Smart Finance - SW
12 subscribers
4 photos
2 files
16 links
Maarifa sahihi, Taarifa sahihi
Download Telegram
Habari za Asubuhi Marafiki, ndugu, na wawekezaji wa fedha, tunaomba mtusaidie kufanikisha jambo hili!

Kama unajifunza kitu kupitia channel hii — hata kama ni kidogo — basi kuna watu wengi huko nje ambao pia wanapenda kupata maarifa haya ya fedha na uwekezaji, lakini hawajui pa kuanzia.

Leo tunaomba kitu kimoja tu kutoka kwako; 

SHARE link ya channel hii kwa watu wako wa karibu. Iwe ni kwenye WhatsApp groups, familia, marafiki, kazini au hata status zako.

Kwa nini?

Kila mtu anahitaji elimu ya fedha

Kuna watu wengi wanaumizwa na madeni au kupoteza pesa kwa sababu hawajui njia bora za kusimamia au kuwekeza pesa zao.

Na wewe unaweza kuwa msaada wao mkubwa kwa kuwaletea mwanga huu.

Tusaidiane kuinua maarifa ya kifedha na uwekezaji kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla. Kama wewe umefaidika, tafadhali fanya na wengine wafaidike pia. Asanteni.
Smart Finance - SW pinned «Marafiki, ndugu, na mashabiki wa fedha, tunaomba mtusaidie kufanikisha jambo hili! Kama unajifunza kitu kupitia channel hii — hata kama ni kidogo — basi kuna watu wengi huko nje ambao pia wanapenda kupata maarifa haya ya fedha na uwekezaji, lakini hawajui…»
🚨Shahada Yako Si Tiketi ya Mafanikio🚨

Watu wengi huamini kuwa wakishahitimu chuo kikuu na kupata degree au Diploma, basi mafanikio yanakuja moja kwa moja kama mvua.

Ukweli ni kwamba — Elimu ya darasani peke yake haitoshi. Kama hujui kusimamia fedha zako vizuri, diploma yako haina msaada mkubwa kwenye maisha halisi.

Fikiria hivi: mtu ana digrii ya biashara lakini anashindwa kuweka akiba, anatumia zaidi ya kipato chake, au anakopa bila mpango. Hapo digrii yake inamsaidia kweli? Hapana.

Alafu unajua hili si jambo jipya. Watu wengi wamekuwa wakifanya kosa hili hili miaka nenda miaka rudi. anajitahidi kusoma, wanafaulu vizuri, lakini bado wanashindwa kufanikiwa miaka mingi baadaye hata kama ana kazi nzuri.

Kwa nini?

Kwa sababu hawakujifunza misingi ya fedha binafsi (Personal Finance).

Ukweli ni Huu: Ili ujenge maisha bora na imara kifedha, unahitaji kujifunza stadi zifuatazo:

1. Linda Mali Zako
Ukipata kitu chochote cha thamani iwe ni gari, nyumba, au hata biashara hakikisha unaijua thamani yake na unaweka utaratibu wa kuilinda isipotee. Kwa mfano, ukiwa na biashara, unaweza kuisajili rasmi au kuwekea bima.

2. Simamia Fedha Zako Vizuri
Lazima ujue unapata kiasi gani kwa mwezi na pia lazima ujue unatumia kiasi gani. Tengeneza bajeti. Kama unapata Laki 5 kwa mwezi, basi hakikisha matumizi yako hayaizidi hiyo Laki 5. Usiishi maisha ya kuiga wengine — ishi kulingana na uwezo wako (Kila mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake).

3. Dhibiti Mzunguko wa Pesa Yako (Cash Flow)
Hakikisha pesa inaingia kwa wakati na matumizi yanaenda kwa vipaumbele. Usiache pesa zako zipotee kwenye mambo madogo yasiyo na maana na ulazima.

4. Epuka Kuongeza Gharama za Maisha Bila Sababu
Watu wengi wakiongeza kipato, wanaongeza na matumizi badala ya kuwekeza au kuweka akiba. Hili linaitwa lifestyle inflation. Unakuta mtu kipindi anaingiza laki 5 Kwa mwezi alikuwa anaishi vizuri tu, alivyopandishwa cheo tu au mshahara anaanza kuandamwa na madeni. Kwanini?

Kwasababu kipato kilipoongezeka akaongeza na matumizi yake pia. Kuongeza matumizi sio kosa, kosa ni hayo matumizi Yana matokeo Gani? Ni matumizi hasi au chanya, yanaleta faida?

5. Jenga Vyanzo Vingi vya Kipato
Usitegemee mshahara peke yake, na kama huna ajira basi usisubiri ajira. Anza kujitengenezea ajira mwenyewe. Anzisha biashara ndogo ndogo, jifunze kuuza bidhaa mtandaoni, au wekeza sehemu yenye kukupa faida.

Hata kuanza na mtaji mdogo kunaweza kukupa kipato cha pili kitakachokusaidia.

