JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Taasisi Zinazounda Utatu, Agosti 18, 2025, Jaji Mkuu George Masaju ametaka Mahakama iondoe ucheleweshaji wa mashauri usio na sababu za msingi, akisema hali hiyo inadhoofisha utoaji wa haki, akisema “Kitu mnachoweza kumaliza kwa siku mbili, unasema mpaka umalize Miezi minne?”

Zaidi soma https://jamii.app/MasajuKesiMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance #UtawalaBora
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Askofu Dkt. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe ameeleza kuwa kuna kundi la Viongozi ambao katika uongozi wao hawaaminiki, wakiahidi hawatekelezi, hawatendi haki, hawaogopi damu za Watu, hawana huruma na wanyonge, wanapenda rushwa na sasa wako tayari kununua Watu ili wawe Viongozi wao.

Ameyasema hayo wakati akiongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Ihembe, Wilaya ya Karagwe, Agosti 10, 2025.

Soma zaidi https://jamii.app/BagonzaViongoziMatendo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Governance #UchaguziMkuu2025
1👍1
Mshiriki wa Stories of Change (#SoC) 2023 anasema ili kuimarisha Utawala Bora inahitajika Uteuzi wa Viongozi wa Serikali ufanyike kwa kuzingatia misingi ya uzoefu na uwezo si kufahamiana au ushirikiano katika siasa.

Ameeleza Mfumo wa uteuzi wa Viongozi wa Serikali umekuwa na changamoto kubwa nchini kwetu, kwani hufanywa kwa misingi ya uhusiano wa kisiasa au urafiki badala ya uwezo na uzoefu wa mgombea na kusababisha kuwepo kwa viongozi wasio na uwezo wa kusimamia vizuri masuala ya umma na kusababisha matatizo makubwa katika utendaji wa Serikali.

Soma https://jamii.app/MisingiUteuzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai huduma ya Kampuni inayokamata Vyombo vya Moto vinavyoegeshwa kimakosa ndani ya Wilaya ya Ubungo na kueleza faini ya Tsh. 80,000 inayotozwa haiendani na kosa, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka inayosimamia.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imesema dereva anayekutwa na kosa hataruhusiwa kuondoka eneo la tukio hadi awe amelipa faini tofauti na utaratibu wa Polisi ambapo faini inaweza kulipwa baadaye hata baada ya kuondoka eneo la tukio.

Halmashauri hiyo pia imetoa maelekezo kwa Watendaji wa Boss Kazi Ltd kufanya kazi kwa kufuata masharti ya mkataba na Sheria za nchi, kuhudumia Wananchi kwa staha, heshima na weledi, kupiga picha kabla ya kutoa faini ili kuepusha sintofahamu na kutoa elimu ya kutosha kwa kila Mwananchi anayekamatwa kuhusu kosa lake na namna ya kulipa.

Zaidi https://jamii.app/WrongParkingUbungo

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #JFMdau2025 #Accountability
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Kamanda wa Polisi Mkoa, Benjamin Kuzaga amesema wanawashikilia Watu Tisa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia Mitandao ya Kijamii ikiwemo Facebook na WhatsApp, ambapo Watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 18, 2025 katika maeneo ya Nsalala na Mapelele, Mbalizi.

Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutangaza nafasi feki za ajira, kuwatapeli Watu kwa kutumia simu na mitandao kwa mtindo wa “Tuma kwenye namba hii,” na kuwarubuni wengine wachangie fedha kujiunga na Kampuni ya Q NET yenye asili ya Malaysia.

Amewataja waliokamatwa ni Nemia Njonga (23), Ombeni Ambilikile (22), Jacob Peter (23), Baraka Mgala (22), Lusajo Jeremiah (45), Adili Mbeyale (19), Shaban Yasin (23), Ester Kimaro (28) na Abdi Awadhi (21).

Zaidi soma https://jamii.app/WakamatwaUtapeli

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFDigitali #DigitalSafety #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Waziri wa Usalama wa Ndani amesema anatamani timu ya Taifa ya Kenya “Harambee Stars” ikutane na Tanzania “Taifa Stars” katika Fainali ya michuano ya CHAN, akiamini utakuwa mchezo mzuri

Kuhusu taarifa kuwa kuna mashabiki wa Kenya wamenunua tiketi za mchezo wa Tanzania dhidi ya Morocco amesema kama ni kweli anawapongeza kwa kufanya hivyo.

Je, Mdau wa Soka una neno la kuchangia kuhusu ujumbe huu?

Soma zaidi https://jamii.app/KenyaTZUtani

#JFSports #JamiiAfrica #JamiiForums
😁1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, leo Agosti 21, 2025, Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime amesema “Ukiona Watu wanashambulia mifumo ya ulinzi, ujue ndiyo tabia za wahalifu, wahalifu wanajua ukiififisha Polisi, basi watavuruga amani ya nchi…tuwaambie sisi tuko imara.”

Zaidi soma https://jamii.app/MifumoYaUlinzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Governance
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa ameeleza katika kipindi hiki cha mchakato wa vyama kuwapata Wagombea, kumekuwa na usambazaji wa vifaa vyenye nembo ya chama. Anadai matukio hayo yanaweza kuibua mjadala kuhusu ushawishi, kwani bado haijathibitishwa kama vinaweza kuathiri maoni ya Wapiga Kura kwa makusudi.

Amehoji, Je, wahusika wanahakikisha hakuna uvunjifu wa Sheria za Uchaguzi wakati wa usambazaji wa vifaa hivyo?

Zaidi Soma https://jamii.app/KablaYaKampeni

#JamiiForums #Accountability #Misinformation #Disinformation #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #TaarifaZaUchaguzi2025
1
Mtaalamu wa Saikolojia, Ndoa, Mahusiano na Malezi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Chris Mauki, amesema “Mara nyingi, mtu anayeandika maneno ya chuki huonesha changamoto zake binafsi za kisaikolojia huenda zimetokana na malezi magumu, ukosefu wa upendo au mazingira yenye chuki aliyokulia. Kwa bahati mbaya, maumivu haya huishia kuwagusa wengine, na walioumizwa nao huanza kuwaumiza watu wengine.”

Aidha amesema “Wanaoshuhudia au kukutana na kauli za chuki mtandaoni nao huweza kuziendeleza kwa kuzisambaza kwa watu wengine na mzunguko wa maumivu unaendelea.”

Tembelea JamiiForums.com

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
1
GEITA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema linaendelea kuchunguza tukio la kutoweka kwa Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Wilaya ya Bukombe, ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 21, 2025, Polisi wameeleza walipokea malalamiko kwamba mnamo Agosti 19, 2025 saa 10:00 jioni, Elisha alichukuliwa na watu watatu wasiojulikana akiwa studio ya MAS J, Kilimahewa kata ya Bulangwa, waliokuwa na gari jeupe lisilojulikana usajili wake.

Aidha, Jeshi limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa ya kuweza kusaidia kupatikana kwa Elisha asisite kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Zaidi soma https://jamii.app/JumaElishaWasiojulikana

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #Accountability #JFMatukio #UtawalaBora #HakiZaBinadamu