Tanzania Aquaculture Organization
14 subscribers
13 photos
5 links
🐋 Online Consultactions and Trainings.
🐋 Aquaculture Business Mediator.
🐋 Aquaculture Systems Design.
🐋 Aquatic Conservations.
Tel. +225 677 991 074.
Download Telegram
Kurutubisha Maji Ya Bwawa

Tengeneza sehemu ya kutunzia mbolea (wigo) ndani ya bwawa kwa kutumia fito na kamba.
Rutubisha kwa kutumia samadi ya wanyama mbalimbali wafugwao kama ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura, bata, kuku, n.k.

Usafirishaji wa Vifaranga

Unaweza tumia ndoo ama mifuko ya plastiki na oksijeni.

Ndoo hutumika ikiwa unasafirisha vifaranga wachache na kwa umbali mfupi.

Kwa kutumia mifuko ya plastiki na hewa ya oksijeni hubeba samaki wengi na kwa umbali mrefu.

Ni vyema kuwatumia wataalamu katika suala la
kusafirisha vifaranga vya samaki ili kuzuia au kupunguza uwezekano mkubwa wa idadi kubwa ya vifaranga kufa.

Jinsi ya Kuweka Samaki kwenye Bwawa

Unapofikisha vifaranga shambani, kabla ya kuviweka kwenye bwawa la kufugia hakikisha joto la maji ya kwenye bwawa na joto la maji yaliyokuja na vifaranga ni sawa.

Unaweza kufanya
hivyo kwa kuweka chombo kilicho tumika kusafirisha samaki kwenye maji bwawani kwa muda wa dakika 15 hivi kabla ya kuwaweka samaki katika bwawa.

Au unaweza kuchota maji kutoka kwenye bwawa na kuyaweka polepole kwenye chombo kilichotumika kusafirishia.

Baadaye mifuko hufuguliwa kuruhusu maji ya bwawa kuchanganyika na maji ya mifuko iliyotumika kusafirishia samaki. Samaki wakisha zoea hutoka wenyewe kwenye mifuko na kuingia ndani ya bwawa la samaki.

NB: Epuka kuwamwaga samaki harakaharaka kwenye bwawa na kuondoka.

Ujazo wa Samaki au Kiasi cha Kupandikiza kwenye Bwawa

Katika ujazo wa kati, samaki watatu au wanne huwekwa kwenye kila mita ya mraba ndani ya bwawa. Ujazo huu huruhusu ubadilishaji wa maji kwenye bwawa la samaki kati ya wiki moja na mbili, pengine hadi mwezi mmoja kulingana na ubora wa maji. Ili kuepuka uchafuzi wa maji, epuka kujaza samaki wengi kwenye bwawa moja pia ulishaji wa samaki uwe wa wasitani.

Kawaida inashauriwa samaki watunzwe kwa miezi 5 hadi 6 halafu wavunwe.
Urefu na maana ya Sech disc
CHAKULA NA ULISHAJI WA SAMAKI


Chakula cha Samaki

Samaki anakula chakula cha asili (hutokana na urutubishaji wa bwawa) na chakula cha
kutengeneza (unga na peleti). Ni mhimu kuzingatia aina na ubora wa chakula cha samaki katika
kipindi chote cha ufugaji samaki. Tafta chanzo/kampuni inayouza ama kuzambaza chakula bora na kwa bei wezeshi.

Katika ufugaji wa samaki, chakula kina chukua robotatu ya jumla ya ghalama zote za ufugaji.


Ulishaji wa Samaki

Kawaida samaki akiwa mdogo hulishwa 11% ya uzito wake kila baada ya masaa mawili au
manne. Walishe samaki wako kwa muda maalum usibadili, wakati wa kulisha weka chakula kidogokidogo pembeni kwenye kona ya bwawa. Samaki walishwe kulingana na uzito wao, ni vyema kuvua samaki wachachi kila baada ya wiki moja au mbili na kuwapima uzito wao.

Samaki wakubwa wanapaswa kulishwa chakula sawa na asilimia 5 ya uzito wao.

Kwa mfano, kama samaki ana uzito wa gramu 100, Chakula cha kulisha kwa siku = 5/100 x 100 = gramu 5.

