JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na aliyekuwa Kada wa CCM, Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa ambayo ilipangwa kusikilizwa Agosti 14, 2025 imeahirishwa hadi Jumanne Agosti 19, 2025.

Shauri hilo linapinga uhalali wa mchakato uliotumika kumpata mgombea wa Urais wa CCM pamoja na Mgombea Mwenza. Dkt. Malisa alipotafutwa kwa simu, amesema shauri hilo limesogezwa hadi Agosti 19, ambapo mawakili wa CCM watatoa utetezi wao.

Awali, kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2025 ambapo Mahakama ilibainisha kuwa ina hoja za msingi zinazostahili kuamuliwa Mahakamani.

Soma https://jamii.app/KesiYaMalisaNaSamia

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
1
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la JF Chit-Chats and Jokes, ameuliza kwenye ajira, Waajiri huwa wanaangalia nini zaidi wakati wa usaili wa kazi? Je, ni CV yako ilivyoandikwa? Uzoefu wa kazi ulionao? Kipaji? Ufaulu wako (GPA)? Au ni Chuo ulichosoma ndicho chenye uzito mkubwa?

Wewe unaamini nini huwa kinaamua zaidi hatma ya muombaji?

Kushiriki mjadala huu bonyeza https://jamii.app/SifaZaKuajiriwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa watoaji maudhui mtandaoni wanaokiuka Sheria za huduma za Utangazaji na kusema haitasita kuchukua hatua kali kwa wanaojihusisha na utoaji wa huduma hizo bila leseni.

Taarifa ya Mamlaka hiyo ya Agosti 16, 2025 imesema Watoa huduma za Mawasiliano ya Simu wanatakiwa kuhakikisha Maudhui ya arafa za mkupuo (bulk messages) kuelekea, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025 yanazingatia Sheria na Kanuni zote za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Uhakiki wa maudhui ufanywe kabla ya kusambaza arafa za mkupuo zinazohusika.

Pia, TCRA imewataka watoa huduma kuhakikisha Maudhui yote yanayohusiana na shughuli za Uchaguzi Mkuu yanapata idhini kutoka kwa taasisi au uongozi wa chama cha #Siasa husika na wanapaswa kuhifadhi kumbukumbu za arafa zote zinazotumwa kwa wingi kwa kipindi kinachotakiwa kisheria kwa ajili ya uthibitisho endapo utahitajika.

Soma https://jamii.app/HudumaMaudhuiBilaLeseni

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #DigitalRights #KuelekeaUchaguzi2025
2
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), leo Agosti 17, 2025 kimetoa taarifa kikieleza Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilivamia kikao cha Chama hicho kilichokuwa kikifanyika, Agosti 16, 2025, Kibaha - Pwani na kuwakamata Wanachama Sita na raia waliokuwa jirani na eneo la kikao.

Taarifa ya Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, imeeleza waliokamatwa ni Pendo Msechu, Pendo Kyosi, Mary Mushi, Samson Mzambia, Focus Laurent na Alfred Bundala ambao wamepelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central), lakini Polisi wa kituo hicho walikana kuendelea kuwashikilia.

Upande wa Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa Agosti 16, 2025, limewakamata Watu 10 waliokuwa katika Ukumbi wa Mwitongo, Mailimoja Shule kwa maelezo kuwa walikuwa wakipanga njama za kufanya uhalifu.

Zaidi soma https://jamii.app/ChademaKibaha

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #JFMatukio #UchaguziMkuu2025
ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imeanza vibaya msimu wa 2025/26 kwa kukubali kichapo cha Goli 1-0 kutoka kwa Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo katika Premier League.

Goli pekee limewekwa wavuni na beki Riccardo Calafiori akimalizia mpira wa kona dakika ya 13.

Mechi ijayo ya United ni dhidi ya Fulham (Agosti 24, 2025), #Arsenal itavaa Leeds United (Agosti 23, 2025).

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #JFEPL2025
Tembelea JamiiForums.com kusoma kwa undani habari hizi na mengine mengi yaliyojiri juma lililopita.

#JamiiAfrica #JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 18, 2025 imepanga kutoa amri kuhusu kurushwa mubashara (LIVE) kwa maelezo ya mashahidi wa siri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu sambamba na kusikiliza vielelezo vitakavyotumika.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alieleza kuwa kurushwa mubashara mwenendo huo ni sawa na kuchapisha ushahidi na kunaweza kukiuka uamuzi wa Mahakama Kuu wa Agosti 4, 2025 uliolenga kulinda utambulisho wa mashahidi.

Lissu alipinga hoja hiyo akieleza uamuzi huo ulikataza kufichua majina na anuani za mashahidi pekee, hivyo akaomba kesi iendelee kurushwa mubashara bila kuathiri usiri wao.

Zaidi soma https://jamii.app/KesiYaLissuLive

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mvutano umezuka ndani ya Ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya eneo linalotakiwa kukaliwa na viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kujazwa na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi waliovaa nguo za kiraia, kinyume na utaratibu.

Hali hiyo ilisababisha wanachama hao kushindwa kupata nafasi ya kukaa ili kufuatilia mwenendo wa Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wao, Tundu Lissu.

Soma zaidi https://jamii.app/MvutanoMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akitoa amri kuhusu kesi dhidi ya Tundu Lissu kurushwa moja kwa moja (#LiveStreaming), Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga amesema Mahakama imesitisha matangazo ya moja kwa moja (LIVE), utangazaji, usambazaji wa moja kwa moja au aina nyingine ya uenezaji wa moja kwa moja kwa umma ikijumuisha na mitandao ya kijamii hadi pale itakapotolewa amri nyingineyo.

Soma zaidi https://jamii.app/KuripotiLissuKibaliMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akitoa amri kuhusu kesi dhidi ya Tundu Lissu kurushwa moja kwa moja (#LiveStreaming), Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga amesema kuchapisha na kusambaza nakala zenye ushahidi au ushahidi wowote utakaoweza kufichua mashaidi wa kiraia kesi ya Lissu inakatazwa na ni marufuku bila idhini ya Mahakama.

Pia ameongeza kwa kusema “Mtu au Vyombo vya Habari vinavyotaka kuchapisha habari kuhusu mwenendo wa kesi ya Lissu “committal proceedings” au mashahidi ni lazima vipeleke maombi mahakamani ili kuonesha kuhariri na kuondolewa kwa utambulisho na Mahakama kuu umekamilika na uchapishaji hautafichua utambulisho wa mashahidi wanaolindwa na Mahakama”

Soma https://jamii.app/VibaliMahakamaKesiLissu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance