Relationship Tips
1.36K subscribers
144 photos
3 links
Join and learn about relationship tips
Download Telegram
ISHARA 6 ZA MWANAMKE ANAYE DATE NA WEWE TU

1πŸ“ŒYeye huwa yupo na wewe muda wote,
Hatoweki ghafla kwa muda mrefu. Huhitaji kujiuliza yuko wapi kwa siku kadhaa. Hukupigia au kukutumia ujumbe mara kwa mara kwa sababu hayuko busy kuongea na wanaume wengine.

2πŸ“ŒHakutafuti tu usiku wa manane au kwa kujificha,
Yeye huwa huru kuwa na wewe muda wowote. Hafichi simu wala mazungumzo. Anataka uwe sehemu ya maisha yake ya kila siku.

3πŸ“ŒAnakutambulisha,
Kama anadate na wewe tu, hatakuficha. Atakutambulisha kwa familia yake, marafiki wake wa karibu na hata wafanyakazi wenzake.

4πŸ“ŒHutumika neno β€œsisi”,
Anapoongea kuhusu maisha ya baadaye hata kama ni mwezi ujao, hutumia β€œsisi” badala ya β€œmimi”. Anakujumuisha kwenye mipango yake ya baadaye.

5πŸ“ŒHafichi kitu chochote kwako,
Hafichi simu wala mazungumzo. Anakuwa huru kabisa unapokuwa naye.

6πŸ“ŒAnakuwa na furaha kukuona,
Yeye huwa anafurahia sana uwepo wako karibu naye.
1❀9πŸ”₯1
Moja ya njia ya kushinda kiburi ni kwa kuwapongeza wale unaowaonea wivu, wale unaowaona wanakuzidi kitu na unatamani ungekuwa kama wao.
1❀4πŸ”₯1
Hallelujah! Amefufuka kweli hallelujah.
Katika siku hii tujufu , tukumbuke upendo, msamaha na tumaini jipya kupitia yesu Kristo.πŸ™
Mungu awajalie Amani,furaha,na baraka Tele Katika maisha yenu.πŸ™Œ
PASAKA NJEMA KWENU WOTE 🀝
πŸ‘2πŸ”₯1
Kumpongeza mwenzako kunakupa nafasi ya kusherekea mafanikio ya mwenzako. Kwa kutambua hilo usijiulize, kwa nini sio mimi badala yake jiulize naweza kujifunza nini kutoka kwa waliofanikiwa.
Wivu ukigeuzwa kuwa pongezi, hugeuka kuwa baraka.

🌱 Kiburi kikivunjwa na unyenyekevu, huzaa amani ya moyo.
❀4
Habari! Umechoka na muwasho usioisha hasa usiku?
Inaweza kuwa UPELE (Scabies). Nimeweka video mpya YouTube nimeelezea dalili zake, jinsi unavyoambukizwa, na tiba ya haraka.
Usikae na mashaka. Tazama hapa
Share na familia yako.
https://youtu.be/lb-VS-fZK5s
https://youtu.be/lb-VS-fZK5s
https://youtu.be/lb-VS-fZK5s
https://youtu.be/lb-VS-fZK5s
🌹🌹TUJIFUNZE SOMO FUPI LA MAISHAπŸ§πŸ½β€β™€οΈπŸ“šπŸŒΉπŸŒΉ

🌹 Marafiki wa kweli ni kama
Nyota.Utawatambuwa wakati
Giza linapoingia.
*___*

πŸŒΉβœ“ Hakuna anae kuzuia kukua,
Kusonga mbele au kuchanua
Kama tu ukiamua ndani
ya Moyo wako.
*____*

πŸŒΉβœ“ Ukiona Kila kitu
kinachokuzunguka ni giza ujue
wewe ndiyo nuru.
*___*

πŸŒΉβœ“ Ukishinda vita vya nafsi
Yako hakuna atakae kushinda.
*__*

πŸŒΉβœ“ Watu watakupenda
kwasababu fulani ila ni Mungu
Tu ndiye anakupenda bila
sababu.
*__*

πŸŒΉβœ“ Usilazimishe mahusiano
na watu.Watu sahihi kwako
watakuja tu wenyewe maishani
mwako.
*_*

πŸŒΉβœ“ Kila kitu unachowafanyia
wengine jua tu na wewe ipo
siku utafanyiwa hata kama
sio leo wala kesho.
*____*

πŸŒΉβœ“ kuwa makini na makosa
madogo madogo.Maana
matundu madogo ndiyo
huzamisha meli.
*_*

πŸŒΉβœ“ Mafanikio sio tu pesa.
Huwezi kuitafuta au kuiwaza
kila siku pesa maishani mwako
lasivyo utakuwa mtumwa.
*____*
❀5πŸ‘1
Furaha haitokani na kile ulicho nacho… bali namna unavyochagua kufikiri kuhusu kile ulicho nacho.

Wengine wana kila kitu lakini hawana amani, na wengine wana kidogo lakini wana furaha ya kweli.

Akili yako ndiyo chanzo ukijifunza kuthamini, kukubali, na kuishi sasa, furaha inakuwa sehemu yako, si kitu cha kusubiri.

Kwa sababu furaha si mahali pa kufika… ni hali unayochagua kuishi nayo kila siku.
1❀3πŸ”₯3
Jicho la kutafuta mke sio sawa na jicho la kutafuta demu. Mke ni majukumu na sio hisia za muda mfupi lakini demu huhitajika kwa mhemko na kupata burudani. Gharama ya kuangalia tv nyumbani sio sawa na Gharama ya kuangalia tv banda umiza. Japo raha ya banda umiza ipo juuπŸ€”πŸ€”
1❀5
`Kwa vijana ambao HAWAJAOA au kuolewa

Wakati sahihi ukifika, kila kitu kitakaa mahali pake.

Usikimbie mahusiano kwa sababu ya maumivu ya zamani… tumia maumivu hayo kujifunza, sio kujifungia moyo.

Focus kwenye malengo yako, lakini usiue uwezo wako wa kupenda na kuamini watu.

Upweke ukiutunza sana unaweza kugeuka tabia, na mwisho ukaanza kuona kila anayekusogelea ni usumbufu.

Sio kila mtu anayekuja kwenye maisha yako anakuja kukuumiza… wengine wanakuja kukuponya πŸ₯Ί

Jifunze kuwa busy kwa maendeleo, sio busy kwa kukimbia hisia zako.

Mwanaume wa kweli sio anayeficha feelings zake muda wote… bali anayejitambua na kujijenga bila kupoteza utu wake.

Na mwisho… usikubali tamaa ya muda mfupi ikaharibu future yako ya kudumu.

Discipline nayo ni upendo kwa maisha yako mwenyewe
1πŸ”₯4
Usilazimishe uwepo wako mahali ambapo hauhisi kuthaminiwa.

Wakati mwingine ukimya na umbali ni majibu ambayo maneno yameshindwa kusema.

Heshimu ishara, linda amani yako, na jifunze kuondoka bila kelele.
1❀4πŸ”₯3πŸ‘1
Wakati mwingine watu hawahitaji ushauri mwingi wanahitaji tu mtu wa kuwaelewa, kuwasikiliza, na kuwaonyesha kwamba hawapo peke yao.

Upole mdogo, moyo wa huruma, na uwepo wa kweli vinaweza kuponya maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea.
1πŸ‘4❀2πŸ”₯1
Usiruhusu hali uliyonayo leo ikupokonye picha ya maisha unayotaka kuyaishi kesho.

Maono makubwa hayahitaji mazingira mazuri kuanza yanahitaji mtu mwenye ujasiri wa kuamini kile ambacho wengine bado hawajakiona.
1πŸ₯°4❀1
Nyumba si kuta, samani, au anwani *unayoishi.*

Nyumba ni mahali unapopata amani, upendo, na hisia ya kuwa wa muhimu.

Wakati mwingine unaweza kuwa mbali na ulipozaliwa, lakini ukazungukwa na watu wanaokuthamini na kukufanya ujisikie salama.

Hapo ndipo nyumbani huanza kujengwa.
1❀6πŸ‘1
Wakati mwingine unafikiri msaada wako ni mdogo

Lakini kwa mtu mwingine unaweza kuwa sababu ya kutabasamu tena kupata nguvu, au kuendelea kuishi kwa matumaini.

Usidharau maneno mazuri, moyo wa huruma, au kusaidia mtu kimya kimya.

Mema hayapotei huacha alama kwenye maisha ya watu hata kama huioni mara moja.
❀5πŸ‘2πŸ₯°1
*Usiruhusu ukimya wa watu uzime sauti ya ndoto zako.*

Jiamini hata kama unasimama peke yako. Endelea kusonga mbele hata kama hatua ni ndogo.

Mara nyingi ushindi mkubwa huanza pale ambapo watu wengine walikata tamaa
πŸ”₯3
*Anguko kubwa la wanaume wengi wanaojitafuta ni kushindwa kudhibiti tamaa zao.*

Wengine huanza safari ya mafanikio wakiwa na maono makubwa, lakini njiani hupoteza mwelekeo kwa kukimbizana na wanawake wengi badala ya kujenga ndoto zao.

Mwanaume mwenye maono hujenga thamani yake kwanza. Anajua kuwa mafanikio yanahitaji nidhamu, umakini, na uwezo wa kusema hapana kwa vitu vinavyopoteza muda na nguvu.

Usiruhusu tamaa ya muda mfupi iharibu maisha ambayo ungeweza kuyajenga kwa miaka mingi.

*Kama haujaelewa niambie nipunguze sauti πŸ˜…πŸ™
❀4πŸ”₯2πŸ₯°1
Maumivu yana uwezo wa kufanya kila kitu kionekane hakina matumaini. Lakini hisia za leo si utabiri wa maisha yako ya kesho.

Wakati mwingine kipindi kigumu unachopitia si mwisho wa safari yako, bali ni sehemu ya kukujenga kuwa imara zaidi.

Endelea kupambana. Endelea kuamini. Maumivu ni ya muda, lakini ukiamua kutokata tamaa, kesho yako bado ina nafasi ya kuwa bora kuliko jana.

*Usiruhusu maumivu ya muda mfupi yaibe ndoto ya maisha yako yote.*
❀7
Sio kila jambo linahitaji maelezo, mabishano, au kulipiza kisasi.

Wakati mwingine, uamuzi wa busara zaidi ni kujiondoa kimya kimya na kulinda amani yako.
πŸ₯°2
𝐀𝐒𝐟𝐨 𝐑𝐚𝐀𝐒𝐀𝐨𝐬𝐒 𝐦𝐒𝐚𝐝𝐒

Kila mmoja wetu ana mipango, ndoto na malengo ya kutimiza. Lakini kuna ukweli mmoja ambao hakuna anayeweza kuukwepaβ€”kifo hakichagui umri, mali, cheo wala umaarufu.

Ndiyo maana usiahirishe kuishi maisha yenye maana. Usiahirishe kuwaomba msamaha uliowakosea, kuwasamehe waliokukosea, kuwathamini wazazi, familia na watu wanaokupenda. Kesho haijaahidiwa kwa yeyote.

Wengi huishi kana kwamba wana miaka mia mbele yao, mpaka siku wanapogundua muda umekwisha. Usisubiri tukio la kusikitisha ndipo uanze kuthamini kila siku uliyopewa.

Ukipoteza nafasi ya kufanya jambo jema leo, huenda usipate nafasi nyingine tena. Ishi kwa hekima, pendana na watu, mtangulize Mungu, na tumia kila siku kana kwamba ni zawadi ya mwisho uliyopewa.
❀7
Wakati mwingine, jambo dogo kabisa unaloliona linaweza kukuambia kila kitu unachohitaji kujua kuhusu mtu.

Usipuuze patterns angalia jinsi mtu anavyokutendea mambo yanapokuwa magumu, jinsi anavyokuheshimu pale ambapo hakuna anayewaona, na zaidi ya yote, jinsi anavyokufanya ujisikie.

Usiendelee kumpa mtu nafasi zisizo na mwisho kwa ajili ya kuthibitisha kile ambacho tayari moyo wako ulikiona mara ya kwanza.

Huhitaji kutengeneza visingizio kwa mtu kwa sababu tu unampenda. Wakati mwingine unapaswa kumkubali mtu kwa namna anavyochagua kujionyesha, si kwa namna unavyotamani siku moja awe.

> Unaweza kuwa na moyo mzuri na bado ukajua wakati wa kusema β€œimetosha.”
❀4