JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu ameutaka uongozi wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati kuhakikisha wanawalipa Wakulima waliocheleweshewa malipo yao Agosti 13, 2025.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya JamiiForums.com kuripoti malalamiko ya Wakulima hao mnamo Agosti 11, 2025 ambao walidai licha ya maelekezo ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutoa maagizo kuwa walipwe kabla ya Sikukuu ya Nanenane 2025 lakini haikuwa hivyo.

Awali Agosti 11, 2025, alipoulizwa kuhusu malipo hayo, Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati, Zaituni Tembo alisema “Kimsingi hatujalipa, tulifunga masoko tangu Julai 11, 2025 sababu Kampuni ambayo tunafanya nazo biashara haikutulipa.”

Soma https://jamii.app/WakulimaKulipwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #JFEconomy #Accountability
MAREKANI: Mtanzania Subiro Osmund Mwapinga amekamatwa nchini Ghana, Aprili 8, 2025 baada ya Idara ya Kudhibiti Dawa za Kulevya ya Marekani (DEA) kutoa taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini humo kuwa anahusika katika mpango wa kusambaza silaha kwa moja ya magenge ya biashara ya Dawa za Kulevya.

Alikamatwa na baadaye kukabidhiwa Marekani mnamo Julai 25, 2025 ambapo Subiro ni miongoni mwa watuhumiwa wanne wa kigeni ambao walikuwa na mpango wa kusambaza silaha zenye thamani ya Tsh. Bilioni 150 (Dola Milioni 58).

Watuhumiwa wengine ni kutoka Kenya na Bulgara, iwapo watapatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha Miaka 10 au kifungo cha Maisha.

Soma zaidi https://jamii.app/MtanzaniaSilahaGenge

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #JFMatukio
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JF Kumbukizi: Aliyekuwa Mbunge wa Kawe kupitia #CCM, Askofu Josephat Gwajima, aliwahi kusema kuwa mafanikio ya mtu hupimwa wakati hayupo.

Alisisitiza kuwa mafanikio ya kweli ni yale yanayoendelea kuishi hata baada ya waanzilishi kutokuwepo, alichokiacha kinatakiwa kuongea bila muhusika kuzungumza.

Soma zaidi https://jamii.app/WanasiasaZilizobamba

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #Uwajibikaji #UtawalaBora #Siasa #JFKumbukizi
4👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa tisa wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU), Wilaya ya Mjini Unguja Agosti 13, 2025, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema kumfundisha Mtoto ndani ya chumba hakumpi nafasi Mwanafunzi kujifunza kwani Watoto wanahitaji eneo la kutosha ili kujifunza.

Waziri Lela amesema hayo yanafanyika kutokana na baadhi ya Wazazi kuendelea kuwapeleka Watoto wao katika maeneo hayo ambayo hayakidhi vigezo vya kuwafundisha Watoto hasa ngazi ya awali, hivyo Serikali imepiga marufuku shule ambazo zipo ndani ya nyumba (skuli nyumba) na kuwataka wamiliki kujenga majengo yanayokidhi utoaji wa huduma kwa Wanafunzi wao.

Ikumbukwe, Mwaka 2023, Ripoti ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ilionesha vitendo vya ukatili wa kijinsia vimeripotiwa kuongezeka #Zanzibar kutoka matukio 1,222 Mwaka 2021 hadi 1,360 Mwaka 2022, ambapo kati ya hayo matukio 1,173 yalijumuisha Watoto.

Soma zaidi https://jamii.app/SkuliNgumbaMarufuku

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFElimu #Uwajibikaji #Accountability #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU) imewakamata Wajumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Kata ya Nyankumbu walioonekana katika picha mjongeo wakigawana rushwa Agosti 2, 2025 katika mchakato wa uchaguzi ndani ya #CCM.

TAKUKURU imeeleza kuwa baada ya tukio hilo kusambaa, ofisi ya mkoa ilichukua hatua ya haraka kwa kuwatambua na kuwakamata wajumbe waliokuwa wakionekana kwenye picha hizo na kwamba Inadaiwa kuwa vitendo hivyo vilifanyika mara baada ya zoezi la kuwanadi wagombea Ubunge kukamilika.

Aidha, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa, James Ruge amesema kutokana na matukio hayo na mengine, ofisi imeanzisha uchunguzi unaoelekea kukamilika, ikiwa ni hatua ya kukusanya ushahidi ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi ya wahusika.

Zaidi soma https://jamii.app/WajumbeUWTTuhumaRushwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #UchaguziMkuu2025 #KataaRushwa
2
GEITA: Jeshi la Polisi linawashikilia Askari wanne wa Jeshi la Uhifadhi (JESHI USU) kwa tuhuma za mauaji ya Eziboni Fikiri (20), Mkulima, Mkazi wa Kijiji cha Msonga, Wilaya ya Bukombe ambaye walimkuta akikata mti eneo la Pori la Hifadhi ya Kigosi, Wilaya ya Bukombe, Agosti 13, 2025.

