JamiiForums
57.9K subscribers
31.4K photos
1.62K videos
29.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
DAR: Wananchi wa Saranga Ubungo wameto wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange kushughulikia kero ya Maji iliyopo eneo hilo kwa maelezo kuwa ni changamoto kubwa kwa Wakazi wa eneo hilo

Akitoa ufafanuzi, Mkuu wa Wilaya amemuagiza Meneja wa DAWASA Kanda ya Kinyerezi kuzungukia nyumba ambazo zimejiunganishia huduma ya maji bila kufuata utaratibu, jambo linalosababisha Wananchi wengine kukosa huduma ya maji, ili marekebisho yafanyike

Naye, Meneja wa DAWASA, Crossman Makere amekiri kufahamu kuhusu kero hiyo na kusema imeanza kufanyiwa kazi kwani zoezi la ulazaji wa mabomba linaendelea

Soma https://jamii.app/UhabaMajiSaranga

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
Namba ya simu ni taarifa binafsi na kama taarifa nyingine yoyote nyeti, inapaswa kulindwa (Iwapo mwenye nayo hajaamua kuiweka wazi kwa Umma)

Kila wakati, uliza idhini kabla ya kutoa namba ya mtu mwingine, kwani ni sehemu ya kuheshimu faragha yao

Soma https://jamii.app/NambaYaMtuRidhaa

#JamiiForums #JFDigitali #DataPrivacy #PersonalDataProtection #TaarifaZakoMaishaYako #JFMdau2025
UWAJIBIKAJI: Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamikia changamoto kwenye zoezi la uboreshaji wa mifumo ya majitaka Mbezi Beach, Dar es Salaam ulioacha barabara zikiwa zimefumuliwa ovyo, changamoto hiyo imetatuliwa

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro inasema Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Mkandarasi wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Mbezi Beach, Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Ltd (BCEG) pamoja na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wameboresha barabara hiyo

Soma https://jamii.app/MifumoMajitakaKurekebishwa

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFHuduma #JFMdau2025
Je, zawadi (takrima) na rushwa zinatofautianaje katika muktadha wa Uchaguzi?

Kufahamu hili na mengine usikose kujiunga nasi katika Mjadala wa “Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?” Kupitia Xspaces ya JamiiForums, Alhamisi hii ya Februari 13, 2025 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 usiku

Tukitumia uzoefu wa Wanasiasa waliowahi kushiriki chaguzi mbalimbali, tutajadili jinsi rushwa inavyoathiri uadilifu wa Uchaguzi, Uwajibikaji wa Viongozi na maisha ya Wananchi kwa ujumla

Kushiriki bofya https://twitter.com/i/spaces/1ZkKzYMNvbDxv

#ChaguaKiongoziSioPesa #Accountability #Demokrasia #ServiceDelivery #Uwajibikaji
Haki za Mtuhumiwa wakati wa Kuhojiwa (Rights During Interrogation) zinamlinda Mshukiwa dhidi ya vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili wakati wa uchunguzi. Haki hizi zinahakikisha Uchunguzi unafanyika kwa Haki na kwa kuheshimu Utu wa Mtuhumiwa

Haki Muhimu zinajumuisha Mtuhumiwa kutolazimishwa kujitoa hatiani au kutoa ushahidi unaoweza kumletea madhara. Pia, ana Haki ya kutotoa maelezo yoyote yanayoweza kutumiwa dhidi yake Mahakamani

Pia, ana Haki ya kuhakikisha Wakili wake anakuwepo wakati wa mahojiano ili kuepuka Unyanyasaji au matumizi mabaya ya Sheria na kuhakikisha ushahidi unapatikana kwa njia halali na ya Haki.

Soma zaidi https://jamii.app/RightToFairTrial

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #KesiYaHaki #HakiZaBinadamu #UtawalaWaSheria
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SINGIDA: Siku chache baada ya Wananchi wa Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama wakiwemo Wanawake wanaotaka kujifungua, kulalamikia uhaba wa maji na kuchota Maji dumu 6 hadi 12 ili wapatiwe Huduma za Afya katika Zahanati ya Dominiki, Mamlaka imekiri uwepo wa changamoto hiyo

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) - Singida, Mhandisi Lucas Saidi amesema kwa Wilaya hiyo hali ya upatikanaji wa Maji kwa sasa ni 70.7% na tayari Serikali imetenga Tsh. Milioni 150 katika bajeti ya Mwaka 2024/25 ili kuchimba visima katika Vijiji kadhaa ikiwemo Asanja, Singa, Mwangeza, Kinto na Dominiki.

Soma https://jamii.app/RUWASAMajiDominiki

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#SIASA: Chama cha #ACTWazalendo kimefungua kesi 51 za kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini, na hadi sasa chama hicho kimeshinda mapingamizi katika kesi moja Mkoa wa Kigoma huku kesi nyingine zikiendelea kusikilizwa

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mahakama ya Wilaya ya Hakimu Mkazi, Februari 10, 2025, Kiongozi Mstaafu wa Chama hicho, #ZittoKabwe ameituhumu Serikali kwa kuweka mapingamizi yasiyo na msingi ili kuchelewesha mchakato wa kusikilizwa kwa mashauri ya msingi wa kesi hizo

Ameongeza kwa kusema kuna vipingamizi vya ajabu vinavyowekwa kwenye kesi hizi kwa makusudi ili kuzuia haki ya Wananchi kutendeka.