Hivyo atakula chakula gramu 5 samaki mmoja, zidisha gramu 5 na jumla ya samaki walioko
kwenye bwawa ili kupata kiasi cha chakula cha samaki wote walioko kwenye bwawa kwa siku.

Ulishaji wa samaki na aina ya chakula cha samaki ni mhimu sana katika ukuaji wa samaki.
Hakikisha unawalisha samaki wako chakula cha kutosha na kiwe na ubora. Ukuaji wa samaki unategemea zaidi katika aina ya chakua wanacho kula na namna wanavyo lishwa.

NB: Samaki wadogo walishwe mala kwa mala inashauriwa kila baada ya masaa mawili au
manne huku ukizingatia uzito wao, pia samaki wakubwa kawaida hulishwa asubuh, mshana na jioni au kila baada ya masaa manne.

Tafadhali kumbuka,! usizidishe chakula au idadi ya samaki
kwenye bwawa.
Utunzaji wa Bwawa la Samaki

Hakikisha bwawa lako liko na Ujazo wa maji ya kutosha ili hewa ya oksijeni iendelee kuwepo ndani ya bwawa. Kina cha maji kisiwe chini ya sm 70 wakati wote, hepuka kujaza maji kwa wingi Kwani Hii husababisha kuoga kwa mimea midogo ambapo ikiwa mingi zaidi uchafua maji.
Ubora wa Maji Bwawani

Ukuaji mzuri wa samaki hutegemea zaidi ubora wa maji, hivyo ni lazima kufanya upimaji wa ubora wa maji kwa kuangalia viashiria vyake kama vile joto, hewa ya oksijeni na pH.

Vifaa vya kupima ubora wa maji huwa ni vya gharama kubwa. Njia rahisi ya kuangalia ubora wa maji kwenye bwawa ni kuangalia tabia za samaki, kama vile samaki kupanda juu na kuachama midomo ili kutafuta hewa . Samaki aina ya sato huhitaji uwepo wa hewa ya okisijeni kwa ujazo kati ya milligram 2.5 hadi 10 kwa lita ya maji, pH kati 6.5 na 7.5, joto kuanzia degree za sentigredi 24 hadi 30 kwa ukuaji mzuri.

Badilisha maji mala baada ya kuona yamechafuka sana
ili kuepuka mripuko wa magonjwa na kudumaa kwa samaki katika ukuaji, maji yakiwa machafu sana samaki hawezi kula chakula na hewa hukosa hivyo atakufa au kudhoofika katika afya na
ukuaji unakuwa wa taratibu sana.

Uvunaji wa Samaki

Mzunguko mmoja wa ufugaji wa samaki hufikia tamati kwa mafanikio ya kuvuna baada ya
miezi sita hadi minane kuanzia muda walipo pandikizwa vifaranga. Katika kipindi hiki,
inategemewa kwamba samaki mmoja afikishe uzito kati ya gramu 250 hadi 400, hivyo kuwa tayari kwa kuvuna kwa matumizi ya kitoweo au kuuza kibiashara. Uvunaji wa samaki kwenye bwawa hutegemea zaidi malengo ya mfugaji na upatikanaji wa masoko. Wateja wanapokuwa wengi, mfugaji huweza kuvuna samaki wote, au anaweza kuvuna kidogo kidogo.

Hivyo uvunaji wa samaki umegawanyika katika sehemu kuu mbili; uvunaji wa rejareja na jumla yaani wote ndani ya bwawa. Nyavu ndogo au kokoro dogo hutumika mala nyingi katika uvuaji wa samaki
kwenye bwawa wakati wa mavuno au mabadiliko yanapo tokea katika bwawa. Katika kipindi cha kuvua samaki hupata mshituko sana (stress), hivyo unashauriwa kutokuwalisha siko moja
kabla ya kuvua kama unataka kuwaamisha kutoka bwawa moja kwenya jingine.

Epuka kuwachezea Sana samaki wakati wa uvuaji pia epuka samaki wako wasipate mkwaruzo au majeraha yeyote.
Kwa leo tutakomea hapo. Usikose kipindi kijacho.

Kama unaswali, ushauri, pendekezo au hoja yeyote, tafadhali tushikishe kupidia discussion chamber au group letu la whatsapp .

Link zipo hapo juu kwenye hii channel.