Taarifa ya Polisi imesema Mwili umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya uchunguzi huku Watuhumiwa wakihojiwa na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.

Ikumbukwe hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni saa chache tangu Mdau wa JamiiForums.com awasilishe andiko akitoa wito kwa Jeshi la Polisi na TFS kufuatilia tukio hilo akidai kuna ukimya na hatua hazijachukuliwa.

Soma https://jamii.app/Askari4MauajiGeita

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji
🤬1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Bereko na Kisese Wilayani Kondoa wametaka mchakato wa kura za maoni za Udiwani na Ubunge wa Kondoa Vijijini urudiwe, wakisema mchakato huo uligubikwa na madai ya #Rushwa na kwamba Viongozi waliochaguliwa kwenye mchakato huo walipendelewa.

Akijibu tuhuma hizo Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Abdulrahim Dogo alipozungumza na ITV amesema “Kura za maoni haimaanishi aliyeongoza kwenye Kura za maoni ndio mshindi na ndio Kanuni yetu ya Uchaguzi, isipokuwa tu kura hizo zimepigwa kwa ajili ya kuvisaidia vikao vya juu vifanye uteuzi wa mwisho.”

Zaidi Soma https://jamii.app/KuraZaMaoniKondoa

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Accountability #Democracy
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na Sekta ya Elimu kuheshimu uhuru wa Vyuo Vikuu katika kuandaa na kusimamia mitaala ili kuondoa mkanganyiko na mabadiliko yasiyo na tija kwenye mitaala hiyo na fani mbalimbali.

Amedai maelekezo yasiyo wazi kutoka mamlaka za udhibiti wa mitaala yamesababisha mkanganyiko na baadhi ya fani kufutwa, akitoa mfano wa Chuo cha #UDOM ambapo Programu ya Education with Psychology ilisitishwa bila ya alichokiita “mashauriano ya kutosha” kati ya chuo na mamlaka husika kufanyika.

Ameshauri mamlaka zishauriane na Vyuo Vikuu na kuhusisha wabobezi pamoja na Sekta Binafsi kabla ya kubadilisha au kusitisha mitaala ili kuhakikisha mitaala hiyo ina manufaa ya muda mrefu na ushindani wa Kimataifa.

Mjadala zaidi Soma https://jamii.app/FaniVyuoni

#JamiiForums #JFElimu #JFMdau2025 #Accountability
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kufuatilia tukio analodai linadalili za ‘kuminywa’ linalohusu Mtoto wa Kiume wa Miaka Minne Mkazi wa Nyakato kulawitiwa na jirani yake na kwamba suala hilo lilipofikishwa Kituo cha Polisi Kirumba kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu kinachoendelea.

Mdau anadai Mtoto anaishi na bibi yake, alipofanyiwa ukatili huo mara mbili mtuhumiwa alimwambia asiseme kwa kuwa akisema bibi yake ‘atamchapa sana’. Bibi alipoona mjukuu anatembea kwa kuchechemea akamlazimisha kusema nini kimemsibu, ndipo Mtoto akaelezea na kumtaja jirani yao.

Mdau anaongeza kuwa Bibi na Mtoto walipoenda kuripoti Kituo cha Polisi Nyakato walimkuta Mtuhumiwa eneo hilo pia akipiga ‘stori’ na Askari, Mtoto akaonesha aliyemfanyia ukatili yupo eneo hilo, mtuhumiwa akakamatwa lakini baada ya kesi kuhamishiwa Kituo cha Polisi Kirumba ndipo kukatokea ‘sintofahamu’ na haijulikani nini kinachoendelea.

Soma zaidi https://jamii.app/UkatiliNyakato

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability
2
MWANZA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji Kiongozi gani wa juu anayemlinda mtuhumiwa wa Ulawiti kwa Mtoto katika Kituo cha Polisi Kirumba, Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda ametoa maelekezo kwa Mwananchi huyo kuhusu kipi anachotakiwa kukifanya.

RC Mtanda ameandika “Namshauri huyo aliyedhurumiwa haki yake kufika pia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Mkoa, kwa Mwanza kila Jumanne tunakutana na Wananchi wenye changamoto za namna hizo, anaweza kuwa hajasikilizwa na taasisi moja lakini Kiongozi wa Serikali katika Wilaya ya Nyamagana ni Mkuu wa Wilaya amuone, yawezekana hajui. Kama hatasikilizwa aje Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku ya Jumanne.”

Ikumbukwe Mdau alisema Mtu huyo ambaye amemlawiti Mtoto wa Miaka minne eneo la Nyakato, alifikishwa Kituo cha Polisi akahojiwa, Mtoto akatoa maelezo, vipimo vya Hospitali ya Sekou Toure vikaonesha ameingiliwa lakini hakuna kinachoendelea, akidai kuna mazingira ya Mtuhumiwa kulindwa na Kiongozi wa ‘juu’.

Zaidi soma https://jamii.app/RCMtandaUfafanuzi

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #ChildRights #Accountability