na Wadau wengine wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini #Tanzania

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022 ambapo Wataalamu mbalimbali wa #Afya wataeleza kwa kina kuhusu Saratani ya Watoto na namna ya kukabiliana nayo

Je, una swali gani au ungependa kufahamu nini kuhusu hali ya #Saratani kwa Watoto? Karibu ujiunge nasi katika Mjadala huu.

#JamiiForums #CancerDay2022 #JFAfya
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa

Ametoa kauli hiyo alipofika Muhimbili leo kumjulia hali

Soma - https://jamii.app/SerikaliProfJ

#JFAfya
MADAGASCAR: WALIOFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA BATSIRAI WAFIKIA 111

#Batsirai kilikuwa Kimbunga cha pili kuathiri Taifa hilo ndani ya muda wa siku 14

Kimbunga Ana kilisababisha Vifo 55 na kupelekea Watu wapatao 130,000 kukosa Makazi

Soma - https://jamii.app/Batsirai111

#JFMatukio
BUNGENI: Mgombea pekee wa nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu (Mbunge wa Ilala) amepata 98.33% ya Kura zilizopigwa

Wabunge 301 walipiga Kura, 296 wamepiga Kura za Ndiyo, 3 wamepiga Kura ya Hapana na Kura 2 zimeharibika

Soma - https://jamii.app/ZunguNaibuSpika

#Democracy
TANZANIA NA UFARANSA ZASAINI MIKATABA SITA

Miongoni mwa Makubaliano ni Mkataba wa Mkopo wa Masharti Nafuu wa Euro Milioni 178 kwa ajili ya kugharamia Mradi wa Ujenzi wa Barabara wa Mabasi Yaendayo Haraka

Soma - https://jamii.app/MikatabaTZFrance

#Governance
#SUDAN: Wanaharakati wanaopinga Mapinduzi wamesema zaidi ya Watu 2,000 wakiwemo Waandishi wa Habari, Wanasiasa wanaokosoa Jeshi na Watetezi wa Haki za Binadamu wamekamatwa bila kushtakiwa tangu Jeshi lilipopindua Serikali Oktoba 2021

Soma - https://jamii.app/SudanArrests
#Democracy
MDAU: WAHITIMU WA VYUO VIKUU WANA MITAZAMO HASI KUHUSU AJIRA

Mdau anasema Wahitimu wa Vyuo wengi wanachagua Kazi kwa kujiona wana hadhi kubwa sana kuliko ambao hawana Elimu kama yao

Aidha, wana mtazamo kwamba kutoajiriwa na Serikali ni kuonewa na kutotendewa Haki hivyo hushinda vijiweni na kwenye Mitandao kuilaumu Serikali

Una maoni gani kuhusu hoja ya Mdau huyu?

Shiriki Mjadala - https://jamii.app/MitazamoVijanaVyuo

#JFMdau
MATAIFA MBALIMBALI YAWATAKA RAIA WAKE KUONDOKA UKRAINE

Baadhi ni Ujerumani, Uingereza, Australia, Canada, Norway, Denmark na Japan

Marekani imeonya kuwa Urusi inaweza kuivamia kijeshi Ukraine muda wowote, jambo ambalo Urusi imekuwa ikikanusha

Soma - https://jamii.app/UkraineCrisis

#Governance
Jamii Forums kwa kushirikiana na Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS), Muhimbili National Hospital (MNH), Tumaini la Maisha (TLM) na Wadau wengine wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini #Tanzania

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022 ambapo Wataalamu mbalimbali wa #Afya wataeleza kwa kina kuhusu Saratani ya Watoto na namna ya kukabiliana nayo

Je, una swali gani au ungependa kufahamu nini kuhusu hali ya #Saratani kwa Watoto? Karibu ujiunge nasi katika Mjadala huu.

#JamiiForums #CancerDay2022 #JFAfya
CHELSEA YAWA KLABU BINGWA YA DUNIA

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuwa Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kuifunga Klabu ya Palmeiras goli 2-1 baada ya dakika 120

Chelsea imeshinda taji hilo kwa mara ya kwanza. Ilishindwa kupata taji hilo 2013 ilipofungwa na Klabu ya Corinthians

#JFSports
NORWAY YAONDOA VIZUIZI VYA #COVID19

Waziri Mkuu asema raia wake wanalindwa vyema kwa Chanjo ya #CoronaVirus

Watu hawatolazimika kuvalia Barakoa ktk maeneo ya Umma wala kukaa umbali wa Mtu na Mtu. Watakaoathirika watakaa Nyumbani siku 4 tu

Soma - https://jamii.app/NoCoronaNorway

#UVIKO3 #JFAfya
UJERUMANI: Raia wanamchagua Rais leo, Februari 13, 2022 kupitia Baraza la Wabunge na Wajumbe wa Majimbo yote 16

Rais wa Ujerumani huchaguliwa kila baada ya miaka 5 ambaye huwa Mkuu wa Nchi, tofauti na Kansela ambaye ni Mkuu wa Serikali

Soma - https://jamii.app/ElectionGermy

#Democracy
DAR: SOKO LA RANGITATU LAUNGUA MOTO

Soko hilo lililopo Mbagala limeungua usiku wa kuamkia leo (Februari 13, 2022) na Chanzo hakijafahamika

Matukio ya moto yameendelea kuripotiwa Nchini. Je, hatua stahiki zinachukuliwa kutatua changamoto hii?

Soma - https://jamii.app/MotoSokoMbagala

#JFMatukio #Accountability
Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio. Licha ya ukuaji wa Sayansi na Teknolojia, Redio imeendelea kuwa moja ya Vyombo vya Habari vinavyotumika na kuaminika zaidi

Hii ni kwasababu inaweza kusikilizwa kokote, hata maeneo yasiyo na Umeme wala Intaneti ya Uhakika. Kwa kiasi kikubwa, Redio imeziba pengo la kupata taarifa katika Jamii

#WorldRadioDay
TANZIA: EDWIN RUTAGERUKA AFARIKI DUNIA

Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka amefariki dunia leo, Februari 13, 2022

> Rutageruka aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)

#RIPRutageruka
TUNISIA: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA RAIS SAIED KUJIONGEZEA MADARAKA

Rais wa #Tunisia, Kais Saied, ameimarisha Madaraka yake dhidi ya Mahakama baada ya kutangaza Kanuni inayomruhusu kuwafukuza kazi Majaji au kuwazuia kupandishwa cheo

Soma - https://jamii.app/KaisTunisia

#Democracy
Jamii Forums kwa kushirikiana na Muhimbili University of Health and Applied Science (MUHAS), Muhimbili National Hospital (MNH), Tumaini la Maisha (TLM) na Wadau wengine wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini #Tanzania

Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022

Link > https://jamii.app/MjadalaSarataniWatoto

#JamiiForums #CancerDay2022 #JFAfya