JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Msajili wa vyama vya siasa nchini amekitaka chama cha ACT Wazalendo kuwasilisha utetezi wao juu ya malalamiko ya Monalisa Ndala - Mwenezi wa ACT
Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, dhidi ya uvunjifu wa kanuni za chama hicho kabla ya kupita tarehe 20 Agosti 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 19, 2025 na Sisty Nyahoza imewataka ACT watoe maelezo juu ya kuvunja kanuni ya chama chao kuhusu uteuzi wa mgombea wa urais wa chama hicho Luhaga Mpina.

Aidha, Monalisa ameilalamikia kanuni ya chama inayoeleza sifa za mgombea wa urais anatakiwa awe mwanachama wa chama hicho kwa muda wa mwezi mmoja na kwamba Mpina hajatimiza mwezi tangu ajiunge na chama hicho.

Zaidi https://jamii.app/ACTKujiteteaKesho

#JamiiForums #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #JFSiasa
👍1
DODOMA: Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (#CCM) dhidi ya Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa, ambaye anapinga uhalali wa mchakato uliompitisha Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwania urais kupitia Chama hicho.

Mawakili wa CCM, Fabian Donates na Alex Mgongolwa, leo Agosti 19,2025 wamewasilisha mapingamizi wakidai hatua za kufungua shauri hilo hazikufuatwa, huku wakisisitiza mlalamikaji alipaswa kuandika barua kwa Katibu Mkuu badala ya mwenyekiti wa Chama.

Aidha, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo, amesema taratibu zilizingatiwa kwani Februari, 2025, Dkt. Malisa alimwandikia barua Rais Samia akilalamikia uteuzi wake, ambapo baada ya hoja za pande zote kusikilizwa, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 22, 2025.

Soma https://jamii.app/MalisaNaCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
SIMIYU: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina akiwa katika zoezi la kutafuta udhamini mkoani humo Agosti 17, 2025.

Soma Zaidi https://jamii.app/MpinaMagufuli

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSiasa #UchaguziMkuu2025
Unapocheka, haujifurahishi tu bali pia unapunguza msongo wa mawazo, unaimarisha kinga ya mwili na kulinda moyo wako.

Kwa kifupi, kicheko ni afya — basi jitafutie sababu ya kucheka kila siku. 😄

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye tija.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
😁1
KATAVI: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Wilaya ya Mpanda anatoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (#TANESCO) kushughulikia changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara, akihoji mbona wanapodai madai yao hutumia magari ya matangazo kuzunguka Mtaani kufikisha ujumbe, lakini suala la kukata umeme hutumia makundi ya WhatsApp ambayo Wananchi wengi hawana au hawatumii?

Zaidi soma https://jamii.app/UmemeMpanda

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025 #JFUwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema "Uchaguzi wetu kila baada ya Miaka mitano ni jambo muhimu sana kwa Taifa letu, ndiyo kielelezo cha #Demokrasia ya #Tanzania. Nchi hii haijawahi kuahirisha uchaguzi hata mara moja na katika mazingira magumu kuliko sasa. Wanaotaka Uchaguzi uahirishwe hawaelewi historia ya nchi hii."

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
ETHIOPIA: Wizara ya Elimu imetoa mwongozo unaopiga marufuku utoaji wa Shahada za Heshima (Honorary Doctorate) kwa Viongozi wa Serikali na Wanasiasa walioko madarakani, agizo hilo limetiwa saini na Waziri wa Elimu, Profesa Berhanu Nega, na limeelekezwa kwa Vyuo Vikuu na taasisi zote za elimu.

Mwongozo huo umeweka masharti mapya, ukiwataka wanaotunukiwa wawe ni waliotoa mchango mkubwa katika taaluma au kazi zao. Viongozi walioko kazini na Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu na Wajumbe wa Seneti, hawataruhusiwa kupokea shahada hizo wakiwa bado kazini.

Aidha, vyuo vitakavyotoa shahada ya heshima vinapaswa kutoa kozi za PhD, viwe na angalau awamu nane za wahitimu, na viwe vinatambulika Kitaifa na Kimataifa.

Upande wa Tanzania, miongoni mwa waliotunukiwa Shahada za Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere (1966, 1986), Balozi Juma Mwapachu (2005), na Rais Mstaafu Hayati Benjamin Mkapa (2006). Licha ya mchango wao mkubwa, hawakuwahi kutumia cheo cha “Daktari wa Heshima”.

Zaidi soma https://jamii.app/EthiopiaMarufukuPhD

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo Agosti 20, 2025 limeeleza kuwa mechi ya Ngao ya Jamii itakayozindua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 itachezwa Septemba 16, 2025 ikizikutanisha Young Africans SC (Yanga) dhidi ya Simba SC.

TFF imesema marekebisho yametokana na ratiba nyingi za Fainali za Kombe la Mataifa la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (#CHAN) 2025 na michezo ya mchujo ya Kombe la Dunia inayohusisha timu ya Taifa #TaifaStars.

Hivyo, mechi hiyo itachezwa kwa mchezo mmoja badala ya mfumo wa mechi tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita ili kuepuka msongamano wa ratiba na kurahisishia maandalizi ya klabu katika mashindano ya #CAF.

Zaidi soma https://jamii.app/WataniKwenyeNgaoYaJamii

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (#BAKITA), Onni Sigala amefafanua kuwa neno ‘Ngono’ limepoteza maana yake halisi kwenye jamii, na kuongeza kuwa halina uhusiano kabisa na maana ambayo wengi kwenye jamii wanayoifahamu.

Kwa mjadala zaidi bofya https://jamii.app/MaanaNgono

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKiswahili #JFLugha
1
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ametoa wito kwa Mamlaka ya Jiji kutafuta suluhisho la Maegesho maeneo ya Ferry ili kuondoa usumbufu kwa madereva wa Taksi Mtandao kukamatwa na kutozwa faini wanaposhusha au kubeba Abiria.

Soma zaidi https://jamii.app/MaegeshoDar

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #ServiceDelivery