JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MGOMBEA URAIS WA ADC ADAI KUPIGWA MAKOFI NA KUVUNJIWA KIOO CHA GARI

> Queen Sendiga amedai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake la matangazo akiwa Stendi ya zamani ya Manispaa ya Iringa akiendelea na Kampeni

Soma - https://jamii.app/MakofiMgombeaADC
#TZ2020
JAMES MBATIA ASIMAMISHWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

- Kamati ya Maadili imemsimamisha Mgombea huyo wa Ubunge wa Vunjo kupitia NCCR Mageuzi kufanya kampeni kuanzia Oktoba 17, 2020

- Ni kwa kutumia kipeperushi cha kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Vunjo

Soma https://jamii.app/MbatiaAsimamishwaKampeni

#Uchaguzi2020
TANAPA: MOTO MLIMA KILIMANJARO UMEDHIBITIWA

> Ukaguzi wa anga umebaini moto wote umedhibitiwa. Hata hivyo vikosi vya askari vimetawanywa kwa tahadhari

> Moto ulizuka Oktoba 11 na kuathiri 5% ya eneo lote la hifadhi lenye km za mraba 1700

Soma https://jamii.app/TANAPAMotoKLM
#JFLeo
LISSU: NIKISHINDWA KWA HAKI NITAKIRI KUSHINDWA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema wakishinda lazima NEC itangaze kwa heri au kwa shari

> Amesisitiza wanataka Uchaguzi wa amani lakini hawatakuwa tayari kugeuza shavu la pili waumie zaidi

Soma https://jamii.app/LissuHakiUchaguzi
#TZ2020
GAIRO: AJINYONGA BAADA YA KUGOMBANA NA MAMA YAKE

> Rahel Yohana (14) aliyemaliza darasa la 7 amejinyonga baada ya kukatazwa kurudi nyumbani usiku

> RPC wa Morogoro amewataka wenye changamoto watafute wataalam wa Saikolojia na sio kujiua

Soma - https://jamii.app/Mwnf7Ajinyonga
ZANZIBAR NA SERIKALI YA MUUNGANO WAKUBALIANA KUFUTA HOJA 5 BAADA YA KUZITATUA

> Baadhi ya hoja zilizoondolewa ni Ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda pamoja na Ushiriki wa Zanzibar ktk Jumuiya ya Afrika Mashariki

Soma https://jamii.app/MuunganoSainiHoja
#JFLeo
ZANZIBAR: VURUGU ZA KISIASA ZATOKEA NA BAADHI YA WATU KUJERUHIWA

> Kamanda wa Polisi Kaskazini Pemba amesema ulitokea ugomvi kati ya Wanachama wa ACT-Wazalendo na CCM eneo la Shumba Mjini ambapo walishambuliana kwa mapanga na kuumizana

Soma https://jamii.app/VuruguSiasaZbar
#Uchaguzi2020
PWANI: TAKUKURU YAOKOA ZAIDI YA TSH MILIONI 200 KWA MIEZI 3

> Julai hadi Septemba 2020, TAKUKURU ilipokea malalamiko 318 ambapo 157 yanafanyiwa kazi, 74 yalionekana kuhusu Sheria nyinginezo

> Kesi 10 zilitolewa hukumu na Jamhuri ilishinda 6

Soma https://jamii.app/PCCBTsh200M
#JFLeo
KILIMANJARO: BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA UCHIRA ISLAMIC LATEKETEA KWA MOTO

> Bweni la Shule hiyo ya Wasichana iliyopo Moshi Vijijini limeteketea jioni ya Oktoba 16

> Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, hakuna kifo kilichoripotiwa

Soma - https://jamii.app/UchiraMoto
#JFLeo
WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU KUWASILI OKTOBA 23

> Waangalizi hao kutoka Jumuiya ya #Afrika Mashariki wataongozwa na Rais Mstaafu wa #Burundi, Sylvestre Ntibantunganya

> Wamo Wabunge wa Bunge la #EAC na Mawaziri wa masuala ya Jumuiya hiyo

Soma - https://jamii.app/WaangaliziEAC
#TZ2020
LIGI KUU ENGLAND: LIVERPOOL NA EVERTON ZATOSHANA NGUVU

- Mchezo wa β€˜Merseyside Derby’ wa mzunguko wa 5 wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool na Everton umemalizika kwa timu hizo kufungana goli 2-2

