JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.04K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 (Kifungu 60 (3)(b) na 60 (6)(a)), kutoa taarifa binafsi za Mtu mwingine kama namba ya Simu bila idhini ya mwenye namba ni kosa linaloweza kukugharimu Faini isiyopungua Tsh. laki moja na isiyozidi Tsh. milioni ishirini au kifungo kwa kipindi kisichozidi Miaka kumi au vyote kwa pamoja.

Tuambie Mdau, Mtu akitoa namba yako ya Simu kwa Mtu mwingine bila kukuomba ruhusa huwa unajisikiaje?

Soma https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 mhusika wa taarifa, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara

Aidha, mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Kifungu cha 21 (1) cha Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini za Simu Mwaka 2025 ni kosa mtu kutumia Laini ya Simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine au kuruhusu laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho chake itumiwe na mtu mwingine

Ukiukwaji wa Kifungu hiki unaweza kusababisha adhabu ya kulipa faini isiyopungua Tsh. Milioni 3 au kifungo cha muda usipongua Miezi Sita au vyote kwa pamoja

Soma https://jamii.app/KosaKumsajiliaMtuLaini

#JFDigitali #DigitalRights #DataProtection #DataPrivacy #JamiiForums #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 mhusika wa taarifa, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara

Aidha, mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 33 (1b) mhusika wa taarifa ana Haki ya kufahamishwa madhumuni ya Taarifa Binafsi zinazomhusu pamoja na maelezo ya wapokeaji watakaopewa taarifa hizo

Aidha, mkusanyaji hatalazimika kutoa maelezo ya ukusanyaji wa taarifa hizo iwapo zinahusika katika uchunguzi kwa mujibu wa sheria au zimezuiliwa kwa amri ya Mahakama

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Ni muhimu kwa anayehitaji kusajili laini yake kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anaweka alama ya kidole mara moja, na ikiwa ipo haja ya zoezi kurudiwa ni muhimu wakala akatoa hakikisho kwamba zoezi halilengi kuchukua alama ya kidole mara mbili

Ikiwa Kitambulisho chako kimetumika na wakala kusajilia laini za Watu wengine bila ridhaa na idhini yako fika katika dawati la Huduma kwa wateja la Mtandao husika ili kutoa taarifa itakayowezesha kufutwa kwa namba ambazo huzitambui

Ni muhimu kuchukua hatua hii ili kulinda Taarifa zako binafsi katika kitambulisho cha NIDA zisitumike vibaya kwenye matukio ya uhalifu

Mjadala zaidi https://jamii.app/UsirudieAlamaZaVidole

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 37, inaeleza mhusika wa taarifa ana Haki ya kulipwa fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji wa Taarifa iwapo atapata madhara kwa sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria hiyo

Endapo Tume itajiridhisha na maombi ya mhusika wa taarifa kuwa amepata madhara katika mazingira yanayompatia haki ya kulipwa fidia inaweza kuamuru kurekebishwa, kuzuiwa, kufutwa au kuharibiwa kwa taarifa hizo.

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kumbuka kulinda taarifa zako na usikubali kuziweka wazi au kumpa mtu mwingine bila kujua lengo na matumizi ya taarifa zako

Usipolinda taarifa zako zinaweza kutumika katika Matukio ya Uhalifu kama vile Uwizi na Utapeli wa Mtandaoni

Mjadala zaidi https://jamii.app/PrivacyIsPower

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 61 inaeleza Mtu kuharibu, kufuta, kupotosha, kuficha au kubadilisha Taarifa Binafsi kinyume na Sheria ni kosa

Endapo atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Tsh. 100,000 na isiyozidi Tsh. Milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Indo-Pacific Center for Civil Society Resilience, jumla ya Nchi 7 katika Bara la Asia na Oceania (Indo - Pacific region) zilipitia changamoto ya kuzimwa kwa mtandao na kuminywa kwa Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni

Nchi zilizofanyiwa Utafiti ni Cambodia, Fiji, Malaysia, Pakistan, Sri Lanka, Taiwan na Thailand

Baadhi ya matukio yaliyojitokeza ni pamoja na ukusanyaji wa Taarifa Binafsi za Watu Mitandaoni, Gharama kubwa za Kanuni za Usalama wa Mtandao na kupelekea kuminywa kwa Uhuru wa Utumiaji Mtandao

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion