JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Aprili 10, 2017, Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitaka Bunge lijadili matukio ya utekaji wa Watu ambapo alidai yeye pia ametumiwa ujumbe wa vitisho, hoja yake pia iliungwa mkono na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi "Sugu"

Akijibu hoja hiyo, Dkt. Tulia alisema“Masuala yaliyoulizwa na Bashe na Mbilinyi yapo chini ya utaratibu wa Sheria, Bunge hili litashughulika na mambo yenye maslahi kwa umma ambayo Sheria haina uwezo wa kuyatolea majibu, hivyo sitalihesabu jambo hilo kuwa ni jambo la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 (4) bali utaratibu wa Kisheria utafanya kazi."

Soma https://jamii.app/BasheUtekaji2017

#JamiiForums #JFKumbukizi #JamiiAfrica #HumanRights #Transparency #Siasa
👍1
DAR: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa Miaka 12 na Kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha Mradi wa BRT Jijini Dar

Mkataba huo ulisainiwa Mei 30, 2025 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema Emirates National Group itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177

Imeelezwa Mchakato huo ulianza Mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi

Ikumbukwe Mwaka 2020, Serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, ambapo Emirates National Group iliibuka mshindi.

Soma https://jamii.app/EmiratesKusimamiaMwendokasi

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Transparency
👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UWAJIBIKAJI: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amesema "Deni letu kwa mwaka lilikuwa linaongezeka kwa 5% tu, sasa hivi deni letu la Taifa kwa mwaka linaongezeka 18%. Hiki ni kiwango kikubwa sana cha ongezeko la deni la Taifa. Inaonyesha tunakopa kupita kiasi, sio kwamba tunakopa kwa kutekeleza miradi."

Ameyasema hayo katika Viwanja vya Bunge, leo Juni 5, 2025

Soma https://jamii.app/DeniTaifaKukua

#JamiiForums #JamiiAfrica #Transparency #Accountability #Uwajibikaji
👍21
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameyasema hayo katika Viwanja vya Bunge Juni 5, 2025

Soma https://jamii.app/DeniTaifaKukua

#JamiiForums #JamiiAfrica #Transparency #Accountability #Uwajibikaji
KENYA: Mamia ya Waandamanaji wamekusanyika katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi na Miji mingine  wakitaka haki itendeke kwa maafisa waliohusika na kifo cha Mwanamitandao Albert Ojwang', pamoja na kupinga mipango ya Serikali kuhusu Bajeti mpya inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni rasmi leo Juni 12, 2025 jioni na Waziri wa Fedha, John Mbadi

Kumekuwa na taarifa kwamba Serikali inapanga kusoma Bajeti mpya bila kubadilisha hatua kali za kodi kama vile kuongeza ada za huduma muhimu au kupunguza kodi kwa bidhaa za msingi kama mafuta na chakula, ambazo zilisababisha #Maandamano makubwa ya Juni 2024 yaliyosababisha vifo, majeruhi, na uharibifu mkubwa wa mali

Hata hivyo, waandamanaji wameeleza hofu yao kuwa huenda Serikali ikatumia mbinu zilezile, wakisisitiza umuhimu wa #Uwazi na ushirikishwaji kamili katika maamuzi yote ya kifedha yanayowahusu moja kwa moja

Soma https://jamii.app/MaandamanoBajeti25

#JamiiAfrica #JamiiForums #Transparency #Governance #Accountability #Uwajibikaji
1
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema uwiano wa mapato ya ndani kwa Pato la Taifa umeongezeka kufikia 15.0% Mwaka 2023/24 kutoka 13.7% Mwaka 2020/21, ambapo amesema Mwenendo huu chanya unadhihirisha mageuzi makubwa kwenye ukusanyaji wa mapato

Aidha, amesema kuwa hadi Mei 2025, Serikali imefanikiwa kusaini mikataba 169 na wawekezaji mbalimbali. Amesema, hii itatusaidia kuondoa uwezekano wa kulea utovu wa tija (inefficiency) kwa wale wanaopata vivutio na kuhakikisha kuwa wanakuwa na kuhitimu kutoka katika mahitaji ya kulindwa.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imesema Tsh. Trilioni 1.58 zilitolewa katika ujenzi wa Barabara, Madaraja na Viwanja vya Ndege; Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Reli ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) Tsh. Trilioni 1.68

Aidha, Mradi wa Kufua Umeme katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) MW 2,115 na Mradi wa kusambaza Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) zilitolewa Tsh. Bilioni 574.8; na Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya Mpira kwa ajili ya Maandalizi ya AFCON 2027 Tsh. Bilioni 179.8

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
Serikali imesema Mwaka 1961 tulikuwa na Shule za Msingi 3,270, Walimu 9,885 na Wanafunzi 486,470. Shule za Sekondari 41, Walimu 764 na Wanafunzi 11,832. Vyuo vya Ualimu 8, Walimu 164, na Wanafunzi 1,723, Chuo kikuu kimoja, Wahadhiri 6 na Wanafunzi 14.

Hadi kufikia Mwaka 2024, Tanzania ilifikisha Shule za Msingi 20,533, Walimu 229,840 na Wanafunzi 11,391,185. Shule za Sekondari 6,269, Walimu 128,686 na Wanafunzi 3,314,198. Vyuo vya Ualimu 65, Walimu 1,633 na Wanafunzi 16,002, Vyuo Vikuu 79, Wahadhiri 8,625 na Wanafunzi 334,854

Serikali pia imeendelea kuongeza Vyumba vya Madarasa ya Elimu ya Msingi kutoka 128,425 Mwaka 2020 hadi Madarasa 155,330 Mwaka 2024 na Vyumba vya Madarasa ya Elimu ya Sekondari kutoka 46,928 Mwaka 2020 hadi 81,052 Mwaka 2024.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
1👍1
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema "Kipindi cha Serikali ya Awamu ya 4 ulitokea uhalifu wenye sura ya Ugaidi uliohusisha urushwaji wa Mabomu kwenye Nyumba za Ibada, Mikusanyiko ya Watu na Mashambulizi ya Mtu mmoja mmoja wakiwemo Watu wenye Ulemavu wa Ngozi. Tumesahau hili? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vilisimama imara na kukomesha Uhalifu huo”

Ameongeza "Kipindi cha Serikali ya Awamu ya 5, ulitokea uhalifu wa Watoto kutekwa na kuuwawa, Mtu mmoja mmoja kupigwa risasi kwenye makazi yake au katika Utekelezaji wa majukumu yake. Waliuawa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wanaotokana na CCM na tulishuhudia pia miili iliyokuwa kwenye Magunia na Mifuko ikiwa imetupwa Baharini. Na haya tumesahau? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vilisimama imara na kukomesha Uhalifu huo.”

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency
1
Serikali imesema Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kupandisha Vyeo Watumishi wa Umma 476,470 ambapo Jumla ya Tsh. Bilioni 689.9 zimetumika

Pia, kipindi cha kuanzia Mwaka 2021/22 hadi Mei 2025, Serikali imelipa madai ya malimbikizo ya Mishahara jumla ya Tsh. Bilioni 318.37 kwa Watumishi na Wastaafu 187,152.

Soma https://jamii.app/BajetuKuu2025

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025 #Governance #Uwajibikaji #Transparency