Nakutakia siku njema.
Habari za uzima ndugu zangu.

Karibu darasani
Leo tutajifunza juu ya

Changamoto za ufugaji samaki
CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA SAMAKI

Kuna changamoto mbalimbali za ufugaji wa samaki ikiwa ni pamoja na wizi, ujangili, uchafu wa maji, ndege wala samaki, samaki kula samaki wengine, mlipuko wa magonjwa, ukosefu wa chakula bora cha samaki, na mbegu bora za vifaranga vya samaki. Katika ufugaji wa samaki ni bora kuwa na mtaalamu aliye na ujuzi, maarifa na elimu juu ya ufugaji samaki.

Changamoto nyingi hutokea kulingana na utunzaji na namna ya ufugaji unao tumika katika kipindi kizima cha ufugaji.


1. Wizi na Ujangili
Hili ni tatizo kwa mabwawa ambayo hayajazungushiwa uzio au hayana ulinzi hivyo kutoa
mwanya kwa watu wasio waaminifu kuvuna samaki pasipo idhini ya mwenye bwawa.

Changamoto hii hukithiri zaidi endapo bwawa la samaki limejengwa mbali na nyumba za makazi.

Weka uzio kuzunguka bwawa la samaki au weka ulinzi ili kulinda uwekezaji na miundo mbinu
ya shamba la samaki isiharibiwe na watu wasio waaminifu. Ni muhimu pia kushirikisha jamii inayozunguka eneo hilo kabla ya kuanza mradi wa ufugaji samaki ili jamii iwe sehemu ya shughuli zako.

Inashauriwa kuweka nyavu juu ya bwawa ili kuzuia ndege kula samaki.

2. Uchafu wa Maji
Uchafuaji wa maji husababisha kupungua kwa hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu katika
maisha ya kiumbe hai yeyote. Uchafu husababishwa na msongamano mkubwa wa samaki ndani ya bwawa au namna ya ulishaji wa samaki ndani ya bwawa. Endapo samaki watakuwa
wanalishwa kupita kiasi kinachotakiwa, mabaki ya chakula ndani ya bwawa yanapooza husababisha uchafu kwenye maji kuongezeka. Pia samaki huchafua maji kutokana na kuzalishwa kwa wingi taka za ammonia na urea kutoka kwenye mwili wa samaki. Kemikali ambazo zinaweza kufanya maji yasifae kwa ufugaji wa samaki ni pamoja na dawa za kuua wadudu
kwenye mashamba ya umwagiliaji, maji taka yanayotoka viwandani au hospitalini kuelekeza kwenye mito, taka ngumu, plastiki, n.k.
Jinsi ya Kutatua

Ni lazima kupima ubora wa maji asubuhi na jioni kila siku. Kubadili maji endapo utaanza kuona samaki wanaanza kuja juu ya maji mara kwa mara kutafuta hewa au wanaanza kukusanyika eneo la kuingizia maji.

Lisha samaki chakula kilicho bora ikiwezekana kiwe cha kuelea juu ya maji.

Epuka chakula kudondoka ovyo ovyo chini ya bwawa wakati unalisha, pia zingatia idadi ya
samaki kwenye bwawa lako iliwe kubwa sana.

Hakikisha maji unayojaza kwenye bwawa lako ni
safi na salama kwa samaki, chunguza vyema chanzo cha maji unayoweka kwenye bwawa kisiwe na uchafu wa aina yeyote ambao ni hatari kwa samaki.

3. Mlipuko wa Magonjwa

Samaki kama walivyo wanyama wengine hushambuliwa na magonjwa mbalimbali
yanayosababishwa na bakteria, virusi na vimelea vingine vya magonjwa. Magonjwa husababisha hasara kwenye uzalishaji wa samaki kupitia vifo vya samaki, gharama za matibabu, kupoteza mauzo na kudumaa kwa samaki walioathirika.

Mlipuko wa magonjwa mara nyingi husababishwa
na samaki kuwa wengi kupita kiasi cha uwezo wa bwawa, kukosa chakula cha kutosha, maji kuchafuka, kuchubuka, na mazingira mengine yasiyo salama kwa viumbe wengine.