6. Tumia Mikopo kwa Akili
Mikopo siyo mbaya, lakini tatizo ni kutumia vibaya. Usikope kwenda likizo au kununua kitu kisicholeta faida. Kopa kwa malengo ya kuleta maendeleo, ukikopa nenda kafanye kile ulichopanga kufanya kabla hujapata huo mkopo.

Yupo mtu; alikuwa na mawazo mazuri kabisa akafungue biashara ya samaki. Alipokopa tu akabadili gia juu Kwa juu kaenda kulima mahindi. Huyo mtu atakuwa yupo hatarini kupoteza hiyo pesa, unajua kwanini? Kabla hajakopa akili yake ilikuwa stable and calm, alishafanya research ya Kila kitu kuanzia gharama za undeshaji wa biashara ya samaki, masoko, na Kila kitu.

Sasa kaenda kwenye mahindi Akiwa na hela mkononi hajui chochote kuhusu ukulima. Unadhani wastaafu wanapoteza vipi pesa zao?

Anza sasa kujifunza kuhusu haya mambo, ni zawadi utakayojipa maisha yako yote.

📚 Personal Finance
📚 Kodi
📚 Ujasiriamali
📚 Uwekezaji

Haya mambo ni muhimu kwa kila mtu. Kama huwezi kuyaelewa:- Elimu Yako haitokuwa na tija na mzunguko wako wa pesa hauwezi kustawi.
Smart Finance - SW
Mfanyabishara wa Nyani Katika kijiji fulani huko Mashariki ya Kati, jamaa mmoja aliwasili. Alijitambulisha kwa wenyeji kwamba yeye ni mfanyabiashara, na amekuja hapo kwa ajili ya kununua nyani. Alisema atanunua kila nyani kwa Shilingi elfu moja. Kwa kuwa…
Mfanyabishara wa Nyani Explained

Habari za Asubuhi My Smart People, ni jumapili nyingine tena. Jumapili ya 15 Kwa Mwaka 2025, na Leo nimeona tuchambue lile andiko la Mfanyabiashara wa Nyani.

Twende Kazi🤗

Ukweli ni kwamba yule mfanyabiashara na yule mfugaji wa nyani walikuwa watu wa kundi moja. Jamaa alikuwa akinunua nyani kwa wastani wa Shilingi elfu tatu na kuwapeleka kwa yule mfugaji. Halafu baada ya muda Fulani akawauzia wanakijiji wale wale kwa Shilingi elfu thelathini kwa kila nyani mmoja.

Mwisho wa siku, wale watu wawili (yule mfanyabishara na yule mfugaji) walitengeneza faida ya Shilingi elfu 27 kwa kila nyani mmoja.

Sasa naelezea:- Fikiria nyani kama hisa (shares) kwenye soko la hisa.

Hatua ya 1: Jamaa anakuja kununua nyani
Jamaa mmoja anakuja kijijini na anasema: "Nitanunua nyani mmoja kwa elfu moja."

📍 Watu wanapenda wazo hilo, kwa sababu nyani ni wengi na hawana faida yoyote. Kwa hiyo wanaanza kuwakamata na kumpelekea jamaa huyo. Wanapata hela, maisha yanaenda.

📚 Hii ni sawa na kampuni au mtu binafsi hasa mfanyabishara mkubwa anatoa taarifa au tangazo linalochochea uuzwaji wa hisa husika. Akishatoa taarifa hiyo mwenyewe anaingia sokoni na kuanza kununua hisa fulani. Wenye shida na wenye kutaka hela ya haraka wanaanza kuuza hisa zao.

Hatua ya 2: Jamaa anapandisha bei
📍 Nyani wanapopungua (share supply inspungus), jamaa anasema sasa atanunua nyani kwa elfu 5. Watu wanarudi tena porini kwa nguvu zaidi, kwa sababu bei imepanda. Lakini nyani sasa ni wachache. Wanapata wachache tu.

📚 Bei ya hisa inapanda kwa sababu bidhaa (nyani/hisa) inakuwa adimu, supply ndogo huku demand ikiwa kubwa. Kupanda kule Kwa hisa itawafanya watu wengi hasa short term investors kuuza hisa zao walizosalia nazo wakidhani hiyo ndo nafasi pekee ya wao kupata faida.

Hatua ya 3: Jamaa asema atanunua kwa elfu 10
📍 Sasa watu wanakimbizana kweli kweli, lakini hakuna nyani tena. Ghafla jamaa anasema anasafiri, lakini atarudi na atanunua nyani kwa elfu 50!

📚 Sasa yule mtu mkubwa au kampuni inatangaza jambo la kusisimua kuhusu hisa hiyo hiyo au kampuni hiyo hiyo na hivyo watu wanazidi kuamini thamani ya hisa hiyo itapanda zaidi na zaidi.

Unajua hisa ni limited resources na watu wengi walishauza zao Ina maana demand itakuwa kubwa zaidi na supply ya hisa hizo imekuwa ndogo sana.

