JamiiForums
56.3K subscribers
32.8K photos
1.82K videos
29.9K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
Mdau waJamiiForums.com anasema kama Ada ya Mtoto wako ya Mwaka mzima ni kubwa kuliko kipato chako cha mwezi, basi hapo Unajifilisi na kiwango chako cha Maisha kitakuwa duni sana

Anasema ukifuata kanuni hii basi utajikuta Kipato chako cha Miezi 10 iliyobaki kinagharamia mahitaji mengine muhimu na utaishi bila madeni wala Msongo wa Mawazo

Umezielewa hesabu za Mdau au unaona haziwezekani?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KipatoAdaKodi

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #JFStories #LifeLessons #JamiiAfrica
Picha zikionesha matukio tofauti ya Washiriki mbalimbali wa mbio (Fun Run) za Kilometa Tano zilizofanyika leo Aprili 27, 2025 ikiwa ni Siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo yanafanyika kwa siku tatu Jijini Arusha

Mbio hizo zilizoshirikisha Wadau mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho hayo zilianzia Uwanja wa Gymkhana/Mgambo na kuhitimishwa katika eneo hilo hilo

Soma https://jamii.app/WPFD2025Day1

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
ARUSHA: Leo Aprili 28, 2025 ni siku ya kwanza ya Maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani (#WorldPressFreedomDay2025). Maadhimisho haya yanafanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia na yanatarajiwa kufanyika kwa siku tatu

Kwenye Maadhimisho haya Wadau watajadili mada mabalimbali ikiwemo mchango wa Akili Mnemba (AI) kwenye Tasnia ya Habari na Mikakati inayoweza kutumiwa na Watengeneza Maudhui kwenye wakati huu ambapo Teknolojia imekua

Maadhimisho ya WPFD 2025 yanaratibiwa na Taasisi ya JamiiAfrica, Serikali, Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Wadau wengine wa Habari ndani na nje ya Tanzania

Soma https://jamii.app/WPFD2025DayOne

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, leo Aprili 28, 2025 JamiiAfrica kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa majadiliano maalum yanayolenga kuchambua Uendelevu wa Vyombo vya Habari Tanzania katika nyakati hizi za Kidijitali

Majadiliano haya yanalenga kuimarisha uhuru wa Vyombo vya Habari, kuchochea ubunifu na uendelevu, pamoja na kuhimiza uandishi wa habari unaotanguliza maslahi ya Umma

#JamiiForums #JamiiAfrica #WPFD2025 #PressFreedom #Democracy