JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akitoa amri kuhusu kesi dhidi ya Tundu Lissu kurushwa moja kwa moja (#LiveStreaming), Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga amesema kuchapisha na kusambaza nakala zenye ushahidi au ushahidi wowote utakaoweza kufichua mashaidi wa kiraia kesi ya Lissu inakatazwa na ni marufuku bila idhini ya Mahakama.

Pia ameongeza kwa kusema “Mtu au Vyombo vya Habari vinavyotaka kuchapisha habari kuhusu mwenendo wa kesi ya Lissu “committal proceedings” au mashahidi ni lazima vipeleke maombi mahakamani ili kuonesha kuhariri na kuondolewa kwa utambulisho na Mahakama kuu umekamilika na uchapishaji hautafichua utambulisho wa mashahidi wanaolindwa na Mahakama”

Soma https://jamii.app/VibaliMahakamaKesiLissu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Imam wa Msikiti wa Manyema, Sheikh Hameed Jongo akizungumza wakati wa kutoa hotuba ya Ijumaa Agosti 15, 2025 amesema kuwa Rais Samia anatenda haki na kufanya vizuri katika uongozi wake ndiyo maana wafanyabiashara wamechangia kikubwa walichochangia.

Ameongeza kuwa kuna Wanawake wana uwezo wa kuongoza kuliko wanaume, uongozi uliopita tumeona jinsi wanaume walivyoongoza, awamu hii ya sita Rais Samia anaongoza 'Fantastic'.

Soma https://jamii.app/HarambeeCCMAmani

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSiasa #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) ya kutaka kutenguliwa kwa uamuzi wa Juni 10, 2025, uliowazuia kuendelea na shughuli za Kisiasa kwa kutumia mali za Chama.

Uamuzi huo mdogo umetolewa leo Agosti 18, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA kuhusu mgawanyo wa rasilimali kati ya Chama hicho Bara na Upande wa Zanazibar.

Wakili wa CHADEMA, Hekima Mwasipu amesema Jaji Mwanga baada ya kukataa maombi yao, pande zote zimekubaliana kuendelea na shauri ambapo Mahakama imeahirisha kesi hadi Agosti 28, 2025 kwa mapitio ya hoja zinazobishaniwa na kupanga utaratibu wa kuendelea na kesi kuu.

Zaidi soma https://jamii.app/OmbiLaChadema

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapejo ameeleza ukomo wa matumizi ya fedha kwa Wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo katika nafasi za Urais ni Tsh. Bilioni 9, Udiwani Tsh. Milioni 16 na katika majimbo imezingatiwa idadi ya Watu, ukubwa wa majimbo na miundombinu na ukomo wa juu ni Tsh. Milioni 136.

Ameeleza hayo katika mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa yaliyofanyika leo Jumatatu Agosti 18, 2025 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (#JNICC).

Zaidi soma https://jamii.app/UkomoPesaUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSiasa #UchaguziMkuu2025 #JFDemocracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Tume ya Uchaguzi (ZEC), leo Agosti 18, 2025, imesema kuwa kampeni za Uchaguzi Mkuu zitaanza rasmi Septemba 11, 2025, Saa 10:01 Jioni mara baada ya uteuzi wa Wagombea na zitaendelea hadi siku ya mwisho kabla ya upigaji kura Oktoba 29, 2025.

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Goerge Joseph Kazi amesema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za Wagombea wa Urais, Baraza la Wawakilishi na Udiwani utafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 10, 2025 Saa 10:00 Jioni, na uteuzi rasmi kufanyika Septemba 11, 2025 Saa 10:00 Jioni kabla ya kuanza kwa kampeni.

Zaidi soma https://jamii.app/UchaguziZbar

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda, leo Jumatatu Agosti 18, 2025 amefafanua suala la Mtoto Mkazi wa Nyakato, Wilayani Ilemela aliyesemekana kulawitiwa na Steven Ibasa (Baba Claudia), kwa kueleza kuwa suala hilo limefikishwa Mahakamani na kwamba mtuhumiwa amekosa mtu wa kumdhamini, amepelekwa Gerezani Butimba.

Akiwa ofisini kwake, RC Mtanda amewataka Wananchi kuwa na imani na Muhimili wa Mahakama kwakuwa utatenda haki katika suala hilo.

Ikumbukwe, suala hilo liliibuliwa na Mdau wa JamiiForums.com akidai kuna mazingira ya kumlinda Mtuhumiwa huyo ambaye alishikiliwa katika Kituo cha Polisi Nyakato kisha Kituo cha Polisi Kirumba, hivyo akaomba Mamlaka za Juu kuingilia kati ili Haki ipatikane.

Soma zaidi https://jamii.app/SaidMtandaUpdates

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa kwenye Ukumbi wa #JNICC, Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (#ADC), Shaban Itutu amelalamikia kile alichodai ni unyanyasaji wa Polisi dhidi ya Wagombea wasiotokana na dola.

Ametoa wito kwa mamlaka kuwaalika katika Mikutano inayohusisha Vyama vya Siasa ili wajifunze kuwa kazi yao siyo kuwatisha na kuwakamata Wanasiasa.

Soma https://jamii.app/PolisiUchaguziWanasiasa

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFSiasa #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Zaidi ya wanachama 50 wa CCM kutoka Kata ya Minepa, Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, wametishia kurudisha kadi zao za uanachama baada ya kulalamikia mchakato wa kura za maoni za udiwani. Wanachama hao wanadai kuwa Mtia nia aliyeshinda, Marugu Manosu hajapewa barua ya utambulisho badala yake amepewa mshindi wa nafasi ya pili.

Wanachama hao walifika katika Ofisi ya CCM Mkoa Morogoro wakitaka majibu ya wazi kuhusu hatua hiyo. Kwa upande wake, Manosu amesema licha ya kufuatilia suala hilo katika ngazi mbalimbali za chama, ameambiwa mchakato bado unaendelea bila kuelekezwa mwisho wake, hali ambayo imezidisha sintofahamu kwa wafuasi wake.

Soma zaidi https://jamii.app/WanachamaCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
NJOMBE: Mkuu wa Wilaya ya Makete, Kissa Kasongwa amewataka Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kuwa wazalendo na kuilinda Nchi kwa wivu mkubwa ambapo pia ametoa ahadi ya Serikali kuwatumia kwa ajili ya kutazama usalama katika kipindi cha Uchaguzi.

DC Kissa ameeleza hayo Agosti 17, 2025 wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu kwa vijana zaidi ya 50 wa Kata ya Tandala wilayani humo.

Soma zaidi
https://jamii.app/MgamboKutumikaUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025