Nini kitatokea? BEI ITAPANDA

Hatua ya 4: Watu wanatafuta nyani wa kununua
📍 Wanasikia kuna mtu kijiji cha mbali ana nyani. Wanaenda kumnunulia nyani wake kwa elfu 30, wakitegemea watamletea yule jamaa wauze kwa elfu 50. Wanarudi na nyani, wakisubiri hela yao...

📚 Kwakuwa wengi walishauza hisa zao na bei ya hisa ilishapanda kuliko walivyouza awali.. basi yule yule mwekazi anaanza kuwauzia tena na wao wanaanza kununua kwa bei kubwa, wakiamini wataziuza kwa bei kubwa zaidi baadae.

Watu hawa wametumia hisia badala ya akili kwenye kufanya maamuzi.

Hatua ya 5: Jamaa harudi tena
📍 Miezi inapita, miaka inapita, jamaa harudi. Wamebaki na nyani wa gharama kubwa, hawana wa kumuuzia. Ndipo wanagundua: kumbe jamaa na yule aliyewauzia nyani walikuwa na lengo moja. Waliwanunulia kwa bei ndogo, wakawauzia tena kwa bei ya juu—na faida yote ikawa yao.

Sasa tunajifunza nini Hapa

Kama utanunua hisa kwa sababu tu "watu wanasema bei itapanda", unajiweka kwenye hatari ya kuingia sokoni wakati bei iko juu — halafu ghafla bei ishuke, ukumbwe na hasara. Vilevile, kama utaamua kuuza kwa sababu "watu wengine wanauza", unaweza kuuza ukiwa na hasara kubwa, kisha bei ipande tena muda mfupi baadaye.

Hii inajulikana kama “panic selling” — na ndiyo inayowafilisi watu wengi.

Ebu Fikiria mtu aliyenunua hisa za TCCL (Twiga Cement) mwanzoni mwa mwaka 2020 baada ya kusikia watu wakisema “ni kampuni imara na faida zipo juu.”

Bila kufanya utafiti, akanunua kwa bei ya juu. Baadaye bei ikashuka kutokana na changamoto za kiuchumi na mabadiliko ya sera — akauza tena kwa hasara kwa sababu “watu walikuwa wanauza.” Kama angefanya tathmini ya kina, angejua kuwa kushuka kwa bei ni kwa muda tu, na angeweza kuvumilia hadi bei irudi juu.
1
Smart Finance - SW
Mfanyabishara wa Nyani Katika kijiji fulani huko Mashariki ya Kati, jamaa mmoja aliwasili. Alijitambulisha kwa wenyeji kwamba yeye ni mfanyabiashara, na amekuja hapo kwa ajili ya kununua nyani. Alisema atanunua kila nyani kwa Shilingi elfu moja. Kwa kuwa…
Habari za Asubuhi My Smart People, ni jumapili nyingine tena. Jumapili ya 15 Kwa Mwaka 2025, na Leo nimeona tuchambue lile andiko la Mfanyabiashara wa Nyani.

Twende Kazi🤗

Ukweli ni kwamba yule mfanyabiashara na yule mfugaji wa nyani walikuwa watu wa kundi moja. Jamaa alikuwa akinunua nyani kwa wastani wa Shilingi elfu tatu na kuwapeleka kwa yule mfugaji. Halafu baada ya muda Fulani akawauzia wanakijiji wale wale kwa Shilingi elfu thelathini kwa kila nyani mmoja.

Mwisho wa siku, wale watu wawili (yule mfanyabishara na yule mfugaji) walitengeneza faida ya Shilingi elfu 27 kwa kila nyani mmoja.

Sasa naelezea:- Fikiria nyani kama hisa (shares) kwenye soko la hisa.

Hatua ya 1: Jamaa anakuja kununua nyani
Jamaa mmoja anakuja kijijini na anasema: "Nitanunua nyani mmoja kwa elfu moja."

📍 Watu wanapenda wazo hilo, kwa sababu nyani ni wengi na hawana faida yoyote. Kwa hiyo wanaanza kuwakamata na kumpelekea jamaa huyo. Wanapata hela, maisha yanaenda.

📚 Hii ni sawa na kampuni au mtu binafsi hasa mfanyabishara mkubwa anatoa taarifa au tangazo linalochochea uuzwaji wa hisa husika. Akishatoa taarifa hiyo mwenyewe anaingia sokoni na kuanza kununua hisa fulani. Wenye shida na wenye kutaka hela ya haraka wanaanza kuuza hisa zao.

Hatua ya 2: Jamaa anapandisha bei
📍 Nyani wanapopungua (share supply inspungus), jamaa anasema sasa atanunua nyani kwa elfu 5. Watu wanarudi tena porini kwa nguvu zaidi, kwa sababu bei imepanda. Lakini nyani sasa ni wachache. Wanapata wachache tu.

📚 Bei ya hisa inapanda kwa sababu bidhaa (nyani/hisa) inakuwa adimu, supply ndogo huku demand ikiwa kubwa. Kupanda kule Kwa hisa itawafanya watu wengi hasa short term investors kuuza hisa zao walizosalia nazo wakidhani hiyo ndo nafasi pekee ya wao kupata faida.