Dalili za samaki kushambuliwa na magonjwa ni pamoja na:-

 Kukosa hamu ya kula chakula.
 Kujikusanya kwenye maingizio ya maji.
 Tabia zisizo za kawaida kama vile kuogelea upande upande, kujizungusha, kutulia sehemu moja kwa muda mrefu.
 Kubadilika rangi na kumomonyoka kwa mapezi au ngozi.
 Kujikwaruza kwenye vitu vigumu ndani ya bwawa, au kwenye kingo za bwawa.
 Kujaa kwa maji kwenye matumbo ya samaki, na
 Kuvimba macho.
Jinsi ya Kuzuia

i.Ni lazima kujiridhisha kwamba chanzo cha maji yanayoingia kwenye bwawa lako ni
salama kwa samaki.

ii.Tumia mbegu za samaki kutoka chanzo kinachoaminika na kuhakikisha samaki
uliochukua ni salama.

iii.Kabla ya kuweka samaki kwenye bwawa kutoka sehemu nyingine, ni lazima kuwatibu ili
kuua vijidudu vilivyojishikiza juu ya ngozi zao. Tumia chumvi ya kupikia (10% concentration) changanya na maji na uwaweke samaki ndani kwa muda mfupi, chini ya dakika moja.

iv.Ni lazima kutoa maji yote na kukausha bwawa, na kunyunyizia chokaa ili kuua masalia ya vimelea vya magonjwa. Acha bwawa likiwa kavu kwa wiki mbili kabla ya kuweka maji kwa ajili ya kuweka samaki tena.


4. Ukosefu wa Chakula Bora Cha Samaki

Ukosefu wa chakula bora ndiyo sababu kuu kwa samaki kutofikia uzito wa kutosha kwa wakati unaotakiwa. Ukuaji wa samaki anayefugwa kwenye bwawa hutegemea zaidi chakula asili kinachopatikana ndani ya bwawa kutokana na rutuba ya mbolea na chakula cha ziada.

Chakula cha ziada huwa bora kutokana na mchanganyiko mzuri wa viini lishe vya vyakula mbalimbali ambavyo ni bora pia. Chakula pia ni changamoto kutokana na upatikanaji wake, gharama za manunuzi kuwa juu, na kutokuwa na kiwango sahihi cha protini kinachohitajika kwa ukuaji bora wa samaki.

5. Ukosefu wa Mbegu bora za samaki

Mavuno bora ya samaki hutegemea sana ubora wa mbegu. Usitumie vifaranga waliozaliwa ndani ya bwawa na baada ya mavuno kuwaacha ili kuwapandikiza kwa ajili ya mavuno yajayo. Njia hii
husababisha samaki kudumaa na pia mara nyingi samaki huzaliana kwa wingi kupita kiasi cha idadi ya samaki wanaotakiwa hivyo husababisha kudumaa.
Jinsi ya Kutatua

i. Agiza mbegu mpya kila unapoanza ufugaji ili kuwa na uhakika na ubora wa mbegu.

ii. Hakikisha mbegu ya vifaranga haitokani na vizazi ulivyofuga kwa muda mrefu katika bwawa lako.


6. Ndege na Wanayama wala Samaki

Ndege wanaokula samaki huwa ni tatizo sana kama mabwawa ya samaki yamechimbwa karibu na miti ambayo inatoa hifadhi kwa ndege na wanyama wengine. Pia nyasi ndefu kwenye kingo za tuta huhifadhi wanyama kama fisi maji, kenge, vyura, na wengine ambao hula samaki.


Jinsi ya Kuzuia

i. Ni lazima kusafisha mazingira yanayozunguka bwawa la samaki ili kuepuka ndege na
wanyama walao samaki kujenga makazi karibu na bwawa.

ii. Kujenga uzio mfupi kuzunguka bwawa ili kuzuia wanyama waharibifu kuingia ndani ya bwawa kiurahisi.

iii. Unaweza kuweka nyavu juu ya bwawa ili kuzuia ndege wasiingie kiurahisi kwenye
bwawa.

iv. Kuwepo kwa mlinzi pia kwaweza kusaidia kufukuza ndege na wanyama waharibifu
kuingia kwenye bwawa.

7. Samaki wala Samaki Wengine


Ukosefu wa chakula cha kutosha kwenye bwawa la samaki husababisha tabia zisizo za kawaida kwa samaki, ambapo baadhi ya samaki dhaifu huliwa na wenzao katika hatua zote za ukuaji.