Soma https://jamii.app/VizingitiKesiUchaguzi24

#JamiiForums #Accountability #Governance #JFMatukio #LGE2024
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Alichokisema Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue, #Bungeni leo Februari 11, 2025 huku akiwapongeza Wabunge wenzake kwa kufanya Kazi Majimboni kwao

Una neno gani kuhusu kauli ya Mbunge huyu?

Tembelea https://jamii.app/SaashishaBungeniFeb11

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #Siasa
Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi huadhimishwa Februari 11 kila Mwaka kusherekea mafanikio na michango ya Wanawake na Wasichana katika Sekta ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM)

Siku hii inahamasisha Wanawake na Wasichana zaidi kufuata na kujiunga na taaluma za Sayansi na Teknolojia lengo likiwa ni kuvunja vizuizi na dhana potofu ambazo Kihistoria zimezuia Ushiriki wa Wanawake katika sekta hizi

Soma https://jamii.app/WanawakeSayansi25

#JamiiForums #STEM #GenderEquality #JFWomen #UNWomen
DAR: Timu ya #Simba imerejea katika usukani wa Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga #TanzaniaPrisons Magoli 3-0 kwenye Uwanja wa KMC, wafungaji wakiwa ni Jean Ahoua (29), Elie Mpanzu (44) na Ladack Chasambi

Mchezaji Chipukizi wa Simba, Chasambi ambaye wiki iliyopita alikuwa gumzo baada ya kujifunga katika mchezo uliopita na kuchangia timu yake kupata sare ya 1-1 dhidi ya Fountain Gate, safari hii amewafurahisha mashabiki wake kwa kufunga goli

Simba sasa imefikisha alama 47 ikiishusha Yanga ambayo ina pointi 46, timu zote zikiwa zimecheza michezo 18

Soma https://jamii.app/SimbaPrisonsFeb11

#JFSports #JamiiForums #JFLigiKuu25
Siku ya Usalama Mtandaoni huadhimishwa Februari 11 kila mwaka ili kuongeza uhamasishaji kuhusu matumizi Salama ya Mitandao

Siku hii ilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kujenga uelewa kuhusu Ulinzi wa Taarifa, Unyanyasaji Mtandaoni (Cyberbullying) na hatari zinazozunguka Dunia ya Kijitali

Soma https://jamii.app/SaferInternetDay25

#JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #DataPrivacy #DataProtection #SaferInternetDay2025
UGANDA: Kiongozi wa upinzani, Dkt. Kizza Besigye amegoma kula Chakula akiwa katika Gereza la Luzira, Mjini #Kampala kwa madai ya kupinga kuendelea kushikiliwa pamoja na kuhofia Maisha yake

#Besigye ambaye alikuwa Daktari Binafsi wa Rais #YoweriMuseveni alikamatwa kinguvu akiwa Nchini Kenya tangu Novemba 2024, na anashtakiwa kwa madai ya kumiliki silaha kinyume cha Sheria

Wajumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Bunge waliotembelea gereza hilo wameeleza kuwa Dkt. Besigye anahisi yuko hatarini kwa kuwa Serikali (ambaye ni mlalamikaji) inadhibiti wa Gereza hilo

Soma https://jamii.app/BesigyeAgomaKula

#JamiiForums #Democracy #HumanRights #CivilRights
MAREKANI: Kampuni ya #META imeanza kutekeleza mpango wake kwa kuwapunguza kazi Wafanyakazi 4,000 katika sehemu mbalimbali Duniani wanaoshindwa kufanya vizuri na kujiandaa kwa ajili ya uwekezaji mkubwa kwenye matumizi ya Akili Mnemba (AI)

Januari 2025, Kampuni ya Meta ilitangaza mpango wa kupunguza takriban 5% ya Wafanyakazi kwa kuzingatia utendaji wao kazini

Aidha, kampuni hiyo imewapa Wafanyakazi walioathiriwa na punguzo hilo nchini Marekani malipo ya kuachishwa kazi ya mishahara ya Wiki 16 na nyongeza ya wiki mbili kwa kila Mwaka wa utumishi

Soma https://jamii.app/MetaJobLayoff

#JamiiForums #Governance #SocialJustice
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#SIASA: Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema ameamua kukaa kando kwa hiari na kuwaachia wengine nafasi ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutumika vya kutosha katika nafasi mbalimbali Serikalini

Ameyasema hayo leo, Februari 11, 2025 alipofungua Kikao Kazi cha Tano cha Mamlaka ya Serikali Mtandao Jijini Arusha

Kauli ya Dkt. Mpango inakuja baada ya yeye (Dkt. Mpango) kuomba kupumzika kutumikia kama Makama wa Rais na Chama cha Mapinduzi (#CCM) kumpitisha Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025

Soma https://jamii.app/MpangoKukaaKando

#JamiiForums #Governance #UchaguziMkuu25