Hatua ya 3: Jamaa asema atanunua kwa elfu 10📍 Sasa watu wanakimbizana kweli kweli, lakini hakuna nyani tena. Ghafla jamaa anasema anasafiri, lakini atarudi na atanunua nyani kwa elfu 50!

📚 Sasa yule mtu mkubwa au kampuni inatangaza jambo la kusisimua kuhusu hisa hiyo hiyo au kampuni hiyo hiyo na hivyo watu wanazidi kuamini thamani ya hisa hiyo itapanda zaidi na zaidi.

Unajua hisa ni limited resources na watu wengi walishauza zao Ina maana demand itakuwa kubwa zaidi na supply ya hisa hizo imekuwa ndogo sana.

 Nini kitatokea? BEI ITAPANDA

Hatua ya 4: Watu wanatafuta nyani wa kununua
📍 Wanasikia kuna mtu kijiji cha mbali ana nyani. Wanaenda kumnunulia nyani wake kwa elfu 30, wakitegemea watamletea yule jamaa wauze kwa elfu 50. Wanarudi na nyani, wakisubiri hela yao...

📚 Kwakuwa wengi walishauza hisa zao na bei ya hisa ilishapanda kuliko walivyouza awali.. basi yule yule mwekazi anaanza kuwauzia tena na wao wanaanza kununua kwa bei kubwa, wakiamini wataziuza kwa bei kubwa zaidi baadae. 

Watu hawa wametumia hisia badala ya akili kwenye kufanya maamuzi. 

Hatua ya 5: Jamaa harudi tena
📍 Miezi inapita, miaka inapita, jamaa harudi. Wamebaki na nyani wa gharama kubwa, hawana wa kumuuzia. Ndipo wanagundua: kumbe jamaa na yule aliyewauzia nyani walikuwa na lengo moja. Waliwanunulia kwa bei ndogo, wakawauzia tena kwa bei ya juu—na faida yote ikawa yao.
👍1
Sasa tunajifunza nini Hapa

Kama utanunua hisa kwa sababu tu "watu wanasema bei itapanda", unajiweka kwenye hatari ya kuingia sokoni wakati bei iko juu — halafu ghafla bei ishuke, ukumbwe na hasara. Vilevile, kama utaamua kuuza kwa sababu "watu wengine wanauza", unaweza kuuza ukiwa na hasara kubwa, kisha bei ipande tena muda mfupi baadaye.

Hii inajulikana kama “panic selling” — na ndiyo inayowafilisi watu wengi.

Ebu Fikiria mtu aliyenunua hisa za TCCL (Twiga Cement) mwanzoni mwa mwaka 2020 baada ya kusikia watu wakisema “ni kampuni imara na faida zipo juu.”

Bila kufanya utafiti, akanunua kwa bei ya juu. Baadaye bei ikashuka kutokana na changamoto za kiuchumi na mabadiliko ya sera — akauza tena kwa hasara kwa sababu “watu walikuwa wanauza.” Kama angefanya tathmini ya kina, angejua kuwa kushuka kwa bei ni kwa muda tu, na angeweza kuvumilia hadi bei irudi juu.

Watu wakubwa na kampuni kubwa hutawala hisia za soko. Ukiona CEO wa kampuni fulani anatangaza mpango wa upanuzi au sera fulani, au mwekezaji maarufu anaweka mamilioni kwenye hisa fulani. Kuwa makini, kuwa macho na tambua kuwa taarifa hiyo ina malengo yake.

Haijatangazwa tu Kwa bahati mbaya, huenda ni ya kuongeza hamasa ili waweze kuuza au kununua kwa bei wanayoilenga baada ya watu wa kawaida kufanya maamuzi kwa presha.

Kumbuka: Kwenye Soko la Hisa, taarifa ni nguvu, lakini ufahamu wa taarifa hizo ni silaha.

Kwa hiyo kabla hujanunua au kuuza hisa: Fanya utafiti wa kampuni husika: Angalia mapato yake, mikakati yake ya ukuaji, na rekodi yake kihistoria.

📚 Soma ripoti za kifedha za kampuni hiyo

📚 Fuata malengo yako, siyo kelele za mitandaoni au vijiweni au makazini au popote pale.

📚 Usiogope kushikilia hisa zako kwa muda mrefu endapo unaona na kujiridhisha kampuni ina misingi mizuri ya biashara.

Jifunze kuelewa soko, Usiigize umati. Faida kubwa haiko kwa wenye taarifa tu, bali kwa wenye uelewa sahihi wa taarifa hizo. wachache wenye kuujua huu mchezo wanapata faida kubwa.

Usiwe kama wanakijiji waliobaki na nyani mikononi wakisubiri mtu asiye na mpango wa kurudi.

