JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema "Uchaguzi wetu kila baada ya Miaka mitano ni jambo muhimu sana kwa Taifa letu, ndiyo kielelezo cha #Demokrasia ya #Tanzania. Nchi hii haijawahi kuahirisha uchaguzi hata mara moja na katika mazingira magumu kuliko sasa. Wanaotaka Uchaguzi uahirishwe hawaelewi historia ya nchi hii."

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
ETHIOPIA: Wizara ya Elimu imetoa mwongozo unaopiga marufuku utoaji wa Shahada za Heshima (Honorary Doctorate) kwa Viongozi wa Serikali na Wanasiasa walioko madarakani, agizo hilo limetiwa saini na Waziri wa Elimu, Profesa Berhanu Nega, na limeelekezwa kwa Vyuo Vikuu na taasisi zote za elimu.

Mwongozo huo umeweka masharti mapya, ukiwataka wanaotunukiwa wawe ni waliotoa mchango mkubwa katika taaluma au kazi zao. Viongozi walioko kazini na Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu na Wajumbe wa Seneti, hawataruhusiwa kupokea shahada hizo wakiwa bado kazini.

Aidha, vyuo vitakavyotoa shahada ya heshima vinapaswa kutoa kozi za PhD, viwe na angalau awamu nane za wahitimu, na viwe vinatambulika Kitaifa na Kimataifa.

Upande wa Tanzania, miongoni mwa waliotunukiwa Shahada za Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere (1966, 1986), Balozi Juma Mwapachu (2005), na Rais Mstaafu Hayati Benjamin Mkapa (2006). Licha ya mchango wao mkubwa, hawakuwahi kutumia cheo cha “Daktari wa Heshima”.

Zaidi soma https://jamii.app/EthiopiaMarufukuPhD

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo Agosti 20, 2025 limeeleza kuwa mechi ya Ngao ya Jamii itakayozindua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 itachezwa Septemba 16, 2025 ikizikutanisha Young Africans SC (Yanga) dhidi ya Simba SC.

TFF imesema marekebisho yametokana na ratiba nyingi za Fainali za Kombe la Mataifa la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (#CHAN) 2025 na michezo ya mchujo ya Kombe la Dunia inayohusisha timu ya Taifa #TaifaStars.

Hivyo, mechi hiyo itachezwa kwa mchezo mmoja badala ya mfumo wa mechi tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita ili kuepuka msongamano wa ratiba na kurahisishia maandalizi ya klabu katika mashindano ya #CAF.

Zaidi soma https://jamii.app/WataniKwenyeNgaoYaJamii

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (#BAKITA), Onni Sigala amefafanua kuwa neno ‘Ngono’ limepoteza maana yake halisi kwenye jamii, na kuongeza kuwa halina uhusiano kabisa na maana ambayo wengi kwenye jamii wanayoifahamu.

Kwa mjadala zaidi bofya https://jamii.app/MaanaNgono

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKiswahili #JFLugha
1
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa wito kwa Mamlaka ya Jiji kutafuta suluhisho la Maegesho maeneo ya Ferry ili kuondoa usumbufu kwa madereva wa Taksi Mtandao kukamatwa na kutozwa faini wanaposhusha au kubeba Abiria.

Soma zaidi https://jamii.app/MaegeshoDar

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery
MWANZA: Mwanachama wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Fichua Uovu ametoa wito kwa mamlaka husika kufuatilia changamoto ya muda mrefu ya Walimu ambao ni Ajira Mpya kutopata malipo ya Fedha ya Kujikimu Wilayani Sengerema licha ya kufuatilia kwa takribani miezi sita.

Mdau anaandika "Majibu ya Afisa Elimu tukiulizia tunaambiwa Mwezi Julai (2025) huwa Mifumo ya Fedha haijakaa sawa, kwa hiyo endeleeni kusubiri”.

Soma zaidi https://jamii.app/MdauSengerema

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #Uwajibikaji #JFMdau2025 #ServiceDelivery
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo Agosti 20, 2025 kwa njia ya Mtandao, Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema miongoni mwa mabadiliko yanayohitajika ni kuwepo na utaratibu wa kupinga matokeo ya Urais Mahakamani iwapo kutatokea mashaka kwenye ushindi huo.

Zaidi soma https://jamii.app/SuguMatokeoUrais

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Akizungumza katika mdahalo kuhusu amani na #demokrasia uliofanyika kwenye Ukumbi wa JNICC, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar, Jumanne Muliro amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha ulinzi, amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Pia, ametoa onyo kuwa masanduku na vifaa vya uchaguzi vitalindwa, hivyo wanaotarajia kufanya vitendo vyovyote vya uhalifu watawashughulikia Kisheria.

Soma zaidi https://jamii.app/MuliroUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro akizungumza leo Agosti 20, 2025 katika Mdahalo wa Wadau wa Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 amesema "Nina hakika, kwa Jeshi hili sidhani kama yupo anayependa kufa hata kama upo chama gani, wote kwa kushirikiana Tanzania itakuwa salama."

Mjadala zaidi soma https://jamii.app/MuliroJeshiKufa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Governance #UtawalaBora
Mtengenezaji maudhui Mtandaoni, Ritha Johansen amesema ni vizuri Watumiaji wa Mitandao kutumia lugha zenye heshima pamoja na kuthibitisha vyanzo sahihi vya habari kabla ya kuanzisha mijadala Mitandaoni ili kuepusha athari za kauli za chuki.

Kufuatilia mijadala mingine tembelea JamiiForums.com

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
1