Jinsi ya Kuzuia

i. Hakikisha samaki wanapata chakula cha kutosha.

ii. Weka samaki wenye umri mmoja kwenye bwawa moja ili kuondoa tatizo la samaki
wakubwa kula samaki wadogo.
Kwa leo tunaishia hapo. Karibu tena.


Karibu kwa majadiliano
Habari za wakati huu

Karibu tena darasani
UTUNZAJI WA BWAWA LA SAMAKI

Hii ni changamoto ambayo huwa inasahaulika mara nyingi. Utunzaji bora wa bwawa la samaki huleta mavuno bora kwa mfugaji anayelenga kupata faida. Ni lazima mfugaji kupata muda asubuhi na jioni kila siku kwenda kuangalia hali ya bwawa na samaki. Utunzaji wa bwawa la samaki hubeba changamoto zote kwa pamoja, hivyo basi kama mfugaji atazingatia utunzaji bora
wa samaki, itakuwa rahisi kwake kutatua changamoto zingine zote.
Vifaa na mahitaji mhimu katika ufugaji wa samaki
HITIMISHO

Kama ilivyo elezwa hapo juu, kabla ya kuanza kufuga samaki zingatia hatua zote mhimu ili
kupata mavuno wezeshi ndani ya muda muhafaka. Unapoanza kufuga samaki tambua kuwa
umeamua kuwekeza nguvu, muda, akili, pesa na mali, hivyo ni mhimu kuwa makini wakati wote na ujali kazi hiyo.


Chagua aina nzuri ya vifaranga na wenye ubora kutoka sehemu inayofahamika vizuri, pia tumia
chakula bora cha samaki kwa wakati wote wa ufugaji wako wa samaki, samaki wakiwa wadogo walishe chakula kilicho katika hali ya unga na pale wanapokuwa wakubwa walishe chakula cha hali ya vidonge (pellets).

Katika ulishaji zingatia kulisha katika kona moja ya bwawa kila siku kuwazoeza ili kurahisisha ulishaji na kupunguza upotevu wa chakula.

Unaweza kufuga samaki na wanyama wengine kama vile ng’ombe, kuku, sungura na bata au ukachanganya na mazao mengine kama vile mbogamboga na matunada kwa pamoja.

Hii inasaidia kurutubisha maji ya bwawani ili kutengeneza chakula cha asili cha samaki lakini pia maji yanayotoka katika bwawa yanamchango mkubwa katika ukuaji wa mazao kwani yanakuwa
na madini na virutubishi mhimu.

Huu ni ufugaji mseto
Ukisha vuna samaki wako kama soko likikata, unaweza kuwatengeneza na kuwauza wakiwa wakavu. Njia za kuwatunza ni kama vile kuweka kwenye jokofu, kutunza kwa kuwaweka kwenye chumvi, ama kuwakausha kwa jua, kubanika au kukaanga.

Kwa ufupi, hatua za ufugaji samaki aina ya sato kwenye bwawa ni kama ifuatavyo; Tafta eneo bora kwa ajili ya ufugaji samaki, Chimba bwawa kwa ufasaha na lijengwe kwa ubora na utaalamu, Chagua chanzo salama cha maji utakayo yatumia kufuga samaki, Chagua mbegu bora ya samaki utakao wafuga, Tumia chakula bora cha samaki wakati wote wa ufugaji wako, hakikisha unawahudumia na kuwatunza vizuri, tumia nyavu kuvua samaki wako, weka
kumbukumbu za kila shughuli inayo tendeka katika shamba lako kuanzia unapo wapandikiza mpaka unapo wavuna na kuuza, na uwe na mtaalau wa mambo ya ufugaji samaki.
Somo letu Kutakuwa imeishia hapa. Endelea kutufatilia. Kama uko na swali lolote tutafte kupitia social media accounts zetu.

Twitter. official4tao
Instagram. official_4tao
Facebook. Officialtao.
Telegram. official_tao


Direct contact us via..

Email. official4tao@gmail.com
Website. Officialtao.blogspot.com

Tel. 0753095800 or 0677991074


NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA.
Hello guys! Soon tutakuwa na somo la UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA.

Usipange kukosa