Umejifunza kitu? Share ujumbe huu Kwa Ndugu na jamaa Ili nao wajifunze pia: 

Telegram:
https://t.me/smartfinancetztz

Whatsapp:
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4KXi3DjiOlFNeofA0w

Facebook:
https://www.facebook.com/profile.php?id=61575099031913
👍1
Katika safari ya maisha ya binadamu, changamoto siyo kikwazo bali ni daraja la kuelekea mafanikio. Mara nyingi matatizo tuliyonayo mfn madeni, ukosefu wa kazi, au kipato kidogo huonekana kama mwisho wa maisha yetu na wengi wet hupoteza kabisa matumaini ya kuishi. lakini bila kujua ndani ya hizo changamoto kuna mbegu ya mafanikio, Pengine mafanikio ambayo yalikuwa ni ndoto tu hapo awali.

maarifa na nidhamu hujengwa na changamoto tunazopitia, Badala ya kukata tamaa, mtu aliye smart kichwani huyachunguza matatizo aliyonayo kwa jicho la fursa na kujiuliza, "Naweza kujifunza nini hapa?" au "Ninawezaje kubadilisha hali hii kuwa chanzo cha kipato?" Hapo ndipo mstari wa kumtenganisha masikini na tajiri unapochorwa.

Kwani humjui
📚 Regina Ndiva
📚 Rehema Kasule
📚 Reginald Mengi
📚 Ally Mafuruki
📚 Mohammed Dewji

Hapa ni baadhi tu ya watanzania maarufu waliogeuza matatizo yao kuwa biashara zenye mafanikio:  Watanzania hawa, walijua jinsi ya kuzigeuza changamoto zao kuwa fursa na hatimaye kuanzisha biashara kubwa zenye mafanikio.

Mafanikio huanza utakapolielewa Tatizo, kutafuta namna ya kulitatua na kuangalia namna unavyoweza faidika na Hilo Tatizo:- iwe Kwa kupata maarifa au mapato kabisa. Tabia hiyo itakuandaa kuwa mwekezaji bora au mjasiriamali Bora.

Kwa mfano, mtu anayekumbwa na changamoto ya fedha anaweza kugundua umuhimu wa kuweka akiba, kujifunza kuhusu uwekezaji mbali mbali, au kuanzisha biashara yenye faida iwe physical au mtandaoni.

Hali ngumu tunazopitia zitufunze kuwa wabunifu, kuwa na nidhamu na pia kuwa na moyo wa uthubutu. Kwa hiyo, kila unapokutana na tatizo lolote, usione mwisho bali mwanzo mpya wa kubadilisha maisha yako hasa kifedha.

Nitafurahi endapo wewe unayesoma andiko hili uje kuwa Regina Ndiva ajae au Ally Mafuruki. Kila la kheri🤗

Umejifunza kitu? Basi usiwe mchoyo.. share ujumbe huu Kwa ndugu, jamaa na marafiki zako nao pia wapate kujifunza.

Smart Finance - Maarifa sahihi, Taarifa sahihi.

Telegram:
https://t.me/smartfinancetztz

Whatsapp:
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4KXi3DjiOlFNeofA0w
1👍1
MwanaSmart - Huwezi kufanikwa kama hujajifunza kuacha baadhi ya vitu. Kuna majukumu, tabia, au hata watu ambao ni lazima uwaache kwa makusudi ili utoe nafasi kwa yale mambo yenye thamani na tija zaidi katika maisha yako.

Muda tulio nao kila siku ni mdogo sana — takriban saa 16 za kuwa macho na kufanya shughuli. Ili uweze kutumia muda huo vizuri, ni muhimu kujitenga na wale wanaokuchelewesha, wanaokukwamisha, au wanaokuchanganya. Badala yake, tumia muda huo kwa watu na shughuli zitakazokupeleka mbele.

Changamoto kubwa kwa watu wengi ni kushindwa kuachana na mazoea yao. Lakini ukweli ni kwamba, huwezi kupanda ngazi ya juu bila kuiacha ile ya chini. Kubadilika ni lazima kama unataka kusonga mbele.

Nakuombea neema ya Mungu — akupe hekima ya kufanya maamuzi bora, na nguvu ya kuachana na yale yanayokurudisha nyuma, ili ufuatilie malengo yako kwa ujasiri na uthabiti.
Wiki ya Kuachana na Vizui vya Mafanikio:

Hii ni wiki ya 16 Kwa Mwaka huu 2025. Ni wiki ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yetu, ni wiki ya mabadiliko hapa Smart Finance! Wiki hii, tunakwenda kujifunza njia saba za kuacha mambo yote yanayokukwamisha kufikia mafanikio yetu.

Kila siku, tutajifunza njia moja muhimu ambayo itatusaidia kuvuka vizingiti na kusogea karibu zaidi na ndoto zetu.

Ukikaa na tabia, watu au mazingira yasiyo na tija — ni ngumu sana kufanikiwa. Lakini ukijifunza namna ya kuachilia vilivyokuzoea, unaweza kuingia kwenye ukurusa mpya wa mafanikio.

Hakikisha hukosi hata siku moja! Jifunze kila somo, na ulifanyie kazi, na anza kutengeneza maisha unayoyataka.