- Mechi inayofuata sasa ni kati ya Chelsea na Southampton na baadaye, Manchester City na Arsenal zitapimana ubavu kabla ya Manchester United kukipiga na Newcastle

#Michezo #Sports #JamiiForums #JFSports #JFMichezo
TUNDU LISSU AWATAKA WATANZANIA KUHAMASISHANA ILI KWENDA KUPIGA KURA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu kuliko wakati wowote kwa sababu utaunda Serikali itakayolinda Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu

Soma - https://jamii.app/LissuManyoni
#Uchaguzi2020
LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI

- Klabu ya Chelsea imetoka sare ya goli 3-3 na Klabu ya Southampton katika mchezo wa Ligi hiyo mzunguko wa 5

- Mchezo unaofuata ni kati ya Manchester City na Arsenal na kisha Manchester United itapambana na Newcastle

#JamiiForums #JFSports #JFMichezo #Michezo #Sports
NEC: WAANGALIZI WA UCHAGUZI WASIWE WASEMAJI WA UCHAGUZI

> Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema, Waangalizi wa Uchaguzi wajibu wao ni kutazama tu namna shughuli zinavyoendeshwa ili kupata fursa ya kuandaa ripoti na kutoa mapendekezo

Soma https://jamii.app/JukumuWaangalizi
#Uchaguzi2020
WATOTO KUTOKWA NA HAJA KUBWA BILA KUJIJUA NI TATIZO KATIKA UTUMBO MPANA

> Kitaalamu Ugonjwa huo unaitwa Hirschsprung’s Disease, na unawakabili watoto wengi

> Ni Ugonjwa unaochukuliwa kama tabia, lakini ni tatizo lililo nje ya uwezo wa mtoto

Soma https://jamii.app/UgonjwaKujinyea
#JFAfya
TCRA: WANAWAKE HUDHALILISHWA SANA MITANDAONI KUTOKANA NA KUPIGA PICHA TATA

> Kwa mujibu wa kesi wanazozipokea, waathirika hubainika walihusika kuchapisha maudhui hayo ya ngono

> Suala hilo linachangiwa na ugawaji wa nywila kwa watu wa karibu

Soma https://jamii.app/SocialMediaBullying
RIPOTI: WATUMIAJI WA INTANETI TANZANIA WAFIKIA MILIONI 27.1

> Kwa mujibu wa takwimu mpya za TCRA, Watumiaji wamefikia idadi hiyo Juni kutoka Milioni 26.8 ya mwezi Machi

> Hii inaashiria ongezeko la fursa mtandaoni kama biashara na maarifa

Soma - https://jamii.app/WatumiajiIntaneti
#JFLeo
KAGERA: MBARONI KWA KUUA AKIJARIBU KUTOA MIMBA

> Frodius Protace (24) anatuhumiwa kumuua Saraiya Idd (25) kwa kujaribu kumtoa mimba ya miezi sita

> Mtuhumiwa alikiri kushiriki mafunzo ya kozi fupi ya Ufamasia lakini hajawahi kuajiriwa

Soma https://jamii.app/TuhumaZaKuua
RAIS MAGUFULI AMKABIDHI NYUMBA MZEE MWINYI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli amemkabidhi nyumba Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi
-
Mzee Mwinyi amekuwa akiishi kwenye nyumba aliyojenga mwenyewe iliyoko Mikocheni jijini Dar, nyumba ambayo ipo karibu na Nyumba ya Mwalimu Nyerere
-
Ally Hassan Mwinyi ni Rais wa Pili wa Tanzania, aliyeongoza tangu mwaka 1985 hadi mwaka 1995
-
#JFLeo #JamiiForums #JFSiasa
KENYA YASHUKU KUPIGWA NA WIMBI LA PILI LA #CORONAVIRUS

> Kenya imethibitisha watu 685 kuambukizwa #CoronaVirus ndani ya saa 24

> Jumla ya walioambukizwa ni 44,881 huku 28 wakiwa mahututi. Wizara imetahadharisha wananchi kufuata kanuni

Soma https://jamii.app/SecondWaveKE
#JFLeo
MAJALIWA: MCHAGUENI DKT. MAGUFULI KWANI SIO MLALAMISHI

> Amesema, Wananchi wanatakiwa kumchagua mgombea huyo kwa kuwa ana uwezo wa kusimamia kazi ipasavyo

> Amewataka wananchi kutofanya makosa kwa kuchagua wagombea wasioweza kuwatumikia

Soma - https://jamii.app/MajaliwaKigoma
#TZ2020