Usipange kukosa😋

Smart Finance - Maarifa sahihi, Taarifa sahihi
SOMO LA KWANZA: Tambua Mambo Yanayokurudisha Nyuma

Umasikini na Utajiri ni kama maradhi yanayo ambukizwa. Ukijiweka karibu na Umasikini utakuwa masikini, vile vile ukijiweka karibu na Utajiri utakuwa tajiri.

Kuna tabia, watu, na mazingira fulani ambayo yanaweza kukurudisha nyuma katika safari yako ya mafanikio.

Nitaelezea🤗

📚 Tabia zinazorudisha nyuma

1. Uvivu:
Siku moja Ina masaa 24, hii ni Kwa Mtu yoyote yule Duniani:- Iwe masikini au tajiri. Kwanini huyu anakuwa tajiri, Alafu huyu anakuwa masikini? Jibu ni rahisi

"Ni jinsi wanavyoyatumia masaa 24 katika Kila siku zao"

Ukijiona unapenda kulala muda mwingi, hutaki kufanya kazi, unataka kupata tu pesa bila juhudi, umeridhika na maisha unayoishi, una biashara Ina kipato kile kile mwaka wa 10 Sasa.. Ndugu yangu utashindwa kukua, utashindwa kufanikiwa.

Tabia zinazorudisha watu nyuma zipo nyingi. Kaa chini utakafakari:- Nini hasa kinarudisha nyuma

Kubeti?
Uwoga? Watu wanaoogopa kuchukua hatua kwa sababu ya kuogopa kushindwa hawawezi kusonga mbele.
Tamaa?
Ngono?


📚Watu wanaorudisha nyuma
Watu wa maneno ya kukatisha tamaa: Marafiki au ndugu wanaokudharau au kusema huwezi kufanikiwa. Unataka kufanya jambo Fulani lakini anatokea mtu na kukwambia "Hiyo kazi haina faida" mtu huyo achana nae

📚 Pia achana na Marafiki/Ndugu wanaotegemea msaada wako kila mara lakini hawakusaidii chochote.

📚 Mazingira yanayorudisha nyuma. Kama nilivyosema hapo awali, Umasikini unaambukizwa. Kukaa katika jamii inayokosoa maendeleo au isiyojali mafanikio binafsi., kutakufanya uzidi kuwa masikini.

Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga Hatua ya kwanza ya mafanikio Yako. Nikutakie usiku mwema na Kila kheria MwanaSmart Mwenzangu.

Usisite kushare ujumbe huu na wengine pia wapate kujifunza. Siku njema

Telegram:
https://t.me/smartfinancetztz

Whatsapp:
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4KXi3DjiOlFNeofA0w
Baada ya kuishi pamoja kwa miaka 16 bila ndoa rasmi, Mkurugenzi wa lebo ya “Cash Money Records”, Birdman (56), na mwimbaji mashuhuri wa RnB, Toni Braxton (57), waliamua kufunga ndoa kimya kimya wiki iliyopita.

Hata hivyo, ndani ya siku 3 tu baada ya ndoa hiyo, Toni Braxton aliwasilisha maombi ya talaka akidai kuwa ndoa hiyo ilifungwa kimakosa kisheria. Kilichovutia zaidi ni madai yake ya kutaka kugawana utajirinusu Kwa nusu, ambao unakadiriwa kuwa dola za Marekani milioni 160 – sawa na zaidi ya TSh bilioni 419.

Hii imeibua mjadala mkubwa kuhusu ulinzi wa mali binafsi katika ndoa, hasa kwa watu wenye utajiri mkubwa. Kesi hii inaonesha umuhimu watu kuingia kwenye ndoa wakiwa na mikataba ya kabla ya ndoa (prenup agreements), ili kuzuia migogoro ya kifedha iwapo mambo yataharibika.

Ni somo muhimu kwa wawekezaji na watu wenye malengo ya kifedha – uhusiano wa kimapenzi haupaswi kufumbiwa macho kwenye mipango ya kifedha. Ulinzi wa investment s zako ni ni sehemu muhimu sana.

Telegram:
https://t.me/smartfinancetztz

Whatsapp:
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4KXi3DjiOlFNeofA0w
Uchambuzi wa Kifedha kwa Hisa za CRDB – by Smart Finance

Kwa sasa, bei ya hisa za CRDB ipo kwenye TZS 790 kwa kila hisa. Kwa mujibu wa uchambuzi wa soko tulioufanya, kuna uwezekano mkubwa bei hii ikasimama hapo ilipo au kushuka kidogo katika kipindi kifupi kijacho.

Iwapo bei itashuka, inakadiriwa kugusa kiwango cha TZS 780. Na kama presha ya mauzo itaendelea, bei inaweza kushuka zaidi hadi kati ya TZS 740 hadi 780.

Kwa Wawekezaji wa Muda Mrefu: Kama lengo lako ni kupata gawio la kila mwaka na pia kuongeza thamani ya mtaji wako (capital gain), basi ni busara kuendelea kushikilia hisa zako.

Kulingana na mwenendo wa kihistoria na matarajio ya kampuni, kuna uwezekano mkubwa bei ya hisa hizi kufikia kati ya TZS 970 hadi 1,020 kabla ya kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2025/2026.

Kumbuka: Soko la hisa lina mabadiliko ya ghafla, na hivyo chochote kinaweza kutokea. Huu ni uchambuzi wa kitaalamu tulioufanya kwa kutumia taarifa zilizopo, lakini nasisitiza ufanye utafiti wako binafsi (Do Your Own Research - DYOR) kabla ya kufanya uamuzi wa kununua au kuuza.

Kila la heri katika safari yako ya uwekezaji, Mshauri wako wa kifedha - Smart Finance SW

https://t.me/smartfinancetztz
👍1
HISA 5 ZILIZOLETA FAIDA/HASARA ZAIDI - 2024

Uwekezaji kwenye hisa ni njia yenye uwezo wa kuongeza thamani ya mali zako, lakini pia unakuja na hatari zake. Hivyo ni kawaida kupata faida kubwa au kidogo lakini pia ni kawaida kupata hasara kubwa ama kidogo, kulingana na mabadiliko ya soko na kiasi Cha uwekezaji wako.

Taarifa za karibuni kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) zinaonyesha kwa uwazi namna hisa mbalimbali zilivyochangia katika kupanda au kushuka kwa thamani ya uwekezaji kwa mwaka 2024.

Hisa Zilizofanya Vizuri Zaidi:
Tanga Cement (TCCL) – Faida ya 93%
Hisa ya Tanga Cement iliongoza kwa ongezeko kubwa la thamani, ikipanda kwa asilimia 93 mwaka 2024.

KCB Bank (KCB) – Faida ya 108.57%
Hisa ya KCB Bank, ambayo ni kampuni iliyoorodheshwa pia katika masoko mengine, iliongezeka kutoka TZS 350 hadi TZS 730, ikiwa ni ongezeko la asilimia 108.57.

East African Breweries Limited (EABL) – Faida ya 82.97%
EABL, kampuni nyingine iliyoorodheshwa katika masoko mbalimbali, iliongezeka kutoka TZS 1,820 hadi TZS 3,330, ikiwa ni ongezeko la asilimia 82.97.


National Investments Company Limited (NICOL) – Faida ya 67%
NICOL, kampuni ya uwekezaji, ilirekodi faida ya asilimia 67 mwaka 2024.


NMB Bank – Faida ya 58%
Hisa ya NMB Bank iliongezeka kwa asilimia 58 mwaka huo.


Hisa Zilizofanya Vibaya Zaidi:
🟥 Swissport Tanzania (SWISS)
Hasara ya 16.67%

🟥 Tanzania Portland Cement Company (TPCC)
Hasara ya 11.93%

🟥 DCB Commercial Bank (DCB)
Hasara ya 6.06%

🟥 National Investment Company Ltd (NICOL)
Hasara ya 5.48%

🟥 Maendeleo Bank Plc (MBP)
Hasara ya 2.86%

Mambo ya Kuzingatia kwa Wawekezaji wa Hisa

📌 _Fanya Utafiti wa Kutosha Kabla ya Kuwekeza._ 
Kabla ya kununua hisa, ni muhimu kufahamu hali ya kifedha ya kampuni, mwenendo wa sekta husika, pamoja na viashiria vya thamani ya soko. Hii itakusaidia kujua kama ni uwekezaji unaofaa na kama bei yake ni ya haki na halisi.

📌 _Gawa Uwekezaji Wako kwa Busara (Diversification)._ 
Usiwekeze pesa zako zote kwenye kampuni moja tu. Badala yake, wekeza kwenye hisa kutoka kampuni na sekta tofauti ili kupunguza hatari iwapo kampuni moja itapata hasara.

📌 _Angalia Faida kwa Ujumla._ 
Thamani ya hisa inaweza kupanda, lakini usisahau gawio (dividends) ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza mtaji wako kwa muda mrefu.

📌 _Tambua Kuwa Masoko Hubadilika._ 
Hata kampuni imara zinaweza kupitia changamoto za muda. Hivyo, kuwa na mtazamo wa muda mrefu na subira ni muhimu katika safari ya uwekezaji.

📚 Je Wajua.!!
Kuna hisa ndani ya Soko la hisa la Dar es salaam, ambayo imeshaleta faida ya zaidi ya 17% Kwa Mwaka 2025 pekee - hii ni ndani ya miezi minne pekee (Jan 2025 - Apr 2025). Unaijua hisa hiyo ni ipi?

Endelea kubaki kwenye Channel yetu ujifunze zaidi jinsi ya kunufaika na fursa kama hizi kwa wakati unaofaa. Share ujumbe huu, Ili nao wapate kufaidika na Maarifa haya.

Telegram:
https://t.me/smartfinancetztz

Whatsapp:
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4KXi3DjiOlFNeofA0w
Uwe na siku Njema🤗
👍1
Kama upo chini ya Miaka 45 Hii inakuhusu

Nikiwa nipo zangu Mgahawani hapa kariakoo napata sharubati ya Maembe. Ng'ambo ya pili likapaki gari la mizigo na wabebaji (Makuli) wakafika na kuanza kazi ya kupakua ule mzigo.

Kile kitendo kilinifikirisha na kuibua wazo Fulani akilini mwangu. Kwanza Ile kazi (ya ubebaji mizigo) lazima watakuwa wameifanya Kwa muda mrefu, kwasababu kabla sijamaliza Sharubati yangu gari lote lilikuwa limeisha na kuondoka.

Sasa..

Leo hii wale wabeba mizigo Wana nguvu ya kuifanya Ile kazi. Vipi wakifikisha miaka 60+? Vipi kama wakiumwa na kukosa nguvu tena ya kufanya Ile kazi? Je wamejiandaa na kesho Yao?

Hilo swali nikajiuliza na Mimi pia. NIMEJIANDAA NA KESHO YANGU?

Leo Nina nguvu ya kufanya hichi nachofanya, kupata kipato; kesho Nikiwa Sina hizi nguvu nitaishije? Em jiulize pia Hilo swali kisha utafakari na majibu jipatie mwenyewe.

Kesho yetu inakuja, ipo njiani. Haiwahi Wala haichelewi. Ipo tu pale inasogea taratiiiiibu.

Hivi unajua jinsi ulivyo Sasa, Hali ya maisha uliyonayo Sasa ni matokeo ya yale uliyochagua kufanya mwenyewe hapo awali. Kwa Asilimia 75% sisi wenyewe ni responsible wa haya maisha tunayoishi.

Kama unaishi maisha mabaya, maisha magumu, usimtafute mchawi. Mchawi ni wewe mwenyewe.

Lakini pia kama unaishi maisha mazuri, maisha ya ndoto zako, usimtafute wa kumpongeza. Jipongeze wewe mwenyewe.

Good news ni kwamba hujachelewa, unayo nafasi ya kubadilisha kile unachoona hakifai. Maisha unayoishi huyapendi? Unayo nafasi ya kuyabadili.

ANZA LEO

Mabadiliko huanza kwako binafsi, Kaa chini tafakari. Nini hutaki? wapi ulikosea? Nini unataka? Ufanyaje kukipata?

Weka mifumo, jiwekee mikakati, jiwekee sheri na uanze kuzifata effectively.

Kwa Leo niishie hapo ila kesho nitapost mkakati madhubuti, wenye Uhalisia wa 100% unaoweza kuutumia kuitengeneza kesho Yako hata kama kipato chako ni kidogo Cha chini ya 300,000 Kwa mwezi. Usipange kukosa.
UMASKINI KWA LUGHA NYINGINE NI UJINGA  😭

Sehemu ambapo ujinga ni mwingi mara nyingi kama si mara zote pana umaskini.

Tunaweza kutumia msamiati ujinga ama msamiati umaskini kuwasilisha hoja moja. 

Ukisikia taifa maskini, maana yake ni taifa lenye watu wajinga wengi. Taifa lenye watu wasioweza kuvuna na kutumia rasilimali zao kwa ufanisi. 

Watu wasiopenda kukosolewa wanaweza kunishambulia lakini haitaubadili ukweli.

Hivyo hivyo kwenye familia.. ukisikia familia Fulani ni masikini, maana yake ni wanafamilia wengi wa hiyo familia ni wajinga na walishindwa au wanashindwa kutumia rasilimali zinazowazunguka vizuri na Kwa ufanisi.

Mkiwa watu 100 na kati yenu wakawepo watu 6 wanaojisomea wenye akili yenye mantiki na kujiendeleza hamuwezi kujiita watu werevu kwa ujumla wenu.

Kwanini? Kwasababu Bado asilimia 94% ni watu wajinga na asilimia 6% pekee ndio wenye akili naa hivyo tunapozungumzia taifa zima tunahitimisha kuwa ni taifa la wajinga japokuwa wapo wachache wenye uwezo mkubwa. 

Rai yangu ni tuongeze kasi ya kushawishi kila mmoja wetu kujenga utamaduni wa kujisomea na kujiendeleza mfululizo ili tuwe na taifa lenye watu waerevui. 

Katika kitabu cha Malcom Gladwell cha "The Tipping Point" anawasilisha dhana inayofafanua kuwa ili taifa liendelee kwa kasi na tena maendeleo yatokane na shughuli za ndani ya nchi kuna mlimbikizo kiasi fulani cha maarifa na ujuzi vinavyotakiwa kufikiwa kwenye taifa kwa ujumla.

Hiko kiasi ndicho kinachoitwa the tipping point ambapo serikali haitakuwa tena chagizo la maendeleo bali jamii ndiyo itakayokuwa chanzo kikubwa cha maendeleo na mabadiliko.

📚 Usilaumi serikali Kwa Umasikini wako, jilaumu wewe mwenyewe.
📚 Usiwalaumu Wazazi Kwa Umasikini wako, jilaumu wewe mwenyewe 

Asanteni... Muwe na usiku Mwema